funzadume
JF-Expert Member
- Jan 28, 2010
- 13,650
- 21,485
Leo nimekaa najikumbusha mambo ya zamani, enzi za Mwl nakumbuka kuna demu mmoja nilikuwa namvizia sasa tekinolojia ya kumtoa kwao kama simu ilikuwa hamna na mimi nilikuwa nakaribia kufungua shule kwa hiyo nikawa napita pita kwao ili hata nimuone nimwombe anuani yake ili nijieleze kwa barua (domo zege enzi hizo):smile-big:
sasa nikawa najipitisha pale karibu siku tatu lakini wapi sikubahatika kukutana nae, sasa kuna siku nikaamua kumtuma mtoto mdogo akaniitie, yule dogo si akaenda kumwambia mbele ya wazazi wake, wazazi wakamuuliza yuko wapi akasema sehemu niliyojibanza kichochoroni basi wazazi wote wawili wakatoka kuja pale nilipo baada ya kuwaona nilitoka mkuku kama mwizi jioni wakaja home kumweleza mdingi. Mdingi akaniwakia akanionya nikirudia hanipi tena hela ya matumizi shuleni (boarding)
hebu tukumbushane vimikasa vya enzi za Mwl kama kuandika barua ya kurasa tatu, kusafiri usiku kwenda shule n.k