Escrow kumuumbua Rais Kikwete

Escrow kumuumbua Rais Kikwete

Prof Anna alipewa hela kama zawadi na yeye hakuwa na maamuzi yoyote hama Wizara Fedha, BoT wala Tanesco. Kwa nini yeye tu ndo ashikiwe bango. Kama ni kiasi cha pesa alichopewa mbona Chenge haguswi. Kama Prof Tibaiijuka anasakamwa kwa kuwa ni Mwanamke na ni Mhaya na kwa sababu ya kupewa hela na Mhaya (kaka yake kama alivyosema yeye) basi hapa Wahaya wote tunasakamwa.

Hivi Prof alikuwa anauza nini?Iweje pesa za Taasisi iwe kwa jina lake badala ya taasisi?Uwaziri ni wakuteuliwa sio wa kuchaguliwa.Prof hana sababu ya kulalamika,Nothing proper and regal .
 
RAIS Jakaya Mrisho Kikwete, anahaha kujiokoa na kashfa ya ukwapuaji wa mabilioni ya shilingi katika akaunti ya Escrow, ndani ya Benki Kuu (BoT).

Mpango wa sasa, ni kuwakamata baadhi ya waliopewa fedha na James Rugemalira, mmoja wa wamiliki wa IPTL ili kuzima mjadala.

Profesa Anna Tibaijuka, mbunge wa Muleba Kusini (CCM), yumo katika orodha ya wanaotakiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote wiki hii.

Tayari Prof. Tibaijuka amehojiwa zaidi ya mara moja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa (TAKUKURU), kuhusu Sh. 1.6 bilioni alizopewa na Rugemalira.

Mkakati wa kumfikisha mahakamani Prof. Tibaijuka, unasukwa kwa ustadi mkubwa na waziri mmoja mwandamizi katika serikali ya Rais Kikwete.

“Watanaka Prof. Tibaijuka apelekwe mahakamani kwa hoja kuwa, kwa hadhi aliyonayo kimataifa, sakata zima la Akaunti ya Tegeta Escrow litakuwa limezimwa,” anaeleza mtoa taarifa.

Anasema, “Lakini nataka nikuhakikishie, kitendo hicho kitasababisha tatizo kukua. Rais Kikwete anafahamu fika Harbinder Singh Sethi wa IPTL kuwa alitokea ikulu kabla ya kukwapua mabilioni ya shilingi kutoka akaunti ya Escrow.”

Anasema, “Ni vigumu kwa Rais Jakaya Kikwete kufanikiwa kujitenga na kashfa ya ukwapuaji wa zaidi ya Sh. 321 bilioni zilizochotwa katika akaunti ya Tegeta Escrow.”

Kiasi cha Sh. 321 bilioni zilikwapuliwa kutoka akanti ya Escrow ndani ya Benki Kuu (BoT), kati ya Septemba na Novemba 2013; na Prof. Tibaijuka alipewa Sh. 1.6 bilioni na mmoja wa waliokuwa wabia katika kampuni ya kufua umeme ya IPTL.

Taarifa zinasema, anayejiita na kuitwa na serikali kuwa ni “mmiliki mpya wa IPTL/PAP,” Harbinder Singh Sethi, aliletwa nchini na mmoja wa wanafamilia wa Rais Kikwete.

Taarifa zinasema, wanaoshinikiza Prof. Tibaijuka kufikishwa mahakamani wanajenga hoja mbili. Kwanza, kwamba hatua hiyo italegeza msimamo wa wahisani wa kuinyima misaada Tanzania; na kwamba kelele zote za ndani zitakuwa zimezimwa.

Pili, hatua ya kumfikisha mahakamani waziri huyo wa zamani wa ardhi, kutasaiidia kumkingia kifua waziri wa nishati na madini, Prof. Sospeter Muhongo na kuzima mjadala bungeni.

Rais Kikwete alimfuta kazi Prof. Tibaijuka katika mkutano wa “Wazee wa Dar es Salaam,” tarehe 23 Desemba 2014.

Inaelezwa kuwa singasinga alikutana na rais, ikulu jijini Dar es Salaam; na kutoka hapo alikwenda kukwapua mabilioni ya shilingi BoT hata bila kumfahamisha Rugemalira – mbia mwenzake.

Taarifa zinasema, sasa rais anashinikizwa kumfukuza Prof. Tibaijuka kutoka Kamati Kuu (CC) ya CCM na baadaye kumfikisha mahakamani kwa madai ya wizi na utakatishaji wa fedha.

