Uporaji BPL, kashfa kubwa ya deep state Tanzania

DaveSave

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
440
634
MACHI 14, 2017, ilikuwa Jumanne. Uvamizi kama Navy Seal ya Marekani kwenye kasri tengwa, Abbottabad, Pakistan. Sinema ya kumuua Osama bin Laden.

Ilikuwa mchana, saa 7. “Watu wote mliopo ndani tokeni nje," sauti iliamrisha.

“Kuna nini tena?" ni swali-mshangao kwa kila mmoja.

Mwanamke, mama, alijitambulisha kuwa mwakilishi wa Ikulu, akatoa utambulisho wa jumla: “Vyombo vyote vya dola vipo hapa. Mnatakiwa muondoke.”

Ni mwanzo wa uporaji wa kiwanda cha uchapaji, kinachomilikiwa na Kampuni ya Business Printers Ltd (BPL), kilichopo Lugoda, Ilala.

“Sababu ya uvamizi huu ni nini?” Mmoja wa wamiliki wa BPL, Rashidi Mbuguni (marehemu), aliuliza.

“Mnadaiwa Shilingi bilioni tano na milioni mia tatu hamsini,” Mama wa Ikulu alijibu.

“Bilioni tano? Hapana, labda mtakuwa mmechanganya. Sisi hatudaiwi deni lote hilo,” Rashidi alijibu.

“Mnadaiwa bilioni tano. Kama mnazo lipeni hapahapa. Vinginevyo, tokeni wote. Tunataka kuuza kiwanda kufidia deni,” Mama wa Ikulu aliendelea.

“Deni letu lilikuwa bilioni moja na milioni mia nne. Baada ya msamaha lingebaki milioni 600, na jana tulikuwa TRA, tulikubaliana jinsi ya kufanya malipo kwa awamu. Hizo bilioni tano zimetoka wapi?” alihoji Rashidi.

Hakuna aliyemjibu Rashidi. Uamuzi ulikuwa mmoja; kuchukua kiwanda. Maswali na maelezo havikuwa na nafasi. Wafanyakazi walisimamiwa kuondoka bila kubeba chochote. Angalau wanawake mikoba yao, ingawa ilipekuliwa.

Pandashuka kufuatilia haki TRA, ikawa kuipiga deki bahari. “Sisi hatuhusiki, waliofunga kiwanda chenu ni Task Force,” majibu kutoka TRA.

Wamiliki wa kiwanda, Rashidi, Gertrude Nyaulawa (mke wa marehemu Richard Nyaulawa), Omar Holaki na familia zao, walibisha hodi kila mlango walioelekezwa na waliodhani ungefanikisha haki.

Kila mahali walipoingia walikutana na majibu ya kukatisha tamaa. Task Force lilikuwa zimwi. Lilitafuna hadi mifupa. Wengi walifilisiwa mali zao na vilio vyao vikabaki machozi ya samaki.

Simu ya namba ngeni ikaingia kwa Zayed (si jina halisi). Ni ofisa wa BPL, na mtoto wa Rashidi.

“Mkurugenzi Mkuu Idara ya Usalama wa Taifa, atawasaidia kupata kiwanda chenu, nakuombea miadi mkutane,” mtu (mwanaume) wa ile simu ya namba ngeni, alimweleza Zayed.

Jina la aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu Tiss, Modestus Kapilimba, Baba Mchungaji, linaingia kwenye sakata.

Kikao cha kwanza baina ya Zayed na Kapilimba kikawa na matumaini makubwa.

Kapilimba, Balozi wa Tanzania Namibia, alimweleza Zayed dhamira ya Tiss kutumia kiwanda cha BPL kwa kazi maalum.

Mosi; Kapilimba alimwambia Zayed kuwa Tiss ingenunua kiwanda cha BPL.

Pili; Tiss wangefanya mahesabu na uongozi wa BPL, halafu wangetumia kiwanda chao mpaka pale deni wanalodaiwa lingeisha.

Swali upande wa BPL likawa, deni lipi Tiss wangelitumia? BPL kulingana na hesabu zao na TRA deni ni Sh1.4 bilioni. Task Force walitoa deni jipya, Sh5.35 bilioni ambalo BPL hawalitambui, na halipo TRA.

