Wakuu
Chige na
neo1 unakumbuka mwaka 2018 tulilizungumzia suala la mtego ambao Marekani amemtegea Iran ili kufanya vikwazo vya Umoja wa Mataifa virudi (Automatic Unilateral Sanctions) huku Iran akishindwa kujitoa kwenye mpango wa kinyuklia aliosaini na mataifa ya Ulaya. Nililielezea hili kwa ufupi kwenye aya ya kwanza hadi ya tano kwenye bandiko namba #103. Bahati mbaya sana kweli yametimia na imefahamika kwamba ulikuwa ni mpango wa Marekani kucheza na sheria za kimataifa ili kumuekea Iran vikwazo huku akitumia mwamvuli wa Umoja wa Mataifa. Hebu someni hizi habari ninazoambatanisha hapa:-
1.
Washington unilaterally reimposes UN sanctions on Iran despite opposition from UN Security Council members – including US allies
2.
U.S. Heads to United Nations to Demand ‘Snapback’ of Sanctions Against Iran
MASWALI YA MSINGI AMBAYO INABIDI YAJIBIWE KISHERIA NA KIDIPLOMASIA NI HAYA YAFUATAYO:
Mosi, Je kwenye sheria za kimataifa kuna kitu ambacho kinaitwa "Snap-Back Sanctions" ambacho ni nyenzo na kanuni halali katika mahusiano ya kimataifa ? Kama kipo basi Marekani watupe tafasiri yake kisheria na nini haswaa ni msingi wa hii kanuni kwenye haya mahusiano ya kimataifa. Lini hii kanuni ilianzishwa na lini ilitumika hadi kupata uhalali kwenye siasa za kimataifa. Hiki ambacho wanakiita "Snap-Back Sanctions" kama ni halali basi lazima kitaangukia kwenye kanuni za ujumla ambazo zimetengenezwa na mataifa yaliyostaarabika (General Principles Accepted by Civilized Nations): Kama
Pacta Sunt Servanda,
Persona non-grata na
utti-possidetis.
Lakini tukitafuta tafasiri ya neno "Snap-Back Sanctions" hatuwezi kulikuta kabisa kwenye kamusi yoyote ya sheria hata ile maarufu kama The Black's Law Dictionary. Hata ukiwauliza wataalamu nguli wa sheria za kama Prof Malcom Shaw, Prof Alan Dershowitz na Eric Posner hawatakupa jibu moja. Tusisahau Marekani ni bingwa wa kutunga kanuni nyingi zisizo za kisheria na kulazimisha ziwe za kisheria, kama ambavyo alifanya miaka ya 80 na 90 kuhusiana na suala zima la ulinzi kabla ya shambulio almaarufu kama "Anticipatory Self-Defense/Pre-emptive Attack" ambalo kisheria halina msingi wowote ule kwenye Hati Idhini ya Umoja wa Mataifa "The UN Charter"
Pili, Vikwazo dhidi ya Iran viliondolewa na Baraza la Ulinzi na Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC) kama moja ya sharti ndani ya mpango wa nyuklia wa Iran. Sasa Marekani anavyorudisha hivi vikwazo kwa lazima bila kushirikisha Baraza la Ulinzi na Usalama la Umoja wa Mataifa na kutishia vikwazo kwa nchi ambazo hazitakubaliana naye ina maanisha kwamba Marekani itauwekea vikwazo Umoja wa Mataifa kwa kutotaka kurudisha vikwazo ??? Marekani hashindwi kufanya hivi, maana kama amediriki hadi kuwekea vikwazo taasisi kama Mahakama ya Uhalifu wa Kivita (ICC) na mabenki makubwa kama Deutsche Bank unadhani anashindwa kuuwekea Umoja wa Mataifa vikwazo, maana alishawahi kutishia kwamba atapunguza kutoa mchango kwa taasisi hiyo ya kimataifa kama haitafuata matakwa yake hasa linapokuja suala la Iran na Israel. Tatizo kubwa hapa ni kwamba taasisi ya Umoja wa Kimataifa ina kinga (Immunity) dhidi ya madai yoyote hasa pale inapofanya kazi: Hii kanuni ya kinga ilishawahi kusemwa na mahakama ya dunia kwenye kesi ya mwaka 1948 iitwayo UN Reparations Case.
Baya zaidi ni kwamba mahakama za Marekani zenyewe zishawahi kukubaliana na kanuni hii ya kinga (Immunity) kwa taasisi ya Umoja wa Mataifa kwenye kesi maarufu kabisa ya Cholera ya mwaka 2010. Ambapo wanasheria mbalimbali walipeleka madai yao dhidi ya Umoja wa Mataifa kwa kusababisha mlipuko wa homa ya matumbo nchini Haiti, ambapo ilidaiwa kwamba wanajeshi wa Umoja wa Mataifa ndiyo waliyoipeleka. Mahakama ya Marekani ilitoa mwongozo na kusema Umoja wa Mataifa haushitakiwi kwa namna yoyote ile. Sasa waliokataa vikwazo visirudi ni mataifa kwa ujumla ndani ya Umoja wa Mataifa, hivyo tunaweza kusema kwamba Umoja wa Mataifa ndiyo umemkatalia Marekani. Sasa Je, Marekani atauwekea vikwazo Umoja wa Mataifa ??? AU anayavizia mataifa fulani fulani ambayo ni mahasimu kama Uchina na Urusi, ambapo atatumia kisingizio hiki kama sababu ya kupambana nayo zaidi ??? Hebu soma kesi hiyo hapa:
U.N. sued in U.S. court over Haiti's cholera epidemic
Tatu, katika sura ya kidiplomasia haya ambayo Marekani anayafanya hayatazidi kumtenga na jumuiya ya kimataifa kama ambavyo Umoja wa Kisovieti ulifanyiwa mwaka 1950 kuhusiana na Vita ya Korea ??? Warusi walidhani kwamba wakisusia vikao vya Baraza la Ulinzi na Usalama la Umoja wa Mataifa basi dunia haiwezi kufanya chochote kwasababu ilikuwa ni lazima mwanachama wa kudumu awepo kwenye kikao ili kura ya kupeleka vikosi kule Korea Kusini ifanikiwe. Urusi kwa maslahi yake binafsi akasusia vikao akidhani yeye ni taifa lenye nguvu na dunia inawaogopa sana. Bahati mbaya sana watu wenye akili walitengeneza kitu kiitwacho "United For Peace Initiative" ambapo kura ya kupeleka majeshi kule Korea Kusini haikupigwa tena na Baraza la Ulinzi na Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC) bali Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa (United Nations General Assembly): Hivyo Joseph Stalin na wakomunisti wake wakashindwa kufanikisha adhma yao. Sasa kama Marekani akiendelea hivi, yale malalamiko ya wakina Mugabe na wengine kwamba baraza la Ulinzi lifanyiwe marekebisho hazitakuwa ???
Je, Marekani hajengi mfano mbaya (Bad Precedent) kwa mataifa mengine makubwa kama Uchina na Urusi: Vipi kama mataifa mengine makubwa kama Uchina ambalo ni taifa mfadhili wa pili wa Umoja wa Mataifa likiamua kuufanyia vurugu Umoja wa Mataifa kama ambavyo Marekani anafanya ???