European Parliament resolution on Tanzania

European Parliament resolution on Tanzania

Kwanini watuingilie kwenye mambo yetu ya ndani?, hawa watu hawamjui Magufuli?.
Tanzania ni sovereign state, hatupangii watu na hatupangiwi.
Subirini tamko
P
Hawezi tia hata mkato kwenye hayo maazimio! Na kwa taarifa yako ni kuwa utekelezaji ulishaanza ila ninyi mtauona kama zawadi ya x mass na mwaka mpya!
Chezea senate la wenyewe na wale wazee wa nato! Hawana msalie mtume katika utekelezaji wa maamuzi yao na lazima yatekelezwe yote kama wqlivyoyaleta! Mliharibu kumtimua yule balozi wa EU kama paka mwizi na sasa mtapiga magoti na kufunga mikono mbele mithili ya mpokea sakramenti!
 
Nimekumbuka utotoni siku moja tunakula chakula cha jioni babu yetu alikuwa kavaa msuli sasa bahati mbaya mzigo ukawa unaonekana akiwa kwenye kigoda chake. Tukaona kuwa babu yuko uchi! Tulibaki tunaangaliana tu kucheka tunashindwa kumwambia tunaogopa na chakula kilikosa ladha kila mmoja wetu alishiba ghafla
 
Nikiona mTanzania mwenye akili ya kuleta maneno kama haya hapa namdharau sana,wewe kumbe mtu anaweza akatoka huko atokako akaja hata nyumbani akakwambia mke wako awe wa kwake kwa uhulu wa mtu binafsi utamkubalia.mzungu atoke huko atokako aje na upumbavu wake kwetu na sisi tuupokee?wakati mwingine watu wanaoandika maneno kama haya ni wale waliobanwa na Makonda hivi majuzi sasa eti wanataka uhulu wao,mTanzania mependa taifa lake na mzalendo hawezi kuja na upuuzi huu
Umeandika nini hapa? Kiswahili kibofu kuliko cha std I c! Uhulu uhulu uhulu! Lowasa njoo uone uliokuwa unawapigania juu ya elimu wakakutosa kwa kipande cha sabuni wanavyohangaika kuandika visivyoeleweka! Na kwanini umuone mwanamke katika mtazamo huo as if yeye ni commodity! Dharau au ujinga mwingi!
Na kwanini pia uilinganishe nchi hii na mwanamke? Ni dharau au unyanyasaji wa kijinsia?!
US na EU kumbe wapo sahihi sana na wamesahau kuongeza kipengele cha unyanyasaji wa wanawake kama alivyofanya huyu aliyetumwa na aliyemtaja humu!
Mlisaini mikataba hiyo mkiwa walevi au lugha ilikuwa ngumu? Jifunzeni kutoivunja mikataba mlioingia kimangumgo!
 
Ni vizuri kujenga mashikamano na china kwani wanaheshimu haki za nchi nyingine kujiamlia mambo yao, kuliko hao wanafiki wanaokupa misaada kwa masharti ya kukubali kuwa shoga
 
Habari za wikiendi wana JF! Baada ya Jumuiya ya Ulaya na maseneta wa Marekani kutoa matamko na maazimio kuhusu Tanzania tunasubiri Vyombo vyetu vya habari hususan Runinga pendwa ya taifa iwajulishe watanzania jinsi ambavyo wazungu hawa hawatutakii mema. Mtanzania wa kijijini asiyesoma mitandao ya kijamii ana haki kujua jinsi tunavyosemwa vibaya na wazungu. Mtanzania ana haki ya kujua anavyotuhumiwa na anavyotetewa. TBC - get this broadcasted to the nation!!!
Mapovu ya jumuiya ya ulaya na marekan kubwa hasa ni baada ya kuskia baadhi ya viongoz tanzania kukemea ama kupinga ushoga hayo mengine ya ukeukwaj wa kidemokrasia yalikuepo mda mrefu kwetu tumesha yazoea hatujaskia hata sku moja jumuia ya ulaya na marekan kuzungumzia sasa kabla ya tbc kusema chochote ninyi wana jf mnasema nn ushoga uwepo na uheshimiwe tanzania?
 