Balozi Kapilimba alitoa wazo la kuona na kukagua kiwanda kabla ya kuketi mezani na wamiliki wa BTL.

Lugoda ikatanda maofisa Usalama wa Taifa. Mkurugenzi Mkuu Tiss alikuwa anakwenda kuona na kukagua kiwanda cha BPL.

Balozi Kapilimba anavutiwa na kiwanda. Mashine zake zilikuwa bado mpya. Si kitambo kirefu tangu mitambo mipya ifungwe. BPL walichukua mkopo benki za NMB na ECO kuboresha kiwanda chao.

Matarajio makubwa kwao yalikuwa kufanya biashara na wangelipa mkopo bila tatizo. Sasa, baada ya kuchukua mkopo na kufunga mashine mpya, kiwanda kikavamiwa na Task Force.

“Inabidi tukifanyie majaribio,” ni wazo kutoka kwa Kapilimba.

Majaribio yakafanyika. Gazeti la Majira, mali ya Business Times Limited (BTL), likateuliwa kuwa chapisho la kipimo, yaani specimen.

“Hiki kiwanda kitatufaa sana,” Kapilimba alifurahia ufanisi wa kiwanda cha BPL, aliporidhishwa na ubora wa gazeti la Majira baada ya kuchapwa.

Matarajio ya wamiliki yalikuwa, baada ya Balozi Kapilimba kuridhishwa na ubora wa kiwanda, yangefuata mazungumzo kama dhamira ilivyotamkwa awali na Mkurugenzi Mkuu huyo wa zamani wa Tiss.

Baada ya Kapilimba kuridhika na ubora, kiwanda kikafunguliwa kuanza kazi. Magazeti yaliyoitwa ya mkakati yakaanza kuchapwa. Yale magazeti ya mwanaharakati huru, Cyprian Musiba. Tanzanite na ukoo wake!

Ni yale magazeti ya kushambulia watu na kumsifu aliyekuwa mpendwa Rais wetu, John Magufuli.

Magazeti yaleyale yaliyotumika kuwashughulikia akina mzee Abdulrahman Kinana, Yusuf Makamba na al-marhum Bernard Membe.

Magazeti yaliyowapa majina mbaya, January Makamba, Nape Nnauye, Zitto Kabwe, Tundu Lissu, Freeman Mbowe na wengine wengi. Wasisahaulike Fatma Karume na Maria Sarungi.

Ndio kazi maalum aliyoisema Kapilimba. Kuchapa magazeti ya kumsifu na kumpamba Magufuli, halafu kuwachawafua na kuwapa majina mabaya wengine. Magazeti ya kimkakati. Ndivyo yaliitwa!

“Tutanunua kiwanda kwa Sh10 bilioni, ila hatutaki kuandikiana mikataba,” Tiss walijipangia bei, wakatoa na masharti. Wamiliki wa BPL wakapewa Sh300 milioni za kianzio. Fedha zilikuwa taslimu.

Baada ya hapo, kila ahadi iliyeyuka. Si kununua kiwanda wala kuchapa kwa makubaliano mpaka pale deni lote lingelipwa.

Safari za Zayed makao makuu ya Tiss kumwona Kapilimba, ni mgaagaa na upwa bila wali, seuze mboga. Njoo kesho ikazaa kesho. Wakati mwingine mpaka usiku wa Manani anangoja kuonana na Kapilimba na akaambulia ahadi.

Kisha, simu za Zayed zikawa hazipokelewi tena. Ujumbe nao haukujibiwa. Kipindi chote kiwanda cha BPL kiliendelea kufanya hiyo kazi maalum. Kuchapa magazeti ya kimkakati. Hata magazeti ya chama, Uhuru na Mzalendo. Kadhalika ya Serikali, Sunday News, Daily News na Habari Leo.

Holaki, mmiliki mwenza wa BPL, akaona Zayed ni kijana, ngoja yeye mtu mzima awasiliane na Kapilimba, pengine wangeelewana. Hakupata matokeo.

Kiwanda hakikupigwa mnada ili kufidia deni lililotajwa, wala hakikutaifishwa kwa mujibu wa sheria, bali kilitekwa na kuendeshwa na Tiss kibabe. Wamiliki wakabaki katikati ya mateso.

Zingatia, Task Force walivamia kiwanda kipindi ambacho BPL walitoka kukopa benki za NMB na ECO ili kuboresha na kukiendeleza kiwanda chao.

Sasa, wakiwa hawajui wafanye nini kuhusu hatma ya kiwanda chao, presha za madeni benki zikawazonga. Ikabidi wauze mali zao nyingine, hadi nyumba ili kupunguza makali ya madeni.

Simulizi ya uporaji kiwanda cha BPL sio hadithi ya dhalimu na dhalili, bali ni kielelezo cha nyakati za unyang'anyi uliovunja dari zote. Waliopaswa kutunza na kulinda haki, wakawa waporaji.

Idara ya Usalama wa Taifa, ikageuka Idara ya Uharibifu wa Taifa. Ikashiriki unyang'anyi wa kiwanda cha BPL. Haitoshi, ikakiendesha na kusimamia uchapaji wa magazeti yenye taswira ya uchonganishi kwa taifa.

Uporaji wa BPL ni kashfa inayogusa moja kwa moja Ikulu. Mpango mkuu ulilenga kumpamba Rais Magufuli na kuwapa majina mabaya waliokuwa kinyume naye.

Kutoka Machi 2017, kiwanda kilipoporwa, ukafuata mwingine, ukawadia 2019. Septemba 12, ikawa siku ya mwisho Kapilimba kuhudumia Tiss. Diwani Athuman aliteuliwa na kuapishwa kuwa Mkurugenzi Mkuu.

Kutoka kwa Kapilimba na kuingia Diwani, hakukuwa na mageuzi yoyote kuhusu BPL. Kiwanda kiliendelea kukaliwa na Tiss. Zaidi, Novemba 24, 2019, ulifanyika Uchaguzi Serikali za Mitaa.

Nyaraka zote za uchaguzi hadi karatasi za kura, zilichapapwa BPL. Mabilioni ya fedha yalitengwa kwa ajili ya kufanikisha Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, ila makaratasi ya kupigia kura na nyaraka nyingine, vikachapwa BPL, bure.

Uchaguzi Mkuu 2020, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), ilitangaza matumizi ya Sh331 bilioni kugharamia uchaguzi. Nyaraka zote na karatasi za kupigia kura, vilichapwa BPL, pasipo wamiliki kulipwa chochote.

Dhuluma ya BPL, unaweza kudhani mapitio ya filamu ya Andha Kanoon au The Godfather. Serikali ya watu, ilisaliti na kuongoza kiharamia. Ni Thugocracy, kama alivyoandika David Feddoso, kwenye kitabu “Gangster Government”.

BPL ni kashfa kubwa ya “Deep State” kuwahi kutokea Tanzania. Idara ya Usalama kusimamia na kufadhili machapisho ya propaganda za kisiasa. Kuhusika moja kwa moja kufanya unyang'anyi. Ikulu ikiwa ngao ya kila tendo.

Ni simulizi ya aibu kuwa ulipita wakati Jamhuri ya Tanzania, TRA, ilifungwa mnyororo. Task Force, wakapewa jukumu kibabe. Undava ukatumika kuliko sheria. Unanyang'anywa mali, unasindikizwa na maneno “nenda popote!”

Kitisho kikuu kikawa kupewa kesi za uhujumu uchumi. Waliotii kulipa madeni na faini za kimchongo, fedha zililipwa kwenye akaunti za watu binafsi. Akaunti za Deep State Gangsters.

Machi 17, 2021, taifa lilitangaziwa kifo cha Rais Magufuli. Machi 19, 2021, Rais Samia Suluhu Hassan alikula kiapo. Hayakuwa mabadiliko kutoka rais hadi rais, bali mtazamo wa Ikulu ulibadilika.

“Sitaki dhuluma,” alisema Rais Samia.

