EU yaivimbia Marekani huku ikiilinda Irani kibiashara

Mkuu Malcom Lumumba,

Ahsante kwa kunikaribisha kwenye huu uzi mujarabu!

Awali ya yote, I doubt ikiwa kweli EU wataendelea kukaza kutokana na sababu mbalimbali!

Mosi, EU as a community, wanaofanya biashara sio wao as a community bali kampuni mbalimbali za kibiashara ambazo ni natives to EU. Hizi ni multinational companies doing billion of dollars businesses across the global. What makes North Korea possibly great is because of their presumably military power but what makes EU great ni hizi multinational companies!

The bold sentence inamaanisha, ni hizi multinational companies ndizo zitakazoamua a fate of US Sanctions to Iran. Hizi multinational companies zikiona ni too risk kuikazia US, I doubt ikiwa EU as a community wanaweza kukaziana na hizi multinational companies ambazo:

1. Zinategemea sana US banking systems! Hizi kampuni zina billion of dollars kwenye US banks duniani ambazo, US wakipiga mkwara wa ku-freeze assets zao kwenye US banks, lazima watasanda tu!

2. US is a big market almost kwa kila bidhaa... from household to corporate level! That having said, I doubt ikiwa EU & UK multinational companies watakuwa tayari kupoteza soko kubwa kama la US!

Kwa haraka haraka (mada nimeivamia nikiwa napita njia), huo ni upande wa kibiashara chini ya EU companies ambazo,nina kila sababu ya kuamini inaweza kuwa kikwazo kwa EU as a community kupingana na Trump!

Kama kweli EU & UK wapo serious, basi waanze na state owned companies! TOTAL kwa mfano, mwezi May walitangaza wazi wangejiondoa Iran kukwepa vikwazo vya Trump! Labda nimepitwa hivyo unaweza kunikumbusha! Kama kweli EU wapo serious, basi nilitarajia kuisikia serikali ya Ufaransa wakiiambia TOTAL wasijiondoe Iran!

Kinyume na hayo, I believe hizi private companies lazima zitakiuka tu wito wa EU na kuitikia ule wa US for the sake of their business! Mtoto akinyea kiganja huwezi kumkata mkono! Wakati AirBus kwa mfano wanaweza kuhofia kuzuiwa kuuza ndege zake US ikiwa wataendelea kufanya biashara na Iran (kukiuka US sanctions), hawaoni uwezekano wa kuzuiwa kuuza ndege zake elsewhere in the world (including EU Market) kwa wao kuwakiuka EU!!!

And in fact, wakati US wanakuwa wametoa ORDER ya kutofanya biashara na kampuni yoyote itakayofanya biashara na Iran, kauli ya EU sio ORDER ya kutofanya biashara na kampuni yoyote itakayoitikia US sanctions to Iran!

Kama ndivyo, ni kwanini basi kampuni ihatarishe kufanya biashara na US (read: US trade network) kwa kukikuka vikwazo vya US wakati kuendelea kufanya biashara na US hakuhatarishi biashara zao na masoko mengine duniani (including EU) except Iran?!

Hapo juu ni upande wa makampuni lakini tukija upande wa EU as a community, hawa nawaona bado ni watumwa tu kwa US pamoja na uchumi wao mkubwa, and possible military power wakiamua kuwa independent! Unless wanakuwa na NATO yao wenyewe yenye lengo la kuilinda Europe bila kuitegemea NATO ya US vinginevyo wataendelea kuwa vijibwa tu vya US!!

With a US "led" NATO, US will always be an inevitable EU ally!

Kwa maoni yangu, uvimbaji huu wa EU kwa US (kwa Trump?) ni too theoretical and less practical! Kwenye viunga vya United Nations HQ, EU wataendelea kutambua Iran Nuclear Deal inayopigwa teke hivi sasa na Trump lakini na yenyewe watakuwa wanaitambua just theoretically!

Watakuwa wanaitambua theoretically kwa sababu, the deal will mean nothing, at least to Iran, endapo hapatakuwa na practical trade between EU and Iran! Ingawaje EU wanaweza wasirudishe vikwazo kwa Iran but still it'll be meaningless ikiwa hapatakuwa na biashara kati yao... endapo hapatakuwa na biashara kati yao kutokana na sababu nilizotaja hapo juu: Will EU & UK multinatuional companies risk their businesses by violating US Sanctions?!

BACK TO IRAN....

Binafsi sioni jipya kutokana na vikwazo hivi vya Trump dhidi ya Iran! Tangu nianze kufuatilia siasa za kimataifa, nimeishuhudia Iran ikiwa ndani ya vikwazo! Iran ime-survive figisufigisu za US for almost 40 years now... kwahiyo, hakuna jipya!!! Ime-survive figisu figisu za kijeshi na za kiuchumi kwa muda wote huo!!

Katika muda huo Iran imekumbana pia na marais vichaa sawa na Trump... mfano mzuri ukiwa Ronald Reagan hususani wakati wa muhula wake wa pili. Reagan aliendesha figisu figisu za kijeshi na kiuchumi dhidi ya Iran only his administration to end with Iran–Contra affair scandal!

If Donald Trump is smart enough, I believe hili pia aanayafahamu yote haya na kwamba, hakuna jipya kwenye vikwazo vyake! Sana sana ninachokiona kwa Trump ni kujaribu kuchochea chuki za wananchi wa Iran dhidi ya serikali yao! Wakiwa smart, wanaweza kufanikiwa kupandikiza hizi fitina lakini haiwezi kuwa kazi ndogo!

What about vikwazo vya mafuta ambavyo ndiyo bakora kali zaidi dhidi ya Iran?

Iran wameshavimba kwamba wataendelea kusafirisha!!!

Russia na China wameshasema wataendelea kununua mafuta ya Iran!!! Russia na China sio EU... wakisema watanunua, watanunua kweli! Kwanza hata pale TOTAL walipotangaza kujiondoa Iran, China National Petroleum Company wakasema wazi watabeba shares za TOTAL ikwa watashindwa kuvumilia sindano za Trump!

Kwa tangazo lile la CNPC, China wanaonesha wazi wataendelea kufanya biashara na Iran! Isitoshe, hawa CNPC wame-invest pesa nyingi sana kwenye Iran's oil & gas industry!

Na kwamba China ndie largest consumer wa Iran's crude oil, hilo ni pigo kubwa sana kwa US!!
 
Mkuu ahsante kwa hoja yako nzuri kabisa,
Lakini nadhani tusiliangalie hili swala katika upande moja peke yake, kwasababu zifuatazo:

Mosi, kufikia Green Economy inawezeka kabisa lakini siyo jambo la leo wala kesho. Mambo haya ya Nishati na mazingira yameanza kuzungumzwa tangia miaka ya 1960's mpaka leo lakini bado dunia inatumia makaa ya mawe, nyuklia, gesi na mafuta.

Pili, swala la Green Economy inabidi uliangalie katika jicho la Uchumi. Ulaya kama anatumia magari ya umeme na vyanzo vingine vya nishati, usisahau kwamba makampuni yake kama TOTAL, BRITISH PETROLEUM na THE ROYAL DUTCH SHELL ndiyo yanatawala soko la dunia la mafuta. Hivyo mbali na kupeleka mafuta Ulaya, hayo makampuni ndiyo yanauza mafuta Africa, America na Asia na wakiwa na masoko makubwa sana. Hivyo hata kama Sekta ya mafuta ya dunia itapewa ushindani mkali na Electrical Vehicles bado Ulaya atahitaji sana kuuza mafuta nje ya mipaka yake.

Mbali na hapo mafuta ni biashara nzuri sana kwa mataifa mengi sidhani kama Ulaya wanaweza wakaharibu hiyo biashara ya nchi kama Urusi, Saudi, Iran, Qatar and Yemen na wakaishiwa kuchekewa tu. Ndiyo maana ukiangalia sababu kubwa za Donald Trump na Vladmir Putin kupinga ishu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa (GLOBAL WARMING) ni kulinda hatma ya masoko yao ya mafuta na gesi.

