Eunice Chiume, kwanini unapotosha wanachama wa NSSF?

Eunice Chiume, kwanini unapotosha wanachama wa NSSF?

Huyu Chiume nae ni jipu tu,sii Mmalawi huyu mama?
Mikoa yote ya Tanzania iliyoko mipakani ina maingiliano na nchi jirani zinazopakana nazo,maana yake ni kwamba hata lugha,utamaduni na mila za baadhi ya makabila zinafanana kwa kuwa mipaka iliwekwa na wakoloni kwa maslahi yao na siyo yetu.Watanzania tuna tabia mbaya ya kubagua watu watokao mikoa ya pembezoni hasa kwa kuhusisha majina,muonekano na lafudhi ya watu wa mipakani na watu wa nchi jirani, hii ni ubaguzi wa hali ya juu ambao haupaswi kufumbiwa macho.Mtanzania ni mtu yeyote aliyezaliwa Tanzania wakati wazazi wake wote au mmoja wao akiwa raia wa Tanzaia au raia yeyote wa kigeni ambaye anapewa uraia wa Tanzania kwa kuandikishwa na idara ya uhamiaji. Hii tabia ya huyu yule siyo mtanzania ni ya kijima zaidi na haina tofauti na xenophobia tuliyoiona RSA miaka mitatu iliyopita. Tubadilike.
 
Hiki kipele very soon kitatumbuliwa
Wizara, taasisi za usalama wa nchini zichukulie suala hili serious. Hii nchini si ya wageni ni ya Watanzania. Maslahi mapana na usalama wa nchini lazima yazingatiwe.

Wana-jf asante kwa kuwataja wahamiaji haramu, maelfu ya vijana hawana kazi kwa sababu ya watu hawa.
 
Wizara, taasisi za usalama wa nchini zichukulie suala hili serious. Hii nchini si ya wageni ni ya Watanzania. Maslahi mapana na usalama wa nchini lazima yazingatiwe.

Wana-jf asante kwa kuwataja wahamiaji haramu, maelfu ya vijana hawana kazi kwa sababu ya watu hawa.


Hilo taifa halikuwa na uongozi lilikuwa lina watawala na tena watawala mbumbumbu maana walikuwa wanawaibia mizoga

To be honest kuna siku nilikuwa nimtie mtu kisu baada ya kuniuliza unanijua Mimi ni nani??

Nchi ilikuwa ya mazombi

Sasa ndo kuna viongozi na si watawala
 
Unakomalia mambo ya kijinga wewe huna hizo taarifa akizitoa huyo ndo utaamini?
Hahahaaa huyu jamaa anweza kuwa Dr Dau. Tatizo lake halieleweki ni nini! Analalamikia Uraia wa Dr Carina hapo hapo anamshambulia Chiume. Hardly tatizo lake ni position ya uDG wa NSSF.
 
Naona kina Mufti Team Dr Dau wanashambulia sana mitandaoni kila wanayeona anaweza kuwa mbaya wao ktk kipindi hiki ambacho jamaa amepewa ubalozi wa nchi isiyojulikana.Watu waliifanya NSSF na mashiriki mengine ya umma kama mali yao binafsi...Wakasahau cheo ni dhamana....Kanyama Chiume,mkwe wa Eunice alikuwa raia wa Nyasalanda(Malawi),akawa waziri wa mambo ya Nje wa Malawi ktk serikali ya Kamzu Banda,wakazinguana na Kamzu Kanyama akaja bongo kwa Nyerere na baadae kukimbilia uhamishoni Uingereza,alifariki na kurudishwa nyumbani kuzikwa
Alhaji anaweza kupangiwa kuwa Balozi wa Segerea. Vijana wake wana msiba mkubwa sana.
 
Maelezo kuhusu uraia wa Dr Carina yaliyotelewa na SSRA ambaye ndiye mwajiri wake hadi anateuliwa kukaimu nafasi ya U-DG NSSF. Na imefanunuliwa vizuri kabisa kuwa Dr Carina ni mtanzania.

