Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 2,397
- 3,884
Nimejaribu kuichunguza karatasi ya kupigia kura ya Urais wa JMT katika uchaguzi huu uliopita, na nina machache ya kuchangia.
Nianze kwanza kwa kusema karatasi ya kupigia kura inabidi kuichukulia kama ni nyaraka muhimu sana. Uzito wa kipekee unahitajika katika kuibuni, kuichapisha, kuisambaza na kuihifadhi. Kwa nilichokiona katika uchaguzi huu wa 2020, sidhani kama lolote kati ya hayo yalizingatiwa. Najua nayasema haya katika nyakati na mazingira ambayo inaonyesha kama wenye mamlaka wameamua waitupe mkono mfumo wa demokrasia na siasa safi, lakini matumaini bado yapo kuwa siku yaja ambayo tutarudi nyuma na kujirekebisha.
Ngoja sasa niorodheshe baadhi ya vitu nilivyoona katika karatasi hii:
Nimalizie tu kwa kusema, ukiacha mapungufu haya niliyotaja hapo juu ambayo nadhani mengine yalifanywa kama maamuzi ya makusudi, sidhani kama hii ikaratasi imekuwa designed na professional designing na printing company inayojitambua. Inaonyesha ni kama karatasi ambayo imetengenezwa katika kaduka ka stationery na dada mmoja ambaye pia anauza vocha za tigo. Maandishi ya majina hayana uwiano, baadhi yako juu zaidi, mengine katikati, mengine kushoto zaidi. Halafu unaniambia kuna mabilioni yametumika hapa kwa kazi hii?
Tanzania ni urithi wetu sote, hakuna atakayeweza kulibadilisha hilo.

- Picha ya mgombea wa Urais inatakiwa ndiyo ianze kushoto na ya mgombea mwenza ifuate, kinyume na walivyofanya.
- Pia nitazungumzia 'inconsistencies' katika karatasi hii. Hapa namaanaisha jambo moja kufanyika kwa mgombea mmoja lakini halikufanyika kwa mgombea mwingine. Nitatoa mifano michache:
- Mgombea mwenza wa CCM, Samia Suluhu Hassan ametajwa kwanza kwa jina la kwanza. Ukiangalia Mgombea mwenza wa CHADEMA, ametajwa kwanza kwa jina lake la Mwisho. Sijajua kwa wagombea wengine kwa sababu siwafahamu vizuri.
- Mgombea wa CCM, John Magufuli ametajwa kwanza kama Dkt. wakati mgombea wa CUF, title yake ya Prof. haikuwekwa.
- Kwenye majina ya vyama, font size hazifanani na zingine kama ziko bold wakati zingine haziko bold, mfano za ACT, CHADEMA, CHAUMMA, etc. ni ndogo zaidi ya nyingine.
- Hakuna haja wala umuhimu wa kurudia title ya 'CHAMA', 'MGOMBEA UMAKAMU WA RAIS', 'MGOMBEA URAIS' wala 'ALAMA' kwa kila mgombea. Hizi titles zingewekwa tu juu pale zikiwa bold na maandishi makubwa zinatosha.
- Kuna hili suala lingine ambalo limeongelewa sawa la utaratibu gani ulitumika katika kuamua orodha hii ya wagombea iwekwe vipi. Ninavyokumbuka, NEC walisema ilitokana na jinsi wagombea walivyorudisha fomu zao. Hili sitaliongelea kwa sababu wote tunajua hizo zilikuwa ni geresha tu. Itoshe kusema huo siyo utaratibu wala majibu ya kisomi kwa watu walioelimika. Nadhani utaratibu sahihi ni kufuata alphabetical order ya majina ya chama au majina ya mwisho ya wagombea. Na hili liwekwe wazi katika kanuni za uchaguzi ili kuepuka 'surprises'.
- Mfano wa karatasi hii utolewe mapema zaidi, ili mapungufu yaweze kurekebishwa na maboresho kufanywa. Kama nilivyosema hapo awali, muundo wa karatasi hii utajwe wazi katika sheria kuu za uchaguzi na kusiwe na room ya kirahisi rahisi ya kuzibadilisha kama inavyofanyika sasa.
- Jukumu la kuelimisha njia sahihi za kuitumia karatasi hii libebwe na NEC wenyewe. Kuna wagombea walitoa matamko ambayo kisheria walitakiwa waadhibiwe. Kuna mmoja alinukuliwa akisema 'wewe angalia mtu wa kwanza tu hapo juu, weka tiki, wengine huko chini siyo wagombea halali'
- Karatasi ya kupigia kura iorodheshwe kama ni nyaraka muhimu sana katika nchi, Sheria itungwe ambayo itasema kuwa atakayekutwa na karatasi hii zaidi ya copy moja nje ya kituo cha kupigia kura, adhabu kali ichukuliwe dhidi yake.