EU yaivimbia Marekani huku ikiilinda Irani kibiashara

EU yaivimbia Marekani huku ikiilinda Irani kibiashara

Waliibeba sana EU sasa wamepunguza ndo maana unaona ajira zinaongezeka USA.kipindi cha obama kila mtu alikuwa akijipigapiga anatimba US .sazi kuna ugumu kidogo na ni nchi zote huingii tu US kisa umeamua.
Hili nimeliona tangu Trump alipoingia madarakani,ni kwamba wanataka kuweka mfumo mpya wa siasa za Dunia.
 
Wadau mi maoni yangu nadhani MAREKANI ameona ni vyema kuikataa EU.Kumbuka kila mwaka kiasi kikubwa sana cha fedha alikitenga kuipa EU.Trump kuna watu wapo nyuma yake ambao bila kujali vyama wameamua kudinda EU.kama Uchumi wa jimbo moja la CARIFONIA kwa mwaka ni sawa na uchumi wa FRANCE yote.majimbo mengine kama matatu ni uchumi wa BRITAIN bado mtu hajiongezi tu?Kiufupi US chini Ya TRUMP inajaribu kuweka system mpya ya kisera kiuchumi,kijamii,na kisiasa huku ikiwa AMERICAN FIRST. Anachofanya wanasain makubaliano wao wanadeal n mtu mojamoja.Walianza na MACRON,akaja MAY,PUTIN,North na South Korea.Japan.na nchi zinginezo.Kiufupi ni kwamba mipango itapangwa ila Marekani anacontrol NATO.akiamrisha Ivamie SRYIA hakuna EU atakae nyanyua mdomo.Wakati wa Spain Vs Catalonia EU ilikaa kimya.Kimsingi ni toothlessdog.ILA MUDA NDIO MWAMUZI BORA ZAIDI.unafiki haupo afrika tu .Upo dunia yote japo huku ndo umeota mizizi nankustawi.
Nukuu ya LEO..." Marekani ana control NATO, akiamrisha ivamie Syria hakuna EU atakae nyanyua mdomo " mwisho wanukuu.

Watu mna maneno nyieeee, ila mpunguze kula Maharage bhana.

Khaaaaaa...!!
 
Nukuu ya LEO..." Marekani ana control NATO, akiamrisha ivamie Syria hakuna EU atakae nyanyua mdomo " mwisho wanukuu.

Watu mna maneno nyieeee, ila mpunguze kula Maharage bhana.

Khaaaaaa...!!
Mkuu hayo ni maoni tu.Nawewe unaweza kutoa ya kwa kwako.Pia maoni yanaweza kuwa yasiwe fact.Hivyo subiri muda uamue ama vipi?
 
Trump ni pasua kichwa kuanzia ndani ya Marekani kwenyewe, EU,Mashariki ya Kati na Ulimwengu wa kiarabu , Africa (rejea Sithole countries) na duniani kwa ujumla.
 
Mkuu hayo ni maoni tu.Nawewe unaweza kutoa ya kwa kwako.Pia maoni yanaweza kuwa yasiwe fact.Hivyo subiri muda uamue ama vipi?
Ahsante mkuu,
nayaheshimu maoni yako tena hongera kwa ulichokiona japo twaweza kutofauti na hata kuelemishana kwa hilo.

Hilo la Marekani kuingia Syria hapana tena hapana aisee,

Na sidhani kama EU watakuwa tayari kwa hilo . James mattin ( Ma dog) alipinga hilo jambo na Seneta ya USA walipinga huo ujinga wa Trump. Sababu wanazijua zaidi ya Mimi na ww...
 
Mkuu Malcolm lumumba nimekuwa interested na hiyo SWIFT issue ya money transfer. Kuna mahali nilisoma kuwa China, anataka kuanza kununua mafuta bila kutumia dola za Marekani. Pia BRICS wana mpango Wa kuanzisha benki zao kushindana na IMF na Word bank ambazo ni himaya za Marekani. Naomba wewe au Mjuzi yeyote anielimishe, hivi hayo yakifanyka bado Marekani atakuwana mwanya Wa kuchezea wenzake? Hata Uingereza waligusia kusupport biashara bila kutumia dola ya Marekani, Hapo itakuwaje maana uchumi Wa Marekani sa sa hivi ni%22.5 hadi 25% ya uchumi wa dunia, atawezaji kuchezea 75% ya uchumi Wa wengine wrote wakiungana li dola lake waliache maananasikia dola inamiliki 75 % ya money international trade , Tafadhali tuelimishane hapo.

Mkuu Muyovozi Katibu wa Hazina wa Marekani Steven Mnuchin amesema wanataka tena kutumia njia ya SWIFT kumtoa tena Iran kwenye mfumo wa malipo huo wa malipo. Je, Iran anaweza kuwa na njia mbadala ya malipo ya nje kwenye mafuta yake zaidi ya SWIFT ??

Upande wa pili unahisi hii SWIFT itakuwa na afya nzuri kibiashara kama mataifa mengi yakijitoa na kutengeneza mifumo yao mingine ya malipo ya nje ya nchi ??

Sources:
1. US lawmakers urge Iran expulsion from SWIFT banking network
2. Mnuchin says it will be harder for Iran oil importers to get waivers | Reuters
3. US pressures SWIFT to cut off Iran from global banking transactions to enforce sanctions

NAKALA IWAFIKIE:
Red Giant , chige , Wick , FisadiKuu , TUJITEGEMEE , fundi25 , Drifter , 1954 , Chamoto , General Mangi , Mbimbinho , Proved , neo1 , Moisemusajiografii , Kiranga , Drifter , Nalendwa , nankumene , ze kokuyo , Consigliere , Sexer , Hussein Melkiory , zitto junior , Richard
 
UPDATE
25/09/2019
Kuonyesha kuwa EU haitanii katika suala lake la kutokubaliana na US, sasa inaandaa utaratibu wa kufanya malipo bila kufuata mfumo wa fedha unaodhibitiwa na US katika biashara yake na Iran. Maelezo zaidi haya hapa
------
5ba9a04efc7e93807a8b45a2.jpg

FILE PHOTO: Iranian Foreign Minister Mohammad Javad Zarif and the High Representative of the European Union for Foreign Affairs and Security Policy Federica Mogherini © Leonhard Foeger / Reuters
European Union foreign affairs chief Federica Mogherini says the EU signatories remain committed to the nuclear deal with Iran that the US has quit. The group is working to create special payment channels to do business with Iran.
EU to create special payment channels with Iran despite US sanctions – Mogherini
UPDATE
25/08/2018
EU imekubali hivi majuzi kuipatia msaada wa maendeleo Iran unaokadiliwa kufika Euro 18 milioni. Marekani wachukia.

Washington said the EU’s latest Iran development aid package of €18 million is “sending the wrong message” and apparently undermining its efforts to isolate the Islamic republic with unilateral sanctions.

“The European Union’s August 23 announcement of a new $20.7 million payment that will widen economic and sectoral relations between Iran and Europe sends the wrong message at the wrong time,” US State Department Special Representative Brian Hook said.

The US official went on to claim that Tehran will gratefully take the EU money and use it to “conduct assassinations in those very European countries.”

DETAILS :RT.com

UPDATE
07/08/2018
Mambo yameiva, EU imesema itaziadhibu kampuni za Ulaya zitakazotii masharti ya US.
=====
European companies doing business with Iran could soon find themselves between a rock and a hard place. Should they comply with US sanctions and abandon Tehran, they may in turn face sanctions in their home EU.
EU will punish own companies if they comply with US sanctions on Iran, says Mogherini aide
===
06/08/2018
EU imekataa kuidhinisha vikwazo dhidi ya Irani vilivyowekwa kibabe na US. Na EU imesema makampuni yake hayataguswa na mashinikizo ya vikwazo vya US kwa mwamvuli wa EU. Kuonyesha wameivimbia kweli kweli wame'washa' na wataanza ku'puliza' kitu kinaitwa 'Blocking Statute' kesho. Hii kitu inakinga makampuni ya EU na bughudha za Marekani katika biashara zao. Maelezo ya Kina haya hapa chini
====
The European Union is enforcing the so-called Blocking Statute to protects its firms operating in Iran from the looming US sanctions against the country.
The first round of renewed US sanctions will take effect on Tuesday after midnight US Eastern time with the harshest sanctions expected to return in early November.
The European Commission has stated that despite US sanctions, European companies will continue doing legal business in Iran under the protection from Brussels.
“The lifting of nuclear-related sanctions is an essential part of the deal – it aims at having a positive impact not only on trade and economic relations with Iran, but most importantly on the lives of the Iranian people. We are determined to protect European economic operators engaged in legitimate business with Iran, in accordance with EU law and with UN Security Council resolution 2231,” the European Commission stated on Monday.
"This is why the European Union’s updated Blocking Statute enters into force on 7 August to protect EU companies doing legitimate business with Iran from the impact of US extra-territorial sanctions," it added.
Brussels announced back in May that it would enable the Blocking Statute starting from August. The law was first adopted in 1996 and forbids EU companies from complying with the extraterritorial effects of US sanctions. It allows companies to recover damages arising from such sanctions, and nullifies the effect in the EU of any foreign court judgements based on them.

