mFuKuZa nDoTo
JF-Expert Member
- Jan 17, 2021
- 492
- 635
Wakuu, Poleni na majukumu ya kila siku, nisiwe na maneno mengi naomba nijikite moja kwa moja kwenye mada husika. Kama kichwa cha uzi kinavyojieleza, binafsi kadri siku zinavyosonga najikuta nahusudu zaidi uafrika na kutupia mbali uzungu.
Spirit hii imeanza kunikaa kwa kiasi cha kutisha lakini kinachonipa raha sana. Unapozungumzia kuachana na uzungu watu wengi huja na hoja mbalimbali ambazo mara zote kwangu huwa naona hazina mashiko, mfano mtu anasema kama hutaki uzungu basi acha kutumia simu zao, acha kuvaa nguo zao, acha kupanda magari yao, usitumie kijiko nk.
Siwezi kuacha kutumia simu kwa sababu hata wazungu wasingekuja bado tungefika huku maana ni maendeleo ya kiteknolojia na ikumbukwe tulikuwa na teknolojia yetu, viwanda, imani na mfumo wetu wa elimu ambapo walilazimika kuviua ili kunyanyua vyao. Kwahiyo hata wasingekuja bado tungetransform kutoka kuvaa magome na kuvaa nguo, tungeacha punda na kuendesha magari tena pengine tungekuwa mbali zaidi.
Hivyo Basi, kwa mtazamo wangu (Narudia tena KWA MTAZAMO WANGU...maana kuna watumwa wa kifikra watadandia tu mjadala utafikiri tunapangiana) nikaona vita kubwa nielekeze katika mfumo wao wa kiimani hasa kuabudu, huko nilishafanikiwa kuachana na dini za kimapokeo na niko very proud kufanikisha hilo.
Pili niliamua kuachana na majina ya kizungu, kwa kuwa mimi sio mtu wa maneno bali vitendo nilianza kwa kuwapa wanangu majina ya asili ya kabila langu, nikishindwa kabisa nitawaita majina ya kiswahili. Kilichonishangaza kila mmoja ananishangaa kijana kabisa naita majina ya ajabu watoto na kuna majina mazuri kabisa ya kizungu, Nikiri wazi kabisa hili suala lilinisikitisha kuliko kawaida na kila nikitembea bado linavinjari kichwani kwangu, ni kwa kiwango gani waafrika tumekuwa malofa na wapumbavu kiasi hiki, Yaani kuna mtu mweusi kona moja ya Afrika katika zama hizi anaamini jina la kizungu ni bora kuliko la kiswahili.
Sasa nijielekeze kwenye hitaji la uzi huu, nina majina matatu, langu la kilugha, la katikati la kizungu, la mwisho la kilugha
Shida iko hapo katikati, hilo jina linanikera mno, silipendi kabisa kwahiyo naomba msaada wenu juu ya hatua ya kuchukua katika haya
(A)
Je, kuna haja ya kumjulisha mwenye jina?(Mzazi)
Je, anaweza kukubali?
Je, akikataa naweza kulazimisha?
Je, nikilazimisha naweza kupatwa na laana?
(B)
Naomba kuelekezwa hatua za kisheria kwa ujumla, gharama na muda wa kutimia kwa jambo
Nawasilisha.