Enzi zetu tulipokuwa Likizo za Shule Wazazi walikuwa wanatenga muda kutuboresha Kitaaluma Siku hizi Mtoto Lwake na Mzazi Lwake

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,738
109,175
Kuna Mzazi Mmoja nasubiria Mwanae akifeli Mitihani ya Kufunga mwaka na akimpiga nami nitatokea kwa nyuma kwa kumrushia Kitofa.

Kwanini?

Huyu Mzazi kwa hiizi Wiki Mbili za Likizo fupi za Shule za Msingi Tanzania nimekuwa nikimtaarifu kuwa Mwanae anashinda katika Kamari na Kubeti hivyo akamkanye na atumie Likizo hii Kumsaidia Kitaaluma Mwanae cha Kushangaza nae pia akienda aliko huyo Mwanae nae anaunganisha nae katika Kibeti huko kisha wanaungana Kunisema na kudai Mimi ni Mnoko na sitaki wapate Mawokoto ( Fedha )

Watoto wa Siku hizi labda leo Uncle wenu na Baba yenu niwasaidieni kwa Kuwaambia kuwa hata Sisi akina GENTAMYCINE enzi zetu huko Mashuleni tulikuwa Masela, Watukutu na Wahuni vile vile ila Kitaaluma tulikuwa tunafanya vyema kwani tuliweza Kuugawa muda wa kufanya kila Jambo tofauti na nyie wa sasa.

Kuna Mwenzenu Mmoja leo nimekutana nae cha Kushangaza Shule zinafunguliwa Kesho hajui Begi lake la Vitabu aliliweka wapi Siku ya Kufunga Likizo fupi.

Na kuna Mmoja huyu ndiyo nilitamani nimzabe Makofi kabisa ili nizimalizie Hasira zangu za Draw ya Simba SC jana Ndola nchini Zambia baada ya Kumuuliza Mwalimu Mkuu wake anaitwa nani hamjui na nikamuuliza Mji Mkuu wa Tanzania ni upi yaani Comfortably kabisa akanitajia Shinyanga.

Na nyie Walimu huko Mashuleni acheni tu Kula Mishahara bali jikiteni zaidi katika kuwajaza Maarifa Wanafunzi wa sasa kwani kiukweli kwa hawa ambao GENTAMYCINE nabahatika Kutwa kukutana nao sioni Aibu kusema kuwa Tanzania ya Miaka 25 ijayo itakuwa na Taifa la Mizuzu ( Mipumbavu ) mingi kuliko inavyodhaniwa hivyo Rasilimali Keki zetu zitachukuliwa kirahisi mno na wenye Akili Americans, Europeans na Asians.

Tuwasaidieni Watoto wetu Kitaaluma.
 
Mbona uzi ni mzuri wa kuelimisha? Au ulitaka aongelee mambo yako ya ushoga?
Nasikitika hujajua kuwa GENTAMYCINE ndiyo naziimarisha IDs za Wengine kwa kufanya zijulikane, ziwe Active na naziongezea Umaarufu hapa JamiiForums.

Anachokitaka huyo Mpumbavu ni Majibizano na Mimi ili nimuongezee Umaarufu wakati tayari ameshatutangazia kuwa Yeye ni Mwanaume Nusu Nusu ( Nyabenga )
 

Attachments

  • IMG-20230912-WA0013.jpg
    IMG-20230912-WA0013.jpg
    26.7 KB · Views: 2
Back
Top Bottom