mzozaji
JF-Expert Member
- Jul 28, 2010
- 255
- 13
Wazee kama mtakuwa mlisikiliza mdaharo wa Mbowe na Hamadi Rashidi mtakuwa mmemsikia Mh Hamadi Rashidi akisema kuna mtu alimwambia kuwa alibadili jina lake ili asijulikane dini gani ndio akipigiwa kura na kushida. Nadhani huyu jamaa anatufanya vilaza sana kuwa hapa bara watu huwa hatujuani. Hivi yeye mpaka leo anaamini majina yana maana sana ya kumtambulisha mtu huku kwetu kuwa ni dini gani? Mimi naamini kabisa watanzania hawatumii majina kumtambua mtu ni dini gani ila tunajuana siku nyingi sana kuwa fulani ni muumini wa dini gani. Sijui hayo madai yake yana malengo gani? Ila nashukuru Mbowe alimjibu kwa busara sana kuwa hakuna mtu anaweza pigiwa kura na dini moja akashinda uchaguzi.