Pia upande mwingine mbali na makampuni ya mafuta, vipi kuhusu hatma ya makampuni ya magari na ndege kama BENZ, LAND ROVER, MAYBACH, ROLLS ROYCE, VOLKS WAGEN na AIRBUS, BOMBARDIER etc Unadhani wanaweza wakabadilika tu ndani ya usiku moja na kuanza kutumia umeme ??? (Gharama itakuwa kubwa kiasi gani hadi kufanya hivyo)

Tatu, gharama za vyanzo vipya vya nishati katika utabiri ni kubwa sana sanaa. Inasemekana magari yatakayotumia vifaa vya umeme na mafuta (Hybrid Cars) yatuzwa kuanzia Euro 6000 hadi 16000, hizi ni hela nyingi kweli. Euro 6000 ni sawa na pesa za Kitanzania Milioni 15888000. Unahisi wangapi hata huko Ulaya wanaweza wakanunua haya magari kwa ghafla tu ??? Africa na Asia ambako masikini ni wengi sana huwezi kunishawishi niache kununua IST ya mtumba kwa milioni 7 zangu halafu niende nikanunue magari ya TESLA kwa milini 15. Ulaya yatakuwepo sana lakini kwetu Afrika sidhani kama GREEN ECONOMY inaweza ikaathiri sana sekta ya mafuta kwa miaka kama 30 ijayo.

Nne, British Petroleum (BP) wametoa matokeo ya utafiti wao ambao unasema kufika mwaka 2030 mafuta yatahitajika sana kwa wingi hapa duniani. Mbali na hapo kutokana na dunia kugundua vyanzo vingi vya mafuta kuanzia kule Marekani,Bahari ya Uchina ambako inasemekana kuna mapipa kama Bilioni 30 ambayo hayajachimbwa na kwingineko bei ya mafuta itapungua kutoka hapa ilipo na kuwezesha watu wengi kuweza kumiliki magari na kuendesha mitambo mbalimbali kwa ajili ya uchumi. Hivyo hii ni sababu tosha sana kwa Sekta ya mafuta kuwa na nguvu kubwa bado hapa duniani.

NB: Ulaya mbali na kutaka kujenga Green Economy, anamiaka siyo chini ya 30 kuweza kuleta jehuri kwa mataifa kama Marekani, Urusi na Saudi Arabia linapokuja suala zima la nishati (Safari ni ndefu mno)
Malcolm Lumumba nimekukubali boss takwimu Sahihi na uchambuzi Sahihi .Hiyo ndio sifa za watoa mada tunazotaka .a real great thinker . Hongera, usichoke kutoa ELIMU ambayo imekuwa bidhaa adimu.
 
Mkuu Malcom Lumumba,
BACK TO IRAN....
Binafsi sioni jipya kutokana na vikwazo hivi vya Trump dhidi ya Iran! Tangu nianze kufuatilia siasa za kimataifa, nimeishuhudia Iran ikiwa ndani ya vikwazo! Iran ime-survive figisufigisu za US for almost 40 years now... kwahiyo, hakuna jipya!!! Ime-survive figisu figisu za kijeshi na za kiuchumi kwa muda wote huo!!

Russia na China wameshasema wataendelea kununua mafuta ya Iran!!! Russia na China sio EU... wakisema watanunua, watanunua kweli! Kwanza hata pale TOTAL walipotangaza kujiondoa Iran, China National Petroleum Company wakasema wazi watabeba shares za TOTAL ikwa watashindwa kuvumilia sindano za Trump!

Kwa tangazo lile la CNPC, China wanaonesha wazi wataendelea kufanya biashara na Iran! Isitoshe, hawa CNPC wame-invest pesa nyingi sana kwenye Iran's oil & gas industry!

Na kwamba China ndie largest consumer wa Iran's crude oil, hilo ni pigo kubwa sana kwa US!!

Mkuu Chige sikutaka kulijibu hili bandiko kabla ya kulisoma vizuri.
Uzoefu umeonesha kwamba Iran ana msuli mkubwa sana kuliko CUBA, IRAQ, SYRIA na LIBYA.
Hivyo kumvamia kijeshi kichwa kichwa italeta taswira mbaya na madhara makubwa sana duniani.

Mosi,
Ukisoma vizuri historia utajua mtego wa Raisi Donald Trump na CIA umelalia kwenye hii kitu inayoitwa (The Brzezinsk Doctrine) - Mchokonoe Iran ili apate sababu ya kujitoa kwenye Mkataba wa Nyuklia na mataifa ya Ulaya (Joint Comprehensive Plan of Action a.k.a The JCPOA) ili Wamarekani wapate sababu ya kumtenga kibishara na washirika wake kama Urusi, Uturuki na Uchina. Ikumbukwe Uturuki na Uchina ni wanunuzi wa mafuta kutoka Iran, huku Urusi akisema ana mpango wa kuuza ndege zake Iran kama Aibus wataondoka.

