Escrow kumuumbua Rais Kikwete

Escrow kumuumbua Rais Kikwete

Usilete ukibaka wako hapa kamtishe yule demu wako ambaye pia ni mtoto wa shangazi yako lakini huwezi kuja kumtisha mtu mzima na utashi wake hapa jf kwenda zako.
HAHAHAHAAAA!!!! naona mke mdogo umeamua kumjibia.. bas poaaa!! ila nakushauri na wewe uwe na huyu mumeo karibu ili umsaidie kushikilia mlingoti
 
Endelea kusubiri hapo hapo usiondoke siye tunakwenda na jk kuendelea kuwatumikia watanzania wanaoipenda nchi yao.
KONYOOOOOO!!! Mfyuuuuuuuu!!!! labda mkamtumikie kiporo wenu MUONGO na CHENGE ............nina zenu
 
RAIS Jakaya Mrisho Kikwete, anahaha kujiokoa na kashfa ya ukwapuaji wa mabilioni ya shilingi katika akaunti ya Escrow, ndani ya Benki Kuu (BoT).

Mpango wa sasa, ni kuwakamata baadhi ya waliopewa fedha na James Rugemalira, mmoja wa wamiliki wa IPTL ili kuzima mjadala.

Profesa Anna Tibaijuka, mbunge wa Muleba Kusini (CCM), yumo katika orodha ya wanaotakiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote wiki hii.


Tayari Prof. Tibaijuka amehojiwa zaidi ya mara moja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa (TAKUKURU), kuhusu Sh. 1.6 bilioni alizopewa na Rugemalira.


Mkakati wa kumfikisha mahakamani Prof. Tibaijuka, unasukwa kwa ustadi mkubwa na waziri mmoja mwandamizi katika serikali ya Rais Kikwete.


“Watanaka Prof. Tibaijuka apelekwe mahakamani kwa hoja kuwa, kwa hadhi aliyonayo kimataifa, sakata zima la Akaunti ya Tegeta Escrow litakuwa limezimwa,” anaeleza mtoa taarifa.


Anasema, “Lakini nataka nikuhakikishie, kitendo hicho kitasababisha tatizo kukua. Rais Kikwete anafahamu fika Harbinder Singh Sethi wa IPTL kuwa alitokea ikulu kabla ya kukwapua mabilioni ya shilingi kutoka akaunti ya Escrow.”


Anasema, “Ni vigumu kwa Rais Jakaya Kikwete kufanikiwa kujitenga na kashfa ya ukwapuaji wa zaidi ya Sh. 321 bilioni zilizochotwa katika akaunti ya Tegeta Escrow.”


Kiasi cha Sh. 321 bilioni zilikwapuliwa kutoka akanti ya Escrow ndani ya Benki Kuu (BoT), kati ya Septemba na Novemba 2013; na Prof. Tibaijuka alipewa Sh. 1.6 bilioni na mmoja wa waliokuwa wabia katika kampuni ya kufua umeme ya IPTL.


Taarifa zinasema, anayejiita na kuitwa na serikali kuwa ni “mmiliki mpya wa IPTL/PAP,” Harbinder Singh Sethi, aliletwa nchini na mmoja wa wanafamilia wa Rais Kikwete.


Taarifa zinasema, wanaoshinikiza Prof. Tibaijuka kufikishwa mahakamani wanajenga hoja mbili. Kwanza, kwamba hatua hiyo italegeza msimamo wa wahisani wa kuinyima misaada Tanzania; na kwamba kelele zote za ndani zitakuwa zimezimwa.


Pili, hatua ya kumfikisha mahakamani waziri huyo wa zamani wa ardhi, kutasaiidia kumkingia kifua waziri wa nishati na madini, Prof. Sospeter Muhongo na kuzima mjadala bungeni.


Rais Kikwete alimfuta kazi Prof. Tibaijuka katika mkutano wa “Wazee wa Dar es Salaam,” tarehe 23 Desemba 2014.