Kwa upande mwingine hizi kelele za uraia wa Dr Carina zinaonesha dalili ya tatizo tulilonalo Watanzania lakini tunajidai hatuna. Watanzania si wamoja kama tunavyojidai na mbaya zaidi ni kushamiri kwa xenophobia.
Ukweli ni kwamba tatizo la xenophobia ni la kundi dogo tu la wafuasi wa Dau, na ninajua tatizo ni ile nafasi ya uDG. Wanadhani kwa kupiga majungu Dau atarudishwa. Ni uhakika hata akipendekezwa simbachawene wa dodoma bado watasema sio mtanzania. Kumbuka Dr Carina amehudumu katika mashirika ya umma kama PPF tena kwa nafasi ya ukurugenzi ila kelele za kuwa ni mganda hazikuwepo, why today NSSF? Mbona hawakuwahi kulalamika kuwa wanakuwa regulated na mganda wakati akiwa SSRA.
 
Wafuasi wa Dr Dau mnahangaika sana na nafasi ya NSSF, ukweli ni kwamba hii ni nafasi ya umma mtake msitake atapewa mtu mwingine na hizi figisu mnazopiga mitandaoni zitafanya waziri aje na mtu wa uhakika ambaye ataibua ufisadi wote wa Dr Dau na uwekezaji uliokuwa umewekwa CHA JUU kingi na kufanya NSSF kuwa kwenye hali mbaya financially
 
View attachment 328015
@Elungata,Kanyama Chiume ni mmalawi,lkn akiwa mtoto mdogo Mama yake alifariki,Mjomba wake aliyekuwa anaishi Morogoro akamchukua toka Malawi na kuishi nae Moro...Kanyama alisoma Shule ya Msingi Uhuru Dsm,huyu ni mwanadarasa wa mmoja wa kina Sykes,lkn pia amesoma na Kawawa hapahapa Tanganyika,Amesoma Tabora School na Dodoma Alliance(Mazengo)
Baadae akaja kuwa mwandishi wa gazeti la Daily News,Uhuru na Mzalendo akiwa na Mkapa..baada ya Uhuru Kamzu Banda alimuita na kumpa Wizara ya Mashauriano ya Kigeni,alikuja kupingana na Kamzu kuhusu msimamo wa Kamzu kuwa na ushirikiano na Makaburu na Wareno wa Msumbiji,akawa Exiled na kuja kuishi Tz...baadae akaenda US kuishi na familia,alifariki mwaka 2007 na kurudishwa kwao Malawi...Kanyama Chiume ni mwanamajumui wa Africa(Pan Africanist),mtoto wa Afrika,aliyekuwa "Mtanzania" wa kuishi na kusoma,na watoto wake wote aliwazalia Tanzania...Eunice ni mtoto wa Upanga,ameolewa na mtoto wa Kanyama Chiume na hivyo kuwa Mrs Chiume.
Mmewe William chiume
 
Sasa kwa nini hufuatilii ofisi na hao wasaidizi unamuandama mtu ?

Na zaidi, Eunice si mtu anayeteua, ni mtangazaji tu. Kwa nini unamshikia bango mtangazaji wakati mteuzi humsemi?

Kama Eunice hasemi chochote kwa sababu hajapewa cha kusema, hajapewa uteuzi mpya wala maelezo, utamuandama kwa lipi?

Unataka atunge habari ambayo haipo?

Kwani mwanzo aliwezaje kutoa taarifa na sasa ashindwe?
 
hivi kumbe kuna wakirsto pale NSSF? mimi nilifikiri ni waislam tu maana Dr. Dau aliajiri waislam peke yao? au huyo kaajiriwa hivi karibuni baada ya Dr. Dau kuondolewa pale NSSF?