EU blocking US sanctions against Iran to protect European companies
---
Update
====
Kumetokea mlipuko mkuwa Bologna, Italy. Italy ni mwanachama wa EU

2 dead, at least 55 injured in massive highway explosion in Bologna (PHOTOS, VIDEOS)
Europe ni wastaarabu sana kwani wamekuwa wakistahamili undumila kuwili,uongo,uchoyo na ulafi kwa miaka mingi kwa sababu ya kulinda umoja wao na hasa kwa heshima ya US kujiingiza na kusaidia WWII kwisha kwa ushindi.
1. Undumila kuwili.
Marekani siku zote ilikuwa inajinadi kuhusu haki za binadam
Mifano ni mingi sana kwa mfano mahusiano yake na makaburu ,kina Mobutu, Savimbi na kina Noriega.
washenzi hawa walilindwa sana na US kutokana na raslimali za madini ambayo yalitumika kuendeleza
uchumi wa marekani bila kujali dunia inasema nini?
2. Ukiangalia matitozo yote ya mashariki ya kati yametokana utashi wa marekani mfano:-
a] Iran walimbeba shah kwa sababu tu walikuwa na mkataba wa kuchimba mafuta wa bei chee na hawakujali wananchi wa nchi hiyo wananufaika vipi na matokeo ya uadui leo ni kutokana na kupinduliwa kwa kibaraka wao shah na katiba ya nchi hiyo kubadilishwa na mikataba yote kuhuishwa na hadi leo wamejenga chuki isiyokuwa na mfano kwa nchi hiyo.
b] Iraq -Aliifitinisha nchi hiyo na iran kwa kutumia kadi ya ushia na usunni na kuzipiganisha huku akitoa msaada mkubwa kwa iraq kwenye vita ya miaka karibu 7 na kuishia na suluhu.
c] Kuwait- Aliichuuza Iraq ikaingia kuwait na uongozi wa kanchi hako wakaomba kukombolewa na marekani ambapo hadi leo nchi hiyo uchumi wake haujakaa sawa kutokana na kulipa gharama ya vita hivyo.
e] Iraq baada ya vita na Iran kwisha na wakati wa iraq wakitibu vidonda vya vita, marekani ikaanza fitna kuwa iraq ina silaha za maanagamizi [sijui kwa nini kama kweli nchi hiyo ilikuwa na silaha hizo isizitumie kwa kuipiga iran] Dunia nzima iliammini maneno ya mkubwa huyo na matokeo yake ni vita ambavyo vimeirudisha nyuma kiuchumi nchi hiyo
hadi leo haijakaa sawa kwani nchi hiyo hadi leo inalipa gharama za vita hiyo
3. Uchoyo -US siku zote imekuwa waroho na wachoyo mfano mzuri ni ujenzi wa Iraq na Kuwait pamoja na uuzaji wa silaha kwa nchi hizo. US imehakikisha kuwa karibu tenda zote wanapata wao.
Matokeo ya sera zake ulaya imeona kwamba uchumi wa nchi zao utatetereka iwapo watamfuata uncle sam na matokeo yake ni kwamba kwa miaka ya karibuni wamekuwa na misimamo yao ambayo hivi sasa wanaionyesha dhahiri.
Kwa sera hizi US imejipunguzia marafiki na imewapa nguvu maadui zake ambao ni china na urusi kwani karibu nchi nyingi hivi sasa zinaziangalia nchi hizi kwa mtazamo mwingine na siyo ule ambao marekani walikuwa wanawadanganya kuwa adui mkubwa na urusi na china na hivi sasa imedhihirika kuwa adui mkubwa duniani kwenye masuala ya uchumi na ustawi wa dunia ni marekani.
 
Germany's Foreign Ministry took to Twitter to defend the Iran deal, also known by the acronym JCPOA (Joint Comprehensive Plan of Action), and to vow that Berlin would continue to trade with legitimate businesses in Iran, as permitted by the agreement.
"The JCPOA is a key element of of global nuclear nonproliferation architecture and of multilateral diplomacy," said the German government in a joint statement with the UK and France. "It is our aim to protect European economic operators engaged in legitimate business with Iran, in accordance with EU law."