Juni 2021, miezi mitatu baada ya Rais Samia kula kiapo, Tiss walijiondoa BPL. Kuanzia hapo, yale magazeti ya kimkakati, Tanzanite na kabila lake, yalipotea. Kiwanda cha kuchapa dezo-dezo kilifungwa.

Si hivyo tu, mradi wa magazeti ya kimkakati uligharimu fedha nyingi. Mishahara ya wafanyakazi, nyumba, magari hadi walinzi binafsi wa akina Musiba. Bajeti ya ‘misheni' hiyo ilikosekana.

Ndio sababu baada ya Samia kuingia ofisini, likaibuka zogo la madai dhidi ya Musiba. Wafanyakazi wa Tanzanite walimfikisha bosi wao kwenye vyombo vya sheria kudai stahiki.

Imezidi miaka miwili tangu Magufuli alipofariki dunia na kiwanda kusitisha shughuli, zilizoitwa za kimkakati, ufumbuzi wa BPL bado kizungumkuti.

Ni zaidi ya miaka sita tangu wamiliki wa BPL waliponyang'anywa haki yao. Kama ni madai, TRA wangeweza kukipiga mnada lakini hawakufanya hivyo. Kikatumika kufanya kazi waliyoiita ya kimkakati chini ya Tiss, kinyume na sheria.

Wiki mbili zilizopita, Rashidi, mmoja wa wamiliki wa BPL, alipokea faradhi ya kifo. Alisota miaka sita pasipo kuona haki na ameondoka kabla haki haijatendeka.

“Justice delayed is justice denied” – “Haki yenye kucheleweshwa ni haki iliyonyimwa.” Ni moja ya nguzo za msingi mkuu wa maadili ya kisheria (general maxim). Tutafakari hilo tukimwombea dua Rashidi katika safari yake mbele ya haki.

Kwako Rais Samia; Jeshi (JWTZ) ni mwili wa nchi. Vyombo vingine chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani, Polisi, Magereza, Uhamiaji, Zimamoto na kadhalika, ni afya ya ndani kwenye mwili wa nchi.

Tiss, ni moyo kwenye mwili wa nchi. Wazo kuu la Tiss kuendeshwa kutokea Ofisi ya Rais, ni mwafaka sana. Hivyo, kwa kuwa ni moyo, Tiss haipaswi kuingizwa kwenye makandokando ya siasa na dhuluma za mali za raia. Nchi itakufa!

Kwa Mkurugenzi Mkuu Tiss, Said Massoro, Idara ya Usalama inapaswa kufanya masahihisho kwa mambo yaliyotokea hususan BPL na mengine kama hayo, ibaki kuwa chombo moyo wa nchi, kama ulivyo msingi wa kuanzishwa kwake.

Ndimi Luqman MALOTO.

FB_IMG_1690535269130.jpg
 
Ulikuwa ubaya, lakini kwa nini uletwe leo?

Hebu tujibiwe ya bandarini na ule mkataba wa hovyo kwanza, kama kuna ubaya, wahanga waende mahakamani kudai fidia.

Nina wasiwasi, hii isijekuwa mbinu nyingine ya chawa wa mama kutumiwa na bosi wao ili kutusahaulisha yale mabaya ya bandarini, kila jambo lijibiwe kwa wakati wake.
 
Nadhani hoja hapa ni kwamba mmojawapo wa wamiliki amefariki wiki mbili zilizopita bila ya kupata haki yake.

Luqman ameandika kuonesha kwamba wapo waliodhulumiwa wakati Magufuli akiwa Rais na wanakufa bila ya kupata haki zao.

Dunia haiwezi kusimama kisa tunajadili bandari. Acha mambo mengine nayo yaendelee.
 
Anataka kutuhamisha.
 
Unafanya vizuri kuweka kumbukumbu za haya kwenye historia yetu. Bila kazi kama hizi watoto wetu watakuja kusomeshwa uongo
Kama tulivyomuimba Idd Amin enzi tukiwa SM miaka ya 80s kwamba alikuwa mtu mbaya kuliko wooote kabisa, anakula watu, anakusanya walemavu na kuwatia ziwani nk.
"Idd Amin akifa, Mimi siwezi Julia, nitamtupa Kagera, awe chakula cha mamba." Kumbe kuna mazuri mengi aliyefanya kwa wananchi wake.