Si hivyo tuu, kanisa la TB Joshua lipo pale mkuu
 
Japo simfagilii, lakini nadhani baada ya kutenguliwa, hakuwa na uhusiano na NSSF tena. Ndio maana SSRA ndio walimtetea.

Ili kuondoa huu utata kwa nini Uhamiaji wasije front na wakaweka wazi mafaili ya huyu mama?
 
Jinsi wanavyomshikia bango huyo Eunice Chiume badala ya kufuatilia uteuzi serikalini huko, ukifikiri kwamba wana chuki binafsi na huyo Eunice Chiume siwezi kukushangaa.

Kiranga kwa michango yako humu ndani nashangaa na wewe umeingia kwenye mitego ya kulalamika kuwa kuna chuki binafsi

sisi wanachama tunataka tuambiwe kuhusu hili shirika ambalo halina mkurugeni, halina kaimu mkurugenzi, na huyo tuliyeletewa ni Raia wa Uganda, na huyo anayetaka hiyo nafasi naye hafai kuwa mkurugenzi. Hivi ingekuwa private corporation unadhani shareholders wangekaa kimya?

Najua una vested interests na huyu Eunice lakini hebu simamia haki. SSRA wametoa Tamko, Wizara imetoa Tamko, kwa nini NSSF wamegoma kutoa tamko?
 
Jamaa wananichosha kabisa. Hoja ya uraia pacha ilipopamba moto watu walidai ukichukua uraia wa nchi nyingine basi papo hapo na uzalendo kwa nchi yako ya asili ukwisha na unakuwa loyal kwa "nchi" yako mpya. Sasa huyu mama kachukuwa uraia wa Tanzania wanauita Utanzania wake wa Plastic! Kwa nini wasimpime kwa kipimo kile kile wanachowapima Watanzania wenzao kwamba wanakuwa loya kwa "nchi" yao mpya? Huyu mama "nchi" yake mpya ni Tanzania hivyo kwa mantiki za hoja zilizokuwa zikipinga uraia pacha huyu mama ni loyal kwa Tanzania kuliko nchi yake ya asili. Kweli kuishi kwingi ni kuona mengi.

Xenophobia imewafanya hata waanze kumpachika mtu Umalawi. Sasa kama Eunice ni Mmalawi kwa kuolewa na "Mmalawi" kwa nini wanasita kusema Dr. Wangwe ni Mtanzania kwa vile kaolewa na Mtanzania (achilia mbali Utanzania wake aliochukua kwa kufuata taratibu za kisheria)? Kha!

Narudia. Dr Caro wangwe ni raia wa UGANDA.

Hata kama kaolewa na Mtanzania loyalty yake itabaki kuwa Uganda

Kwa maneno mengine, Nguruwe kuzaliwa kwenye zizi la ngombe hakumfanyi kuwa Ngome. Atabaki nguruwe tuuu

Kwa nini asifanye kazi ubalozi wa Uganda? Kwa nini apewe NSSF? au kama anataka sana kazi si akalime tuu kwani lazima apewe kazi nyeti kama hiyo NSSF?
 
Issue hapa sio uraia wa EUNICE CHIUME issue hapa ni yeye kama mkurugenzi wa mawasiliano kukaa kimya na kutowajuza wanachama kinachoendelea kwenye hilo shirika.
Hivi vitimbakwiri vya Ramadhani Dau mnaweweseka sana, umeambiwa mtu ana msiba mzito kwenye familia, je wewe ukifiwa huwa unaendelea na kazi? chuki za kipuuzi zisiondoe hata ubinadamu mdogo mlionao.
 
Ukweli ni kwamba tatizo la xenophobia ni la kundi dogo tu la wafuasi wa Dau, na ninajua tatizo ni ile nafasi ya uDG. Wanadhani kwa kupiga majungu Dau atarudishwa. Ni uhakika hata akipendekezwa simbachawene wa dodoma bado watasema sio mtanzania. Kumbuka Dr Carina amehudumu katika mashirika ya umma kama PPF tena kwa nafasi ya ukurugenzi ila kelele za kuwa ni mganda hazikuwepo, why today NSSF? Mbona hawakuwahi kulalamika kuwa wanakuwa regulated na mganda wakati akiwa SSRA.

