EU yaivimbia Marekani huku ikiilinda Irani kibiashara

EU yaivimbia Marekani huku ikiilinda Irani kibiashara

Mambo yameiva, EU imesema itaziadhibu kampuni za Ulaya zitakazotii masharti ya US.
=====
European companies doing business with Iran could soon find themselves between a rock and a hard place. Should they comply with US sanctions and abandon Tehran, they may in turn face sanctions in their home EU.
https://www.rt.com/news/435352-eu-sanctions-companies-iran/
 
Anachofanya EU ni kujaribu kuitia moyo Iran ila kiukweli hamna kikubwa watakachofanya kuizuia Marekani kuibinya Iran ukizingatia kwa Sasa chumi za EU haziko vizuri ukilinganisha na Marekani ambayo pia inajitegemea kwa nishati hivyo haitaathirika kwa kiasi kikubwa.
Pitia post ya kwanza ya uzi huu yenye update ya leo juu ya sakata hili, pia pitia na kipande hiki cha habari hapa chini
====
Iran is a major crude supplier to China. US sanctions on Iran pushed China's yuan-denominated oil futures contract nearly five percent higher, the biggest daily move since the petro-yuan's inception in March. The main contract SC1809 closed at 537.2 yuan per barrel, rising by 25.5 yuan or 4.98 percent, according to Shanghai International Energy Exchange.
 
Mambo yameiva, EU imesema itaziadhibu kampuni za Ulaya zitakazotii masharti ya US.
=====
European companies doing business with Iran could soon find themselves between a rock and a hard place. Should they comply with US sanctions and abandon Tehran, they may in turn face sanctions in their home EU.
https://www.rt.com/news/435352-eu-sanctions-companies-iran/
Hapa EU anaanza kutepeta,na sidhani kama ataweza kuziadhibu hizo Companies. Kikubwa hapa Iran anachezewa chekundu cheusi.
 
Uchumi ni namba , na namba hazidanganyi. Wakiona kupoteza biashara na Marekani INA hasara zaidi zaidi kuliko kuliko kufanya biashara na Iran basi ujue Iran wataachwa . ila wakitumia kigezo kuwa, je kutonunua mafuta ya Iran kukiongeza bei ya soko la mafuta mardufu na EU akapoteza pesa nyingi za kununua mafuta , wakati huo Marekani yeye sasa hivi anajitosheleza mafuta na gas kwa teknolojia ya cracking na shale gas basi EU atakuwa upande Wa Iran. Na lengo LA Marekani no kuona bei ya mafuta inapanda ili Trump alipe fad hila za matajiri Wa biashara waliomuweka madarakani wanafaidi urais wake akiwemo mrusi. Hiyo ndiyo hoja itakayoamua Mchina na EU wanagemea upande UPI? Mengine yote tutasikia porojo tupu, haipendwi nchi Bali mchango kwenye maslahi mapana hasa uchumi wake. Huo ndio ukweli Wa mchina kumbinya Kim Wa Korea akubali ya mbabe Marekani ili mchina asikose export ya $ 600 bln za kuuza Marekani wakati Marekani ananunua $ 130 bln toka uchina kwa mwaka . Turufu ya Iran ni bei ya mafuta kupanda ndio itwaokoa. Lakini Marekani akimshawishi Saudi Arabia aongeze uzalishaji na bei isipande believe me Iran atapiga magoti kwa Eagle(Evil) empire.
Nondo zimeshiba!!! Duuh kwa wanaopenda ku"take" sides ni vigumu kuelewa ujumbe huu. Dah yakini wewe ni mchumi by professional.
 
Bank yoyote ya dunia hii inapotaka kusafirisha pesa nje ya mipaka lazima kwanza ipewe CODE kutoka SWIFT ndiyo wakamilishe muhamala. Sasa Iran alitolewa nje ya huu mfumo na ikawa haiwezekani nchi kununua mafuta kutoka Iran kwa pesa za kawaida na hivyo wateja wakapata shida na mabenki ya Iran yakaumizwa. Anayetoa hizo code ni World bank/IMF au ni nani mkuu?
 