Kupatikana kwa taarifa kuwa serikali ya Rais Kikwete inapanga njama za wizi kwa kupeleka baadhi ya waliochotewa fedha na Rugemalira, kumekuja wiki tatu baada ya Kikwete kudai kuwa fedha katika akaunti ya Escrow, hazikuwa za umma.

Akihutubia wanaoitwa, “Wazee wa Dar es Salaam,” katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Rais Kikwete alisema, mabilioni ya shilingi katika akaunti ya Escrow yalilipwa kwa PAP baada ya Mahakama Kuu kutoa “amri” tarehe 5 Septemba 2013.”

Akaunti ya Escrow ilifunguliwa ili kusubiri kumalizika kwa mgogoro kati ya Tanesco na IPTL, uliohusu madai ya udanganyifu katika uwekezaji; na hata gharama za kuweka mitambo – Capacity Charge – ambavyo vilifanywa na kampuni hiyo ya kigeni.

Kampuni ya IPTL ni muungano wa kampuni mbili – VIP Engineering and Marketing Limited ya James Rugemalira, iliyokuwa ikimiliki asilimia 30 ya hisa na MECHMAR ya Malaysia iliyokuwa na asilimia 70 za hisa.

Habari za uhakika ni kwamba watuhumiwa (dagaa) waliofikishwa mahakamani na kuwaacha mapapa yakizidi kutanua uswahilini ni kuhakikisha wanawafunga midomo wabunge kwa kigezo kuwa issue hii ya escrow haitoweza kujadiliwa bungeni kwa kigezo kuwa issue hii ipo mahakamani.
 
Kwani kwenye ripoti ya CAG na TAKUKURU kuna mahala amehusishwa Rais KIKWETE?

sikiliza alichosema kwenye utangulizi makamo mwenyekiti wa PAC wakati wakiwasilisha report ya kamati juu ya Escrow
 
Kwani kwenye ripoti ya CAG na TAKUKURU kuna mahala amehusishwa Rais KIKWETE?
Kuna siku inakuja ambapo yaliyositrika gizani yatawekwa nuruni. Hapo ndipo kila mtu atashangaa! Mwizi hlisi atajulikana hadharani!
 
..za alinacha hizo....

napenda kukukumbusha kwamba hata Gadafi aliwaita waliokuwa wanampinga sisimizi na usisahau majuto ni mjukuu,sisi kazi yetu ni kutoa taadhari kwa yale yanayoelekea kutokea,kama wewe ni miongoni mwa familia ya Kikwete usipuuze tunayosema,sisi kina gogo la shamba ni kiona mbali
 
Kwa tz hii ya watawaliwa majuha....labda miaka 100 ijayo.tutapiga kelele siku mbili halafu yanapita...kwani mangapi yametokea hapa .? .chukua hatua sio kunngojea hiyo siku yao.kiama kitafika bado tunatumainia hiyo siku ije.!
 
Hao ndo akina neema mpaka kaburini......
 
Sidhani kama Jk alikuwa na nia ya kumfukuza tibaijuka..kelele na minong'ono ya wazee pale ukumbini ndio ilimfukuza prof.tibaijuka..kama kuna mtu anaweza kupata alichokuwa anakisoma(hotuba)atagundua hilo

namimi ningeamini ivyo kama SI KUSHUHUDIA WANAWAKE WA MITAANI (mashangingi) walio letwa RASMI PALE KIKAO CHA WAZEE KUJA KUZOMEA WAKATI MWANAMKE MWENZAO AKIONEWA WAZI WAZI,HAPO NDIPO MWANAMKE ANAPOKUA KIUMBE DHAIFU CHA KUTUMIKA.MAKE WAZEE WOTE WALIPIGWA NA BUTWAA NA KUSHANGAAA UAMUZI HUO AKIWEMO MHE.SHIBUDA ALIEONEKANA AKITIKISA KICHWA KWA MASIKITIKO,PICHA TUNAZO.AIBUUU KUBWA YA KIKWETE HIYOOO
 
Ama anamtumia kujisafisha ama anatumia haki ya kuksheria kwa Tibaijuka kujibu iweje mtumishi wa umma/waziri apewe pesa yote hiyo na mfanyabiashara yote ni kuwa tunataka wafike mahakamani kujibu maswali yenye mashaka
 
Wizi wa Kikwete unavunja rekodi zote za wizi kwani ni skandali baada ya skandali: Deep Green, Richmond, EPA, Escrow na Vibali vya sukari bila kudharau mabomu ya Mbagala na Ukonga. Mbona Majanga tena Majanga!