Nawaza hivyo tu

Maana Bunge ni wawakilishi wa wananchi

Maslahi ya nchi yawekwe mbele...na wajadili vipengele vyote

Au Halmashauri kuu ya Ccm ikae na kuamua
 
BUNGE LA UMOJA WA ULAYA (EU) LATOA MAAZIMIO 15 KWA TANZANIA
AL-NOFLI 15/12/2018 0

Roeland van de Geer

George Njogopa – Mwananchi
Jumamosi, Disemba 15, 2018

Bunge la Umoja wa Ulaya (EU) limepitisha azimio lenye vipengele 15 vinavyohusu Tanzania kwa kugusia masuala ya utawala wa sheria, haki za binadamu na kamatakamata ya viongozi wa wapinzani.

Lakini, Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Dk Augustine Mahiga amesema anasubiri maelekezo kutoka kwa Rais kuzungumzia suala hilo.

Azimio hilo namba 2018/2969 ni mwendelezo wa hoja zilizowahi kuibuliwa na jumuiya hiyo ya kimataifa kuhusu Tanzania.

Hoja hizo zinahusu mambo kama haki za binadamu, masuala ya afya, elimu, haki za kupata habari, kuzuiwa kwa matangazo ya moja kwa moja ya Bunge, mikutano ya kisiasa, sheria kandamizi na matamko.

Aidha, Waziri Mahiga jana alinukuliwa akisema kuwa hawezi kutolea majibu yoyote azimio hilo.

“Siwezi kuzungumzia lolote kuhusu hili. Bado nasubiri maelekezo kutoka kwa Rais. Eh nasubiri maelekezo ya Rais,” alisema kwa kifupi.

Bunge hilo la EU lilipitisha azimio hilo lililoandikwa Desemba 12, baada ya majadiliano yaliyofanyika mjini Brussels, Ubelgiji ikiwa ni mara ya kwanza kwa chombo cha kimataifa kutoa azimio dhidi ya Tanzania.

Huku likiwa limenukuu vifungu kadhaa vya kimataifa na kugusia uhusiano wake na Tanzania, azimio hilo ambalo limesambazwa sehemu mbalimbali linataka Tanzania irekebishe baadhi ya sheria.

Bunge hilo limebainisha matukio kama kupigwa marufuku mikutano ya kisiasa, kuandamwa kwa waandishi wa habari na watetezi wa haki za binadamu, kufungia vyombo vya habari, kuzuia Bunge Live kuwa ni kati ya mambo yanayokwenda kinyume na misingi ya haki za binadamu.

Azimio hilo limehoji kampeni iliyotangazwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ya kuwasaka watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja. Azimio limetaka serikali imzuie Makonda, kuendelea na kampeni hiyo.

Hata hivyo, hivi karibuni serikali ilishabainisha kuwa kampeni hiyo haikuwa na ridhaa yake na alichokuwa akikifanya Makonda ni maoni yake binafsi.

Bunge hilo limetoa wito likitaka kuachiliwa kwa wafungwa wote wa kisiasa, kufanyiwa marekebisho kwa baadhi ya sheria.

Sheria hizo, inayohusu makosa ya mtandao, sheria ya vyombo vya habari, sheria ya Elektroni na Mawasiliano ya Posta (Epoca) na kuachiwa uwanja wa watetezi wa haki za binadamu kufanya shughuli zao.

Pia, limetaka tume huru itakayochunguza matukio yenye utata kama kutekwa na kukamatwa kwa waandishi wa habari na matukio ya watu kutoweka katika mazingira ya kutatanisha.

“Tungependa kuona wale watakaobaini kuwa nyuma ya matukio hayo, hatua za kisheria zinachukuliwa dhidi yao,” linasema azimio hilo.

Hii ni mara ya pili kwa EU kuelezea jinsi isivyoridhishwa na mwenendo wa Tanzania baada ya awali kumuita mwakilishi wake Brussels kwa ajili ya majadiliano.

Akizungumza baada ya kuombwa kutoa maoni yake kuhusu sakata hilo, Profesa Kitojo Wetengere wa Chuo cha Diplomasia (CFR) alisema Serikali isipuuzie azimio hilo.

“Kuna umuhimu wa kukaa meza moja ya majadiliano na EU ili serikali iwaelimishe kwa nini inafanya inachokifanya sasa,” alisema Wetengere.

Wakati huo huo VOA News Swahili, Imeandika:

Maseneta wa Marekani wamemuandikia barua Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo, Mike Pompeo wakieleza wasiwasi wao juu kushuka kwa kuheshimiwa kwa haki za binadamu na demokrasia nchini Tanzania.

Maseneta hao wamesema: “Tangu mwaka 2015 nchi hiyo inaongozwa kwa sera zinazotengeneza mazingira ya uvunjifu wa amani, vitisho na ubaguzi.

Haki za binadamu

Wamedai katika barua iliyotumwa Desemba 12, serikali inaminya haki za binadamu na demokrasia. Wameongeza kuwa tangu mwaka 2016 nchi hiyo haina Balozi rasmi nchini Tanzania hivyo ni lazima Balozi ateuliwe.

Maseneta wanataka ubalozi wao uanze kufanya juhudi za kuhakikisha kunakuwa na uchaguzi huru na wa haki mwaka 2020.

Pia wameitaka Marekani ihakikishe hakuna fedha zinazotolewa na taasisi yoyote ya kimataifa kufadhili sera zinazoonekana kuwa kinyume na haki za binadamu.

“Tunakuandikia tukiwa na wasiwasi mkubwa juu ya kuminywa kwa uhuru wa kisiasa Tanzania, na tunahimiza uongozi wa Marekani kuongeza mawasiliano kuonyesha ongezeko la mmomonyoko wa haki za raia na uhuru wa kidemokrasia katika nchi hiyo.”

Uongozi wa Magufuli

Tangu uongozi wa Rais John Magufuli uchukue madaraka mwaka 2015, umekuwa ukiendeshwa na sera za kutumia mabavu, vitendo vya uvunjifu wa amani, vitisho dhidi ya jumuiya za kiraia, vyombo vya habari na vyama vya upinzani.

Barua hiyo imeandika pia, wasichana wanalazimishwa kupimwa mimba; wale walio wajawazito wanafukuzwa na kuzuiwa kumaliza masomo yao.

Imeeleza kuwa Rais Magufuli amezuia ufadhili wa Marekani wa programu ya HIV/AIDS iliyokuwa inawafikia na kutoa huduma ya afya kwa mashoga, idadi muhimu ya watu wanaolengwa na jitihada za kupambana na HIV/AIDS.

Vyombo vya habari

Barua hiyo inaeleza kuwa magazeti yamekuwa yakidhibitiwa kwa kutozwa faini au kufungiwa kwa kuripoti habari ambazo zinaonekana kuikosoa serikali.

Sheria ambazo zinaminya uhuru wa vyombo vya habari na kuzuia maudhui kwenye mitandao ya jamii zimepitishwa kuwa sheria. Yote hayo ni wakati wa utawala wa Magufuli.

Viongozi wa upinzani

Viongozi wa upinzani bungeni wamepigwa risasi baada ya kumkosoa Rais, wamekamatwa na kubughudhiwa na polisi, na wengine wameshtakiwa kwa makosa ya uchochezi.

Barua hiyo inaelelza hatua za wadau katika jumuiya ya kidiplomasia walizochukuwa kukabiliana na kutetereka kwa demokrasia na kuzuka kwa vitendo vya ubaguzi.

