Enzi zetu za utoto..........

EJM_

JF-Expert Member
Jul 8, 2011
3,836
2,093
Wengi wetu humu wakati tukiwa watoto tumekuwa katika mfumo tofauti kabisa wa maisha tofauti na yalivyo sasa kwa mfano mi nikiwa mtoto karibu kila sikukuu tulikuwa lazima tule pilau haijalishi ni xmas au eid na ikiwezekana na nguo mpya. Cine Clubndio yalikuwa maeneo yetu ya kutembelea na mashindano ya kudance nyimbo kama OPP, Ice Ice baby, Nzawisa na kadhalika.

Chakula favaourite kwa watoto enzi hizo kilikuwa ni wali maharage, mchezo mkubwa ukiwa mpira, kutengeneza magari, kuendesha baiskeli na kwenda kuogelea beach. Nakumbuka pale Cine Club ndipo tulikuwa tunapita kuoga tukitoka kuogelea enzi hizo pakiwa panamalizikia kuwa Tanzania Film Cooperation (TFC) nakumbuka tulikuwa tunaokota ile mikanda ya filamu za zamani inafanana na negative za picha za analojia hivi.

Dah Kombolela na kidali po........

Nini unakikumbuka enzi zako za utoto ambacho kwa watoto wa sasa hakipo?
 
Yaani wewe ulikuwa mtoto wakati ngoma ya OPP iko kwenye chati? Daaah ama kweli sasa wengine tumeanza kuzeeka lol.
 
Yaani wewe ulikuwa mtoto wakati ngoma ya OPP iko kwenye chati? Daaah ama kweli sasa wengine tumeanza kuzeeka lol.
Umeona eeh? Hasa wakati ule yule jamaa anaitwa Saleh Jabir alipotoa ile OPP ya kiswahili the Naught by nature wakatoa Hip Hop ree sijui hata sikumbuki jina lake
 
Haaa we si tulikuwa tunacheza wote KOMBOLELAAAAA! Yaani umesahau?

Ntachezaje kombolela na wazee mimi?
Au wewe ndo ulikua like fataki la mtaani kwetu? Maana lilikua linapenda kweli kukimbiza vibinti migombani.
 
Ntachezaje kombolela na wazee mimi?
Au wewe ndo ulikua like fataki la mtaani kwetu? Maana lilikua linapenda kweli kukimbiza vibinti migombani.
Dah kama we enzi hizo ulikuwa kibinti basi we ndio mzee halafu nakumbuka ulikuwa unapenda kuniomba nikusindikize ukitumwa.......hahahhaaa we nae bhana eti ulikuwa unaogopa kuvuka kale ka mto ka pale njiani
 
Mimi niliyekulia kijijini wakati mwengine sitaki kukumbuka life ilivyokuwa tafu huku kijijini kwetu. ratiba ilikuwa kuamka saa kumi na moja alfajiri kwenda kutegua nyavu za samaki ziwani, sas ana kale kaubaridi ka asubuhi, ukitoka hapo na manyavu yako pamoja na samaki wako waliopatikana ni kwenda shambani mpaka saa tisa ndo upate ugali wako wa mhogo na sato fresh ama san! Kale kalikuwa kajela aisee japo kamenifundisha maisha
 
Mbona hata sikua mtundu?
Watundu ni wale waliokua wanakimbizwa na Jr hapo.
Tena nimekukumbuka we wakati huo ulikuwa darasa la tano mi niko la pili ulikuwa kiranja wa mifagio shuleni
 
Dah kama we enzi hizo ulikuwa kibinti basi we ndio mzee halafu nakumbuka ulikuwa unapenda kuniomba nikusindikize ukitumwa.......hahahhaaa we nae bhana eti ulikuwa unaogopa kuvuka kale ka mto ka pale njiani

Mto tena?
Basi we utakua umetokea Sitimbe.
 
Mimi niliyekulia kijijini wakati mwengine sitaki kukumbuka life ilivyokuwa tafu huku kijijini kwetu. ratiba ilikuwa kuamka saa kumi na moja alfajiri kwenda kutegua nyavu za samaki ziwani, sas ana kale kaubaridi ka asubuhi, ukitoka hapo na manyavu yako pamoja na samaki wako waliopatikana ni kwenda shambani mpaka saa tisa ndo upate ugali wako wa mhogo na sato fresh ama san! Kale kalikuwa kajela aisee japo kamenifundisha maisha
Dah unakumbuka zile nyimbo mlizokuwa mnaimba wakati mnavuta kokoro?
 
Back
Top Bottom