Pili,
Iran akiona kuwa makampuni ya Ulaya yametoa makampuni yake basi ataghafirika na kuamua kujitoa kwenye ule mkataba wa Nyuklia. Iran aliingia kwenye ule mkataba kwa mara ya kwanza kwasababu alitaka nchi yake iondolewa vikwazo kutoka kwenye Jumuiya ya Kimataifa. Ikumbukwe hivi vikwazo vya Marekani haviko kisheria (Unilateral Sanctions) hivyo havizuii kabisa nchi nyingine kubwa kama Urusi na Uchina kuendelea kufanya biashara nchini Iran. Hivyo itahitaji vikwazo ambavyo vipo kwenye mipaka ya Sheria za Kimataifa (Internatinal Law) ili kuzuia nchi kama Uchina, Uturuki na Urusi kufanya biashara nchini Iran. Ukifanikiwa kuwafanya Uchina na Urusi wakubaliane na vikwazo dhidi ya Iran basi Iran hatakuwa na ujanja mkubwa zaidi ya kukubali kukaa mezani, Serikali ya Ayatollah kupinduliwa au uvamizi wa kijeshi kama hayo yatashindikana.

Hivyo Akijitoa kwenye ule Mkataba Marekani atapata sababu za uongo za kusema kwamba Iran amerudi kwenye kuzalisha nyuklia kwa ajili ya kutengeneza silaha. Marekani atapata sababu ya kwenda Baraza la Ulinzi la Umoja wa Mataifa na kuweka vikwazo vya kisheria kabisa kwasababu Iran hatakuwa na sababu ya kusema kwanini ametoka kwenye ule Mkataba. (Kutoka kwenye Mkataba kutatafsiriwa na dunia kama nia ya Iran kuendeleza mpango wake wa nyuklia kama ilivyokuwepo awali)...Asijiroge kutoka kwenye ule Mkataba itakula kwake.

Mfano halisi wa hii hoja yangu:
Iran alikubali kukaa mezani na Marekani baada ya vikwazo vilivyopitishwa Kisheria na Baraza la Ulinzi na Usalama wa Umoja wa Mataifa (UNSC) kuanzia mwaka 2008 kupitia Azimio namba 1803 na mwaka 2010 kupitia Azimio namba 1929. Haya maazimio yalipitishwa na mataifa yote kwenye makubwa kwenye lile baraza la umoja wa mataifa yakiwemo Urusi na Uchina. Haya maazimio yalilenga sana mabenki ya Iran, viongozi wa Iran, Meli za Iran, Mali za jeshi la Iran, Kuzuia manunuzi ya silaha na vitu vinginevyo. Hadi Tanzania tulipigwa mkwara zilivyokutwa meli za Iran kule visiwani Zanzibar zikipeperusha bendera za Tanzania.

Iran aliumia sana na mwishowe akakubali kukaa kwenye meza ya mazungumzo na ndiyo wakatengeneza The Joint Comprehensive Plan of Action.Ambapo Iran aliambiwa akubali kusitisha mpango wake wa silaha za kinyuklia ili vikwazo viondolewe. Iran alikubali kusitisha mpango wake wa kinyuklia ili vikwazo vitolewe. Mwaka 2015 Baraza la Umoja wa Matiafa likapitisha Azimio namba 2231 ambalo lilitambua ule mkataba wa Nyuklia wa Iran na kusema hivi "Vikwazo vyote dhidi ya Iran viondolewa kwasababu Iran amekubali kusaini Mkataba wa nyuklia na vitarudi endapo Iran ataamua kujitoa kwenye ule Mkataba nyuklia al maarufu kama The JCPOA"

Tatu,
Marekani amejitoa kwa maksudi kabisa akidai kwamba ule mkataba hauna usawa kwasababu haujazungumzia Iran kusitisha teknolojia yake ya makombora. Hiki ni kitu Marekani anakizungumza kwa maksudi kwasababu anajua Iran hawezi kukubali kabisa. Hivyo amejitoa kwenye ule mkataba na kuanza kuwalazimisha mataifa makubwa ya Ulaya nayo yajitoea ili mwishoni Iran aone kwamba Ulaya hawatimizi matakwa ya Mkataba na aghafirike ili apate sababu ya kujitoa kitu ambacho kitakuwa kinyume na Azimio namba 223 la Baraza la Ulinzi la Umoja wa Mataifa. Nini kitatokea hapa kama Iran atajitoa ???