Umoja wa Ulaya

Tayari Umoja wa Ulaya umemwita Balozi wake kutoka Tanzania baada ya kile kilichoitwa ni ‘kulazimishwa kuondoka’ kutoka Tanzania, na msaada wake wa kifedha na sera zake kwa Tanzania zinajadiliwa.

Serikali ya Denmark

Mfadhili mwengine muhimu, Denmark, amesema itazuia msaada wa kifedha wenye thamani dola za Marekani milioni 10, ikieleza wasiwasi wake juu ya uvunjifu wa haki za binadamu na “kauli za sheria kali na vitisho zisizo kubalika dhidi ya wapenzi wa jinsia moja” zilizotolewa na maofisa wa serikali.

Benki ya Dunia

Benki ya Dunia ilikuwa tayari imezuia ujumbe wake kwenda Tanzania, na kusema itaruhusu ujumbe huo kuzuru nchi hiyo iwapo tu serikali itawahakikisia kuwa itajizuia na kuwabughudhi na kuwabagua watu kutokana na mwenendo wa jinsia zao.

Benki hiyo imetishia kufuta mpango wa mkopo wa dola za kimarekani milioni 300 ziilizotengwa kwa ajili ya Tanzania baada ya nchi hiyo kurejea tena msisitizo wa sera yake ya kuwapiga marufuku wasichana wenye mimba kurudi shuleni.

Na serikali kuacha mpango wake wa kufanya ni kosa la jinai “kuhoji takwimu rasmi” za serikali hadharani.

Lakini akizungumza katika uzinduzi wa maktaba ya kisasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Jumanne, Novemba 27 Magufuli awaambie viongozi wa upinzani watulie “la sivyo wataishia gerezani”.

Rais Magufuli alipeleka ujumbe mpya kwa viongozi wa vyama vya upinzani wa Tanzania akiwaonya kuwa iwapo ‘hawataheshimu sheria’ wataishia magerezani.

Rais huyo alimpa ujumbe huo Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa ambaye sasa ni mjumbe wa kamati kuu ya chama cha upinzani cha Chadema.

Magufuli aliongeza: “Hii ndio Tanzania mpya tunayoitaka…Nimeona hili nilizungumze kwa heshima kubwa, Mzee Lowassa, ili wale unaowaongoza kule, uende ukawashauri…’otherwise’ (la sivyo) wataishia kwenye magereza ili wakajifunze namna ya kuheshimu sheria za Watanzania.”

Tayari viongozi kadhaa wa upinzani Tanzania wakiwemo wa chama cha Chadema ambacho Lowassa ni mjumbe wa kamati kuu wanashtakiwa kwa tuhuma mbalimbali.
 
Anaeamua ya bungeni ndo kaleta haya yote unadhani ataruhusu hayo yajadiliwe?
 
Bunge ndiyo halina nguvu kabisaa afadhali hata ya upinzani waendelee kupiga makelele
 
Mkuu Mjusi Mweupe, hata wakituwekea vikwazo vya kiuchumi, misaada ya kibinaadamu iko pale pale, hivyo support ya TB na ARV itaendelea sambamba na misaada ya USAID itaendelea.
P
Ni mchawi mweupe!!! Hata jiwe akizidisha kiburi?? Kwani jiwe na lenyewe hadi lilainike sio mchezo!!
 
USIKUBALI KUPOTOSHWA HAYA NDIYO MAAZIMIO YA BUNGE LA ULAYA EU

Waziri wa mabo ya nje asema awezi kuzungumzia azimio hilo anasubiri Raisi atoe tamko

>>>Utawala wa sheria
>>>Haki za binadamu
>>>Kamata kamata ya wapinzani
>>>Elimu
>>>Afya
>>>Haki ya kupata habari
>>>Sheria kandamizi na matamko
>>>Mikutano ya kisiasa kupigwa marufuku
>>>Kuandamwa kwa watetezi wa haki za binadamu
>>>Kufungiwa vyombo vya habari
>>>Kuandama watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja

BUNGE HILO LIMETAKA PIA HAYA YATEKELEZWE

>>>Kuachiliwa wafungwa wote wa kisiasa
>>>Kurekebisha baadhi ya sheria ikiwemo ya makosa ya mtandao , sheria ya vyombo vya habari
>>>Kuachia uwanja kwa watetezi wa haki za binadamu kufanya shughuli zake

LIMETAKA PIA HAYA YAWEPO

>>>Tume huru ya kuchunguza kutekwa na kuakamatwa kwa waandishi wa habari na watu kupotea katika mazingira ya kutatanisha
>>>Hatua za kisheria kuchukuliwa kwa wale wataobainika kuvunja haki za binadamu
Historia huwa haipotei na kamwe haidanganyi. Wananchi wa Libya waliambiwa na Mabeberu kwamba Ghadafi ni tatizo na iwapo akiondoka madarakani wananchi wa Libya wataishi maisha mazuri sana. Hebu tujiulize: Wamarekani waliongoza mapambano ya kumuua na kumuondo madarakani Rais Muamar Ghadafi, JE, Libya wana maisha gani mazuri leo hii zaidi ya mateso makali?

Walibya waliahidiwa kwamba Ghadafi akiondoka madarakani nchi ya Libya itakuwa na Demokrasia safi na ya kweli. Hebu tujiulize: Iko wapi hiyo Demokrasia nchini Libya baada ya Mabeberu kumuua Ghadafi? Hakuna Demokrasia zaidi ya mateso nchini Libya na maisha magumu.

Tusisahau yanayowakuta Iraki na Siria kwa Bashar Asad ambapo mabeberu wanataka kupandikiza vibaraka wao ili wachote rasilimali ya mafuta kwa manufaa yao. Kote huko ni mateso makali. Walimuua Rais Saddam Hussein na kuwahakikishia wana dunia hii kwamba Iraki itakuwa na Demokrasia na maisha mazuri. Tujiulize yako wapi maisha mazuri Iraki zaidi ya machafuko yasiyoisha tangu Mwaka 2003 hadi leo hii?

Watanzania tunapaswa kutumia yanayowapata Walibya na wairaki kujifunza kwamba kamwe Mabeberu wa Ulaya na kwingineko duniani hawawezi kusimama na serikali yetu pale wanapoona tunajenga uchumi wetu ili tujitegemee. Lazima tufahamu kwamba watatuchonganisha na kupandikiza vibaraka wao nchini wakiwemo waafrika wenzetu ambao leo hii tunawaona wakidiriki kupigia upatu Mashinikizo yao ya kijinga yakiwemo ushoga, Mara wanatetea demokrasia yetu nk.

Wameshindwa kuisadia Libya na Iraki kama walivyoahidi na kuaminisha ulimwengu kwamba kuna matatizo makubwa ya kidemokrasia katika nchi hizo nk, hakuna amani huko zaidi wamesababisha machafuko makubwa katika nchi hizo; watawezaje kutusaidia sisi watanzania tena Taifa letu ambalo tuko salama sana, hatuna matatizo kama wanavyoeleza mabeberu na vibaraka wao?

Mabeberu hao wasiofaa hata kidogo wamekaa kimya kuhusu yanayoendelea nchini Ufaransa kana kwamba hawaoni kitu. Watu wanaandamana mwezi mzima kumshinikiza Rais Emmanuel Macron aondoke madarakani lakini tujiulize ni lini Mabeberu wa EU na vibaraka wao walitoa tamko lolote kumshinikiza beberu mwenzao aondoke madarakani? Watanzania sharti kustukia maigizo ya mabeberu na uonevu dhidi ya mataifa ya kiafrika.

