Escrow kumuumbua Rais Kikwete

Escrow kumuumbua Rais Kikwete

Agenda kuu ktk uchaguzi 2015 nikuwa RAISI JK kutoka CCM kaiba pesa za wananchi, hili lazima liingie vizuri kwenye vichwa vya wananchi na lazima lihubiriwe kila kona na kila pembe ya nchi

mkuu, haitoshi tu kusema kuwa JK kaiba bali unapaswa kutuambia kaiba nini na kiasi gani. Tunaposema Dr Slaa kapora mke wa mtu then tuna ushahidi kuwa kachukua Josephine, mke wa Mahimbo
 
so agenda ya kutafutia kura ni kupakazia watu wizi?
nayo itagonga mwamba vilevile
 
mkuu, haitoshi tu kusema kuwa JK kaiba bali unapaswa kutuambia kaiba nini na kiasi gani. Tunaposema Dr Slaa kapora mke wa mtu then tuna ushahidi kuwa kachukua Josephine, mke wa Mahimbo
Millioni 800. unadhani wananchi hawajui, tunasuburi amalize muda wake, nahasa akiwa rais Lowassa na hapo kikwete atakiona
 
Prof Anna alipewa hela kama zawadi na yeye hakuwa na maamuzi yoyote hama Wizara Fedha, BoT wala Tanesco. Kwa nini yeye tu ndo ashikiwe bango. Kama ni kiasi cha pesa alichopewa mbona Chenge haguswi. Kama Prof Tibaiijuka anasakamwa kwa kuwa ni Mwanamke na ni Mhaya na kwa sababu ya kupewa hela na Mhaya (kaka yake kama alivyosema yeye) basi hapa Wahaya wote tunasakamwa.

Nenda kasome Money Laundering act 2006
 
RAIS Jakaya Mrisho Kikwete, anahaha kujiokoa na kashfa ya ukwapuaji wa mabilioni ya shilingi katika akaunti ya Escrow, ndani ya Benki Kuu (BoT).

Mpango wa sasa, ni kuwakamata baadhi ya waliopewa fedha na James Rugemalira, mmoja wa wamiliki wa IPTL ili kuzima mjadala.

Profesa Anna Tibaijuka, mbunge wa Muleba Kusini (CCM), yumo katika orodha ya wanaotakiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote wiki hii.


Tayari Prof. Tibaijuka amehojiwa zaidi ya mara moja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa (TAKUKURU), kuhusu Sh. 1.6 bilioni alizopewa na Rugemalira.


Mkakati wa kumfikisha mahakamani Prof. Tibaijuka, unasukwa kwa ustadi mkubwa na waziri mmoja mwandamizi katika serikali ya Rais Kikwete.


“Watanaka Prof. Tibaijuka apelekwe mahakamani kwa hoja kuwa, kwa hadhi aliyonayo kimataifa, sakata zima la Akaunti ya Tegeta Escrow litakuwa limezimwa,” anaeleza mtoa taarifa.


Anasema, “Lakini nataka nikuhakikishie, kitendo hicho kitasababisha tatizo kukua. Rais Kikwete anafahamu fika Harbinder Singh Sethi wa IPTL kuwa alitokea ikulu kabla ya kukwapua mabilioni ya shilingi kutoka akaunti ya Escrow.”


Anasema, “Ni vigumu kwa Rais Jakaya Kikwete kufanikiwa kujitenga na kashfa ya ukwapuaji wa zaidi ya Sh. 321 bilioni zilizochotwa katika akaunti ya Tegeta Escrow.”


Kiasi cha Sh. 321 bilioni zilikwapuliwa kutoka akanti ya Escrow ndani ya Benki Kuu (BoT), kati ya Septemba na Novemba 2013; na Prof. Tibaijuka alipewa Sh. 1.6 bilioni na mmoja wa waliokuwa wabia katika kampuni ya kufua umeme ya IPTL.


Taarifa zinasema, anayejiita na kuitwa na serikali kuwa ni “mmiliki mpya wa IPTL/PAP,” Harbinder Singh Sethi, aliletwa nchini na mmoja wa wanafamilia wa Rais Kikwete.


