Tunapitia mengi katika kutafuta. Tusikate tamaa (Kutoka kuwa walimu wa nursery hadi mkufunzi wa elimu ya juu)

Ahmet

JF-Expert Member
Oct 15, 2019
1,537
3,404
Aisee maisha yana kila aina ya furaha na karaha, tunapitia mengi lakini mwisho wa watu wengi ni mzuri, amini hivyo.

Nakumbuka namaliza chuo ile sina hili wala lile, naingia mtaani na mabaki ya boom (kiinua mgongo), with hope nitakuja kutoboa tu. But kitaa ndio hichoo kikaniita mzee. Daah mdogo mdogo siku zikaenda, wiki, miezi ikapita. Kuja kustuka mwaka umekata.

Hapo sina chochote cha kuniingizia kipato, kiinua mgongo nacho kikaisha kitambo, nikajisemea sasa mtaa unanikaribisha rasmi. Ukiangalia huku kweusi, huku kweusi. (Huku pii, huku pii), daah🤔.

Huu ndio muda ambao wale wadada nilioahidiana nao ndoa, wakaanza kuolewa. Daah Leo unasikia prisca kaolewa, kesho fatuma nae kaolewa. Wachumba wa vyuoni wengi waliolewa alafu nikijiangalia mimi sina hata ela la kununua maji na sina hata njia ya kuipata, labda niombe.

Baada maisha kunipiga kisawasawa, nikaona bora nikajitolee shule niliyosoma O-level, nikaandika barua, then nikaitwa, nikapewa madarasa ya kufundisha. But kujitolea ndio kukawa kujitolea Kweli. Ikakata miezi mitatu bila malipo, nilikuwa ni kama mwanafunzi niliechangamka tu maana sabuni ya kufulia nategemea nyumbani, kula nyumbani, mpaka Kuna siku Maza akaniuliza hivi wewe huko shuleni hupewi hata ela ya sabuni, nikamwambia ndio hivyo, dah basi Maza alikuwa anaponda sana elimu ukizingatia na bro nae yuko kitaa tangu alipomaliza chuo 2015.

Kuna mshikaji wangu (nilisoma nae primary) akanipa connection ya kazi shule moja hivi ya nursery. Nikasema ni bora nifundishe nursery nipate chochote kuliko kukomaa na shule ambayo haikupi hata sabuni. Nikafanya kweli bhana, nikachora barua, nikapeleka kwa mkurugenzi, akaipokea, tukapiga story sana na yule mkurugenzi.

Akanishawishi nifanye kazi pale, ingawa mimi ni degree holder lakini nitaweza tu hiyo kazi na akaniambia usijali maneno ya watu kwani siku zote walimu wa nursery wanadharaulika na wao huonekana kama wana tabia za kitoto. Basi akaniahidi atanilipa 150k per month. Ilikuwa ni jumamosi, Basi mkurugenzi akaniambia nikaage nilipokuwa nafundisha na jumatatu nikaanza kazi rasmi.

Ilikuwa sina experience na kufundisha nursery, sina hata ABC, but nikawa najifunza kwa wenzangu wanafanyaje, shule ilikuwa na walimu wa nne, kwaiyo mimi nikawa wa tano. Siku zikaenda bhana nikaanza kuzoea taratiibuu. Nafasi za kazi ya ualimu zilitangazwa mara kadhaa na TAMISEMI lakini sikufanikiwa kupata kabisa, Nikaendelea kukomaa na kazi yangu ya ualimu wa nursery.

Ndugu zangu kufundisha nursery sio kazi rahisi hata kidogo, kwanza muda wote unatakiwa kuwa muangalifu, ukizubaa kidogo tu, watoto washaumizana. Muda wote unatakiwa kutuliza kelele na kuwasimamia watoto kwa kila wanachokifanya.

Mwl pia unatakiwa kufanya usafi wa darasa lako, kujaza maji chooni na kudeki vyoo ikifika zamu yako. Daah ilikuwa ikifika zamu yangu kudeki vyoo nilikuwa najisemea mwenyewe, "eti nilikuwa best student mimi na GPA yangu ya 4+, daah😔". Kuna siku unakuta mtoto kajichafua (kajishushia mzigo nguoni) alaf walimu wa kike hawapo, aisee hapo lazima mtoto awe safi ndio arudi kwao. Nilikuwa nawaza sana siku linalotokea tukio hili. Ila nilichukulia ni maisha ya kawaida, na kwakua niliishi vizuri na walimu wenzangu basi siku zilisonga, nikazoea kazi.

Watoto walinipenda sana na wakawa rafiki zangu, hawakuniogopa ikawa mpaka wananikumbuka wakiwa kwao na wazazi wao. Nilijituma katika kazi, kuimba kwa sana, ikawa nachora picha naweka ukutani. Mpaka nimekuwa expert katika elimu ya watoto.

Nikajichanga mpaka nikanunua pikipiki kwa mtu. Ikawa inaniingizia pesa kidogo kwenye bodaboda na kwa usafiri binafsi.

Sasa nikasema nisikae kizembe, acha sasa nipambane na PSRS. nikakamilisha kujaza ajira portal yangu, nikacertify vyeti vyote nikawa tayari kwa mapambano. Nikaomba kazi kadhaa, nikawa shortlisted lakini nikaamua kutoenda kwenye usaili ukizingatia watu walioitwa ni wengi na nafasi ni moja moja. Nikaendelea kusubiri.

Zikatangazwa nafasi Mbalimbali vyuoni, nafasi za TAs, assistant lecturers na lecturers, research fellows na nyengine nyingi. Nikasema acha sasa niombe kwelikweli kwenye hizi nafasi. Nikaomba vyuo kadhaa na nikawa shortlisted almost kote. Yule mkurugenzi wa pale napofundisha hakuwa na shida kabisa, nilimuaga naenda kwenye interview na alikubali bila shida yeyote. Nikatumia pesa zangu mwenyewe kwenda kwenye interview na kila kitu nilijihudumia mwenyewe (nilijimudu kutokana na mshahara wa pale shuleni).

Interview yangu ya kwanza ya utumishi niliifanya pale MUCE, huwezi amini, interview yangu ya kwanza tu nikafanikiwa kuingia oral, then nikaja interview ya pili ya IAE, nayo nikafanikiwa kuingia oral, Sasa nikaona green light inawaka. Nikapiga na ya MUHAS ambayo iyo ilikuwa ni oral tu. Sasa kimbembe majibu yalipoanza kutoka. Yakatoka ya MUHAS, sikupata. MUCE wakapigiwa simu juu kwa juu, nikaja kupata taarifa baada kama ya wiki hivi kuwa watu walishaitwa huko. Sasa ikabaki moja tu ya IAE, Aisee hiki kipindi nilimuomba sana Mungu, Nikiona njia pekee ni kumkabidhi Mungu lile nalolipenda ili yeye awe muamuzi.

Hatimae siku ikafika, ilikuwa kama saa saba usiku natoka kucheki game moja ya kombe la Dunia. Kuingia PSRS naona mzigo wa IAE huu hapa. Kucheki jina langu limo. Daah!! nikaanza kujiuliza hivi huyu ni mimi au, naota au haya majina ya kuitwa kwenye interview. Daah basi nikafurahi mwenyewe usiku ule maana watu walikuwa wameshalala.

Then nikamuaga mkurugenzi wangu wa pale nilipokuwa nafundisha, yeye binafsi alifurahi saana kuona kijana wake nimechaguliwa kulitumikia Kwa namna nyengine. Baasi tuliongea sana na mkurugenzi, akanihusia jinsi ya kuishi katika utumishi wa Umma. Na baada ya mazungumzo marefu akanikadhi fedha kiasi Cha elfu 70 kama pongezi na shukrani Kwa huduma niliyoitoa pale, aisee nilishukuru sana.

Then nikafanya taratibu zote za ajira na sasa ni mtumishi mpya wa Umma. Najua huku pia kuna changamoto zake lakini nafurahia mazingira mapya ya kazi.

