Hongera sana, tena sana kwa huyo dada kutaka kujua 'uhai' wa mume wake mtarajiwa!!.
Kuna watu waliishi uchumba kadiri ya mafundisho, wakaja kufunga ndoa. Baada tu ya kukubali "nitaishi naye kwa shida na raha", huku bado watu wakiwa wanasherekea, dada akaanza kuonja shida.
Kwa bahati mbaya, 'jogoo' wa mume alikuwa 'hawiki mtungini'. Ndani ya kipindi cha miezi isiyopungua sita, dada ameshakwenda kwa wazee, Padri...kuta talaka.
Kama mnavyojua ndoa kanisa Katoliki, hakuna talaka, sasa kesi ipo mahakamani, mahakama inatakiwa imshinikize jamaa aende hosptali ili kuthibitishwa kwamba 'shughuli haiwezi', ndipo dada apate ruksa ya kuendelea na mambo yake.
Dada amekwisha ondoka tangu miezi ya awali, sasa anahudhuria mahakamani.
Japo, binafsi sioni sababu ya kuhangaika ili kupata ruhusa ya mahakama, kwa kuwa vipimo vya maabara havithibitishi uhai wa uume.
Dada zangu mlio kwenye uchumba wa heshima, chukueni ushauri.