European Parliament resolution on Tanzania

European Parliament resolution on Tanzania

Utasikia wanasema mabeberu wanataka kutuibia, hivi Mmarekani anatuibia nini?

Kuna majambazi kama China, Ila hatajwi...

Wamemaliza na kufilisi mifuko ya jamii...sasa sijui watafyeka mini
Mchina atatajwaje wakati hahoji masuala ya utawala bora anawaacha wapete
 
Mimi kama mwananchi wa kawaida niombe Wizara ya mambo ya nje iyamalize ,matatizo yetu na nchi za ulaya ,tunajua wazi hao wenzetu huringia nini ,na sisi tunataka nini basi,waswahili walisema Adui mupishe siyo lazima mupigane ,sisi tuonyeshe kukubaliana na tusiyotaka kukubaliana
Tushindane au tusishindane Nchi yetu itabaki Tanzania.
Niwaombe wanaoshangilia hili ni sawa na Ngamia kuweka kichwa kwenye Mchanga kuwa hawezi zulika,ukweli tutakao umia na aina yoyote ya vikwazo ni watu wa kada ya chini hasa vijijini ambako gharama za mafuta ya taa itapanda ,usafiri utapanda ,waalimu mishara kutopata kwa muda ,na n.k Heri nusu Shari kuliko Shari kamili.tukubari wao ni wababe kwani sie hatuna uwezo wa kuwaonya.
AMANI NI TUNU YETU
 
Kwanini watuingilie kwenye mambo yetu ya ndani?, hawa watu hawamjui Magufuli?.
Tanzania ni sovereign state, hatupangii watu na hatupangiwi.
Subirini tamko
P
Uandishi wako huwa nauelewa sana. Siku zote mkuu unajitahidi kutokuwa trapped. Hata hapa kwetu ukimdhuru mwanao lazima sheria ikuhukumu hata kama ni mwanao.
 
Huyu mchina anaependwa kwa sasa ni mbaya zaidi kwa Africa na dunia yote.
Zamani alipokuwa na dhiki alikuwa mzuri sana yaani kawa kama mtu wa kijijini na sasa kawa wa mjini, maana ule ukarimu hana tena baada ya uchumi wake kuwa juu.

Sasa anapambana na kuwa juu zaidi ila mbaya zaidi mchina ni mwizi na ni muharibifu
Hata akikuta nge na watoto wake anawala wote.
Atamaliza mpaka vizazi vya viumbe vyote
Kuhusu hawa wazungu watupe amani ila kwa masharti hayo sijui kama yatakubalika labda kidiplomasia kama ya watangulizi
Mchina sio mtu mzuri na hana huruma hata chembe. Bora hao wazungu wana utu lakini mchina afadhali ukutane na simba anaweza kukuonea aibu akakuacha
 
Vijana wa Lumumba mazuri sana kucheza na akili za jiwe,kwenye id zilizozoeleka wanampa kichwa jiwe kwamba akomae hawatubabaishi.then Wana id zao za kuueleza ukweli halisi.ukute huyu ni Isis.
 
Marekani wamesema watahakikisha kuakuwa na uchaguzi wa huru na haki ifikapo 2019/2020.

Sasa akili.mkichwa akishupaza shingo atalipuliwa
Hata haya yatokeayo target ni uchaguzi wa 2020 hakuna jingine
 
Nenda magogoni ukampe ushauri maana ndo kuna shida kule
 
Nikiona mTanzania mwenye akili ya kuleta maneno kama haya hapa namdharau sana,wewe kumbe mtu anaweza akatoka huko atokako akaja hata nyumbani akakwambia mke wako awe wa kwake kwa uhulu wa mtu binafsi utamkubalia.mzungu atoke huko atokako aje na upumbavu wake kwetu na sisi tuupokee?wakati mwingine watu wanaoandika maneno kama haya ni wale waliobanwa na Makonda hivi majuzi sasa eti wanataka uhulu wao,mTanzania mependa taifa lake na mzalendo hawezi kuja na upuuzi huu

Bora Kuku anaakili kuliko wewe

Bwege kabisa
 
USIKUBALI KUPOTOSHWA HAYA NDIYO MAAZIMIO YA BUNGE LA ULAYA EU

Waziri wa mabo ya nje asema awezi kuzungumzia azimio hilo anasubiri Raisi atoe tamko

>>>Utawala wa sheria
>>>Haki za binadamu
>>>Kamata kamata ya wapinzani
>>>Elimu
>>>Afya
>>>Haki ya kupata habari
>>>Sheria kandamizi na matamko
>>>Mikutano ya kisiasa kupigwa marufuku
>>>Kuandamwa kwa watetezi wa haki za binadamu
>>>Kufungiwa vyombo vya habari
>>>Kuandama watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja

BUNGE HILO LIMETAKA PIA HAYA YATEKELEZWE

>>>Kuachiliwa wafungwa wote wa kisiasa
>>>Kurekebisha baadhi ya sheria ikiwemo ya makosa ya mtandao , sheria ya vyombo vya habari
>>>Kuachia uwanja kwa watetezi wa haki za binadamu kufanya shughuli zake

LIMETAKA PIA HAYA YAWEPO

>>>Tume huru ya kuchunguza kutekwa na kuakamatwa kwa waandishi wa habari na watu kupotea katika mazingira ya kutatanisha
>>>Hatua za kisheria kuchukuliwa kwa wale wataobainika kuvunja haki za binadamu
Magufulification
 
Kwanini watuingilie kwenye mambo yetu ya ndani?, hawa watu hawamjui Magufuli?.
Tanzania ni sovereign state, hatupangii watu na hatupangiwi.
Subirini tamko
P
Pasco kaka yako ajitathmini kabla ya kutoa tamko, hao jamaa sio kama anajibu watu wa Chadema au CUF hao ni "wanaume " kama anavyo waita yeye mwenyewe hivyo awe makini.
Asidhani kuwaonyesha jeuri wakati wanayo muambia ni ya kweli na mengine tuliyaridhia kwenye mikataba ya kimataifa ni ushujaa, dhiki ikiangukia nchi asidhani atasamehewa kama Mugabe aliye onewa huruma kwa vile ni baba wa taifa la Zimbabwe
 
Ni afadhari kuuficha upumbavu wako kuliko kuuonyesha,shinzi kabisa lisilo na akili.Afrika hii mnatuletea kauli ya eti mzungu kasema?pumbavu wewe
Bora Kuku anaakili kuliko wewe

Bwege kabisa
 
Jephta2003:
Umejipinda kweli na kututisha aiisee kana kwamba sisi hamnazo kabisa.
Mjuaji wewe, mtaalam wa mambo haya unatufundisha sisi tusiojua kitu tusifanye makosa kama ya hao wengine!

Sisi hatujawahi kuishi Libya kujua yaliyowatokea huko. Sisi tunayoyajua ni ya hapa hapa kwetu Tanzania. Tunayaishi na kuyaona sisi wenyewe. Wewe mtaalam wa mambo haya unataka hata haya tunayoyashuhudia sisi wenyewe tusiyaamini kuwa ni ya halisi?

Basi sawa, ngoja niungane nawe kuhusu hayo makaburu yasiyotutakia mema na nikubali kabisa kwamba wasiingilie mambo yetu. Je, uko tayari, wewe na hao waliokutuma kutuachia tujichagulie wenyewe viongozi tunaowataka hapo 2020 chini ya tume huru ya uchaguzi?

Ni hili ombi moja tu ninalotaka wewe na hao waliokutuma mlifikirie. Tupeni uhuru wa kujichagulia viongozi tunaowataka. Kama wengi wetu watapenda muendelee nyinyi wenyewe, hakuna atakayewabishia kama mtakuwa mmechaguliwa kwa haki.

Ombi langu kwako. Acha kututishia nyau na hayo maLibya nakadhalika. Hii Tanzania ni nchi yetu, na sisi sote tunaipenda sana. Hii sio nchi yenu pekee, sio mali yenu.
 
Kwanini watuingilie kwenye mambo yetu ya ndani?, hawa watu hawamjui Magufuli?.
Tanzania ni sovereign state, hatupangii watu na hatupangiwi.
Subirini tamko
P
Kwa ninavyo mjua tamko lake halitakuwa la heri kwa nchi yetu itakuwa ni sawa na kumwagwa petro kwenye moto unaowaka na watakao endelea kuumia ni wananchi.
 
Nakuhakikishia ni wazungu na tutawakamata popote duniani walijifanya wajanja kuvuka mipaka Jeshi letu la polisi linafanya kazi kwa weredi na utaalam wa hali ya juu
Hata walipokuwa wamemteka Mo tulijua walipo uzuri tulijua anaishi vizuri na watamuachia vizuri
Si mliona alitoka na kitambi wakati kabla ya kutekwa afya yake ilikuwa goigoi walimuachia akiwa na ari mpya nguvu mpya.

Walimteka wakamuachia wakampa simu awasiliane na Baba yake amfate [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

Natamani nitekwe Kama mo.
😀😀😀😀😀😀😀 wanatuletea "MANJEGEKA". aka FUTUHI.
 
Habari za wikiendi wana JF! Baada ya Jumuiya ya Ulaya na maseneta wa Marekani kutoa matamko na maazimio kuhusu Tanzania tunasubiri Vyombo vyetu vya habari hususan Runinga pendwa ya taifa iwajulishe watanzania jinsi ambavyo wazungu hawa hawatutakii mema. Mtanzania wa kijijini asiyesoma mitandao ya kijamii ana haki kujua jinsi tunavyosemwa vibaya na wazungu. Mtanzania ana haki ya kujua anavyotuhumiwa na anavyotetewa. TBC - get this broadcasted to the nation!!!
Wanatuletea HIV then hawatutakii mema mtu anawajibu jeuri then unataka waendelee kuwasaidia.
 
Back
Top Bottom