EWURA: Taarifa kwa umma kuhusu bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli kuanzia 1 Desemba 2021

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,481
2,000
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU BEI KIKOMO ZA BIDHAA ZA MAFUTA YA PETROLI KUANZIA JUMATANO, TAREHE 1 DESEMBA 2021

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), inatangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini. Bei hizi zitaanza kutumika kuanzia Jumatano, Tarehe 1 Desemba 2021. Pamoja na kutambua bei hizo, ni muhimu kuzingatia yafuatayo:-

(a) Kama inavyoonekana katika Mchoro Na. 1, bei za mafuta katika soko la dunia zimekuwa zikiongezeka kila mwezi ambapo:​

(i) bei ya petroli imeongezeka kwa asilimia 23 kutoka dola za Marekani 644.01 kwa tani kwa mwezi Mei 2021 na kufikia dola za Marekani 793.14 kwa tani mwezi Oktoba 2021. Kwa kipindi hicho, bei ya petroli katika soko la ndani zilipaswa kuwa zimeongezeka kwa jumla ya Shilingi 241 kwa lita na kufikia Shilingi 2,610 kwa lita mwezi Desemba 2021;​
(ii) bei ya dizeli imeongezeka kwa asilimia 30 kutoka dola za Marekani 550.68 kwa tani kwa mwezi Mei 2021 na kufikia dola za Marekani 713.28 kwa tani mwezi Oktoba 2021. Kwa kipindi hicho, bei ya dizeli katika soko la ndani zilipaswa kuwa zimeongezeka kwa jumla ya Shilingi 311 kwa lita na kufikia Shilingi 2,492 kwa lita mwezi Desemba 2021; na​
(iii) bei za mafuta ya taa imeongezeka kwa asilimia 30 kutoka dola za Marekani 558.90 kwa tani kwa mwezi Mei 2021 na kufikia dola za Marekani 726.56 kwa tani mwezi Oktoba 2021. Kwa kipindi hicho, bei ya mafuta ya taa katika soko la ndani zilipaswa kuwa zimeongezeka kwa jumla ya Shilingi 120 kwa lita na kufikia Shilingi 2,235 kwa lita mwezi Desemba 2021​

e1.JPG

Mchoro Na. 1: Mwenendo wa Bei za Mafuta katika Soko la Dunia​


(b) Kwa lengo la kupungu ongezeko la bei za mafuta hapa nchini, Serikali ilifanya juhudi za makusudi ambapo tarehe 5 Oktoba 2021, Serikali ilipunguza tozo mbalimbali za taasisi zake kwa kiwango cha Shilingi 29.38 kwa lita ya petroli, Shilingi 30.05 kwa lita ya dizeli na Shilingi 26.99 kwa lita ya mafuta ya taa.​
(c) Pamoja na juhudi hizo, Serikali imeendelea kuchukua hatua zaidi kutokana na kuendelea kuongezeka kwa bei za mafuta katika soko la dunia. Hivyo, kwa mwezi Desemba 2021, Serikali imeahirisha kukusanya Ada ya Mafuta (Petroleum fee) ya Shilingi 100 kwa lita kwenye mafuta ya petroli na dizeli.​
(d) Kulingana na mwenendo wa bei za mafuta katika soko la dunia, bei za mwezi Novemba 2021 zimeanza kushuka. Kwakuwa bei za soko la dunia zinaakisiwa katika soko la hapa nchini baada ya miezi miwili, unafuu wa bei za soko la dunia ulioanza kujitokeza katika mwezi Novemba 2021 unatarajiwa kuonekana katika soko la hapa nchini katika bei za mwezi Januari 2022.​
(e) Vilevile, kama ilivyoelezwa hapo awali, Shirika la Maendeleo ya Mafuta Tanzania (TPDC) ilishiriki katika zabuni za kuleta mafuta mwezi Desemba 2021 na kushinda zabuni mbili za kuleta mafuta ya dizeli na mafuta hayo yatategemewa kuleta unafuu wa bei nchini. Kulingana na ratiba za upokeaji wa mafuta katika bandari ya Dar es Salaam, unafuu wa mafuta hayo utaakisiwa katika bei za hapa nchini mwezi Februari 2022.​
(f) Ni vyema ikafahamika kuwa, Serikali inaendelea kufuatilia kwa karibu mabadiliko ya bei za mafuta katika soko la dunia na kufanya kila linalowezekana ili kuepukana na madhara yanayoweza kujitokeza katika mnyororo mzima wa uchumi hapa nchini iwapo bei zitaongezeka kwa kiwango kikubwa. Hii ni pamoja na kuendelea kufanya marekebisho yatakayohitajika katika tozo na kodi mbalimbali za Serikali.​
(g) Kufuatia maelezo hayo, bei za mafuta za rejareja kwa mwezi Desemba 2021 zitakuwa kama ifuatavyo:​

(i) kwa mafuta ya petroli, bei itakuwa Shilingi 2,510 kwa lita kwa Dar es Salaam, huku Tanga na Mtwara bei itakuwa Shilingi 2,525 kwa lita na Shilingi 2,569 kwa lita, mtawalia;​
(ii) kwa mafuta ya dizeli, bei itakuwa Shilingi 2,392 kwa lita kwa Dar es Salaam, wakati Tanga na Mtwara bei itakuwa Shilingi 2,413 kwa lita na Shilingi 2,423 kwa lita, mtawalia; na​
(iii) kwa mafuta ya taa, bei itakuwa Shilingi 2,235 kwa lita kwa Dar es Salaam na bei za bidhaa hiyo kwa mikoa yote nchini zimekokotolewa kwa kujumuisha gharama za usafirishaji mpaka miji husika.​

(h) EWURA inapenda kuukumbusha umma kwamba bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli kwa eneo husika zinapatikana pia kupitia simu za mkononi kwa kupiga namba *152*00# na kisha kufuata maelekezo. Huduma hii ni bure na inapatikana kupitia mitandao yote ya simu za mkononi hapa nchini.​
(i) Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2015, kifungu namba 166, bei za bidhaa za mafuta ya petroli zitaendelea kupangwa na soko. EWURA itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta. Taarifa hizi zina lengo la kuwasaidia wadau kufanya maamuzi stahiki kuhusu manunuzi ya bidhaa za mafuta.​
(j) Kampuni za mafuta ziko huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani mradi tu bei hizo zisivuke bei kikomo (price cap).​
(k) Vituo vyote vya mafuta vinatakiwa kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana na yakionesha bei ya mafuta katika kituo husika. Pale ambapo inawezekana kuchagua, wateja wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta katika vituo vinavyouza mafuta kwa bei nafuu zaidi ili kushamirisha ushindani. Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja. Adhabu kali itatolewa kwa kituo husika kwa kutotekeleza matakwa ya kisheria kwa mujibu wa kanuni husika.​
(l) Wauzaji wa mafuta ya petroli wanatakiwa kutoa risiti za mauzo kutoka kwenye mashine za EFPP (Electronic Fiscal Pump Printers) na Wanunuzi wahakikishe wanapata stakabadhi hizo za malipo zinazoonyesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita. Stakabadhi hizo za malipo zitatumika kama kidhibiti kwa wanunuzi wa mafuta endapo kutajitokeza malalamiko ya aidha kuuziwa mafuta kwa bei ya juu kuliko bei kikomo au kuuziwa mafuta yasiyo na kiwango cha ubora kinachofaa, na pia, risiti hizo zitasaidia kurahisisha ukusanyaji wa kodi za Serikali zitokanazo na mauzo ya mafuta ya petroli.​
 

Attachments

  • File size
    429 KB
    Views
    26

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
7,711
2,000
Naona bei inazidi kupanda tu.
Kuna kila dalili kuwa kabla ya kufikia 2025 huenda bei ya Petrol/Diesel ikawa imevuka shilingi elfu tatu kwa lita.

Kama tutaendelea kukaa kimya bila kumtimua chap chap huyu mama basi tutaangamia. Dawa ni kupachimbisha tu.
 

Memento

JF-Expert Member
Jun 13, 2021
1,943
2,000
Ewura imetoa taarifa ya kupanda kwa bei ya mafuta kwa mwezi December unaoanza kesho, Bei hii itafanya baadhi ya mikoa kununua mafuta kwa Sh.2750.

Lakini kwa sasa kwenye soko la dunia Bei ya Mafuta imeshuka, Ewura wamesema kushuka huko mafuta kwenye soko la dunia kutaleta mabadiliko mwezi January na February.

Poleni kwa wale wote mtaoathirika hasa wa mikoani, 2750 si Mchezo.
Screenshot_20211130-214015_1.jpg
Screenshot_20211130-213813_1.jpg
Screenshot_20211130-214200_1.jpg
Screenshot_20211130-213228_1.jpg
 

Memento

JF-Expert Member
Jun 13, 2021
1,943
2,000
Tanzania wapi wanachimba mafuta?? Huyo unaesema watamkumbuka aliwezesha mafuta kupatikana bila kufanya importation?

Yaani CCM hovyo kabisa hamjui nani hata anacontrol uchumi wa dunia na biashara kama hizo zinakuwa controlled vipi!

Hafufuki ng'o hata mfanyeje
Ila mafutq kwenye soko la dunia yameshuka toka mwezi huu mwanzoni, sikuona sababu ya kusubiria january
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom