MGODOLO
JF-Expert Member
- Oct 23, 2020
- 209
- 172
Naombeni wana sheria na wadau mliopitia hizi changamoto mnisaidie!
Habari zenu wana Jf, nina changamoto na mzazi mwenzangu ambaye nia yangu ilikua ni kumuoa lakini kwa mabadiliko yake kuwa mabaya, nia ikatoweka na sitaki hata mtoto.
Nitazungumzia kwa ufupi ili kufupisha maelezo.
Mimi(28) Nilianza mahusiano na Bint mmoja(24) ambaye nilimpenda sana, lengo ni kumuoa binti huyo.
Kwakua alikua hataki kuchezewa kimapenzi, tuliyapanga kisha nikamwagiza awaeleze wazazi wake kua kapata mchumba hivyo aje ajitambulishe.
Ndugu wadau, nilikua na kakibunda kangu kalikokuwa kananipa kiburi cha kuoa, na hata hivyo nilikua na nia.
Bint huyo anaishi na mama yake mdogo, lakini mama huyo alipofikishiwa taarifa hizo, alikataa, hata aliporudia kuongea naye alikataa katukatu alijibu (SITAKI KUSIKIA SWALA HILO).
Kwa bahati mbaya, mama yangu aliugua kijijini, kale kapesa kote, kakaishia huko. Kwa bahati mbaya shetani kapita, nasi tukaambatana naye.
Ilikua ni mwezi wa 9 mwaka jana
Mwezi wa kumi mwishoni, binti akalalamika kua ana ujauzito, na anataka kuutoa kwasababu wazazi wake wakijua itakua tabu.
Nikamsihi asitoe kwakua mimi nipo, sikua na wasiwasi wowote kwasababu nia ya kumuoa bado ipo palepale.
Mimba iliendelea kukua, changamoto ni kwamba binti anaogopa kuwaeleza wazazi wake kuhusu hali aliokua nayo.
Ilifikia hatua binti katoroka mara kadhaa kuja kwangu, ilimradi wazazi wake wasijue kua kapatia mimba pale.
Kwa busara, nikamuomba na kumrudisha kwao na mabegi yake, mimi nayeye tukashirkiana kutumia njia mbalimbali ili mama yake huyo ajue kua mtoto wake ni mjamzito.
Tukafanikiwa Mama yake akaamua kumwambia (MWITE HUYO KIJANA)
Nakumbuka ilikua ni mwezi wa pili tarehe za katikati mwaka huu, tuliongea mengi kuhusu malengo juu ya binti yao, nia yangu ikabaki palepale, nataka kumuoa ila kwa sasa hali yangu sio nzuri(kuhusu mahari).
Wakaniambia, wiki ijayo nilete mzazi wangu waongee naye, nikapuuza lile swala. Baada ya wiki hiyo kuisha nikashangaa binti kaja kwangu asubuhi, akasema kafukuzwa kwao.
Nikatoka mpaka kwao kujua kulikoni, wakasema huyo binti akae huko mpaka utakapo tuletea mzazi wako. Ikabidi nishirikishe familia sasa, ila kwakua nilikua na lengo na yule binti, kiukweli tulifurahi kwa kufukuzwa kwake!
Baada ya wiki kufika siku ya kikao cha familia zote, wakazungumza mahari zao walizotaka, tukakubali lakini tuka waambia kwa sasa hali sio nzuri hatuna hata mia(kuhusu mahari).
Mmoja wa mjomba wake, akataka kutufungisha ndoa siku ileile, lakini sheria za dini zikatubana, kua hatuwezi kufunga ndoa ilihali mwanamke ni mjamzito. Na huyo binti atoke huko kwako aje hapa kwa wazazi wake akisha jifungua ndipo tuwafungishe ndoa, na binti huyo akisha rudi, hutapangiwa matumizi ya kuleta, ila chochote ulicho nacho lete.
Kwa mimi na huyo binti, hatukupenda kauli ya mjomba, Kuwa binti arudi kwao, hata binti hakupenda kurudi kwao, ila kwa amri ya wakubwa ikabidi iwe hivyo kishingo upande(nilikaa naye wiki moja kwangu).
Nguo zake zote zilianza kumbana kadri mimba ilivyozidi kukua. Nikampeleka mjini, akakusanya kile alicho ona hana, magauni ya ujauzito, nguo za ndani, viatu na kadhalika, ishu za hospitali zote natoa pesa.
Familia ile ilikua ikikazania nitoe mahari angalau hata kidogo ili wajomba na yule mama yake atulie, nikawaambia nikitoa mahari na ilihali hali ya ujauzito inazidi kukua, je nani atawajibika?
Hawakua na la kujibu, na najua fika wasingeweza ishu ya uzazi kwa yule binti(hawako poa kimaisha). Nguo za uzazi zote walizo taka nilisha nunua.
Mimi ni dereva, 17/05/2022 nilipata ajali(traffic case) nikawekwa ndani kuanzia siku hio(hata kwao wanajua) mpaka tarehe 20/05/2022, saa tisa alasiri, nafungua simu nikakutana na ujumbe wa yule binti kua kapelekwa hospitali saa tano ya siku hio(alipata uchungu).
Nikarudi nyumbani, nikaoga kisha nikaenda hospitali husika alipo pelekwa, nikawakuta wazazi wake wapo nje ya hospitali hio wakinisubiri. Nikaingia na kuonana na nesi amwangalie huyo binti mpaka atakapo jifungua.
Kipesa nilicho kiwekeza kwa ajili ya uzazi wake, kikaishia kwenye kesi na hakikutosha, kampuni ikamalizia palipobaki(deni)
Mungu mkubwa, tarehe 21/05/2022 alijifungua salama salimini.
Ndani sina hata mia ya ngama, Nilikwenda kazini kwangu, nikakopa kiasi fulani cha pesa ambacho kingeweza kukidhi mzunguko mzima wa uzazi (KUMBUKA HAPO NINA DENI NA KAMPUNI, AFU NIKAKOPA TENA)
Namshukuru Mungu uzazi ulianza salama.
Katikati ya arobaini, binti akaanza kudai kua anataka nguo mpya za kuvaa, anataka nguo za mtoto. Hapo nilipo sina hata mia, na hata nyama zenyewe nimefanya kueka oda buchani ili nilipe kwa wiki. Nikamwambia wacha arobaini iishe, pengine nitapata pesa.
Ndugu zangu changamoto zikaanzia hapo, hela na wao, wao na hela. Nilikua nakwenda ukweni kila siku jioni kuwajulia hali ila kila baada ya siku mbili, wanataka pesa na hapo nilisha nunua kila kitu kinacho husu uzazi. Kila nikipiga simu niwajulie hali, hiyo simu mpaka najuta hata kupiga, wanataka hela tu.
Kazini kwangu mshahara unakatwa mara tatu... kama unavyo elewa mishahara ya kibongo, ni miambili hutaki kazi acha.
Nakatwa NSSF, nakatwa ule msaada wakesi na nakatwa mkopo niliyokopa kwa ajili ya uzazi.
Yaani nikipokea kile kilicho baki, hata hakinitoshi maana ni nusu ya mshahara ndio napokea. Pamoja na hayo, chochote kinacho pungua kule nanunua hata kwa kukopa mahali, ila wao hawajui.
Ndugu zangu, nilishindwa hata kununua vinguo vya mwanangu, maana wao wanalia, familia yangu nayo kijijini inanitegemea mimi, hivyo kwakua yule yupo nyumbani na wazazi wake wapo, nikawa natoa chochote kitu haswa elfu 20 kwa wiki au hata mbili, lakini nikijua yupo nyumbani.
Arobaini imaisha, Nikasema Afadhali hata nipumue wanipe mke wangu nikaishi nae.
Naona tena kimyaaa, nikimuuliza binti anasema wananisubiri mimi, lakini kwa jinsi tunavyojua taratibu za kitanzania, familia ya mke ndio inatakiwa kumwita kijana na kumpa mkewe, ila sio kijana akadai mke kwa nguvu ilihali hakuna alichotoa(mahari).
Wiki moja baada ya arobaini nilikwenda nikawaeleza matatizo yangu na jinsi kipato changu kilivyo kwa sasa. Ila nikawaambia kama mtanipa mke wangu sitashindwa kuishi naye, ila kama hamtonipa kwakuwa sikutoa chochote, basi nisubirieni mpaka nitakapo pata.
Changamoto iliopo ni kwamba, wanao ishi nae hawana maamuzi kamili juu ya bint huyo, wenye maamuzi ni wajomba na hawaishi hapo, wakaniambia tutafikisha ujumbe.
Wakati huo bado namujitaji yule binti, japokuwa yule binti naye keshaanza kubadilika, ananijibu anavyotaka hata anapohitaji matumizi anapandisha sauti ya juu, kana kwamba alikua akitumwa kudai pesa kwangu, alikua akinijibu anavyo jisikia.
Lakini nikawa na moyo wa subira, sasa nikawa nataka mtoto wangu nimtafutie cheti cha kizaliwa, mana kila nikiongea na mama mtoto, naona majibu hayako sawa. Baba yake binti akasema fuatilia mwenyewe, yaani mimi maongezi haya yalifanyika kwao tarehe 30/07/2022 usiku wa saa mbili, siku ya Jumamosi.
Tarehe 01/08/2022, Nilipo toka kuripoti kituoni (bado naripoti kwa ile kesi) nikapitia hospitali aliojifungulia kuulizia taratibu za kupata cheti cha mtoto, wakasema niende na kadi ya ujauzito na kadi ya mtoto. nikampigia simu yule binti atume hizo kadi kwa dereva toyo, nitamlipa mimi. Binti akasema nikachukue mwenyewe.
Ikabidi nikaenda mpaka kwao, nikawaambia wanipatie hizo kadi. Ndugu zangu, watu wale waligoma kunipa kadi za mtoto wangu!
Nikamwambia yule binti, mimi natoka, ila jua kuwa sina mtoto hapa. Nikaondoka, na kuanzia siku hio sikupiga simu wala kutuma chochote.
Tarehe 10/08/2022, binti akapiga simu, aliuliza tu ukimya wangu, nikamjibu sina wakumjulia hali, maana nikiwa kama baba nikanyimwa kadi za mtoto wangu je, nitamjulia hali mtoto wa nani(maongezi ni mengi na majibu yake ya karaha).
Tarehe 22/08/2022, akapiga simu, maongezi ni yaleyale ukimya wangu sijui atalea na nani mtoto, maana baba ndio mimi. Majibu yangu ni yaleyale kwanini waninyime kadi za mwanangu kuna nini kilicho endelea? Kosa langu ni kukosa pesa, ndio chanzo.
DHUMUNI LA KUANDIKA HAYA.
Kwa ninavyo waona, lazima watafuata sheria, sasa ombi langu kwa wana sheria na wadau mliopitia changamoto hizi, mnisaidie.
1) Je, sheria itanibana kwa lipi?
2) Je, nijiandae na nini?
3) Nataka niwaachie mtoto kisheria je, inawezekana, nifuate njia gani?
Naombeni msaada wenu tafadhali, kwasasa nia ya kumuoa huyo binti sina tena, kwani hafai tena kuwa mke.
Nawasilisha uzi huu, karibuni, kama una swali uliza, nitakujibu.