Sent from my SM-G977B using JamiiForums mobile app
 
Ila Kipilimba alikuwa mtu wa ajabu kweli. Afadhali Diwani, roho mbaya lakini ni mtu wa haki na mzalendo kote alikopita.

Ubaya wa awamu ya JPM ulisababishwa na enablers kama akina Kipilimba na Sirro. JPM alikuwa kiongozi mzuri, mwenye maono ya mbali na uchungu na nchi.

Vyombo vya ulinzi na usalama vilipaswa kumsaidia pale kwenye mapungufu yake kama vile hasira na ubabe badala ya kuchochea tabia hizo. Nchi nyingine zenye watu wenye akili wanafanya hivyo.
 
Nadhani hoja hapa ni kwamba mmojawapo wa wamiliki amefariki wiki mbili zilizopita bila ya kupata haki yake.

Luqman ameandika kuonesha kwamba wapo waliodhulumiwa wakati Magufuli akiwa Rais na wanakufa bila ya kupata haki zao.

Dunia haiwezi kusimama kisa tunajadili bandari. Acha mambo mengine nayo yaendelee.
Asante kwa kumpa za uso huyo anayedhani bila bandari hakuna maisha na anafanya hivyo kisa kahongwa
 
MACHI 14, 2017, ilikuwa Jumanne. Uvamizi kama Navy Seal ya Marekani kwenye kasri tengwa, Abbottabad, Pakistan. Sinema ya kumuua Osama bin Laden.

Ilikuwa mchana, saa 7. “Watu wote mliopo ndani tokeni nje," sauti iliamrisha.

“Kuna nini tena?" ni swali-mshangao kwa kila mmoja.

Mwanamke, mama, alijitambulisha kuwa mwakilishi wa Ikulu, akatoa utambulisho wa jumla: “Vyombo vyote vya dola vipo hapa. Mnatakiwa muondoke.”

Ni mwanzo wa uporaji wa kiwanda cha uchapaji, kinachomilikiwa na Kampuni ya Business Printers Ltd (BPL), kilichopo Lugoda, Ilala.

“Sababu ya uvamizi huu ni nini?” Mmoja wa wamiliki wa BPL, Rashidi Mbuguni (marehemu), aliuliza.

“Mnadaiwa Shilingi bilioni tano na milioni mia tatu hamsini,” Mama wa Ikulu alijibu.

“Bilioni tano? Hapana, labda mtakuwa mmechanganya. Sisi hatudaiwi deni lote hilo,” Rashidi alijibu.

“Mnadaiwa bilioni tano. Kama mnazo lipeni hapahapa. Vinginevyo, tokeni wote. Tunataka kuuza kiwanda kufidia deni,” Mama wa Ikulu aliendelea.

“Deni letu lilikuwa bilioni moja na milioni mia nne. Baada ya msamaha lingebaki milioni 600, na jana tulikuwa TRA, tulikubaliana jinsi ya kufanya malipo kwa awamu. Hizo bilioni tano zimetoka wapi?” alihoji Rashidi.

Hakuna aliyemjibu Rashidi. Uamuzi ulikuwa mmoja; kuchukua kiwanda. Maswali na maelezo havikuwa na nafasi. Wafanyakazi walisimamiwa kuondoka bila kubeba chochote. Angalau wanawake mikoba yao, ingawa ilipekuliwa.

Pandashuka kufuatilia haki TRA, ikawa kuipiga deki bahari. “Sisi hatuhusiki, waliofunga kiwanda chenu ni Task Force,” majibu kutoka TRA.

Wamiliki wa kiwanda, Rashidi, Gertrude Nyaulawa (mke wa marehemu Richard Nyaulawa), Omar Holaki na familia zao, walibisha hodi kila mlango walioelekezwa na waliodhani ungefanikisha haki.

Kila mahali walipoingia walikutana na majibu ya kukatisha tamaa. Task Force lilikuwa zimwi. Lilitafuna hadi mifupa. Wengi walifilisiwa mali zao na vilio vyao vikabaki machozi ya samaki.