Vikwazo vinarudi moja kwa moja (Automatically)kwasababu Iran atakuwa amevunja matakwa ya Azimio la Umoja wa mataifa ambalo ndili lilisema vikwazo vitoke kama Iran endapo tu Iran atabaki kwenye mkatabwa wa nyuklia. Pia kwa upande wa pili itatafsiriwa kwamba Iran anataka kujitoa ili arudie mpango wake wa nyuklia. Hapa Marekani na Israel watapata sababu kubwa sana ya kufanya propaganda dhidi ya Iran, huku jumuiya ya kimataifa ikiuliza kwanini Iran ajitoe kwenye mkataba kama ana nia njema ya nishati salama ya nyuklia ???

Nne,
The Brzezinski Doctrine
ilitumika dhidi ya Urusi ya Kisovieti mwaka 1979. Marekani alifanya Mkataba na Urusi ya Kisovieti kwamba waiache Afghanistani huru (Neutral) na dunia nzima ikafurahi kuona vile. Lakini huku chini Marekani akawa anafanya vitendo vya kukera ambavyo vilionesha kwamba Raisi wa Afghanistani analalia upande wa Marekani na hivyo itamgharimu Urusi. Viongozi wa Urusi bila ya kufikiria wakajua kweli Afghanistani anakuwa upande wa Marekani na hivyo wakavamua nchi mwaka 1979 kinyume kabisa na makubaliano. Nini kilitokea baada ya ule uvamizi ???

Urusi alilaaniwa na Jumuiya ya Kimataifa na kujikuta kwenye ile vita yuko peke yake. Hadi UCHINA mkomunisti mwenzake iliwaunga mkono The Mujahedeen kwasababu Marekani aliiaminish dunia kwamba Urusi akifanikiwa nchini Afghanistani, nini kitamzuia asiende Pakistan au Uchina ??? Lakini kumbe ule uvamizi ulikuwa ni mtego tu wa kumtenga Urusi na washirika wake........(The Soviets took the bait na ikala kwao)

Marekani atamfanyia Iran vikwazo na vimbwanga vya kila aina, ili tu ajitoe kwenye ule Mkataba. Iran akijiroga kutoka atakuwa amekwisha maana Marekani, Uingereza na Israel watatumia mwamvuli wa sheria kuendesha operesheni za waziwazi kabisa dhidi ya Iran.

Tano,
Iran akicheza karata zake vizuri na kutojitoa kwenye JCPOA atakuwa salama sana tu na atapata huruma ya jumuiya ya kimataifa dhidi ya Marekani na Israel. Juzi Uchina amasema kwamba hatambui vikwazo vya Marekani (Unilateral Sanctions) dhidi ya Iran kwasababu haviko kisheria. Hivyo ataendelea kufanya biashara ya mafuta na Iran tena kwa kiasi kikubwa zaidi.

Hivyo watafanya kama ule mkataba wa Uchina na Urusi (GAZPROM PIPELINE DEAL) wa mwaka 2014. Wachina watanunua sehemu kubwa ya mafuta kutoka Iran kwa bei ndogo kama ambavyo walivyonunua gesi ya Urusi chini ya bei ya kawaida (Below the Market Price). Hivyo Iran ataendelea kuwa na soko la uhakika nchini Uchina.

Japo sasa ataumia kwa namna moja au nyingine kwasababu atakumbwa na matatizo kama: Kukosa teknolojia ya kisasa kutoka nchi za Magharibi (Lack of progressive technological transfer) na Uhaba wa bidhaa na huduma za muhimu kwa matumizi ya raia (Shortage of Goods and Services for civilian consumption). Hivyo atakuwa anategemea kuuza mafuta peke yake na Silaha kama chanzo kikuu cha mapato (Source of hard currency) haya lazima yatapunguza kasi ya kukua kwa uchumi wako.

MTAZAMO WANGU BINFSI NDIYO HUO:
IRAN akijiroga kujitoa kwenye dili hili akidhani anawakomoa Ulaya itakuwa imekula kwake........
 
Mkuu Chige sikutaka kulijibu hili bandiko kabla ya kulisoma vizuri.
Uzoefu umeonesha kwamba Iran ana msuli mkubwa sana kuliko CUBA, IRAQ, SYRIA na LIBYA.
Hivyo kumvamia kijeshi kichwa kichwa italeta taswira mbaya na madhara makubwa sana duniani.

Mosi,
Ukisoma vizuri historia utajua mtego wa Raisi Donald Trump na CIA umelalia kwenye hii kitu inayoitwa (The Brzezinsk Doctrine) - Mchokonoe Iran ili apate sababu ya kujitoa kwenye Mkataba wa Nyuklia na mataifa ya Ulaya (Joint Comprehensive Plan of Action a.k.a The JCPOA) ili Wamarekani wapate sababu ya kumtenga kibishara na washirika wake kama Urusi, Uturuki na Uchina. Ikumbukwe Uturuki na Uchina ni wanunuzi wa mafuta kutoka Iran, huku Urusi akisema ana mpango wa kuuza ndege zake Iran kama Aibus wataondoka.

Pili,
Iran akiona kuwa makampuni ya Ulaya yametoa makampuni yake basi ataghafirika na kuamua kujitoa kwenye ule mkataba wa Nyuklia. Iran aliingia kwenye ule mkataba kwa mara ya kwanza kwasababu alitaka nchi yake iondolewa vikwazo kutoka kwenye Jumuiya ya Kimataifa. Ikumbukwe hivi vikwazo vya Marekani haviko kisheria (Unilateral Sanctions) hivyo havizuii kabisa nchi nyingine kubwa kama Urusi na Uchina kuendelea kufanya biashara nchini Iran. Hivyo itahitaji vikwazo ambavyo vipo kwenye mipaka ya Sheria za Kimataifa (Internatinal Law) ili kuzuia nchi kama Uchina, Uturuki na Urusi kufanya biashara nchini Iran. Ukifanikiwa kuwafanya Uchina na Urusi wakubaliane na vikwazo dhidi ya Iran basi Iran hatakuwa na ujanja mkubwa zaidi ya kukubali kukaa mezani, Serikali ya Ayatollah kupinduliwa au uvamizi wa kijeshi kama hayo yatashindikana.

Hivyo Akijitoa kwenye ule Mkataba Marekani atapata sababu za uongo za kusema kwamba Iran amerudi kwenye kuzalisha nyuklia kwa ajili ya kutengeneza silaha. Marekani atapata sababu ya kwenda Baraza la Ulinzi la Umoja wa Mataifa na kuweka vikwazo vya kisheria kabisa kwasababu Iran hatakuwa na sababu ya kusema kwanini ametoka kwenye ule Mkataba. (Kutoka kwenye Mkataba kutatafsiriwa na dunia kama nia ya Iran kuendeleza mpango wake wa nyuklia kama ilivyokuwepo awali)...Asijiroge kutoka kwenye ule Mkataba itakula kwake.

Mfano halisi wa hii hoja yangu:
Iran alikubali kukaa mezani na Marekani baada ya vikwazo vilivyopitishwa Kisheria na Baraza la Ulinzi na Usalama wa Umoja wa Mataifa (UNSC) kuanzia mwaka 2008 kupitia Azimio namba 1803 na mwaka 2010 kupitia Azimio namba 1929. Haya maazimio yalipitishwa na mataifa yote kwenye makubwa kwenye lile baraza la umoja wa mataifa yakiwemo Urusi na Uchina. Haya maazimio yalilenga sana mabenki ya Iran, viongozi wa Iran, Meli za Iran, Mali za jeshi la Iran, Kuzuia manunuzi ya silaha na vitu vinginevyo. Hadi Tanzania tulipigwa mkwara zilivyokutwa meli za Iran kule visiwani Zanzibar zikipeperusha bendera za Tanzania.

Iran aliumia sana na mwishowe akakubali kukaa kwenye meza ya mazungumzo na ndiyo wakatengeneza The Joint Comprehensive Plan of Action.Ambapo Iran aliambiwa akubali kusitisha mpango wake wa silaha za kinyuklia ili vikwazo viondolewe. Iran alikubali kusitisha mpango wake wa kinyuklia ili vikwazo vitolewe. Mwaka 2015 Baraza la Umoja wa Matiafa likapitisha Azimio namba 2231 ambalo lilitambua ule mkataba wa Nyuklia wa Iran na kusema hivi "Vikwazo vyote dhidi ya Iran viondolewa kwasababu Iran amekubali kusaini Mkataba wa nyuklia na vitarudi endapo Iran ataamua kujitoa kwenye ule Mkataba nyuklia al maarufu kama The JCPOA"

