Musoma Vijijini Waendelea Kujenga Maabara za Masomo ya Sayansi Kwenye Sekondari Zake za Kata

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
942

MUSOMA VIIJIJINI WAENDELEA KUJENGA MAABARA ZA MASOMO YA SAYANSI KWENYE SEKONDARI ZAKE ZA KATA

Kwenye miradi ya ujenzi wa maabara tatu za masomo ya sayansi (fizikia, kemia na bailojia) kwenye Sekondari zetu za Kata, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo anashirikiana na: (i) Serikali yetu, (ii) Wanavijiji (iii) Wadau wa Maendeleo na (iv) Baadhi ya Wazaliwa wa Musoma Vijijini

Maabara za Etaro Sekondari:
Sekondari hii ni moja ya Sekondari 25 za Kata za Jimbo la Musoma Vijijini. Ilifunguliwa Mwaka 2006 na hadi sasa maabara zake ni hizi zifuatazo:

(i) Maabara ya Bailojia - imekamilika na itatumiwa

(ii) Maabara ya Kemia - itakamilishwa kabla ya tarehe 15.1.2024. Serikali imechangia Tsh milioni 30

(iii) Maabara ya Fizikia - boma limekamilika kwa michango ya fedha na nguvukazi za wananchi wa Kata ya Etaro.

Harambee ya leo ni ya kukamilisha ujenzi wa Maabara ya Fizikia kabla ya tarehe 30.1.2024

Michango ya wananchi ni:
*Tsh 850,000 (zikiwemo za Walimu Makada wa CCM wa Kata ya Etaro, Tsh 42,000)
*Saruji Mifuko 3.

Michango ya Mbunge wa Jimbo ni:
*Saruji Mifuko 100 (binafsi)
*Mabati 100 (Mfuko wa Jimbo)

Somo la Kompyuta kufundishwa Etaro Sekondari:
*Kompyuta 25 - zimetolewa na Northern Illinois University (NIU, kilianzishwa Mwaka 1895) ya USA kupitia ushirikiano wa kirafiki kati ya Chuo hicho na Etaro Sekondari

TTCL imekamilisha leo ufungaji wa mawasiliano ya internet shuleni hapo.

Tafadhali sikiliza CLIP/VIDEO iliyoambatanishwa hapa ambayo inatoa taarifa zaidi kuhusu ujenzi wa Maabara za Masomo ya Sayansi za Etaro Sekondari ya Kata ya Etaro, Musoma Vijijini.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumamosi, 23.12.2023
 
Na uprofesa wote wa madini, na kujua yanapopatikana, hana hata mgodi wa chumvi, madogo wa chunya na katoro na geita wanatusua. Yeye anayasimulia kwenye papers tu, na kutamba kwamba ni msomi
 
Back
Top Bottom