Inaelezwa kuwa singasinga alikutana na rais, ikulu jijini Dar es Salaam; na kutoka hapo alikwenda kukwapua mabilioni ya shilingi BoT hata bila kumfahamisha Rugemalira – mbia mwenzake.


Taarifa zinasema, sasa rais anashinikizwa kumfukuza Prof. Tibaijuka kutoka Kamati Kuu (CC) ya CCM na baadaye kumfikisha mahakamani kwa madai ya wizi na utakatishaji wa fedha.


Kupatikana kwa taarifa kuwa serikali ya Rais Kikwete inapanga njama za wizi kwa kupeleka baadhi ya waliochotewa fedha na Rugemalira, kumekuja wiki tatu baada ya Kikwete kudai kuwa fedha katika akaunti ya Escrow, hazikuwa za umma.


Akihutubia wanaoitwa, “Wazee wa Dar es Salaam,” katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Rais Kikwete alisema, mabilioni ya shilingi katika akaunti ya Escrow yalilipwa kwa PAP baada ya Mahakama Kuu kutoa “amri” tarehe 5 Septemba 2013.”


Akaunti ya Escrow ilifunguliwa ili kusubiri kumalizika kwa mgogoro kati ya Tanesco na IPTL, uliohusu madai ya udanganyifu katika uwekezaji; na hata gharama za kuweka mitambo – Capacity Charge – ambavyo vilifanywa na kampuni hiyo ya kigeni.


Kampuni ya IPTL ni muungano wa kampuni mbili – VIP Engineering and Marketing Limited ya James Rugemalira, iliyokuwa ikimiliki asilimia 30 ya hisa na MECHMAR ya Malaysia iliyokuwa na asilimia 70 za hisa.

Wanasheria mje mtusaidie..hili suala la mtoaji na mpokeaji rushwa liko vipi?Au Rugemalira ali act kama AGENT wa PCCB kuwatembezea za moto kina Tiba?
 
Wanasheria mje mtusaidie..hili suala la mtoaji na mpokeaji rushwa liko vipi?Au Rugemalira ali act kama AGENT wa PCCB kuwatembezea za moto kina Tiba?
Kakudanganya nani kuwa fedha zile ni za moto? Nakuhakikishia hakuna mwanasiasa atakayepelekwa mahakamani
 
Mi naona km hamuelewi sakata zima lilivo,kwa nn tibaijuka anasakamwa? Jua ripot ya CAG,na kamati ya bunge alaf fata hotuba ya rais mwisho km ni muelewa utaelewa. Asante
 
Endelea kusubiri hapo hapo usiondoke siye tunakwenda na jk kuendelea kuwatumikia watanzania wanaoipenda nchi yao.
Even me i have passion with my country shida watu hawataki kuambiwa ukwel.Et una ona kuna loop hole huzib s mwishowe nn kinatokea so rahis kuambiwa hawawajibishe watu si kana kwamba watu hawaipend nchi au wana west time thats wrong.
 
Mi naona km hamuelewi sakata zima lilivo,kwa nn tibaijuka anasakamwa? Jua ripot ya CAG,na kamati ya bunge alaf fata hotuba ya rais mwisho km ni muelewa utaelewa. Asante
Nani kamuandama Tibaijuka?
 
Muhongo anawaumiza sana kichwa. Na mtaumia sana mwaka huu
hiviii unadhani mwaka huu ni nani wa kuumia kama si wewe na mabwana zenu mafisadi...
tena atakae waumiza ni huyoo fisadi mkuu LOWASSA. sijui mtakimbilia wapi.
ila wewe na chaburuma, faizafox msalani simiyu na vibaraka wenzio tayari tumesha watafutia sehem yenu ya kuwahifadhi msitaabike sana.
 
Zungu pule jua kuwa wote waliofikishwa mahakamani walinufaika rejea hati za mashitaka zao
 
Mwalimu Nyerere alijiweka mbali na Wahaya na Wachaga. Alijua ni watu wachafu

Alijiweka mbali nao vipi wakati alifanya nao kazi. Shida yako ni kuwa unaugua ugonjwa wa ukabila ambao kwa kitaalamu unafahamika kama ufashisiti kama aliokuwa nao Hitler na Mussolini. Wahi Milembe upate tiba haraka kwani wewe ni Interahamwe!
 
Nenda kasome Money Laundering act 2006

Mimi sipendi na wala sifurahii ufisadi wa hela za umma. Ila nami nina haki pia ya kuhoji ikiwa waliopata mgao wa Rugemalira ni wengi mbona wao hawakufukuzwa na kufikishwa mahakamani na pia kuvuliwa nafasi walizo nazo c.c. na nec? Kwa kweli wakiyaendeleza haya kwa huyu mama peke yake nitaamini zilikuwepo sababu nyingine zaidi ya hii ya escrow. Utawala wasijidanganye kuwa watanzania hawana uelewa kiasi hicho bado tutadai kuyajua majina yote yaliyopokelea migao yao kupitia stanbic bank. Hayo tutayadai kwenye mikutano ya kampeni za mwezi wa kumi.
 
Tibaijuka alipokea rushwa, bila kujali "undani" wa fedha alizopokea. Watu wanachanganya kitendo cha kupokea rushwa na chanzo cha fedha zilizotumika. Hivi ni vitu viwili tofauti. Je unamaana kuwa kama fedha alizopokea Tibaijuka zisingekuwa zimetoka kwenye akaunti ya escrow, basi ingekuwa ethical kwake kupokea fedha hizo? Au TAKUKURU wasingenyanyua bendera kuashiria kuwa kiongozi kapokea mlungula kinyume cha sheria?


Rushwa kwa kazi ipi? Katika sakata zima la Escrow wizara ya aridhi haikua na uhusiano wowote na sakata hilo wizara zilizohusika zinajulikana. Ukienda mahakamani na ushahidi huu wa kusema amepokea rushwa utagaragazwa na utaishia kulipa dhamana. Huingii akilini mtu ambae hana influence katika maamuzi na wala hakuna popote alipotoa ushauri na ripoti zote za Takukuru na CAG hakuna popote zinapomtaja zaidi ya kuonekana kwenye orodha ya mgao useme kua amepokea rushwa.
 
Yaani kama kuna mtu anaonewa ni huyu mama Ana tibaijuka wezi wapo wanajulikana
sasa iweje huyu mama wamfanye mbuzi wa kafara? kumpeleka huyu mama mahakamani
hapo serikari itaonyesha ni namna gani ilivyo dhaifu kiutendaji

singa singa yupo Luge yupo na wengine waliochukua zile za stanbic wapo mbona
hawaongelewi wala kutajwa? na huyu Raisi Kesha tufanya mafala mara aseme pesa siyo
za umma sasa ni nani mlalamikaji kwa prof Tibaijuka? tuache kuonana mabwege

watajwe waliobeba fedha pale stanibic kwenye malumbesa siyo hicho kiasi kidogo
alichochotewa huyo mama pls vinginevyo tutaonana wabaya.
 
Ona huyu nae mpaka rangi kucha sinza,inamaana wewe husikii wala hauoni,au tukuweke kwenye kundi la watu maalumu?,mana inaonyesha dish lako linayumba datta reading error!!!

Mkuu huyu na wenzie wengi tu kwenye jukwaa hili ni wavamizi hawana uwezo wa kutoa mchango kwenye hili jukwaa la great thinkers. Majukwaa yao yapo na hata wenzao wanawashangaa huo uwezo na uthubutu wa kuwemo kwenye jukwaa hili.
 
Je hao wanaochunguza wataweka vitu vyote online for the public?


Je kuna mtu yoyote ame demand minutes za vikao kayi ya singasinga na JK?
 
Back
Top Bottom