Tatu,
Marekani amejitoa kwa maksudi kabisa akidai kwamba ule mkataba hauna usawa kwasababu haujazungumzia Iran kusitisha teknolojia yake ya makombora. Hiki ni kitu Marekani anakizungumza kwa maksudi kwasababu anajua Iran hawezi kukubali kabisa. Hivyo amejitoa kwenye ule mkataba na kuanza kuwalazimisha mataifa makubwa ya Ulaya nayo yajitoea ili mwishoni Iran aone kwamba Ulaya hawatimizi matakwa ya Mkataba na aghafirike ili apate sababu ya kujitoa kitu ambacho kitakuwa kinyume na Azimio namba 223 la Baraza la Ulinzi la Umoja wa Mataifa. Nini kitatokea hapa kama Iran atajitoa ???

Vikwazo vinarudi moja kwa moja (Automatically)kwasababu Iran atakuwa amevunja matakwa ya Azimio la Umoja wa mataifa ambalo ndili lilisema vikwazo vitoke kama Iran endapo tu Iran atabaki kwenye mkatabwa wa nyuklia. Pia kwa upande wa pili itatafsiriwa kwamba Iran anataka kujitoa ili arudie mpango wake wa nyuklia. Hapa Marekani na Israel watapata sababu kubwa sana ya kufanya propaganda dhidi ya Iran, huku jumuiya ya kimataifa ikiuliza kwanini Iran ajitoe kwenye mkataba kama ana nia njema ya nishati salama ya nyuklia ???

Nne,
The Brzezinski Doctrine ilitumika dhidi ya Urusi ya Kisovieti mwaka 1979. Marekani alifanya Mkataba na Urusi ya Kisovieti kwamba waiache Afghanistani huru (Neutral) na dunia nzima ikafurahi kuona vile. Lakini huku chini Marekani akawa anafanya vitendo vya kukera ambavyo vilionesha kwamba Raisi wa Afghanistani analalia upande wa Marekani na hivyo itamgharimu Urusi. Viongozi wa Urusi bila ya kufikiria wakajua kweli Afghanistani anakuwa upande wa Marekani na hivyo wakavamua nchi mwaka 1979 kinyume kabisa na makubaliano. Nini kilitokea baada ya ule uvamizi ???

Urusi alilaaniwa na Jumuiya ya Kimataifa na kujikuta kwenye ile vita yuko peke yake. Hadi UCHINA mkomunisti mwenzake iliwaunga mkono The Mujahedeen kwasababu Marekani aliiaminish dunia kwamba Urusi akifanikiwa nchini Afghanistani, nini kitamzuia asiende Pakistan au Uchina ??? Lakini kumbe ule uvamizi ulikuwa ni mtego tu wa kumtenga Urusi na washirika wake........(The Soviets took the bait na ikala kwao)

Marekani atamfanyia Iran vikwazo na vimbwanga vya kila aina, ili tu ajitoe kwenye ule Mkataba. Iran akijiroga kutoka atakuwa amekwisha maana Marekani, Uingereza na Israel watatumia mwamvuli wa sheria kuendesha operesheni za waziwazi kabisa dhidi ya Iran.

Tano,
Iran akicheza karata zake vizuri na kutojitoa kwenye JCPOA atakuwa salama sana tu na atapata huruma ya jumuiya ya kimataifa dhidi ya Marekani na Israel. Juzi Uchina amasema kwamba hatambui vikwazo vya Marekani (Unilateral Sanctions) dhidi ya Iran kwasababu haviko kisheria. Hivyo ataendelea kufanya biashara ya mafuta na Iran tena kwa kiasi kikubwa zaidi.

Hivyo watafanya kama ule mkataba wa Uchina na Urusi (GAZPROM PIPELINE DEAL) wa mwaka 2014. Wachina watanunua sehemu kubwa ya mafuta kutoka Iran kwa bei ndogo kama ambavyo walivyonunua gesi ya Urusi chini ya bei ya kawaida (Below the Market Price). Hivyo Iran ataendelea kuwa na soko la uhakika nchini Uchina.

