Eti watu 10 wamekamatwa Mwanza kwa kumzomea Pinda Mwanza?

Ukosefu wa adabu watazomeaje??wafikishwe mahakamani wale wote waliozomea wakashike adabu
 
ngwendu said:
kuzomea si kitendo cha kiustaarabu kabisa. kama hujisikii kwenda kumsikiliza siushinde nyumbani? huu ujinga upo bongo tu. watu hushindana kwa hoja na si kuzomea. hao ndo chadema, ni zaidi ya tuijuavyo.
Kakudanganya nani? Hivi wewe unaishi dunia gani? Sasa usipomsikiliza utajuaje kaongea pumba? Ukishinda nyumbani si utakosa nafasi ya kumsikiliza na kumzomea ikibidi? Na usipomzomea atajifunzaje kutoongea pumba? Yeye yuko jukwaani anaongea pumba, kuna njia moja tu ya kushindana naye kwa hoja, kumzomea! Hivyo ndivyo ilivyo! Au wewe ungependa apopolewe mawe, wee nawe!
 
kuzomea si kitendo cha kiustaarabu kabisa. kama hujisikii kwenda kumsikiliza siushinde nyumbani? huu ujinga upo bongo tu. watu hushindana kwa hoja na si kuzomea. hao ndo chadema, ni zaidi ya tuijuavyo.

ebu usitudanganye uko, eti uko bongo, bora anazomewa tu na si kurushiwa mayai viza na ma pie kama wa uko west
 
Hizi ni ishara za anguko kuu la ccm,kama ilivyo kushangilia ndivyo ilivyo kuzomea.Na kamwe watawala wasifikiri kuwa wataweza kutumia polisi au jeshi kuzuia hisia za wananchi.Badala yake waboreshe maisha ya wananchi kiuchumi
 
Mwanza tumeishakataa ujinga wa kishamba unaolefanywa na viongozi dhaifu wa CCM, wakitia sura jijini kwetu kutujaza ujinga tutawazomea tu. kilichomkuta Pinda ni mwanzo tu, tutawazomea zaidi bin zaidi
 
hakuna wa kukuzomea kama utaongea points, tena bongo ndio kuna nidhamu ya hali ya juu ndio maana watu wanazomea, nchi zenye watu wasioogopa unashushwa jukwaani kwa mawe mfano ni hapo tu kenya!

pumba hazikubaliki mkuu

Nachukiaga hawa useless people kuwabeza chadema. Hivi wewe CCM imekusaidia nini kama kukusaidia wewe na tumbo lako na fanilia yako. Bunge limejaa maskini wakubwa tena wenye ulafi wenye kukosa uzalendo maana ni CCM ambayo imeonyesha ukitaka kufanikia njoo CCM na upate ubunge au lah, ujikombe tu uonekane. Hatuwezi kuwa wote wanasiasa. Sioni ubaya mtu kuzomewa maana haeshimiki. Heshima hainunuliwi, bali inajengwa. Kama unataka kuheshimiwa basi ujiheshimu.
 
kuzomea si kitendo cha kiustaarabu kabisa. Kama hujisikii kwenda kumsikiliza siushinde nyumbani? Huu ujinga upo bongo tu. Watu hushindana kwa hoja na si kuzomea. Hao ndo chadema, ni zaidi ya tuijuavyo.
booooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooh
 
Wakuu! Hili wala lisitusumbue. Kukamatwa kwa watu hao ni upuuzi wa polisi. Rejeeni majibu ya Kamuhanda kuhusu suala la kujiuzuru. Mi naona ujumbe ulifika na "Mtoto wa Mkulima" aliupata na kuhadharisha viongozi wenzake. Hebu ninukuu gazeti la Tanzania Daima la trh 19 Sept kidogo. "...Alisema hii ni mara yake ya kwanza kukumbana na zomeazomea, hivyo lazima kero zinazowasibu wananchi zitatuliwe kwani hali hiyo siyo nzuri kutokea kwa kiongozi wa taifa kama yeye.Pinda aliyasema hayo jana wakati alipokuwa akizungumza kwenye kikao cha majumuisho ya ziara yake ya siku saba mkoani Mwanza, kilichofanyika kwenye ukumbi wa jiji la Mwanza.
"Kwa kweli hali ya jana (juzi), ilinitisha sana. Kama mimi nimezomewa, kiongozi gani atakayesalimika kuzomewa akienda uwanjani hapo?". Kama vile haitoshi Mtoto wa Mkulima akaendelea akarejea maneno ya Mbunge wa jimbo husika "Na akaniambia Wenje kwamba tangu umalizike uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, CCM haijafanya mkutano eneo hilo kuzungumzia kero za wananchi… sasa hii ni hatari sana," alisema Pinda huku akionekana kusononeshwa na hali hiyo". Hapo ujumbe umefika na kuwakamata watu hao ni kutoelewa wajibu wao na alichokisema PM.
 
kuzomea si kitendo cha kiustaarabu kabisa. kama hujisikii kwenda kumsikiliza siushinde nyumbani? huu ujinga upo bongo tu. watu hushindana kwa hoja na si kuzomea. hao ndo chadema, ni zaidi ya tuijuavyo.

mdau unazijua siasa za dunia nzima,au unakurupuka tu,tena kuzomea bongo ndo imeanza hivi karibuni,,,,,huko nchi za wenzetu wabunge hadi wanatwangana,ujue kuzomea imeishapita siku nyingi,ikiwa wao wanatwangana wapiga kura wao wanafanyaje???UKISEMA IPO BONGO TU,NABAKI KUKUSHANGAA
 
Kuzomea sio kosa la jinai wakiwafikisha mahakamani mahakama itawaachia kuna namna ya kupingana na mtu anayekuambia uongo moja nikumzomea ili asiendelee kudanganya haya yanatokea kwenye viwanja vya mipira,sokoni,na mahala pengi kwenye mikusanyiko wanawatisha tuu watawaachia

Nafikiri unazungumzia Nchi zenye mitizamo kama hiyo na sio Tanzania
 
kuzomea si kitendo cha kiustaarabu kabisa. kama hujisikii kwenda kumsikiliza siushinde nyumbani? huu ujinga upo bongo tu. watu hushindana kwa hoja na si kuzomea. hao ndo chadema, ni zaidi ya tuijuavyo.

NGWENDU usitudanganye eti huu uji*** upo bongo tu, wakati Rais wa Marekani mwenyewe mwezi uliopita ALIZOMEWA na mkusanyiko wa watu baada ya kusema kauli ambayo hawakuikubali. Lakini yeye wala hakukasirika, alijibu hivi tena tit for tat...."DONT BOO, VOTE!!"
Hakuna aliiyekamatwa wala kuambiwa hana adabu. Swala si adabu hapa. Ni swala la kukubaliana au kutokukubaliana na mtoa hotuba.
 
Wanaweza bambikiwa ata Bangi hao ili mradi wafungwe maana kwa kosa la kuzomea sijui watatumia kifungu kipi cha seria
 
Waje wawakamate huku JF maana wazomeaji wa magamba wako wengi sana mmojawapo mie!
 
Back
Top Bottom