Kudhibiti Makinikia na biashara harama za kutupora madini yetu haijawapendeza wazungu hata kidogo na kwa hiyo basi wameamua kupambana na sisi kwa namna mbalimbali ikibidi hata watufarakanishe ili nchi yetu ipoteze mwelekeo na isitawalike. Mabeberu wanatueleza wanapigania demokrasia ndani ya nchi yetu wakati wanajua fika walitoa ahadi ya aina hiyo kwa Libya na kwingineko duniani lakini hadi leo hii Libya hakuna demokrasia wala amani bali machafuko.

Walibya wanajuka kukubali kuhadaiwa na mabeberu, wanamkumbuka ghadafi na kujuta sana kuuawa kwa Rais Muamar Ghadafi. Wanakumbuka fadhila za Ghadafi aliyekuwa akiwapatia malipo ya chakula kila mwezi wananchi masikini, leo hakuna malipo hayo. Wanamkumbuka ghadafi aliyekuwa akiwalipia mahali za kuoa walibya masikini lakini leo hakuna fadhila hizo. Wanamkumbuka ghadafi aliyeapa kupambana na ubeberu ili usiitawale afrika. Ghadafi alijipambanua kama kiongozi asiyetaka kuona Afrika inaonewa na kushikizwa kufanya mambo ya kijinga kwa maslahi ya mabeberu.

Watanzania tupeuke mtego uliowamaliza walibya ili tusije kujuta kama walibya leo hii. Hawa vibaraka na vijakazi wa mabeberu wanaopiga kelele kwamba Tanzania tunaenda vibaya hawana mana kabisa bali wanatumikia mabeberu wanaotaka kututawala ili wapole rasilimali zetu. Hawa vibaraka na mabeberu wao tuwaogope kama Ukoma.

Pinga UBEBERU NA VIBARAKA wao wote kwa maslahi ya Taifa hili.
 
Ni vizuri kujenga mashikamano na china kwani wanaheshimu haki za nchi nyingine kujiamlia mambo yao, kuliko hao wanafiki wanaokupa misaada kwa masharti ya kukubali kuwa shoga
China hata Jiwe atwange risasi Wapinzani wote na familia zao, Wao wataendelea kutoa mikopo tu mradi gesi ya Mtwara wamepewa.
 
Nyie wazungu mnawafurahia bila kufahamau. Mnawachekelea bila kufikiria na mnawashangilia bila kufahamu mchezo wauchezao. Kwa kifupi ni hivii, wazungu hawapendi tupige hatua hata kama ni sentimita moja. Kununua ndege kwa cash kwao ni matusi. Kujenga reli ya SGR kwao ni kero. Kujenga lile bwawa la Stiglas kwao ni kasheshe kubwa sana. Mchanga wao mpaka sasa tunao na tumesiliba mianya yao ya kupata vitu na mali zetu chelelee hawatatupenda wala kukubali. Kwa anaedhani wazungu wanatupenda saaana na wanatuomnea tutoke siku moja anajidanganya sana na sana. Waliweza kumgombanisha Mzee Muamal Gadafi na watu wake ambao waliishi bure wakipewa kila kitu na selikari na sasa wanajuta kupita kiasi na naona hatujajifunza tuu. Jifunzeni kwa Sadam, Gadafi na hata Mubarak na muangalie kama kuna kitu cha maana wamepata baada ya waliouita msaada wa wazungu ili kupata demokrasia. Hawa wanataka dhahabu, almasi, na vito vingine bila kizuizi na wala sio demokrasia. Waogopeni kama ukoma na kama mnaweza unganeni muwe kitu kimoja hawatatuweza. Someni hata histiria kidogo mtawaelewa. Hakuna mzungu anapenda mswahili but wanataka mali zetu tuu na hakuna jipya.
Huo mchanga bado unao??? Acha masihala kama vitu hujui bora ukae kimya tu!!! Hata leo nenda bandarini pale kama utaukuta!! Yaani mtu atese, wanaokuwa na mawazo tofauti na yake, kila kitu ni yeye, unaona sawa? Bora mkoloni mweupe kuliko hawa weusi!! Ni hatari sana,
 
Back
Top Bottom