Japo sasa ataumia kwa namna moja au nyingine kwasababu atakumbwa na matatizo kama: Kukosa teknolojia ya kisasa kutoka nchi za Magharibi (Lack of progressive technological transfer) na Uhaba wa bidhaa na huduma za muhimu kwa matumizi ya raia (Shortage of Goods and Services for civilian consumption). Hivyo atakuwa anategemea kuuza mafuta peke yake na Silaha kama chanzo kikuu cha mapato (Source of hard currency) haya lazima yatapunguza kasi ya kukua kwa uchumi wako.

MTAZAMO WANGU BINFSI NDIYO HUO:
iRAN akijiroga kujitoa kwenye dili hili akidhani anawakomoa Ulaya itakuwa imekula kwake........

CC: TUJITEGEMEE , Wick ,FisadiKuu , Nalendwa , hearly , muyovozi , Red Giant, Consigliere
Usiwe unaacha kunitag kwenye nondo kama hizi..
 
Wabongo ni wazuri sana sana kuijadili America, Ulaya, na Asia, wapo makini, wanajua kila kitu, utasikia "Marekani kasema", " Iran wapo vile", Urusi anatekeleza". Lakini nchi yao inayoitwa Tanzania, toka inaitwa Tanganyika, ipo hoi taabani, duni kabisa kiakiri mpaka maisha. Wema uanzia nyumbani(tumesahau).
 
Tuanze na wewe,
Umeifanyia nini Tanzania ???
 
Nina wasiwasi kama Moro One unaelewa analysis ya Lumumba ,ufarijikekuwa hauko peke yako. Sasa anzisha mada makini kuhusu Tanzania uone kuwa great thinkers hawatoi nondo kama hizo za international affairs. Sema hata ukitoa nondo humu zitadakwa na dwarf minds na kuzitafsiri kwa imani binafsi za uchama, udini. sex, na mambo kama hayo. Usiingilie jambo usolielewa maana halitakuvutia na hutapata cha kuchangia. Tukubaliane tu kuwa JF ni kwa wote bila kujali ELIMU. ya MTU, vinginevyo kuna michango humu ingefutwa kwa ukakasi na kuwa hamna cha kujifunza kwa mchango husika
 
Kuna nchi tajiri sana lakini itaanguka na baada yake kuanzisha vita vya 3 duniani na apo ndio vita haitanyamaza
 
hakuna kitu kama icho,Hakuna kampuni itakayotaka kufilisiwa na USA ili ifanye biashara na Iran.Nenda na dola Moja huko Iran uone kama ujarudi na Rambo LA manoti ya pesa zao.Vikwazo vya kawaida vinaanza mwezi huu,na ikifika November hawataruhusiwa kuuza mafuta nje ya Iran.Wanachofanya EU in kujikosha wasionekane wamewasaliti Iran kutokana na mkataba walioingia nao before Trump.
Acha upumbavu yaani US amkataze Iran kuuza mafuta? u should not be serious
 
Wadau mi maoni yangu nadhani MAREKANI ameona ni vyema kuikataa EU.Kumbuka kila mwaka kiasi kikubwa sana cha fedha alikitenga kuipa EU.Trump kuna watu wapo nyuma yake ambao bila kujali vyama wameamua kudinda EU.kama Uchumi wa jimbo moja la CARIFONIA kwa mwaka ni sawa na uchumi wa FRANCE yote.majimbo mengine kama matatu ni uchumi wa BRITAIN bado mtu hajiongezi tu?Kiufupi US chini Ya TRUMP inajaribu kuweka system mpya ya kisera kiuchumi,kijamii,na kisiasa huku ikiwa AMERICAN FIRST. Anachofanya wanasain makubaliano wao wanadeal n mtu mojamoja.Walianza na MACRON,akaja MAY,PUTIN,North na South Korea.Japan.na nchi zinginezo.Kiufupi ni kwamba mipango itapangwa ila Marekani anacontrol NATO.akiamrisha Ivamie SRYIA hakuna EU atakae nyanyua mdomo.Wakati wa Spain Vs Catalonia EU ilikaa kimya.Kimsingi ni toothlessdog.ILA MUDA NDIO MWAMUZI BORA ZAIDI.unafiki haupo afrika tu .Upo dunia yote japo huku ndo umeota mizizi nankustawi.
 
Hili nimeliona tangu Trump alipoingia madarakani,ni kwamba wanataka kuweka mfumo mpya wa siasa za Dunia.
 
Back
Top Bottom