UPDATE
07/08/2018
Mambo yameiva, EU imesema itaziadhibu kampuni za Ulaya zitakazotii masharti ya US.
=====

https://www.rt.com/news/435214-bologna-airport-explosion-videos/
Wanavimba huku Makampuni karibu yote yashasitisha huduma hata ile kampuni ya Ndege ya Ufaransa umedelivery ndege zake chache ilizomaliza kutengeneza faster ili kuwahi vikwazo na for sure balance ya ndege zilizobakia ni majaariwa am sure watawarejeshea tu fedha zao wafungie maandazi...
nitakuletea list ya makampuni yaliyosepa nikipata muda
 
Bank yoyote ya dunia hii inapotaka kusafirisha pesa nje ya mipaka lazima kwanza ipewe CODE kutoka SWIFT ndiyo wakamilishe muhamala. Sasa Iran alitolewa nje ya huu mfumo na ikawa haiwezekani nchi kununua mafuta kutoka Iran kwa pesa za kawaida na hivyo wateja wakapata shida na mabenki ya Iran yakaumizwa. Anayetoa hizo code ni World bank/IMF au ni nani mkuu?

Society for Worldwide Interbank Financial Telecommunication (SWIFT) ni umoja wa mabenki makubwa dunia ambao uko nchini Ubelgiji na wao ndiyo wanatoa hizo CODES ili kuwezesha nchi mabenki ya nchi mbalimbali kufanya mihamala ya kimataifa. Sasa kama hayo mabenki yakiungana kukataa benki za nchi yako isipitishe pesa kwenye mabenki yao imekula kwako.

Hapa IMF na WORLD BANK havihusiki kabisa hapa kwasababu kazi zao ni tofauti. IMF kazi yake ni kusimamia mwenendo wa chumi za dunia na kushauri serikali zifanye nini kukwepa matatizo ya kiuchumi kama yake ya 2008 Marekani wakati World Bank ilianzishwa kwa lengo la kusaidia shughuli mbalimbali za kimaendeleo duniani kupitia mikopo.
 
Nguvu ya Trump inatokana na mabavu yake kweny maendeleo ya teknolojia.
Mfano miezi kadhaa iliyopita aliipigisha magoti ZTE kwa kufanya biashara na Iran.
Bidhaa za Ulaya mfano ndege za ATR alizonunua Iran hivi karibun ni 20% US products.

Hapo silaha ya Trump ni kupiga marufuku makampuni yake kuwauzia vifaa kadhaa Ulaya (kama alivyomfanyia ZTE ya China) na Ulaya hawatafurukuta.
 
Society for Worldwide Interbank Financial Telecommunication (SWIFT) ni umoja wa mabenki makubwa dunia ambao uko nchini Ubelgiji na wao ndiyo wanatoa hizo CODES ili kuwezesha nchi mabenki ya nchi mbalimbali kufanya mihamala ya kimataifa. Sasa kama hayo mabenki yakiungana kukataa benki za nchi yako isipitishe pesa kwenye mabenki yao imekula kwako.

Hapa IMF na WORLD BANK havihusiki kabisa hapa kwasababu kazi zao ni tofauti. IMF kazi yake ni kusimamia mwenendo wa chumi za dunia na kushauri serikali zifanye nini kukwepa matatizo ya kiuchumi kama yake ya 2008 Marekani wakati World Bank ilianzishwa kwa lengo la kusaidia shughuli mbalimbali za kimaendeleo duniani kupitia mikopo.
Asante kwa maarifa kaka, naam darasa zuri kwa mdogo wako.
 
Kikubwa hapa Iran anachezewa chekundu cheusi.
Na kwa kweli kama anachezewa chekundu cheusi...nadhani ule msemo, wa EU ni mateka wa US utakuwa umekamilika kuthibitishwa. Na kwa mataifa mengine yenye 'akili' inabidi sasa yasiingie mikataba na nchi za EU kwani wao (EU) ni mateka wa US. Hivyo, inatakiwa kuingia mikataba na US moja kwa moja. Kwa ufupi, EU itakuwa imedhalika machoni pa nchi za ulimwengu kuanzia Amerika mpaka Asia na Australia. Na hapa ndipo ninapopasubiri kuona panathibitishwa ama la!!
 
Society for Worldwide Interbank Financial Telecommunication (SWIFT) ni umoja wa mabenki makubwa dunia ambao uko nchini Ubelgiji na wao ndiyo wanatoa hizo CODES ili kuwezesha nchi mabenki ya nchi mbalimbali kufanya mihamala ya kimataifa. Sasa kama hayo mabenki yakiungana kukataa benki za nchi yako isipitishe pesa kwenye mabenki yao imekula kwako.
Asante Mkuu kwa maelezo safi kabisa. Mkuu kwa utaratibu wa Petro-yuan, na vipande vya dhahabu, hauwezi kusaidia Irani kukwepa mkwamo huu wa vikwazo vya US?
------
Iran is a major crude supplier to China. US sanctions on Iran pushed China's yuan-denominated oil futures contract nearly five percent higher, the biggest daily move since the petro-yuan's inception in March. The main contract SC1809 closed at 537.2 yuan per barrel, rising by 25.5 yuan or 4.98 percent, according to Shanghai International Energy Exchange.