Simu ya namba ngeni ikaingia kwa Zayed (si jina halisi). Ni ofisa wa BPL, na mtoto wa Rashidi.

“Mkurugenzi Mkuu Idara ya Usalama wa Taifa, atawasaidia kupata kiwanda chenu, nakuombea miadi mkutane,” mtu (mwanaume) wa ile simu ya namba ngeni, alimweleza Zayed.

Jina la aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu Tiss, Modestus Kapilimba, Baba Mchungaji, linaingia kwenye sakata.

Kikao cha kwanza baina ya Zayed na Kapilimba kikawa na matumaini makubwa.

Kapilimba, Balozi wa Tanzania Namibia, alimweleza Zayed dhamira ya Tiss kutumia kiwanda cha BPL kwa kazi maalum.

Mosi; Kapilimba alimwambia Zayed kuwa Tiss ingenunua kiwanda cha BPL.

Pili; Tiss wangefanya mahesabu na uongozi wa BPL, halafu wangetumia kiwanda chao mpaka pale deni wanalodaiwa lingeisha.

Swali upande wa BPL likawa, deni lipi Tiss wangelitumia? BPL kulingana na hesabu zao na TRA deni ni Sh1.4 bilioni. Task Force walitoa deni jipya, Sh5.35 bilioni ambalo BPL hawalitambui, na halipo TRA.

Balozi Kapilimba alitoa wazo la kuona na kukagua kiwanda kabla ya kuketi mezani na wamiliki wa BTL.

Lugoda ikatanda maofisa Usalama wa Taifa. Mkurugenzi Mkuu Tiss alikuwa anakwenda kuona na kukagua kiwanda cha BPL.

Balozi Kapilimba anavutiwa na kiwanda. Mashine zake zilikuwa bado mpya. Si kitambo kirefu tangu mitambo mipya ifungwe. BPL walichukua mkopo benki za NMB na ECO kuboresha kiwanda chao.

Matarajio makubwa kwao yalikuwa kufanya biashara na wangelipa mkopo bila tatizo. Sasa, baada ya kuchukua mkopo na kufunga mashine mpya, kiwanda kikavamiwa na Task Force.

“Inabidi tukifanyie majaribio,” ni wazo kutoka kwa Kapilimba.

Majaribio yakafanyika. Gazeti la Majira, mali ya Business Times Limited (BTL), likateuliwa kuwa chapisho la kipimo, yaani specimen.

“Hiki kiwanda kitatufaa sana,” Kapilimba alifurahia ufanisi wa kiwanda cha BPL, aliporidhishwa na ubora wa gazeti la Majira baada ya kuchapwa.

Matarajio ya wamiliki yalikuwa, baada ya Balozi Kapilimba kuridhishwa na ubora wa kiwanda, yangefuata mazungumzo kama dhamira ilivyotamkwa awali na Mkurugenzi Mkuu huyo wa zamani wa Tiss.

Baada ya Kapilimba kuridhika na ubora, kiwanda kikafunguliwa kuanza kazi. Magazeti yaliyoitwa ya mkakati yakaanza kuchapwa. Yale magazeti ya mwanaharakati huru, Cyprian Musiba. Tanzanite na ukoo wake!

Ni yale magazeti ya kushambulia watu na kumsifu aliyekuwa mpendwa Rais wetu, John Magufuli.

Magazeti yaleyale yaliyotumika kuwashughulikia akina mzee Abdulrahman Kinana, Yusuf Makamba na al-marhum Bernard Membe.

Magazeti yaliyowapa majina mbaya, January Makamba, Nape Nnauye, Zitto Kabwe, Tundu Lissu, Freeman Mbowe na wengine wengi. Wasisahaulike Fatma Karume na Maria Sarungi.

Ndio kazi maalum aliyoisema Kapilimba. Kuchapa magazeti ya kumsifu na kumpamba Magufuli, halafu kuwachawafua na kuwapa majina mabaya wengine. Magazeti ya kimkakati. Ndivyo yaliitwa!

