EU yaivimbia Marekani huku ikiilinda Irani kibiashara

EU yaivimbia Marekani huku ikiilinda Irani kibiashara

Naionea huruma Venezuela tayari ishakuwa Zimbabwe ya Mugabe.Yaani Mali yako lakini unapangiwa matumizi na mbabe,Hata DRC Mali zao zinawatesa wataendelea kuwa mashamba ya bibi miaka yote
 
Pitia post ya kwanza ya uzi huu yenye update ya leo juu ya sakata hili, pia pitia na kipande hiki cha habari hapa chini
====
Iran is a major crude supplier to China. US sanctions on Iran pushed China's yuan-denominated oil futures contract nearly five percent higher, the biggest daily move since the petro-yuan's inception in March. The main contract SC1809 closed at 537.2 yuan per barrel, rising by 25.5 yuan or 4.98 percent, according to Shanghai International Energy Exchange.
Hiyo mikataba yenyewe ambayo ipo kwenye Petro-yuan haifiki hata 30%. Kingine akipata hiyo Chinese yuan akitaka kufanya biashara kimataifa atapata wapi fedha nyingine za kigeni(Dollar) au ndo kila kitu atakua ananunua China?![emoji3]
 
Mambo yameiva, EU imesema itaziadhibu kampuni za Ulaya zitakazotii masharti ya US.
=====
European companies doing business with Iran could soon find themselves between a rock and a hard place. Should they comply with US sanctions and abandon Tehran, they may in turn face sanctions in their home EU.
EU will punish own companies if they comply with US sanctions on Iran, says Mogherini aide
Hamna kitu hapo huo ni mkwara tu,EU hawana ubavu wa kuyapiga penalties Makampuni yao wenyewe pia kumbuka EU ni Muungano wa nchi 28 hivyo kinachosemwa hapo lazima kikubaliwe na wanachama Wote 28 na si tu France,German na UK
 
Ngoja tuone mbabe kwenye huu mtanange hapa, japo alietangulia katangulia tu mwishowe bingwa atabaki yule yule
Ukiamini hivyo ni makosa ndugu, ni sawa na kuamini baada ya bombadier hatutanunua tena nyingine. Hao waliotangulia nao wana matatizo yao kama binadamu wengine ndio maana wanahitaji msaada AU kuidhibiti Iran.
 
Malcom Lumumba

tunaona sasa umoja wa ulaya wanaenda kwenye ecogreen maana wanaachana na mafuta ya kuchumba sasa wanaenda kwenye umeme hapo huoni kwamba mmarekani anakaribia kutiwa kitanzi ukitegemea na sisi tunajingongoja kweny pipeline yetu ya Hoima-Chongoleani.

Mawazo yangu naona Iran mwisho wake u karibu zaidi kama ulivyokuwa kwa Ghadaffi. Maana yule muajemi mkorofi sana anaweka mapandikizi kila upande wa mashariki mpaka akatishia tena kule Myarmaa kwa Aung San Syuu Chii kuwasaidia ndugu zake waislamu. Mi naona Iran afanywe kam Afuganistan
 
Muiran atajamba che! che! Jeuri ya Ayatollah ndio Shida maana anaishi kwa raha sana huku raia wakipata taabu sana na maandamano kila uchao na washafikia kumtukana na kumuombea kifo exchange rate ya iran Tanzania huku ni peponi Just Imagine kwa Nchi tajiri kama Irani
 
Malcom Lumumba

tunaona sasa umoja wa ulaya wanaenda kwenye ecogreen maana wanaachana na mafuta ya kuchumba sasa wanaenda kwenye umeme hapo huoni kwamba mmarekani anakaribia kutiwa kitanzi ukitegemea na sisi tunajingongoja kweny pipeline yetu ya Hoima-Chongoleani.
Mkuu ahsante kwa hoja yako nzuri kabisa,
Lakini nadhani tusiliangalie hili swala katika upande moja peke yake, kwasababu zifuatazo:


Mosi, kufikia Green Economy inawezeka kabisa lakini siyo jambo la leo wala kesho. Mambo haya ya Nishati na mazingira yameanza kuzungumzwa tangia miaka ya 1960's mpaka leo lakini bado dunia inatumia makaa ya mawe, nyuklia, gesi na mafuta.