Kupata kazi ni jambo la kawaida na si kitu cha kutangazwa lakini naamini kuna la kujifunza katika kila historia ya mtu. Naamini kila mwenye kutafuta jambo fulani basi ipo siku atalipata.
 
Aisee maisha yana kila aina ya furaha na karaha, tunapitia mengi lakini mwisho wa watu wengi ni mzuri, amini hivyo.

Nakumbuka namaliza chuo ile sina hili wala lile, naingia mtaani na mabaki ya boom (kiinua mgongo), with hope nitakuja kutoboa tu. But kitaa ndio hichoo kikaniita mzee. Daah mdogo mdogo siku zikaenda, wiki, miezi ikapita. Kuja kustuka mwaka umekata.

Hapo sina chochote cha kuniingizia kipato, kiinua mgongo nacho kikaisha kitambo, nikajisemea sasa mtaa unanikaribisha rasmi. Ukiangalia huku kweusi, huku kweusi. (Huku pii, huku pii), daah.

Huu ndio muda ambao wale wadada nilioahidiana nao ndoa, wakaanza kuolewa. Daah Leo unasikia prisca kaolewa, kesho fatuma nae kaolewa. Wachumba wa vyuoni wengi waliolewa alafu nikijiangalia mimi sina hata ela la kununua maji na sina hata njia ya kuipata, labda niombe.

Baada maisha kunipiga kisawasawa, nikaona bora nikajitolee shule niliyosoma O-level, nikaandika barua, then nikaitwa, nikapewa madarasa ya kufundisha. But kujitolea ndio kukawa kujitolea Kweli. Ikakata miezi mitatu bila malipo, nilikuwa ni kama mwanafunzi niliechangamka tu maana sabuni ya kufulia nategemea nyumbani, kula nyumbani, mpaka Kuna siku Maza akaniuliza hivi wewe huko shuleni hupewi hata ela ya sabuni, nikamwambia ndio hivyo, dah basi Maza alikuwa anaponda sana elimu ukizingatia na bro nae yuko kitaa tangu alipomaliza chuo 2015.

Kuna mshikaji wangu (nilisoma nae primary) akanipa connection ya kazi shule moja hivi ya nursery. Nikasema ni bora nifundishe nursery nipate chochote kuliko kukomaa na shule ambayo haikupi hata sabuni. Nikafanya kweli bhana, nikachora barua, nikapeleka kwa mkurugenzi, akaipokea, tukapiga story sana na yule mkurugenzi.

Akanishawishi nifanye kazi pale, ingawa mimi ni degree holder lakini nitaweza tu hiyo kazi na akaniambia usijali maneno ya watu kwani siku zote walimu wa nursery wanadharaulika na wao huonekana kama wana tabia za kitoto. Basi akaniahidi atanilipa 150k per month. Ilikuwa ni jumamosi, Basi mkurugenzi akaniambia nikaage nilipokuwa nafundisha na jumatatu nikaanza kazi rasmi.

Ilikuwa sina experience na kufundisha nursery, sina hata ABC, but nikawa najifunza kwa wenzangu wanafanyaje, shule ilikuwa na walimu wa nne, kwaiyo mimi nikawa wa tano. Siku zikaenda bhana nikaanza kuzoea taratiibuu. Nafasi za kazi ya ualimu zilitangazwa mara kadhaa na TAMISEMI lakini sikufanikiwa kupata kabisa, Nikaendelea kukomaa na kazi yangu ya ualimu wa nursery.

Ndugu zangu kufundisha nursery sio kazi rahisi hata kidogo, kwanza muda wote unatakiwa kuwa muangalifu, ukizubaa kidogo tu, watoto washaumizana. Muda wote unatakiwa kutuliza kelele na kuwasimamia watoto kwa kila wanachokifanya.

Mwl pia unatakiwa kufanya usafi wa darasa lako, kujaza maji chooni na kudeki vyoo ikifika zamu yako. Daah ilikuwa ikifika zamu yangu kudeki vyoo nilikuwa najisemea mwenyewe, "eti nilikuwa best student mimi na GPA yangu ya 4+, daah". Kuna siku unakuta mtoto kajichafua (kajishushia mzigo nguoni) alaf walimu wa kike hawapo, aisee hapo lazima mtoto awe safi ndio arudi kwao. Nilikuwa nawaza sana siku linalotokea tukio hili. Ila nilichukulia ni maisha ya kawaida, na kwakua niliishi vizuri na walimu wenzangu basi siku zilisonga, nikazoea kazi.

Watoto walinipenda sana na wakawa rafiki zangu, hawakuniogopa ikawa mpaka wananikumbuka wakiwa kwao na wazazi wao. Nilijituma katika kazi, kuimba kwa sana, ikawa nachora picha naweka ukutani. Mpaka nimekuwa expert katika elimu ya watoto.

Nikajichanga mpaka nikanunua pikipiki kwa mtu. Ikawa inaniingizia pesa kidogo kwenye bodaboda na kwa usafiri binafsi.

Sasa nikasema nisikae kizembe, acha sasa nipambane na PSRS. nikakamilisha kujaza ajira portal yangu, nikacertify vyeti vyote nikawa tayari kwa mapambano. Nikaomba kazi kadhaa, nikawa shortlisted lakini nikaamua kutoenda kwenye usaili ukizingatia watu walioitwa ni wengi na nafasi ni moja moja. Nikaendelea kusubiri.

Zikatangazwa nafasi Mbalimbali vyuoni, nafasi za TAs, assistant lecturers na lecturers, research fellows na nyengine nyingi. Nikasema acha sasa niombe kwelikweli kwenye hizi nafasi. Nikaomba vyuo kadhaa na nikawa shortlisted almost kote. Yule mkurugenzi wa pale napofundisha hakuwa na shida kabisa, nilimuaga naenda kwenye interview na alikubali bila shida yeyote. Nikatumia pesa zangu mwenyewe kwenda kwenye interview na kila kitu nilijihudumia mwenyewe (nilijimudu kutokana na mshahara wa pale shuleni).

Interview yangu ya kwanza ya utumishi niliifanya pale MUCE, huwezi amini, interview yangu ya kwanza tu nikafanikiwa kuingia oral, then nikaja interview ya pili ya IAE, nayo nikafanikiwa kuingia oral, Sasa nikaona green light inawaka. Nikapiga na ya MUHAS ambayo iyo ilikuwa ni oral tu. Sasa kimbembe majibu yalipoanza kutoka. Yakatoka ya MUHAS, sikupata. MUCE wakapigiwa simu juu kwa juu, nikaja kupata taarifa baada kama ya wiki hivi kuwa watu walishaitwa huko. Sasa ikabaki moja tu ya IAE, Aisee hiki kipindi nilimuomba sana Mungu, Nikiona njia pekee ni kumkabidhi Mungu lile nalolipenda ili yeye awe muamuzi.

Hatimae siku ikafika, ilikuwa kama saa saba usiku natoka kucheki game moja ya kombe la Dunia. Kuingia PSRS naona mzigo wa IAE huu hapa. Kucheki jina langu limo. Daah!! nikaanza kujiuliza hivi huyu ni mimi au, naota au haya majina ya kuitwa kwenye interview. Daah basi nikafurahi mwenyewe usiku ule maana watu walikuwa wameshalala.

Then nikamuaga mkurugenzi wangu wa pale nilipokuwa nafundisha na sasa ni mtumishi mpya wa Umma. Najua huku pia kuna changamoto zake lakini nafurahia mazingira mapya ya kazi.

Kupata kazi ni jambo la kawaida na si kitu cha kutangazwa lakini naamini kuna la kujifunza katika kila historia ya mtu. Naamini kila mwenye kutafuta jambo fulani basi ipo siku atalipata.
Hongera sana mkuu,,, shukran zako zote zipeleke kwa Mungu aliye hai maana wahitaji wa hiyo nafasi ni wengi lakin neema imeangukia kwako,,, si akili Zako wala nguvu zako bali yeye aliye juu ya vyote!!
 
Hakika Mungu ni mkuu
 
Back
Top Bottom