Hapo kuna mambo mengi sana hakuna jjbu la moja kwa moja :-
1. Inawekana mama mwenye nyumba kweli akawa anachakachua.
2. Inawezekana mlikuwa na deni wakati mnatumia mita ya kawaida sasa deni limehamishiwa kwenye LUKU kwa hivyo kila mkinunua umeme wanafidia deni lao, mara nyinyi huwa wanakata nusu ya hela unayonunulia umeme yaani kama unanunua umeme wa tshs 20,000.0 basi tshs. 10,000.0 inalipa deni na inayobaki wanakupa umeme ila kwenye stakabadhi wanaonyesha.
3.Inawezekana mmewekwa kwenye tarrif ambayo mnanunua umeme kwa bei ya juu yaani kuna tarrif 1 mpaka tarrif 4 sasa hizi zimepangwa kutokana na matumizi, kwa hivyo unit moja anavyonunua mteja wa tarrif 1 na tarrif 4 ni tofauti.
4. Yawezekana wapangaji hamuambiani ukweli watu wana heater, majiko ya umeme vifaa vinavyoyumia umeme mwingi halafu kila mtu anazuga kwamba hatumii umeme, kwa mujibu wa maelezo yako ulisema mmechangishana tshs. 5,000.0 na mkapata ths 50,000.0 ina maana kuna wapangaji 10, lakini hujaeleza ukubwa wa familia za wapangaji.
5. Mfumo wa uwekaji nyaya za nyumba haupo vizuri (wiring) yaani umeme mwingi unapotea. Pia kuwa na vifaa vingi vya umeme vichakavu kama fredge nk ukiona fredge linapiga sana kelele ujue ni umeme utumika sana, electrical energy has been converted to sound energy.