China is expected to become a chief beneficiary of the US unilateral sanctions against the world’s biggest energy producers, including Russia, Iran and Venezuela. The petro-yuan would save China the cost of exchanging dollars, the main global currency used in oil trade. It would also increase the use of the Chinese national currency in global financial trade, challenging the greenback.
 
Na kwa kweli kama anachezewa chekundu cheusi...nadhani ule msemo, wa EU ni mateka wa US utakuwa umekamilika kuthibitishwa. Na kwa mataifa mengine yenye 'akili' inabidi sasa yasiingie mikataba na nchi za EU kwani wao (EU) ni mateka wa US. Hivyo, inatakiwa kuingia mikataba na US moja kwa moja. Kwa ufupi, EU itakuwa imedhalika machoni pa nchi za ulimwengu kuanzia Amerika mpaka Asia na Australia. Na hapa ndipo ninapopasubiri kuona panathibitishwa ama la!!
Kama ukifuatilia historia utafahamu kwamba mataifa makubwa ya Ulaya (Washirika wakubwa wa Marekani) wameshawahi kudhalilishwa na Marekani pale walipotaka kuhatarisha maslahi yake. Mwaka 1956 kwenye mgogoro wa mfereji wa Suez (Suez Canal Crisis) Israeli, Uingereza na Ufaransa zilijiamulia kuvamia Misri ili kunyang'anya mfereji na kumpindua Raisi Gamal Abdi Nassser lakini Raisi wa Marekani alitia mkwara na kusema waondoke mara moja nchini Misri.

Wayahudi, Waingereza na Wafaransa walitaka kushupaza shingo lakini waliondoka kwa aibu baada ya kufahamu kwamba Marekani alikuwa hatanii pale ambapo swala la maslahi yake linakuja (Mataifa ya Ulaya hayakuamini kabisa). Hivyo umoja wa Ulaya unadhalilishwa mara nyingi sana lakini hawawezi kufanya kitu dhidi ya Marekani, tena kwa haraka.
 
Asante Mkuu kwa maelezo safi kabisa. Mkuu kwa utaratibu wa Petro-yuan, na vipande vya dhahabu, hauwezi kusaidia Irani kukwepa mkwamo huu wa vikwazo vya US?
------
Inawezekana vizuri tu lakini bahati mbaya ni kwamba mbali na kuuza mafuta kwa Uchina kwa kutumia Chinese Renminbi au Dhahabu Iran hataweza kununua vitu vingine vya muhimu kuendesha uchumi wake kwa kukosa pesa za kigeni. Siyo kila nchi inaweza kuwa na jehuri ya kununua kwa kutumia sarafu yake au dhahabu kama Uchina bila kupigwa kiboko cha nguvu na Marekani.

Halafu lile jibu langu bado hujanipa,
Au bado hujapitia makabrasha yako mzee ???
 
Mkuu Myovozi huwezi kununua dunia nzima lakini unaweza ukawa mbele ya wenzako wote katika ushawishi. Unachohitaji ni kukamata vitu ambavyo dunia nzima inahitaji pamoja na kujenga ushawishi katika maeneo muhimu ya kimkakati. Professor John Mearsheimer anasema hivi, chanzo cha nguvu ya Marekani kimkakati ni sehemu hizi zifuatazo, ambazo ukimpiga lazima atetereke:
1. The Western Hemisphere
2. The Persian Gulf
3. The European Continent
4. The Pacific

The Western Hemisphere ndiyo nyumbani kwa Marekani ambako anaishi. Tangia anapata Uhuru mwaka 1776 aligundua kwamba kama ataweza kuwafanya maadui wake wasifike kwenye huu ukanda basi atakuwa ana nafasi kubwa sana kupigana vita na adui huko mbali na hata kama atapigwa siku zote atakuwa salama nyumbani. Raisi James Monroe alifika hadi kipindi akasema kwamba nchi yoyote itakayopeleka pua kwenye ule ukanda basi Marekani itaitangazia vita. Akenda mbali zaidi akasema kwamba hata serikali za America Kusini zikiwa vibaraka wa mataifa adui atazivamia. Leo Marekani anaionea sana Venezuela kwasababu anajua dhahiri nchi hizo zitakapokuwa na uchumi mkubwa zitamsumbua sana na atakuwa na maadui mlangoni mwake.

