Eti kati ya Nyumba na Ndege ipi ina paa?

Eti kati ya Nyumba na Ndege ipi ina paa?

Ritz

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2011
Posts
57,235
Reaction score
46,646
Wanabodi,
Najua Chit-Chat kuna vichwa makini vyenye uelewa na weledi wa hali ya juu...nisaidieni kujibu.
 
Dah!!!
BTW hiyo ni Sentensi tata Ritz.
 
Last edited by a moderator:
duh!! tungo tata hiyo.
vyote vina paa.
 
Nyumba ina paa,ndege inapaa(Tofauti kwenye nyumba kuna nafasi kati ya ina na paa wakati kwa ndege hamna nafasi kati ya ina na paa.)
 
Mkuu Ritz

Paa katika nyumba ni Jina (noun) ila Paa katika ndege ni kitendo (verb)
 
Last edited by a moderator:
Nyumba ina roof na ndege ina fly, nimepatiwa eeeh makofi tafadhali.
 
Mkuu Ritz

Paa katika nyumba ni Jina (noun) ila Paa katika ndege ni kitendo (verb)

ha haa ha! Mkuu wangu Albedo, naona umeamua kutumia kiingereza ili watu wakuelewe.
 
Last edited by a moderator:
Na kati ya Paa na Ndege ipi ina Nyumba ?
(ndoo maake pasua kwa pasua kichwa!)
 
Sidhani kama kuna utata wowote,utunzi wa sentensi zifuatazo utatofautisha;
Ndege inapaa (paa - kitenzi)
Nyumba ina paa (paa - nomino)
 
Back
Top Bottom