Epukeni bidhaa za Game Mlimani City!

Epukeni bidhaa za Game Mlimani City!

Lole Gwakisa

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2008
Posts
4,773
Reaction score
2,383
Wanunuzi wa bidhaa pale GAME Mlimani Sity jihadharini na bidhaa hizo.Kuna tetesi kuwa bidhaa nyingi hapo dukani ni mbovu na zina matatizo.Mimi mwenyewe nienunua karibu bidhaa tatu ambazo ziliharibika kipindi kifupi tu baada ya matumizi.These items are used and repacked!!!
 
Taarifa hizi tulishawatumia TBS na TFDA wafuatilie kwa ukaribu kwani wafanyakazi wa Game wenyewe walituhabarisha juu ya hili. Kama wanataka facts tunaweza kuziweka hapa pindi zikihitajika!

Not only Game, hata Shoprite nao walewale.
 
Ingekuwa busara kama mkitupa mfano wa bidhaa hizo za kuwanazo makini. Ni kama nini mikate?blanket?Soda?Nyama? freezer? nini wakuu ni vyakula au music system.
 
Taarifa hizi tulishawatumia TBS na TFDA wafuatilie kwa ukaribu kwani wafanyakazi wa Game wenyewe walituhabarisha juu ya hili. Kama wanataka facts tunaweza kuziweka hapa pindi zikihitajika!

Not only Game, hata Shoprite nao walewale.

Invisible,

Hivi kwanini kama kuna matatizo pasifungwe tu kwa muda maka hapo watakopokamilisha uchunguzi?mie huwa nashangaa sana nchi yangu inavyoendeshwa.

Mataka kakosea ,kwanini asifukuzwe kwanza!Shame
 
Suala la bidhaa ambazo hazikidhi viwango kwa Tanzania nafikiri ni tatizo kubwa kwa sasa ambalo naweza kusema ni zaidi ya ugonjwa wa malaria ama ukimwi. Bidhaa hizi zinaanzia vyakula vya binadamu, madawa, vifaa vya nyumbani, nguo na vyombo vya usafiri. Wakuu naomba hili la GAME na bidhaa feki lipigiwe kelele kwa nguvu zote na lisishie hapo kwani Samora, Kariakoo na sehemu nyinginezo bidhaa hizi zimezagaa mno na nyingi zinatoka China, Middle East na Far East.
 
Mnaposema bidhaa mbovu mimi roho inaniuma sana nimetokea kuopoa friji pale na gurantee mwaka mmoja sasa ni mbovu mmmmh machungu.
 
Vyakula kwa sana ndivyo tatizo katika maduka haya. Baada ya kuarifiwa juu ya hili tulijaribu kuziarifu mamlaka husika zifuatilie, nadhani walipuuza. Impact yake ni watanzania kuugua magonjwa yasiyoeleweka!
 
Mnaposema bidhaa mbovu mimi roho inaniuma sana nimetokea kuopoa friji pale na gurantee mwaka mmoja sasa ni mbovu mmmmh machungu.
Upuuzi wa kuwambia watanzania kuwa wana guarantee ya mwaka ndio unaowaingiza hasara. Vitu vingi wanavyouza hawa Game viko chini ya viwango. Vingi vyake vinang'ara mle dukani lakini ni fake sana. TBS walisema wanafuatilia, inaelekea kuna watu washapewa za sikukuu wakakaa kimya. Ni wakati wa wao kuchukua hatua kali dhidi ya wafanyabiashara wa namna hii.

Aidha nadhani Tume ya Ushindani ingeingilia kati suala hili
 
Vyakula kwa sana ndivyo tatizo katika maduka haya. Baada ya kuarifiwa juu ya hili tulijaribu kuziarifu mamlaka husika zifuatilie, nadhani walipuuza. Impact yake ni watanzania kuugua magonjwa yasiyoeleweka!

Duu?? twafa mwe!
 
Ufisadi kila kona.. Sasa tukimbilie wapi wajameni? Hivi mwenye duka ni Muhindi?
 
Duu?? twafa mwe!

Rwabungiri, hakuna kukata tamaa, inatakiwa wote tupige kelele, nchi inageuzwa kama jaa, bidhaa feki toka China. Mavitu yaliyotumika toka Japan, UK, USA nk. Na hatuna uangalizi wa hivi vitu, Marekani yaliingizwa ma wanasesere (dolls) toka China, wakachunguza wakagundua yana "Lead Elements" kwa ndani, ikaagizwa yote mpaka yaliyo madukani yarudishwe China, sasa tujiulize TZ vingapi vinaingia na kuuzwa. Dawa za kichina zinatembezwa mikononi, bado tunakubali, vitu sensitive kama Dawa tunaruhusu vitembezwe mikononi na kuuziwa raia?. Hivi hawa jamaa wanaoharibu TVs, Nyaya za Umeme nk wa Tume ya Ushindani wa Haki (Fair Competition Commission-FCC) wamezidiwa ama ndio 10%, huyu aingize bidhaa ziharibiwe na mwingine aingize zilezile ziwepo sokoni?.
 
Kila siku najiuliza hao TFDA, TBS na mkemia mkuu wa serikali kazi yao nini hasa ? what are their core duties ?
 
wakati mwingine huwa wanasema hawana wataalamu wa kukagua bidhaa hizo na vifaa ili kuweza kudhibitisha na kuchukuliwa hatua
 
wewe bado una mawazo wa kwenda motoni na mbinguni uko ulimwengu wa ngapi kijana
 
Nilinunua ka'home theatre (LG)' kangu pale kama mwaka mmoja na kitu uliopita lakini hivi sasa kanachanganyiwa....in short ni mbovu. (unlucky me, the so called warrantee has already expired)
 
munashindwa kuelewa kuwa tbs na tfda sio wataalamu wakugundua vyakula vilivyoalibika ila hayo ni majengo yanayoajiri watu waliomeza desa,mkaddhani ni wataalamu

Mfano maziwa mpaka africa kusini wachunguze ndo na wattalamu wetu waliakiti hapa,,subiri s/a wafanye uchunguzi wakimaliza watawapa taarifa wataalamu wetu watoe ripoti.
 
Nilinunua ka'home theatre (LG)' kangu pale kama mwaka mmoja na kitu uliopita lakini hivi sasa kanachanganyiwa....in short ni mbovu. (unlucky me, the so called warrantee has already expired)

Mini nilinunua jiko la gesi zaidi ya mwaka mmoja uliopita na bado linafanya kazi vizuri (labda ni kwa ajili ya matunzo). lakini juzijuiz nimenunua microwave na toaster, ngoja niviangalie vitafanyaje kazi, labda na mimi nitakuwa kati ya waathirika sasa hivi. Vikileta longolongo tu hawanipati tena maana nilikuwa nadunduliza nikanunue fiji kubwa hapohapo
 
Hawa TBS hawjui nao madhara watayapata since ivyo vitu vitaingia kwenye mzunguko watashangaa watoto wao au nduugu zao wanaanza ugua magonjwa ya ajabu.
Mbona yule mama wa TFDA namwonaga yuko serious u meana nao wana TAAARIFA alafu hawajaact?
Isije ikawa wamepozwa.
Alafu nasi raia tuna matatizo tatizo likitokea report kwa wahusika haraka tena ufanye follow up kama wametekeleza wakipuuza unajilipua kwa namna nyingine kwa ushahidi ulio zahili.
Lazima kuwe na collective responcibility inchi ni yetu sote wewe au mimi twaweza iharibu sio TFDA AU TBS peke yao.
Play your part it must be done
 
Back
Top Bottom