Kama unakumbuka jinsi ambavyo alikuwa anapindua serikali za America kusini na kuzifanyia vurugu kuanzia Guatamela mwaka 1957, Cuba mwaka 1961 (Bay of pigs) na Nicaragua miaka ya 1980's kwenye The Contra affair. Hii yote ni sehemu ya Sera ya James Munroe (Munroe Doctrine) kupunguza upinzani nyumbani. Hivyo Uchina kukatazia kununua mafuta Venezuela na mkakati kwasababu mafuta yanalipa sana sanaa na Venezuela ikianza kuuza mafuta itakuwa tajiri ndani ya muda mfupi kweli.

The Persian Gulf (Ghuba ya Uajemi) ndiyo lilikuwa bakuli kubwa la uchumi wa Marekani kipindi chote cha Vita Baridi. Mafuta ya wale waarabu ndiyo yalifanya Marekani kuwa na sauti nzito hapa duniani pamoja na kueneza sera ya dola (The Dollar Diplomacy) ambayo ndiyo pesa inayotumiwa kama nyenzo kuu ya biashara za kimataifa. Mbali na kunufaisha uchumi wake Marekani pia alitumia ukanda huu kuharibu Uchumi wa Urusi ya Kisovieti baada ya Ronald Reagan kuwatia moyo waarabu wazalishe mafuta kwa wingi ili kushusha bei za mafuta katika soko la dunia. Ikumbukwe Urusi ailikuwa inategema asilimia 50% ya pato la nchi kutoka kwenye mafuta (Oil was a source of hard currency). Bei ilivyoshuka Urusi ikala kwake na nchi ikawa juu ya mawe. Upande mwingine Marekani anajua kabisa mataifa makubwa ya Ulaya na Asia (Uchina, Japan, India) yanategemea sana mafuta kutoka kwenye huu ukanda hivyo uwepo wake pale ni rungu tosha la kuweza kuzichezea hizi nchi atakavyo.

The European Continent (Ulaya Magharibi) hawa ndiyo waliokuwa matajiri wakubwa duniani kwa kipindi cha zaidi ya miaka 500. Baada ya vita ya pili ya dunia Marekani alijua kabisa kwamba wapinzani wake wakubwa kiuchumi ni Ulaya kwasababu wana teknolojia na makoloni ambayo ni chanzo cha rasilimali na pia masoko. Akaamua kuwaweka kwenye madeni mazito huku akiwaambia kwamba ili wapate mkopo lazima waacha ukoloni (The Marshal Plan and Open Door Policy). Akaenda mbali zaidi kusema kwamba mikopo yote na biashara ni lazima ziwe katika dola za kimarekani. Uingereza na ujanja wake wote ule amameliza kulipa awamu yake ya mwisho ya madeni ya vita ya pili ya dunia mwaka 2012-2013. Upande mwingine Ulaya anategemea sana Ulinzi wa Marekani kutoka kwa mataifa yenye nguvu kama Urusi. Katika matumizi (Military Expenditure) yeye ndiyo ana takwimu kubwa sana na kajaza kambi za jeshi kuanzia Ujerumani hadi Moldova (Full Spectrum Dominance).

The Pacific (Ukanda wa Pasifiki) kuna wapinzani wake wakubwa sana kibiashara na kiuchumi, isitoshe kuna masoko yake makubwa sana ambayo Uchina anayavizia. Usisahau kwamba huu ukanda ndiyo unaongoza kwa shughuli nyingi za kiuchumi majini hapa duniani ambapo takwimu za Umoja wa Mataifa zinasema zaidi ya Asilimia 50% ya bidhaa za dunia (Merchandise) hupita pale kutokea Ulaya. Meli zanaanzia Ulaya, Bahari ya Mediterania, Mfereji wa Suezi, Bahari ya Hindi, Mfereji wa Malacca, Bahari ya Uchina na kwenda Asia. Mwanajeshi moja wa Marekani alinukuliwa akisema hivi "We are obsessed with the Pacific and if the Chinese try something stupid we will fucking sail in those waters" Akasema kwamba Uchina akiwasumbua ile kambi yao ya Singapore inaweza ikatumika kufanya Blockade kwa bidhaa zinazoenda na kutoka Uchina (Very Dangerous) Kipindi chote cha Raegan Marekani alikuwa na manowari ndogo na kubwa kama 600 kwenye ule ukanda. Siku hizi anazo 300 za kisasa kabisa ambapo nyingine hazitumiki tena.

Hapa hoja ni kwamba Marekani ana msuli mkubwa kwasababu hajaujenga leo wala jana, ulijengeka kwa kipindi cha muda mrefu sana akianza na kutengeneza Uchumi kwanza. Marekani ananufaika na matumizi ya dola ya dunia kwasababu anaweza kuchapisha pesa na kujipa mikopo katika dola za Kimarekani kwa riba ndogo sana. Kama Chinese Renminbi ndiyo itaanza kutumia kama mbadala wa Dola basi nasema GOOD BYE AMERICA. Lakini mpaka Uchina afanikiwe kutupa kabisa dola ni lazima ajenge ushawishi mkubwa sana kisiasa na kiuchumi kitu ambacho bado ana safari ndefu sana kukifanya.

Kwanini inakuwa ngumu kufanya hivyo ???
Gideon Rachman anasema The Institutional Advantage of the Western Societies. Ambapo mbali na biashara kufanywa tu, huwa kunakuwa na taaisi na sheria maalumu za kimataifa ambazo zinalinda biashara hizo. Kuanzia World Trade Organisation (WTO) ambako Uchina na Marekani wote ni wanachama watiifu kabisa. Mbali na hapo kuna taasisi nyingine kubwa kama Bank ya Dunia au World Bank (Ambayo Raisi wake mara nyingi hupendekezwa na Marekani) na International Monetary Fund (Ambayo Raisi wake lazima atokee Ulaya). Sasa hivi vyombo hadi kufika hapo vilipo vilifadhiriwa na kutengenezwa na Marekani kwa makusudi ya kulinda maslahi yake binafsi. Maana hata upigaji wake kura mle ndani unalalamikiwa sana na Uchina na baadhi ya Mataifa.

Uchina ili kufanikisha mpango wake wa kutumia Chinese Renminbi itabidi atengeneze taarisi kubwa ambazo zitakuwa ambazo zitahusisha mataifa makubwa ambayo atayapa mikopo na kufanya uwekezaji kutumia sarafu yake. Amenza vizuri sana na Asia Infrastructure Investment Bank (AIIB) ambapo hadi Uingereza mwaka 2015 alijiunga nayo, kuna The Shanghai Cooperation, halafu kuna BRICS ambayo binafsi naamini inaweza kubadilisha mambo sana kama itahusisha nchi za Kiafrika na zile za Mashariki ya kati. Hivyo huwezi kuanza kutumia sarafu yako bila kuwa na taasisi Imara ambazo zitakuwa zinakushauri na pia zinawapa wadau wako wakubwa sauti ya kusema juu ya sheria na sera ambazo zinasimamia biashara na ugawanywaji wa mikopo ili kujenga Imani.

NB: Kubwa na la mwisho kuhusiana na taasisi za kimataifa, mfano mzuri ni Ufalme wa Uingereza ambapo hata baada ya kuanguka mwaka 1945-1957. Taasisi zake za kimataifa kama The Common Wealth ndizo zilimfanya awe na sauti juu ya makoloni yake na pia kwenye siasa za kimataifa. Ufalme wa Roma ulianguka lakini taasisi zake Imara zilikuwepo kuanzia The Vatican, The Holy See, The Sovereign Order of Malta zipo mpaka leo na ndiyo zimeshikilia nguvu ya Kanisa. Urusi yeye alikuwa anawaza vita tu na kufanya mapinduzi ya Kikomunisti dunia mbali na COMECON na WARSAW PACT hakujenga taasisi Imara za kiuchumi ambazo zingamsaidia kusambaza pesa yake hata baada ya yeye kuanguka kwasababu taasisi hizi zinaendeshwa kwa mikataba na siyo matakwa ya nchi peke yake.

CC: Nalendwa
Mkuu umesomea uchumi nini? Siyo nondo hizi.
 
Na kwa kweli kama anachezewa chekundu cheusi...nadhani ule msemo, wa EU ni mateka wa US utakuwa umekamilika kuthibitishwa. Na kwa mataifa mengine yenye 'akili' inabidi sasa yasiingie mikataba na nchi za EU kwani wao (EU) ni mateka wa US. Hivyo, inatakiwa kuingia mikataba na US moja kwa moja. Kwa ufupi, EU itakuwa imedhalika machoni pa nchi za ulimwengu kuanzia Amerika mpaka Asia na Australia. Na hapa ndipo ninapopasubiri kuona panathibitishwa ama la!!
Hii inaitwa usiongee na mbwa ongea na mwenye mbwa.
 
Back
Top Bottom