“Tutanunua kiwanda kwa Sh10 bilioni, ila hatutaki kuandikiana mikataba,” Tiss walijipangia bei, wakatoa na masharti. Wamiliki wa BPL wakapewa Sh300 milioni za kianzio. Fedha zilikuwa taslimu.

Baada ya hapo, kila ahadi iliyeyuka. Si kununua kiwanda wala kuchapa kwa makubaliano mpaka pale deni lote lingelipwa.

Safari za Zayed makao makuu ya Tiss kumwona Kapilimba, ni mgaagaa na upwa bila wali, seuze mboga. Njoo kesho ikazaa kesho. Wakati mwingine mpaka usiku wa Manani anangoja kuonana na Kapilimba na akaambulia ahadi.

Kisha, simu za Zayed zikawa hazipokelewi tena. Ujumbe nao haukujibiwa. Kipindi chote kiwanda cha BPL kiliendelea kufanya hiyo kazi maalum. Kuchapa magazeti ya kimkakati. Hata magazeti ya chama, Uhuru na Mzalendo. Kadhalika ya Serikali, Sunday News, Daily News na Habari Leo.

Holaki, mmiliki mwenza wa BPL, akaona Zayed ni kijana, ngoja yeye mtu mzima awasiliane na Kapilimba, pengine wangeelewana. Hakupata matokeo.

Kiwanda hakikupigwa mnada ili kufidia deni lililotajwa, wala hakikutaifishwa kwa mujibu wa sheria, bali kilitekwa na kuendeshwa na Tiss kibabe. Wamiliki wakabaki katikati ya mateso.

Zingatia, Task Force walivamia kiwanda kipindi ambacho BPL walitoka kukopa benki za NMB na ECO ili kuboresha na kukiendeleza kiwanda chao.

Sasa, wakiwa hawajui wafanye nini kuhusu hatma ya kiwanda chao, presha za madeni benki zikawazonga. Ikabidi wauze mali zao nyingine, hadi nyumba ili kupunguza makali ya madeni.

Simulizi ya uporaji kiwanda cha BPL sio hadithi ya dhalimu na dhalili, bali ni kielelezo cha nyakati za unyang'anyi uliovunja dari zote. Waliopaswa kutunza na kulinda haki, wakawa waporaji.

Idara ya Usalama wa Taifa, ikageuka Idara ya Uharibifu wa Taifa. Ikashiriki unyang'anyi wa kiwanda cha BPL. Haitoshi, ikakiendesha na kusimamia uchapaji wa magazeti yenye taswira ya uchonganishi kwa taifa.

Uporaji wa BPL ni kashfa inayogusa moja kwa moja Ikulu. Mpango mkuu ulilenga kumpamba Rais Magufuli na kuwapa majina mabaya waliokuwa kinyume naye.

Kutoka Machi 2017, kiwanda kilipoporwa, ukafuata mwingine, ukawadia 2019. Septemba 12, ikawa siku ya mwisho Kapilimba kuhudumia Tiss. Diwani Athuman aliteuliwa na kuapishwa kuwa Mkurugenzi Mkuu.

Kutoka kwa Kapilimba na kuingia Diwani, hakukuwa na mageuzi yoyote kuhusu BPL. Kiwanda kiliendelea kukaliwa na Tiss. Zaidi, Novemba 24, 2019, ulifanyika Uchaguzi Serikali za Mitaa.

Nyaraka zote za uchaguzi hadi karatasi za kura, zilichapapwa BPL. Mabilioni ya fedha yalitengwa kwa ajili ya kufanikisha Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, ila makaratasi ya kupigia kura na nyaraka nyingine, vikachapwa BPL, bure.

Uchaguzi Mkuu 2020, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), ilitangaza matumizi ya Sh331 bilioni kugharamia uchaguzi. Nyaraka zote na karatasi za kupigia kura, vilichapwa BPL, pasipo wamiliki kulipwa chochote.

Dhuluma ya BPL, unaweza kudhani mapitio ya filamu ya Andha Kanoon au The Godfather. Serikali ya watu, ilisaliti na kuongoza kiharamia. Ni Thugocracy, kama alivyoandika David Feddoso, kwenye kitabu “Gangster Government”.

