GRAND MUFTI
Senior Member
- Jun 3, 2015
- 136
- 104
Huyu mama ndio mkurugenzi wa Mawasiliano wa shirika la NSSF. Huyu miaka yote amekuwa mwoga wa kujitokeza kujibu hoja mbali mbali zinzohusu shirika hili kwa waandishi wa habari na umma kwa ujumla.
Lakini wiki iliyopita kwa spidi ya ajabu kabisa, kwa kushirikiana na waziri wa Kazi na Ajira, Jenista Mhagama alijotokeza kutangazia dunia kupitia mitandao kama vile Whatsapp, facebook, twitter, instagram, viber,google+, na vizingnezo uteuzi tata wa raia wa Uganda (DR CARINA) kuwa kaimu mkurugenzi mkuu wa shirika la hifadhi la NSSF.
Cha ajabu ni kuwa masaa 4 baada ya Jamiiforums kujulisha dunia kuwa huyu aliyepewa hiyo nafasi si mTanzania na ku challenge Waziri Mhagama na watu wake waonyeshe ushaidi kuwa ni mTanzania ilibidi wizara itoe Tamko la kuondoa uteuzi wake
Na ajabu zaidi ni kuwa huyu huyu Mama (Eunice Chiume), amekuwa kimya kwani:
Hajatoa taarifa yoyote ile kwa wanachama, umma na dunia kwa ujumla juu ya kutenguliwa kwa uteuzi wa Dr (MGANDA) Carina.
Sasa inamaana huyu Eunice Chiume anafanya kusudi au hataki kuujulisha umma na wanachama wa NSSF kinachoendelea kwenye hilo shirika au kuna siri gani ambayo hataki tujue au naye anasubiri maelekezo toka kwa Magori?