US announces broad new sanctions against Iran | DW | 02.11.2018
 
Kuwa mshabiki na iran hasa muafrica ni ujinga mwanzo nilikuwa nauna km mmarekan anaroh mbaya kumbe sivyo ase hawa waarabu sio watu wazuri wasipozibitiwa vilivyo dunia tutaiwek mahali pabaya sn go us go
 
Mkuu mimi nina maswali hapa:
Mosi, Umoja wa Ulaya unapitisha sheria ya kuyalinda makampuni yao yanayofanya kazi nchini Iran. Hivi hiyo sheria mbali na kulipa fidia za hasara na kutotii maamuzi ya mahakama ya nchi za nje, inawezaje kuyalinda hayo makampuni ???

...
Mkuu, kwanza kumradhi kwa kuchelewa sana kujibu swali lako.
Kama nilivyoahidi kwenye post # 19 ya uzi huu kwamba nitaleta majibu baada ya kupitia makabrasha yangu. Nimefanya hivyo. Nimepitia makabrasha mengi kidogo lakini nitasimamia makabrasha matatu ya NATO treaty (1949), EU constitution (2005), na EU guidence note (EUGN) on blocking statute ya August, 2018).

Mkuu, uliuliza, "Hivi hiyo sheria mbali na kulipa fidia za hasara na kutotii maamuzi ya mahakama ya nchi za nje, inawezaje kuyalinda hayo makampuni ??? ".

Wasomaji, sheria inayozungumzwa hapa ni ile kwa kiingereza inaitwa " blocking statute" . Sheria hii imefafanuliwa zaidi kwa kiingereza katika mkutadha huu kuwa " It allows EU operators to recover damages arising from US extraterritorial sanctions from the persons causing them (US) and nullifies the effect in the EU of any foreign court rulings based on them. It also forbids EU persons from complying with those sanctions, unless exceptionally authorised to do so by the Commission in case non-compliance seriously damages their interests or the interests of the Union. ". Kwa tafsiri isiyorasimi na kwa nyongeza ya maelezo aliyokwisha toa muuliza swali juu ya sheria hii nikuwa makampuni yatafidiwa gharama ya hasara kutoka kwa aliyesababisha hasara hiyo yaani Marekani; pia raia wa EU anakatazwa kabisa kutii vikwazo vilivyowekwa na Marekani labda kwa ruhusa ya mamlaka ya tume ya EU endapo tu kutotii vikwazo hivyo kutaathiri tija zao na za EU. Ufafanuzi wa sheria hii kwa mujibu wa EU unapatikana hapa:
Updated Blocking Statute in support of Iran nuclear deal - Service for foreign policy instruments (FPI) - European Commission
https://eur-lex.europa.eu/legal-content/EN/TXT/PDF/?uri=CELEX:52018XC0807(01)&from=EN (EUGN, 2018)

Mkuu, Malcom Lumumba ukisoma EUGN (2018) ambayo ilichapishwa na jarida rasimi la EU (huku kwetu tunaweita gazeti la serikali); kuanzia kipengele cha 4 mpaka 7 utaona kwamba EU kweli wana maanisha ingawa kipengele cha 5 kinaweza kutumika kama maficho ya EU 'kuinafiki' Iran. Kipengele cha 4 kinaeleza vizuri namna ya kulinda makampuni (EU operators), kipengele cha 6 na 7 vinaeleza kwanini sheria imeuishwa na nani kasababisha. Hapa wamemtaja kabisa US kwa kutishia kuiwekea vikwazo Iran na wale watakao pinga vikwazo hivyo. Lakini kipengele namba tano, kinatoa mwanya wa makampuni kutii vikwazo vya US kwa kutoa sababu amabazo 'zitairidhisha' EU. Hapa na mimi ndipo ninapata mashaka.

Mkuu nikirejea kwenye katiba ya EU: Sehemu 3 kichwa cha 3 sura ya 3(6, 10)-ulinzi wa mlaji na nishati; sehemu ya 3 kichwa cha 3 sura ya 2(2,3)-sera ya fedha; sehemu ya 3 kichwa cha 4,5. Na sehemu ya 4 inayoeleza kwa pamoja na annex na protocols za katiba hiyo; utagundua kabisa EU wana 'instruments' za kusimamia kile walichokubaliana hata ndani ya katiba yao kuilinda EU kwa namna yoyote. Rejea vifungu hivi kutoka katiba ya EU kupitia hapa
https://europa.eu/european-union/si...establishing_a_constitution_for_europe_en.pdf

Pia ukirejea NATO treaty (1949). Ile Article 1, ambayo inasema, nanukuu, "The Parties undertake, as set forth in the Charter of the United Nations, to settle any international dispute in which they may be involved by peaceful means in such a manner that international peace and security and justice are not endangered, and to refrain in their international relations from the threat or use of force in any manner inconsistent with the purposes of the United Nations." mwisho wa kunukuu.