Taarifa zinasema, wanaoshinikiza Prof. Tibaijuka kufikishwa mahakamani wanajenga hoja mbili. Kwanza, kwamba hatua hiyo italegeza msimamo wa wahisani wa kuinyima misaada Tanzania; na kwamba kelele zote za ndani zitakuwa zimezimwa.


Pili, hatua ya kumfikisha mahakamani waziri huyo wa zamani wa ardhi, kutasaiidia kumkingia kifua waziri wa nishati na madini, Prof. Sospeter Muhongo na kuzima mjadala bungeni.


Rais Kikwete alimfuta kazi Prof. Tibaijuka katika mkutano wa “Wazee wa Dar es Salaam,” tarehe 23 Desemba 2014.


Inaelezwa kuwa singasinga alikutana na rais, ikulu jijini Dar es Salaam; na kutoka hapo alikwenda kukwapua mabilioni ya shilingi BoT hata bila kumfahamisha Rugemalira – mbia mwenzake.


Taarifa zinasema, sasa rais anashinikizwa kumfukuza Prof. Tibaijuka kutoka Kamati Kuu (CC) ya CCM na baadaye kumfikisha mahakamani kwa madai ya wizi na utakatishaji wa fedha.


Kupatikana kwa taarifa kuwa serikali ya Rais Kikwete inapanga njama za wizi kwa kupeleka baadhi ya waliochotewa fedha na Rugemalira, kumekuja wiki tatu baada ya Kikwete kudai kuwa fedha katika akaunti ya Escrow, hazikuwa za umma.


Akihutubia wanaoitwa, “Wazee wa Dar es Salaam,” katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Rais Kikwete alisema, mabilioni ya shilingi katika akaunti ya Escrow yalilipwa kwa PAP baada ya Mahakama Kuu kutoa “amri” tarehe 5 Septemba 2013.”


Akaunti ya Escrow ilifunguliwa ili kusubiri kumalizika kwa mgogoro kati ya Tanesco na IPTL, uliohusu madai ya udanganyifu katika uwekezaji; na hata gharama za kuweka mitambo – Capacity Charge – ambavyo vilifanywa na kampuni hiyo ya kigeni.


Kampuni ya IPTL ni muungano wa kampuni mbili – VIP Engineering and Marketing Limited ya James Rugemalira, iliyokuwa ikimiliki asilimia 30 ya hisa na MECHMAR ya Malaysia iliyokuwa na asilimia 70 za hisa.
jamani hatujawahi kuwa na rais kama huyu, ni waajabu kupindukia, anawaheshimu waovu, na wala rushwa, wezi, basi na yeye yumo humo, tusubiri amalize urais wake ili Abuluzwe kortini
 
jungu la kipolo bado halija pakuliwa ila bado mnang'ang'ania jungu ambalo wali wake ushapakuliwa na kubaki ukoko

yaani raisi naelekea anapata kigugumizi na jazba kweli akikumbushiwa kuhusu huyu waziri kiburi muhongo maana anashindwa kutamka chochote juu yake na kubaki kumbuluza tu mama wa watu aliekalibishwa kwenye ngoma ya watu
 
Hukuielewa ripoti ya PAC kama uliisoma.Kuna pesa ilikuwa inalipwa IPTL moja kwa moja. Hivyo hizo bil 306 toa izo bil 202 ujue hicho kiasi kilichokuwa kimelipwa IPTL moja kwa moja.
Mkuu haya magazeti yanasema 'Pesa zilizochotwa kweye account ya Tegeta ESCROW' sio zilizolipwa moja kwa moja+zilizo chotwa ESCROW account
 

Kama ni kweli ndivyo kinachoendelea... Anna Tibaijuka is a SCAPEGOAT... na Anajulikana fika alikuwa hana Makundi ndani ya CCM hence ni rahisi kumsengenya na kumuangusha...

Sababu, ni kwanini CHENGE hawamjadili huko CC aondoke kwenye CCM ? kwanini Anna Makinda bado anamtumia CHENGE kwenye maamuzi mengi tu BUNGENI ni kwasababu alisoma HARVARD ??? Anna Tibaijuka is Bright as well!!!

Nchini Kenya Wanasifia Uamuzi wa Rais Kikwete sababu -- Rais katoka kabila dogo na kamfukuza kazi mtu wa kabila kubwa na hakuna mtafakuru wa kikabila nchini...

Is there ENOUGH is ENOUGH ??? Yeye Hakuiba hizo PESA... Wezi wapo na Wengine around Rais wetu na hakuna wa kuwashitaki... Is there a REAL JUSTICE in OUR BELOVED NATION ??

Unajua wahaya ni wasomi wastaarabu,pia wakwele ni kama ka kijiji kachovu huko huayani,hapo ni sawa na mende kuangusha kabati.
Lakini kwa kashifa ya huyu mama na maneno yake ya nyodo wahaya wamemwacha azame dimbwini.
 
mkuu, haitoshi tu kusema kuwa JK kaiba bali unapaswa kutuambia kaiba nini na kiasi gani. Tunaposema Dr Slaa kapora mke wa mtu then tuna ushahidi kuwa kachukua Josephine, mke wa Mahimbo

Ona huyu nae mpaka rangi kucha sinza,inamaana wewe husikii wala hauoni,au tukuweke kwenye kundi la watu maalumu?,mana inaonyesha dish lako linayumba datta reading error!!!
 
Unajua wahaya ni wasomi wastaarabu,pia wakwele ni kama ka kijiji kachovu huko huayani,hapo ni sawa na mende kuangusha kabati.
Lakini kwa kashifa ya huyu mama na maneno yake ya nyodo wahaya wamemwacha azame dimbwini.

Oooooh TYPICAL...
 



Is there ENOUGH is ENOUGH ??? Yeye Hakuiba hizo PESA... Wezi wapo na Wengine around Rais wetu na hakuna wa kuwashitaki... Is there a REAL JUSTICE in OUR BELOVED NATION ??

Tibaijuka hasafishiki. Ktk justice system, anayepatikana na kitu kilichoibiwa NI MWIZI. Kakutwa na kitu kilichoibiwa, kwa vipi siyo mwizi?
 
Kubenea ni mpuuzi tena amepindukia
Kubenea alikufuatilia akakuanika mchana kweupe jinsi ulivyompiga mzee Warioba ukishirikiana na vibaka wenzako....huwa akiamua kumfuatilia mtu anahakikisha anafanikisha na kutoa ushahidi usikuwa na mashaka yoyote.
 
Tibaijuka hasafishiki. Ktk justice system, anayepatikana na kitu kilichoibiwa NI MWIZI. Kakutwa na kitu kilichoibiwa, kwa vipi siyo mwizi?

Vipi CHENGE vingapi vya WIZI amepatikana navyo na bado anadunda MJINI???
 
Ni nchi hii pekee ambapo Rais anachota fedha za watanzania bila hata ya huruma.Kwakweli nchi hii inahitaji ukombozi.
 
Unajua wahaya ni wasomi wastaarabu,pia wakwele ni kama ka kijiji kachovu huko huayani,hapo ni sawa na mende kuangusha kabati.
Lakini kwa kashifa ya huyu mama na maneno yake ya nyodo wahaya wamemwacha azame dimbwini.
Inashangaza hadi karne hii bado unatafuta umaarufu wa kikabila
 
Kosa kubwa alilofanya Mkulu ni kukaribisha wahaya ikulu na kujiweka karibu nao. Serikali zilizopita ilikuwa kinyume chake!

Ubaguzi wako utakuua kwani Wahaya si Watanzania? Utake usitake wao ni Watanzania na wana kila haki ya kufanya kazi popote vile kama walivyo watu wa makabila mengine. Ushindwe katika uovu wako na tena ulegee!
 
Tibaijuka hasafishiki. Ktk justice system, anayepatikana na kitu kilichoibiwa NI MWIZI. Kakutwa na kitu kilichoibiwa, kwa vipi siyo mwizi?

Anasafishika kwani hakuiba wala alichokutwa nacho si cha wizi kwani aliyempa alilipwa kihalali na Raisi Kikwete kasema alilipwa kihalali. Wezi ni wale waliochukua pesa hizo Benki Kuu na kuzipeleka Stanbic na kugawana katika mifuko ya rambo na lumbesa. Kama unataka ukweli ungetaka kuwajua hao ambao wameliibia taifa letu. Kwa wenye kuelewa ukweli na walio tayari kuelimishwa Tibaijuka ni msafi kama theluji!
 
Back
Top Bottom