Bila kusahau udini, kuchoma makanisa,uhamsho,na vituo vya polisi kushambuliwa na magaid bila yeye hakusema kitu chochote
 
It will be a bit too harsh to say that your observations are based on stupidity. So, I 'll just say that your observations are baseless.
Phew!! .. What an a$$!

I think the point the guy was trying to make is......The Wahaya are a big tribe but they have remained silent, regardless of one of theirs being ousted from her position. It could have been way different had it happened in Kenya because of tribalism.
 
Kwa tz hii ya watawaliwa majuha....labda miaka 100 ijayo.tutapiga kelele siku mbili halafu yanapita...kwani mangapi yametokea hapa .? .chukua hatua sio kunngojea hiyo siku yao.kiama kitafika bado tunatumainia hiyo siku ije.!

kweli wewe uko tofauti na tuyaonayo sisi kina gogo la shamba,maana kwa hatua tuliyofikia kama ni mafuriko basi maji yako shingoni
 
Taarifa zinasema, sasa rais anashinikizwa kumfukuza Prof. Tibaijuka kutoka Kamati Kuu (CC) ya CCM na baadaye kumfikisha mahakamani kwa madai ya wizi na utakatishaji wa fedha.[/SIZE]

Kupatikana kwa taarifa kuwa serikali ya Rais Kikwete inapanga njama za wizi kwa kupeleka baadhi ya waliochotewa fedha na Rugemalira, kumekuja wiki tatu baada ya Kikwete kudai kuwa fedha katika akaunti ya Escrow, hazikuwa za umma.

Akihutubia wanaoitwa, “Wazee wa Dar es Salaam,” katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Rais Kikwete alisema, mabilioni ya shilingi katika akaunti ya Escrow yalilipwa kwa PAP baada ya Mahakama Kuu kutoa “amri” tarehe 5 Septemba 2013.”

Akaunti ya Escrow ilifunguliwa ili kusubiri kumalizika kwa mgogoro kati ya Tanesco na IPTL, uliohusu madai ya udanganyifu katika uwekezaji; na hata gharama za kuweka mitambo – Capacity Charge – ambavyo vilifanywa na kampuni hiyo ya kigeni.

Kampuni ya IPTL ni muungano wa kampuni mbili – VIP Engineering and Marketing Limited ya James Rugemalira, iliyokuwa ikimiliki asilimia 30 ya hisa na MECHMAR ya Malaysia iliyokuwa na asilimia 70 za hisa.

We jamaa uko vizuri
 
Rais Kikwete anamfahamu fika Harbinder Singh Sethi wa IPTL kwa kuwa singasinga huyo alitokea ikulu kabla ya kukwapua mabilioni ya shilingi kutoka akaunti ya Escrow katika Benki Kuu. Saed Kubenea anaandika… (endelea)

Ni vigumu kwa Rais Jakaya Kikwete kufanikiwa kujitenga na kashfa ya ukwapuaji wa zaidi ya Sh. 321 bilioni zilizochotwa katika akaunti ya Tegeta Escrow, MwanaHALISI Online, limeelezwa.

"Mimi sina tatizo na maelezo ya rais," anaeleza waziri na kuongeza, "umma unasubiri kujua huyo ‘mmoja wa wanafimilia wa Kikwete' aliyempeleka singasinga ikulu, ni nani.
❝

Taarifa zinasema , anayejiita na kuitwa na serikali kuwa ni "mmiliki mpya wa IPTL/PAP," Harbinder Singh Sethi, aliletwa nchini na mmoja wa wanafamilia wa Rais Kikwete.

Inaelezwa kuwa singasinga alikutana na rais, ikulu jijini Dar es Salaam; na kutoka hapo alikwenda kukwapua mabilioni ya shilingi BoT hata bila kumfahamisha Rugemalira – mbia mwenzake.

"Kikwete anajua kila kitu. Yule singasinga alitokea ikulu. Huenda ndiyo maana sasa anaonekana kumtetea kwa kila jambo, likiwamo hata suala la kodi ya serikali," ameeleza waziri mmoja mwandamizi serikalini kwa sharti la kutotajwa jina.

"Nakuambia, Kikwete hatoki katika hili. Barua ya msaidizi wake akimwandikia katibu mkuu Hazina, inadhihirisha kuwa rais anajua kila kitu na hasa alibariki kila kitu. Rais mwenyewe hajakana hilo," ameeleza waziri huyo.