BPL ni kashfa kubwa ya “Deep State” kuwahi kutokea Tanzania. Idara ya Usalama kusimamia na kufadhili machapisho ya propaganda za kisiasa. Kuhusika moja kwa moja kufanya unyang'anyi. Ikulu ikiwa ngao ya kila tendo.

Ni simulizi ya aibu kuwa ulipita wakati Jamhuri ya Tanzania, TRA, ilifungwa mnyororo. Task Force, wakapewa jukumu kibabe. Undava ukatumika kuliko sheria. Unanyang'anywa mali, unasindikizwa na maneno “nenda popote!”

Kitisho kikuu kikawa kupewa kesi za uhujumu uchumi. Waliotii kulipa madeni na faini za kimchongo, fedha zililipwa kwenye akaunti za watu binafsi. Akaunti za Deep State Gangsters.

Machi 17, 2021, taifa lilitangaziwa kifo cha Rais Magufuli. Machi 19, 2021, Rais Samia Suluhu Hassan alikula kiapo. Hayakuwa mabadiliko kutoka rais hadi rais, bali mtazamo wa Ikulu ulibadilika.

“Sitaki dhuluma,” alisema Rais Samia.

Juni 2021, miezi mitatu baada ya Rais Samia kula kiapo, Tiss walijiondoa BPL. Kuanzia hapo, yale magazeti ya kimkakati, Tanzanite na kabila lake, yalipotea. Kiwanda cha kuchapa dezo-dezo kilifungwa.

Si hivyo tu, mradi wa magazeti ya kimkakati uligharimu fedha nyingi. Mishahara ya wafanyakazi, nyumba, magari hadi walinzi binafsi wa akina Musiba. Bajeti ya ‘misheni' hiyo ilikosekana.

Ndio sababu baada ya Samia kuingia ofisini, likaibuka zogo la madai dhidi ya Musiba. Wafanyakazi wa Tanzanite walimfikisha bosi wao kwenye vyombo vya sheria kudai stahiki.

Imezidi miaka miwili tangu Magufuli alipofariki dunia na kiwanda kusitisha shughuli, zilizoitwa za kimkakati, ufumbuzi wa BPL bado kizungumkuti.

Ni zaidi ya miaka sita tangu wamiliki wa BPL waliponyang'anywa haki yao. Kama ni madai, TRA wangeweza kukipiga mnada lakini hawakufanya hivyo. Kikatumika kufanya kazi waliyoiita ya kimkakati chini ya Tiss, kinyume na sheria.

Wiki mbili zilizopita, Rashidi, mmoja wa wamiliki wa BPL, alipokea faradhi ya kifo. Alisota miaka sita pasipo kuona haki na ameondoka kabla haki haijatendeka.

“Justice delayed is justice denied” – “Haki yenye kucheleweshwa ni haki iliyonyimwa.” Ni moja ya nguzo za msingi mkuu wa maadili ya kisheria (general maxim). Tutafakari hilo tukimwombea dua Rashidi katika safari yake mbele ya haki.

Kwako Rais Samia; Jeshi (JWTZ) ni mwili wa nchi. Vyombo vingine chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani, Polisi, Magereza, Uhamiaji, Zimamoto na kadhalika, ni afya ya ndani kwenye mwili wa nchi.

Tiss, ni moyo kwenye mwili wa nchi. Wazo kuu la Tiss kuendeshwa kutokea Ofisi ya Rais, ni mwafaka sana. Hivyo, kwa kuwa ni moyo, Tiss haipaswi kuingizwa kwenye makandokando ya siasa na dhuluma za mali za raia. Nchi itakufa!

Kwa Mkurugenzi Mkuu Tiss, Said Massoro, Idara ya Usalama inapaswa kufanya masahihisho kwa mambo yaliyotokea hususan BPL na mengine kama hayo, ibaki kuwa chombo moyo wa nchi, kama ulivyo msingi wa kuanzishwa kwake.

Ndimi Luqman MALOTO.

Jjiwe alikuwa shetani mmaluuni
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom