Eric Shigongo, umemwona kaka yako?

Eric Shigongo, umemwona kaka yako?

Jini Kisiranii

Mengine unaweza ukawa sahihi ila hapo kwenye 4mil na 200k umetudanganya brother..
Leave allowance + house sio favor hapana hilo kwenye mkataba wako ajira na lazima pia liwe kwenye policy ya kampuni, mwajiri anapoacha kukulipa hivyo vitu kwanza anakuwa amevunja mkataba wako na yeye na pili anakuwa amekiuka sheria za nchi.
 
Kauli yoyote atakayo inena JPM lazima kundi fulani lipinge tu, kwa kuwa hawana sera nyingine kama sio ya kukaa golini na kusubiri kauli! Pathetic walahi!
China na nchi za kiarabu huwa hawana mchezo kabisa!
Mbona wafungwa Tz wanafanya kazi? Wafungwa walikua wanakuja kufanya kazi mpaka kwa marehemu Kingunge.

Moshi wanalima Karanga. Na ukonga nilikuta wanafyatua matofali na utengenezaji samani.

Pengine raisi hajui na walio bize kubishana hapa hawajui pia.
 
Tofautisha kati ya kufanyakazi za uzalishaji na kazi za kumkomoa mtu kisa yeye ni mfungwa.

“Unakuta hata maaskari na watumishi hawana nyumba za kukaa na wafungwa wapo tena wa bure kabisa ambao unaweza kuwaambia wafyatue matofali na teke ukawapiga. Askari huna pa kulala na wafungwa wapo, lakini unawatafutia Bajeti ya Serikali," Rais John Magufuli.

Hapo sijaelewa kabisa inamaana huyu mfungwa akamjengee askari nyumba? Mbona huko mitaani kuna maboma mengi wananchi wamejenga lakini Serikali imeshindwa kumalizia. Mpaka yanabomoka. Piteni huko mahosptalini, mashuleni na Kwenye taasisi mtayaona.

Kwa hiyo CCM mnaomba huruma ya wafungwa wasaidie. Au mnamkakati wa kukamata vijana mtaani wakafanyekazi za Serikali?
 
Kufanyakazi kama wengine sio tatizo ni huo ukatili
Kuna majitu makatili kama wachina na wakorea au waarabu?
Haya mambo ya unafiki mkuu ndiyo yanayo angamiza nchi yetu, sasa MAMA TANZANIA ameamka walahi!
 
Kuna majitu makatili kama wachina na wakorea au waarabu?
Haya mambo ya unafiki mkuu ndiyo yanayo angamiza nchi yetu, sasa MAMA TANZANIA ameamka walahi!
Hukumu inasomeka kifungo miaka kadhaa na kazi ngumu!na viboko kadhaa siku ya kutoka. Halafu watu analala tu na kusodomana.
 
Ni mfanyakazi wa kwanza duniani asiyefahamu nini maana ya paid leave allowance let alone house allowance!

Backnowledge in the days shafanya sana as Online Freelancer! Mara nyingi kila nilipopata mkataba unaozidi mwaka mmoja; one of the benefits ilikuwa paid leave. Hiyo ni freelancing; virtual working, maarufu kama online jobs...seuze desk job!!

Kwanza unaonekana muongo! Huwezi kupata paid leave TSH. 4M halafu house allowance upate sh. 200K.

Laki 2 ni gharama ya chumba kimoja (self) tu Uswahilini wakati kwa serikalini anayefikia kulipwa 4M ni boss kwelikweli ambae there's no way anaweza kulipwa house allowance ya kuishi Uswahilini kwenye chumba kimoja!!

Peleka uongo wako Lumumba mtu usiyefahamu hata uwiano kati ya paid leave allowance na house allowance!!
Nimeisikia kauli ya wafungwa wapigwe na kufanyishwa kazi nzito baadae nikakaa na kujisemea moyoni kama kweli mtu yule alipita seminari wanakoandaliwa mapadri
 
Mkuu,hakuna mtu hatar hapa Tanzania kama Shigongo,huyu jamaa hata huo utajir wake kadhulumu watu wengi sana kama akna Abbasi Mwinyi,Wasanii na watu anaowabambikia skendo then wanaenda kumwona kimyakimya

Shigongo amekuwa kwenye upande wa CCM siyo kwamba anaipenda CCM,ni kwa sababu jamaaa alikuwa analitaka jimbo la Buchosa (hapa alikuwa anajua akiupata ubunge wa Buchosa lazma pia atateuliwa kuwa Wazir wa habar au msemaji wa Taasisi nyeti ya serikali),matokeo yake akapigwa chini...huyu jamaa pia inavyosemekana ni mlokole na huwa anawagonga mpaka wake za watu na usisahau kuwa ndye anayemiliki Corner bar (then connect the dots)
Mpaka mashoga refer Bilali miaka ileee alionekana nae sana tu
 
Hukumu inasomeka kifungo miaka kadhaa na kazi ngumu!na viboko kadhaa siku ya kutoka. Halafu watu analala tu na kusodomana.
Wafanyishwe kazi tu, hamna namna walahi!
Tena wakitoka watakuwa sio wavivu, Maana wamesha zoea kazi walahi
 
keko, na magereza mengine yanayofanana na hayo wamefugwa kama kuku wa amadori
 
Wafungwa wafanye kazi mbona nchi zingine wanafanya kazi mfano rwanda nimeshuhudia kwa macho yangu wafungwa wakilima mpunga
Kwani Tanzania wafungwa yawafanyi kazi? Na kama hawafanyi, unadhani nani wa kulaumiwa?
 
kuna mambo yanafikirisha sana. kwa jinsi nilivyoelewa hili bandiko ni dhahiri watanzania wengi bado wana makovu ya uchaguzi uliopita mioyoni mwao. ni wakaati sasa wa kuyaponya. lakini mfalme anazidi kuyaongeza kwa lugha na matendo yake
 
Ni kuhusu mentality tu! Ukifahamu kuwa gerezani Ni sehemu ya Kumtrekebisha mtu ili akitoka awe Raia Mwema, hatutawakomoa Wafungwa. Najua Wafungwa wanazalisha Sana hususani chakula, Tatizo hicho chakula kinaenda wapi? Wafungwa wetu Wana mlo mmoja kwa siku, hiyo nguvu ya kutaka wa overwork wanaitoa wapi? Hawa Wafungwa wanajengewa skills zipi zinazowawezesha kufanya uzalishaji wenye tija? Mfano gereza la Karanga Moshi wanazalisha Viatu, ukija Tabora naona wanatengeneza Sana furnitures, haya magereza mengine yanawajengaje Wafungwa? Au ndo tuwakomoe? Tuondokane na Mentality za KIKOLONI na tuwe na jukumu la KUWAREKEBISHA Hawa ndugu zetu ili wakirudi mtaani wawe RAIA WEMA, wenye KUWAJIBIKA! WAPEWE HAKI ZAO ZA MSINGI HUKOHUKO WALIPO, NAJUA HAKI PEKEE MTU ANAYONYANG'ANYWA BAADA YA HUKUMU NI HAKI YA KUWA HURU, HAKI NYINGINE ZOTE ZINABAKI PALEPALE, WAZALISHE CHAKULA, ILA NAO WALE MILO ANAYOKULA MTU YEYOTE, WAPEWE MUDA WA MICHEZO, WALALE JIONI BADALA YA ALASIRI, HAKI ZAO ZA KUABUDU ZIHESHIMIWE, NK!

TUSIWAKOMOE, TUWAREKEBISHE!
 
Jini Kisiranii
Usi generalise mambo, kila nchi inautaratibu wake. Nchi kama Norway wafungwa hawafanyi kazi kabisa na wanawekewa TV. Nchi kama China wafungwa wanafanyishwa kazi hasa, ila usisahau wafungwa wanahaki zao ndio maana China wanalalamikiwa kukiuka haki za binadamu wanapowatumikisha wafungwa katika kuzalisha bidhaa kwaajili ya biashara. Sisi wafugwa wameambiwa wazalishe chakula wajilishe, hapo sioni kosa maana hata vitabu vitakatifu vinasema asiyefanya kazi na asile. Ni kweli kuna wengine wapo magerezani kwa makosa ya kubambikizwa ingawa hajui idadi, la msingi tu ni kwamba wasitumikishwe kupita kiasi ubinadamu utumike
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom