Eti watu 10 wamekamatwa Mwanza kwa kumzomea Pinda Mwanza? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Eti watu 10 wamekamatwa Mwanza kwa kumzomea Pinda Mwanza?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kwitega, Sep 22, 2012.

 1. k

  kwitega Senior Member

  #1
  Sep 22, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari wakuu,

  Kuna taarifa nimezipata kutoka kwa mmoja wa makada wa CCM Mkoani Mwanza kuwa watu 10 wamekamatwa kwa kitendo cha kumzomea Waziri Mkuu Pinda pale uwanja wa Sahara Jijini Mwanza. Kada huyo ya CCM ameonyeshwa kusikitishwa na kitendo hicho akisema kuwa kitendo hicho ni uhuni na kwamba kuzomewa kwa Pinda ni ujumbe unaotakiwa kufanyiwa kazi na CCM na serikali yake na si kukamata watu.

  Nimejaribu kuzungumza na baadhi ya askari polisi jijini Mwanza juu ya taarifa hizi, wamekiri kwamba juzi watu sita walikuwa wamekamatwa na polisi kitengo cha intelijensia kwa mahojiano kuhusiana na Pinda kuzomewa hata hivyo wamesema hawajui kama waliendelea kushikiliwa au waliachiwa. Aidha nimezungumza na mmoja wa askari wa kitengo hicho yeye amekanusha vikali habari hizi.

  Tufuatilie ili tujue ukweli kisha tujadiri kama ni halali kumkamata mtu eti kisa kamzomea kiongozi wa serikali kwa kusema hatuitaki CCM!
   
 2. F

  Froida JF-Expert Member

  #2
  Sep 22, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Kuzomea sio kosa la jinai wakiwafikisha mahakamani mahakama itawaachia kuna namna ya kupingana na mtu anayekuambia uongo moja nikumzomea ili asiendelee kudanganya haya yanatokea kwenye viwanja vya mipira,sokoni,na mahala pengi kwenye mikusanyiko wanawatisha tuu watawaachia
   
 3. Sabung'ori

  Sabung'ori JF-Expert Member

  #3
  Sep 22, 2012
  Joined: Jul 19, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 150
  Trophy Points: 160
  ...mbona akipigiwa makofi na kushangiliwa watu hawatafutwi na kupewa zawadi!?...
   
 4. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #4
  Sep 22, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Great thinking!
   
 5. Autorun

  Autorun JF-Expert Member

  #5
  Sep 22, 2012
  Joined: Mar 21, 2008
  Messages: 556
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  kwani kuzomea ni dhambi? mimi naona kuzomea nikama kinyume cha kupiga makofi au kushangilia ni ishara ya kuwasilisha mawazo ya wanadamu pale inapo bidi kuonesha kutokubaliana na jambo au watufulani
   
 6. Thanda

  Thanda JF-Expert Member

  #6
  Sep 22, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,915
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Sabung'ori deserve the best, not a person of End of Thinking Capacity (ETC).
   
 7. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #7
  Sep 22, 2012
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  kuzomea si kitendo cha kiustaarabu kabisa. kama hujisikii kwenda kumsikiliza siushinde nyumbani? huu ujinga upo bongo tu. watu hushindana kwa hoja na si kuzomea. hao ndo chadema, ni zaidi ya tuijuavyo.
   
 8. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #8
  Sep 22, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  hakuna wa kukuzomea kama utaongea points, tena bongo ndio kuna nidhamu ya hali ya juu ndio maana watu wanazomea, nchi zenye watu wasioogopa unashushwa jukwaani kwa mawe mfano ni hapo tu kenya!

  pumba hazikubaliki mkuu
   
 9. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #9
  Sep 22, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Mkuu Sabung'ori..absolutely true...viongozi wasitake kusikia yale wanayotaka kusikia..kizazi hiki wanaamviwa ukweli tu..!
   
 10. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #10
  Sep 22, 2012
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Nani kakuambia kuzomea iko Bongo tu1 ulishawahi sikia neno "BOOOH!
   
 11. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #11
  Sep 22, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,528
  Likes Received: 10,441
  Trophy Points: 280
  CCM wanapenda misifa tu hata penye kuudhi.!
   
 12. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #12
  Sep 22, 2012
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Wengine wanarushia viatu na ch***p kabisa unafanya mchezo na wananchi waliochoka na uongo!
   
 13. M

  Mpwechekule JF-Expert Member

  #13
  Sep 22, 2012
  Joined: Jul 8, 2012
  Messages: 221
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ndugu unaonaje pia makofi ukipigia nyumbani kwako wakati viongozi wanahutubia mkutano? Italeta maana? Pia nataka kukueleza kuwa kiongozi ni mtu sio malaika kama unavyojenga picha kuwa hawapaswi hata kulaumiwa, ni watumishi wetu wale ni kama beki tatu tu akikosea lazima umweleze
   
 14. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #14
  Sep 22, 2012
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,875
  Likes Received: 1,561
  Trophy Points: 280
  Mungu wangu iokoe ccm
   
 15. J

  Joachim Morgan Member

  #15
  Sep 22, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hapo umesema na sie tunomshangilia tutafutwe tupewe zawadi au hongera.
   
 16. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #16
  Sep 22, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Mizengo Pinda anaposema uongo bungeni anafiri wananchi hatuoni!!!!!! Makinda anapozuia hoja mujarabu kujadiliwa bungeni anafikiri wananchi hatuoni!!! ccm wanapopitisha miswada kandamizi bungeni wanafikiri wananchi hatuoni!!!!

  Na wajiulize,
  wapige bla bla bungeni ambako hatuwezi kuingia kubishana nao tuwavumilie, wakija na kitaani, ndani ya 18 zetu ukweli wetu waufanye kuwa uongo machoni petu?
  KAMA KUZOMEWA INAWAKERA NA KUJIREKEBISHA HARAKA HAWATAKI BADALA YA KUZOMEA MAYAI VIZA NDIO DAWA YAO ILI WASIENDELEE KULAZIMISHA KUHUTUBIA UONGO!! WAJIANDAE.
   
 17. M

  Mgelukila JF-Expert Member

  #17
  Sep 22, 2012
  Joined: May 27, 2012
  Messages: 224
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na bado watazidi kuchanganyikiwa, wananchi wamechoka kuwakamata ni kumwaga petrol madhara ni makubwa wanyonge wapo na Mungu hawashindwi.
   
 18. wijei

  wijei JF-Expert Member

  #18
  Sep 22, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 469
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  kama unaona kuzomea sio ustaarabu,ngoja tutaanza kuwarushia nyanya au mayai viza.LIWALO NA LIWE
   
 19. Muangila

  Muangila JF-Expert Member

  #19
  Sep 22, 2012
  Joined: Feb 24, 2010
  Messages: 1,854
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  kungekuwepo na jinsi ya kukuzomea wewe ningekuzomea ,tambua kuwa watu walikuja kusikiliza point sio ujinga wala propaganda za kisiasa
  angetaka aczomewe angongea ukweli,uliwahi kuona wapi kwenye mkutano wa viongozi msikilzaji anasimama kupingana na anayehutubia kwa hoja hata kama unaosemwa ni uongo viva wana mwanza.
   
 20. B

  Bubona JF-Expert Member

  #20
  Sep 22, 2012
  Joined: Aug 31, 2011
  Messages: 449
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Watawala wa kidemokrasia wenye fikra za kifalme!!
   
Loading...