EWURA: Wasambazaji wa bidhaa mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara kuchukua bidhaa kutoka bandari ya Tanga pekee

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,112
EWURA imeagiza wasambazaji wote wa bidhaa za petroli mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara kuanza kuchukua bidhaa hizo kutoka Bandari ya Tanga, na si sehemu nyingine.

Atakayekiuka agizo hilo atatozwa faini TZS Milioni 100 au kifungo kisichopungua miaka 10, au vyote.

EWura.jpg
 
Ewura imewataka wauzaji wote wa bidhaa za petrol kutoka mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Tanga kuchukua bidhaa hizo katika bandari ya Tanga na siyo sehemu nyingine yoyote.

Atakayekiuka agizo hili atatozwa faini isiyopungua sh milioni 100 ama kifungo kisichopungua miaka 10 au vyote kwa pamoja.

Source Swahili Times

Maendeleo hayana vyama!
 
Kiufupi hatua hiyo inaumiza wafanyabiashara Sio kwamba hawana akili kupapita Tanga wakachukulie mZigo Dar paspo na faida
 
Watu wafanye kazi na kutafuta maendeleo lakini wakiwa huru. Kwa nini umlazimishe mfanyabiashara wapi kwa kuchukua mzigo wake
 
This is good, na kusini ifanyike hivyo, tupunguze utitir wa malot usiokuw wa lazima kwa baadhi ya barabara
 
Hii ni nzuri sana

Lakini kwanini siku zote wafuate mafuta Dar es salaamu?
 
Kiufupi hatua hiyo inaumiza wafanyabiashara Sio kwamba hawana akili kupapita Tanga wakachukulie mZigo Dar paspo na faida
Wanaumia vipi?? wakati mwingine tuwe wakweli hivi unapochukua mafuta Dar ukauze Segera wakati Tanga ni Km 70 tu kutoka Segera na unaweza kuyapata Pale Tanga ni kipi bora?? maana ya serikali ni kuwa na maamuzi Mazuri ambayo yanasaidia watu wengi kwa pamoja na hilo ndio maana ya kuwainua watu. Kuwainua sio kuwapa mihela hilo halipo wala kuwambia kaaeni tu nyumbani bila kazi!!!

Kazi ni wewe ujitaftie serikali inakuwekea Mazingira rafiki, tushukuru jameni hata kwa kile kidogo serikali hii inafanya, Mfano suala la Mafuta ni zuri sana watu wengi sana wanasahau kwamba kwa muda mrefu sana mafuta yalikua yanapanda kienyeji tu tena kila Budget mafuta yanapanda ila kwa miaka hii mitano Magufuli kadhibiti hili jambo vizuri.Hili halimanishi amepatia yote ila mnyonge mnyongeni...
 
Wanaumia vipi?? wakati mwingine tuwe wakweli hivi unapochukua mafuta Dar ukauze Segera wakati Tanga ni Km 70 tu kutoka Segera na unaweza kuyapata Pale Tanga ni kipi bora?? maana ya serikali ni kuwa na maamuzi Mazuri ambayo yanasaidia watu wengi kwa pamoja na hilo ndio maana ya kuwainua watu. Kuwainua sio kuwapa mihela hilo halipo wala kuwambia kaaeni tu nyumbani bila kazi!...
Tatizo msiojua kitu huwa mnaandika sana.

Hivi unazan bei ya mafuta ya kichukuliwa Tanga na ya kichukuliwa Dar kwa mtumiaji wa Dongobesh,hydom,longido,Pasua na hata maramba ya Tanga zitapishanaa?

Kuna kitu hujui hii kitu inampango wa kuua biashara ya mafuta nchini
 
Back
Top Bottom