Dr Carina Wangwe kama anataka sana kazi serikalini arudi kwa Kaguta atapewa hizo kazi

Ikishindikana afungue kampuni yake Binafsi lakini sio kumpa nafasi nyeti serikalini kama hiyo.
 
Hivi vitimbakwiri vya Ramadhani Dau mnaweweseka sana, umeambiwa mtu ana msiba mzito kwenye familia, je wewe ukifiwa huwa unaendelea na kazi? chuki za kipuuzi zisiondoe hata ubinadamu mdogo mlionao.

Ushaambiwa kuwa huyo Eunice ana wasaidizi 5 hao nao hawawezi kutoa press release?

Kwa hiyo akiumwa idara yake itakuwa haiwezi kufanya kazi?
 
Kiranga kwa michango yako humu ndani nashangaa na wewe umeingia kwenye mitego ya kulalamika kuwa kuna chuki binafsi

sisi wanachama tunataka tuambiwe kuhusu hili shirika ambalo halina mkurugeni, halina kaimu mkurugenzi, na huyo tuliyeletewa ni Raia wa Uganda, na huyo anayetaka hiyo nafasi naye hafai kuwa mkurugenzi. Hivi ingekuwa private corporation unadhani shareholders wangekaa kimya?

Najua una vested interests na huyu Eunice lakini hebu simamia haki. SSRA wametoa Tamko, Wizara imetoa Tamko, kwa nini NSSF wamegoma kutoa tamko?
Mimi ni mwanachama wa NSSF pia, nadhani shida yetu kubwa ilikuwa Ramadhani Dau atueleze pesa zetu kwa miaka yote aliyowekeza kwenye miradi sisi wanachama tunaochanga pesa zetu tumewekewa faida ya asilimia ngapi kwa kila mwanachama? na siyo kutuletea hoja za kitoto kama hizi. na ni kwa nini wanachama tutibiwa kwenye hospitali moja tu? je hiyo ni bima ya afya au upuuzi mtupu?
 
Hizi habari za Utanzania zitatumaliza.

Huyo Dr. Carina ni Mtanzania. Lakini kashikiwa bango kwamba Mganda.

Huyo Eunice ni Mtanzania, tunamjua kasoma Muhimbili, dada yake Steven, walikuwa wanakaa Maweni St. Upanga, kaolewa na one of the late Kanyama Chiume's sons.

By te way, Eunice ana msiba mkubwa wa wifi yake aliyefariki Mount Vernon, NY, wamezika jana nafikiri Kinondoni.

Hivyo siwezi kushangaa kama hayupo kazini na ndiyo maana hajatia tamko lolote
Well Said Eunice ni Mtanzania halisi hana umalawi wowote! Na origin yake ni Kilimanjaro Chagga by trible ameolewa na chiue
 
Huo ubini wa Chiume una harafu ya unyasa. Just joking!

Huyu mumewe nadhani anafanyakazi kampuni ya Mafuta kama sikosei. Kama ni ndugu yake na Nathan (jamaa namkubali sana) lakini huyu binti wala sio kabisaa. Sasa nilikuwa najiuliza iweje Nathan awe na akili vile halafu huyu awe hana confidence?

Kumbe ni mtu na shemejiye

Nimeandika e-mail kwenda NSSF kuuliza kulikoni wakinijibu nitawafahamisha
 
Mmalawi ni nani na Mtanzania ni nani?

Mimi nikichukua uraia wa Marekani leo na kuukana uraia wa Tanzania na kurudisha mpaka hati ya kusafiri ya Tanzania, nitakuwa Mmarekani au Mtanzania?
Utakuwa Plastic American
Na kuna kazi huwezi kupewa kwenye serikali ya Marekani
 
Back
Top Bottom