Nchi zenye nguvu ndani ya NATO ndiyo hao pia wapo EU. Ukisoma maelezo ya awali ya treaty hii hayapishani kimlengo na yale yaliyo kwenye katiba ya EU. Na sasa inaposomwa Article 1 ya treaty, unaona kabisa EU ndiyo wameshika mpini kwani JCPOA iliidhinishwa na UN. NATO katika Article 1 yake inahimiza kuheshimu maamuzi ya UN. Treaty nzima inapatikana hapa
https://www.nato.int/nato_static/as...ations/20120822_nato_treaty_en_light_2009.pdf

Mkuu, EUGN (2018) inajibu swali lako la ni namna gani sheria hii itawalinda makampuni ya EU dhidi ya vikwazo vya US. Pia katiba ya EU na treaty ya NATO vinawapa EU sababu, nia na uwezo wa kusimamia na kuendelea kufanya biashara na Iran.

Mkuu yangu ni hayo. Kwa mara nyingine kumradhi kwa kuchelewa kukujibu.
 
Kuwa mshabiki na iran hasa muafrica ni ujinga mwanzo nilikuwa nauna km mmarekan anaroh mbaya kumbe sivyo ase hawa waarabu sio watu wazuri wasipozibitiwa vilivyo dunia tutaiwek mahali pabaya sn go us go
Iran sio muarabu mkuu hawa ni waajemi(Persians).Sijui tuwalaumu hawa walimu wanaowafundisha shuleni sijui ni uzembe wako mwenyewe
 
Nimeona mshauri, mzee Bolton anasema EU wachague moja US, ama IRAN ngoja tusubiri kuona.
Utendaji wa serikali ya US inatatiza, hivi Ukiwa Mshauri wa Rais ndiyo unakuwa tayari wewe ni Waziri wa Ulinzi wa Marekani?
====
US ameisha 'yield' ameanza kulegeza misimamo yake kwa baadhi ya nchi kama India nakadhalika kuwa wanaruhusiwa kuendelea kufanya biashara na Iran ila kwa muda maalumu na muda huo wala hajautaja. Hata hivyo tusubiri tuone.
 
Yes, tusubiri kuona.
Lakini najiuliza kwamba inamana US hajui madhara anayoweza kupata ikiwemo kudaraulika na nchi kama china Russia hindia irani yenyewe na hata ulayapia iwapo amefanya maamuzi ya kukurupuka katika hii sanction kwa irani?.

Inamana hawajui wanachofanya?
Je wanajaribu tu kupima watu wana watii kiasigani, hasa EU?.
Ngoja tuone labda ana plani B, maana naona kama kuna madhara makubwa kwake ikitokea huu mpango ukashindwa.

Utendaji wa serikali ya US inatatiza, hivi Ukiwa Mshauri wa Rais ndiyo unakuwa tayari wewe ni Waziri wa Ulinzi wa Marekani?
====
US ameisha 'yield' ameanza kulegeza misimamo yake kwa baadhi ya nchi kama India nakadhalika kuwa wanaruhusiwa kuendelea kufanya biashara na Iran ila kwa muda maalumu na muda huo wala hajautaja. Hata hivyo tusubiri tuone.
 
Mkuu, kwanza kumradhi kwa kuchelewa sana kujibu swali lako.
Kama nilivyoahidi kwenye post # 19 ya uzi huu kwamba nitaleta majibu baada ya kupitia makabrasha yangu. Nimefanya hivyo. Nimepitia makabrasha mengi kidogo lakini nitasimamia makabrasha matatu ya NATO treaty (1949), EU constitution (2005), na EU guidence note (EUGN) on blocking statute ya August, 2018).

Mkuu, uliuliza, "Hivi hiyo sheria mbali na kulipa fidia za hasara na kutotii maamuzi ya mahakama ya nchi za nje, inawezaje kuyalinda hayo makampuni ??? ".

Wasomaji, sheria inayozungumzwa hapa ni ile kwa kiingereza inaitwa " blocking statute" . Sheria hii imefafanuliwa zaidi kwa kiingereza katika mkutadha huu kuwa " It allows EU operators to recover damages arising from US extraterritorial sanctions from the persons causing them (US) and nullifies the effect in the EU of any foreign court rulings based on them. It also forbids EU persons from complying with those sanctions, unless exceptionally authorised to do so by the Commission in case non-compliance seriously damages their interests or the interests of the Union. ". Kwa tafsiri isiyorasimi na kwa nyongeza ya maelezo aliyokwisha toa muuliza swali juu ya sheria hii nikuwa makampuni yatafidiwa gharama ya hasara kutoka kwa aliyesababisha hasara hiyo yaani Marekani; pia raia wa EU anakatazwa kabisa kutii vikwazo vilivyowekwa na Marekani labda kwa ruhusa ya mamlaka ya tume ya EU endapo tu kutotii vikwazo hivyo kutaathiri tija zao na za EU. Ufafanuzi wa sheria hii kwa mujibu wa EU unapatikana hapa:
Updated Blocking Statute in support of Iran nuclear deal - Service for foreign policy instruments (FPI) - European Commission
https://eur-lex.europa.eu/legal-content/EN/TXT/PDF/?uri=CELEX:52018XC0807(01)&from=EN (EUGN, 2018)

Mkuu, Malcom Lumumba ukisoma EUGN (2018) ambayo ilichapishwa na jarida rasimi la EU (huku kwetu tunaweita gazeti la serikali); kuanzia kipengele cha 4 mpaka 7 utaona kwamba EU kweli wana maanisha ingawa kipengele cha 5 kinaweza kutumika kama maficho ya EU 'kuinafiki' Iran. Kipengele cha 4 kinaeleza vizuri namna ya kulinda makampuni (EU operators), kipengele cha 6 na 7 vinaeleza kwanini sheria imeuishwa na nani kasababisha. Hapa wamemtaja kabisa US kwa kutishia kuiwekea vikwazo Iran na wale watakao pinga vikwazo hivyo. Lakini kipengele namba tano, kinatoa mwanya wa makampuni kutii vikwazo vya US kwa kutoa sababu amabazo 'zitairidhisha' EU. Hapa na mimi ndipo ninapata mashaka.

Mkuu nikirejea kwenye katiba ya EU: Sehemu 3 kichwa cha 3 sura ya 3(6, 10)-ulinzi wa mlaji na nishati; sehemu ya 3 kichwa cha 3 sura ya 2(2,3)-sera ya fedha; sehemu ya 3 kichwa cha 4,5. Na sehemu ya 4 inayoeleza kwa pamoja na annex na protocols za katiba hiyo; utagundua kabisa EU wana 'instruments' za kusimamia kile walichokubaliana hata ndani ya katiba yao kuilinda EU kwa namna yoyote. Rejea vifungu hivi kutoka katiba ya EU kupitia hapa
https://europa.eu/european-union/si...establishing_a_constitution_for_europe_en.pdf

Pia ukirejea NATO treaty (1949). Ile Article 1, ambayo inasema, nanukuu, "The Parties undertake, as set forth in the Charter of the United Nations, to settle any international dispute in which they may be involved by peaceful means in such a manner that international peace and security and justice are not endangered, and to refrain in their international relations from the threat or use of force in any manner inconsistent with the purposes of the United Nations." mwisho wa kunukuu.

Nchi zenye nguvu ndani ya NATO ndiyo hao pia wapo EU. Ukisoma maelezo ya awali ya treaty hii hayapishani kimlengo na yale yaliyo kwenye katiba ya EU. Na sasa inaposomwa Article 1 ya treaty, unaona kabisa EU ndiyo wameshika mpini kwani JCPOA iliidhinishwa na UN. NATO katika Article 1 yake inahimiza kuheshimu maamuzi ya UN. Treaty nzima inapatikana hapa
https://www.nato.int/nato_static/as...ations/20120822_nato_treaty_en_light_2009.pdf

Mkuu, EUGN (2018) inajibu swali lako la ni namna gani sheria hii itawalinda makampuni ya EU dhidi ya vikwazo vya US. Pia katiba ya EU na treaty ya NATO vinawapa EU sababu, nia na uwezo wa kusimamia na kuendelea kufanya biashara na Iran.

Mkuu yangu ni hayo. Kwa mara nyingine kumradhi kwa kuchelewa kukujibu.
Alaaah,
Basi Mungu akinijalia muda ntakuja tuaichambue hoja moja baada ya nyingine.
 
Back
Top Bottom