Pili, swala la Green Economy inabidi uliangalie katika jicho la Uchumi. Ulaya kama anatumia magari ya umeme na vyanzo vingine vya nishati, usisahau kwamba makampuni yake kama TOTAL, BRITISH PETROLEUM na THE ROYAL DUTCH SHELL ndiyo yanatawala soko la dunia la mafuta. Hivyo mbali na kupeleka mafuta Ulaya, hayo makampuni ndiyo yanauza mafuta Africa, America na Asia na wakiwa na masoko makubwa sana. Hivyo hata kama Sekta ya mafuta ya dunia itapewa ushindani mkali na Electrical Vehicles bado Ulaya atahitaji sana kuuza mafuta nje ya mipaka yake.

Mbali na hapo mafuta ni biashara nzuri sana kwa mataifa mengi sidhani kama Ulaya wanaweza wakaharibu hiyo biashara ya nchi kama Urusi, Saudi, Iran, Qatar and Yemen na wakaishiwa kuchekewa tu. Ndiyo maana ukiangalia sababu kubwa za Donald Trump na Vladmir Putin kupinga ishu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa (GLOBAL WARMING) ni kulinda hatma ya masoko yao ya mafuta na gesi.

Pia upande mwingine mbali na makampuni ya mafuta, vipi kuhusu hatma ya makampuni ya magari na ndege kama BENZ, LAND ROVER, MAYBACH, ROLLS ROYCE, VOLKS WAGEN na AIRBUS, BOMBARDIER etc Unadhani wanaweza wakabadilika tu ndani ya usiku moja na kuanza kutumia umeme ??? (Gharama itakuwa kubwa kiasi gani hadi kufanya hivyo)

Tatu, gharama za vyanzo vipya vya nishati katika utabiri ni kubwa sana sanaa. Inasemekana magari yatakayotumia vifaa vya umeme na mafuta (Hybrid Cars) yatuzwa kuanzia Euro 6000 hadi 16000, hizi ni hela nyingi kweli. Euro 6000 ni sawa na pesa za Kitanzania Milioni 15888000. Unahisi wangapi hata huko Ulaya wanaweza wakanunua haya magari kwa ghafla tu ??? Africa na Asia ambako masikini ni wengi sana huwezi kunishawishi niache kununua IST ya mtumba kwa milioni 7 zangu halafu niende nikanunue magari ya TESLA kwa milioni 15. Ulaya yatakuwepo sana lakini kwetu Afrika sidhani kama GREEN ECONOMY inaweza ikaathiri sana sekta ya mafuta kwa miaka kama 30 ijayo.

Nne, British Petroleum (BP) wametoa matokeo ya utafiti wao ambao unasema kufika mwaka 2030 mafuta yatahitajika sana kwa wingi hapa duniani. Mbali na hapo kutokana na dunia kugundua vyanzo vingi vya mafuta kuanzia kule Marekani,Bahari ya Uchina ambako inasemekana kuna mapipa kama Bilioni 30 ambayo hayajachimbwa na kwingineko bei ya mafuta itapungua kutoka hapa ilipo na kuwezesha watu wengi kuweza kumiliki magari na kuendesha mitambo mbalimbali kwa ajili ya uchumi. Hivyo hii ni sababu tosha sana kwa Sekta ya mafuta kuwa na nguvu kubwa bado hapa duniani.

NB: Ulaya mbali na kutaka kujenga Green Economy, anamiaka siyo chini ya 30 kuweza kuleta jehuri kwa mataifa kama Marekani, Urusi na Saudi Arabia linapokuja suala zima la nishati (Safari ni ndefu mno)
 
Back
Top Bottom