EWURA: Taarifa kwa umma kuhusu bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli kuanzia 1 Desemba 2021

Kwa iyo izi Ndo bei walizosema wamepunguza sijui bil mia MOJA na mwenye tozo za mafuta ili yashuke,

Aisee Tz tuna bahati mbaya sana
 
Hapa mwisho wa siku waumini wa team mbili watatupiana vijembe weee... itakuwa usiku, itakuwa asubuhi, siku nyingine.
 
huko mikoani ni sahihi tu hyo bei
We hujielewi.. kwa mantiki yako, Dar, Tanga na Mtwara (kwenye bandari) ndo kungekuwa na bei rahisi ya mafuta... !! Is not always the case na siyo hivyo. Kuna wakati Chalinze, Kibaha na Mlandizi huwa na bei rahisi ya mafuta kuliko huko kwenye bandari
 
Sasa Mama yeye ndio anapanga bei ya dunia? Pamba yako unazalisha na bei hupangi wewe sembuse mafuta ya watu uwapangie bei. muwe mnafikiria kabla ya kuandika.
 
Wakuu wa JF, nawasalimu kwa Jina la JMT.
Nitafurahi kupata mtizamo kinzani kutoka kwenu wadau juu ya nitakachoongea. Nimefanya utafiti usio rasimi katika vituo kadhaa vya Mafuta baada ya tangazo ya bei elekezi ya mafuta kwa kuanzia tarehe 01/December/2021 na nimeona ulinganifu wa bei za mafuta kwa vituo vyote vyenye majina makubwa (Oryx, Puma, Total etc) na vile ambavyo mafuta yake ubora wake hutiliwa shaka. Kutokana na hayo niliyotaja hapo juu ndipo nikajiuliza kwamba kilichotangazwa juzi ni "Bei Elekezi" au " Bei rasmi' kwa maeneo husika? Ndipo nikawaza nje ya "Box", Je kama kuna "Uelekezi" katika hizi "Bei Elekezi", Vile vituo vya mafuta ambavyo ubora wa mafuta yake hutiliwa shaka na wateja wengi, havitopata "Anguko Baya sana".
Je wana JF mnamtizamo gani juu hili nililoliona kwenye bei elekezi kwa Mwezi December 2021?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…