Kupatikana kwa taarifa kuwa Rais Kikwete alifahamu kila hatua kuhusu uchotaji mabilioni ya shilingi kutoka Benki Kuu (BoT), na hata yule Harbinder Sethi alitokea ikulu, kumekuja siku tatu baada ya Kikwete kudai kuwa fedha katika akaunti ya Escrow, hazikuwa za umma.

Akihutubia wanaoitwa, "Wazee wa Dar es Salaam," katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Jumatatu wiki hii, Rais Kikwete alisema, mabilioni ya shilingi katika akaunti ya Escrow yalilipwa kwa PAP baada ya Mahakama Kuu kutoa "amri" tarehe 5 Septemba 2013," kauli ambayo imethibitika kutokuwa kweli na sahihi.

Taarifa zinasema, kinachoitwa amri ya mahakama, kilikuwa ni kumaliza mzozo wa wanahisa wa kampuni ya kufua umeme wa dharula ya IPTL (Independent Power Tanzania Limited).

Usahihi na ukweli unapotea pale rais anaposema fedha ni mali ya IPTL huku wanaoshughulikia "fedha binafsi" kuchukuliwa ni pamoja na wasaidizi wake ikulu, mawaziri, makatibu wakuu, wabunge na gavana wa BoT.

"Mimi sina tatizo na maelezo ya rais," anaeleza waziri mwandamizi na kuongeza, "umma unasubiri kujua huyo ‘mmoja wa wanafimilia wa Kikwete' aliyempeleka singasinga ikulu, ni nani.

Akaunti ya Escrow ilifunguliwa ili kusubiri kumalizika kwa mgogoro kati ya Tanesco na IPTL, uliohusu madai ya udanganyifu katika uwekezaji; na hata gharama za kuweka mitambo – Capacity Charge – ambavyo vilifanywa na kampuni hiyo ya kigeni.

Kampuni ya IPTL ni muungano wa kampuni mbili – VIP Engineering and Marketing Limited ya James Rugemalira, iliyokuwa ikimiliki asilimia 30 ya hisa na MECHMAR ya Malaysia iliyokuwa na asilimia 70 za hisa.

Katika mazingira haya, wachunguzi wa mambo wanasema ya IPTL yatakuwa kama ya Richmond/Dowans. Waziri mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa aliwahi kuambia kikao cha CCM mjini Dodoma kuwa "kila kitu" alichofanya katika uwekezaji huo wa kifisadi, kilikuwa kinajulikana kwa rais.

Hapa ndipo unakuja mshangao. Kama singasinga alitokea ikulu; wasaidizi wa rais ndio waliandika barua za kuruhusu kuchota fedha BoT; na rais anajua kila kitu kilichokuwa kinatendeka; serikali inaweza kusemaje kuwa "inatafuta" kampuni ya Machmar, ambayo ndiye singasinga, ili ilipe kodi ya VAT?

Kwa waliomwona Rais Kikwete akihutubia, watakuwa waligundua kuwa sura yake, mpangilio wa maneno yake na jinsi alivyokuwa akihangaika kitini; bila shaka alikuwa akijitahidi kuficha ukweli fulani kadri inavyowezekana," ameeleza mtumishi mmoja wa ikulu.

Miongoni mwa waliotajwa kupewa fedha na Rugemalira, kama alivyopewa Profesa Anna Tibaijuka, ni mwandani wa rais kiofisi (mnikulu), Shabani Gurumo. Hajafukuzwa kazi.

Mtu mwingine ambaye ametajwa kunufaika na fedha za Escrow zilizopitia benki ya Stanbic, na ambaye jina lake lilitajwa bungeni na mmoja wa wabunge wa upinzani, ni Albert Marwa.

Wapo wengine waliochotewa mamilioni ya shilingi kupitia kwa Rugemalira na Stanbic akiwemo mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Mashimba.

Kufikia hatua hii, Prof. Muhongo yumo katika mazingira kama yale ya Lowassa. Wandani wake wamesikika wakisema kuwa wamemnukuu akisema kwamba akichukuliwa hatua, basi "ataanika kila kitu."

MwanaHALISI Onlile, liliripoti mwishoni mwa wiki iliyopita kuwa, Rais Kikwete "…amepanga kulinda watuhumiwa," na kwamba anayetarajiwa kutoswa katika sakata hili, ni Prof. Tibaijuka tu. Ndivyo ilivyotokea.
 
Back
Top Bottom