Polisi wa Zanzibar kuwakamata watu kisa kuwakuta wakila mchana kipindi cha Ramadhan ni uvunjifu wa sheria za Nchi

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,866
Zanzibar sio Nchi inayoongozwa na Sheria za Kiislamu, Zanzibar ni nchi inayoongozwa na katiba huru.

Inakuwaje unamkamata mtu kwa sababu ya kutokufunga Ramadhan, ni wapi kwenye katiba wamesema kwamba usipofunga inapaswa kuswekwa Ndani. Mkianza kutuletea sheria za kiarabu Kwenye ardhi za Tanzania basi kuna uwezekano mkaleta pia mambo ya Udini na vikundi vyenye itikadi kali kama ilivyo kwenye majimbo ya Nchi ya Nigeria yanayoongozwa na sheria kali za kiislamu. Na maeneo hayo hayo ndio makazi ya vikundi kama Boko Boys au Boko Haram.

Uwezi kumlazimisha mtu kufunga kwa sababu hiyo ni kati yake yeye na MUNGU wake, ukimpazimisha mtu kufunga kama hajasadiki au kuridhia ni sawa na kutwanga maji tu kwa sababu hatopata swawabu yoyote kwa mujibu wa imani ya kiislamu atafunga kwa kuwaridhisha watu tu. Mwili ni wake, mbona hakikosa chakula hamuwapelekei kuwalazimisha wale kama jinsi mnavyowalazimisha kushinda njaa.

Badala ya kushurutisha watu kushinda njaa kwa lazima, wafundisheni misingi ya Dini ya kiislamu na wafundisheni umuhimu wa mfungo wa ramadhani hili mtu atambue umuhimu wa kufunga na afunge kiroho safi.

Sheria hiyo ya kamata kamata watu wasiofunga inakiuka haki za mtanzania na vifungu vya katiba.

Pia Soma:
Marufuku nyingine Zanzibar soma:

Yanayoendelea Zanzibar tusubiri majibu ya Wahanga na kuzaa gharika
 
Kukamata mtu kisa amekula mchana siyo ukandamizaji wa haki za binadamu?
Tundu Lisu mbona haukemei?

Hili wimbi la ukamataji watu huko Zanzibar limeagizwa na nani?

Katiba ya Tanzania inasemaje?
 
Tangu zamani hata kabla yake huu Utaratibu haukuwepo sasa sijui imekuwaje
 
Sio kweli labda huna kumbu kumbu.
Haijawahi kupita mfungo wowote bila watu kukamatwa kwa kula mchana huko Zanzibar.
 
Zanzibar sio Nchi inayoongozwa na Sheria za Kiislamu, Zanzibar ni nchi inayoongozwa na katiba huru.

Inakuwaje unamkamata mtu kwa sababu ya kutokufunga Ramadhan, ni wapi kwenye katiba wamesema kwamba usipofunga inapaswa kuswekwa Ndani. Mkianza kutuletea sheria za kiarabu Kwenye ardhi za Tanzania basi kuna uwezekano mkaleta pia mambo ya Udini na vikundi vyenye itikadi kali kama ilivyo kwenye majimbo ya Nchi ya Nigeria yanayoongozwa na sheria kali za kiislamu. Na maeneo hayo hayo ndio makazi ya vikundi kama Boko Boys au Boko Haram.

Uwezi kumlazimisha mtu kufunga kwa sababu hiyo ni kati yake yeye na MUNGU wake, ukimpazimisha mtu kufunga kama hajasadiki au kuridhia ni sawa na kutwanga maji tu kwa sababu hatopata swawabu yoyote kwa mujibu wa imani ya kiislamu atafunga kwa kuwaridhisha watu tu. Mwili ni wake, mbona hakikosa chakula hamuwapelekei kuwalazimisha wale kama jinsi mnavyowalazimisha kushinda njaa.

Badala ya kushurutisha watu kushinda njaa kwa lazima, wafundisheni misingi ya Dini ya kiislamu na wafundisheni umuhimu wa mfungo wa ramadhani hili mtu atambue umuhimu wa kufunga na afunge kiroho safi.

Sheria hiyo ya kamata kamata watu wasiofunga inakiuka haki za mtanzania na vifungu vya katiba.

Pia Soma:
- Watu 12 wakamatwa kwa kula hadharani mchana Zanzibar
Hiyo sheria ipo toka wewe hujazaliwa tii sheria bila shuruti huwezi baki kwenu tanganyika
 
Kukamata mtu kisa amekula mchana siyo ukandamizaji wa haki za binadamu?
Tundu Lisu mbona haukemei?

Hili wimbi la ukamataji watu huko Zanzibar limeagizwa na nani?

Katiba ya Tanzania inasemaje?
Wacha porojo hizo sheria zipo kabla wewe hujazaliwa tena hilo kosa hukumu yake ni mwaka mmoja jela na viboko 12 sita ukiingia na sita ukitoka tii sheria bila shuruti huwezi baki kwenu tanganyika
 
Zanzibar sio Nchi inayoongozwa na Sheria za Kiislamu, Zanzibar ni nchi inayoongozwa na katiba huru.

Inakuwaje unamkamata mtu kwa sababu ya kutokufunga Ramadhan, ni wapi kwenye katiba wamesema kwamba usipofunga inapaswa kuswekwa Ndani. Mkianza kutuletea sheria za kiarabu Kwenye ardhi za Tanzania basi kuna uwezekano mkaleta pia mambo ya Udini na vikundi vyenye itikadi kali kama ilivyo kwenye majimbo ya Nchi ya Nigeria yanayoongozwa na sheria kali za kiislamu. Na maeneo hayo hayo ndio makazi ya vikundi kama Boko Boys au Boko Haram.

Uwezi kumlazimisha mtu kufunga kwa sababu hiyo ni kati yake yeye na MUNGU wake, ukimpazimisha mtu kufunga kama hajasadiki au kuridhia ni sawa na kutwanga maji tu kwa sababu hatopata swawabu yoyote kwa mujibu wa imani ya kiislamu atafunga kwa kuwaridhisha watu tu. Mwili ni wake, mbona hakikosa chakula hamuwapelekei kuwalazimisha wale kama jinsi mnavyowalazimisha kushinda njaa.

Badala ya kushurutisha watu kushinda njaa kwa lazima, wafundisheni misingi ya Dini ya kiislamu na wafundisheni umuhimu wa mfungo wa ramadhani hili mtu atambue umuhimu wa kufunga na afunge kiroho safi.

Sheria hiyo ya kamata kamata watu wasiofunga inakiuka haki za mtanzania na vifungu vya katiba.

Pia Soma:
- Watu 12 wakamatwa kwa kula hadharani mchana Zanzibar
Kumbuka tu hilo kosa hukumu yake ni mwaka mmoja jela na viboko 12 sita ukiingia jela na sita ukitoka tii sheria bila shuruti huwezi baki kwenu tanganyika
 
Tangu zamani hata kabla yake huu Utaratibu haukuwepo sasa sijui imekuwaje
Hizo sheria zipo kabla wewe hujazaliwa tena hilo kosa hukumu yake ni mwaka mmoja jela na viboko 12 sita ukiingia jela na sita ukitoka tii sheria bila shuruti huwezi baki kwenu tanganyika
 
SAUMU YA RAMADHANI

Kufunga Saumu ni nguzo ya nne ya Kiislamu na hakika ya Kufunga ni kuacha kula na kunywa toka asubuhi mpaka magharibi kama Mungu alivyoamrisha. Na kuacha kila mambo mabaya, kama Qur'an tukufu isemavyo kwamba:-

يٰٓـاَيُّهَا الَّذِيۡنَ اٰمَنُوۡا كُتِبَ عَلَيۡکُمُ الصِّيَامُ کَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِيۡنَ مِنۡ قَبۡلِکُمۡ لَعَلَّكُمۡ تَتَّقُوۡنَۙ‏

Enyi mlioamini, mmelazimishwa kufunga Saumu kama walivyolazimishwa wa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu.

Kusudi la Saumu limeelezwa kuwa ni kupata Taq-waa, yaani, ucha-Mungu. Neno Taq-waa, linatumiwa katika Qur'an kwa maana tatu:
(1) Kuepukana na maumivu,
(2) kuepukana na dhambi,
(3) kufikia utakatifu ulio juu wa mambo ya kiroho.

Kufunga saumu ya Ramadhani ni lazima juu ya kila Mwislam isipokuwa watoto wadogo, wagonjwa, wadhaifu sana, wenye mimba, wanyonyeshao na wasafiri.

Ijapokuwa hakuna adhabu ya kimwili ikiwa mtu ataamua kutofunga, ila Mwenye kuacha kufunga saumu ya Ramadhani bila udhuru wowote anapata dhambi kubwa na mwenye kufunga kisha akafungua bila sababu basi juu yake afunge siku sitini kwa mfululizo, au alishe maskini sitini.

Mwezi wa Ramadhani ni mwezi mtukufu zaidi kwenye kalenda ya mwaka wa kiislamu. Ni mwezi pia unaofahamika kama mwezi wa toba, kipindi ambacho waumini wa dini hiyo wanajisogeza karibu zaidi na Mola wao kwa ibada mbalimbali ili wavune thawabu.

Ni dhahiri pia kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani kunakuwa na mabadiliko mengi katika mfumo wa maisha na matendo ya watu.

Katika nchi ambazo raia wake ni wa dini mbalimbali kama Afrika Mashariki, maswali mengi huibuka kipindi hiki juu ya nini kinatakiwa kifanyike ama kisifanyike. Wale ambao si waislamu huwa na maswali mengi juu ya nini wanaweza kufanya ama kutofanya mbele ya ndugu, jamaa au marafiki wa kiislamu.

Tendo kubwa ambalo linaonekana moja kwa moja kufanywa na waislamu katika kipindi hiki cha mfungo ni kujizuia kunywa na kula kutoka alfajiri (kuchomoza kwa jua) mpaka magharibi (kuzama kwa jua).

Haijalishi, mtu awe masikini ama tajiri, awe na chakula ndani ama asiwenacho, madhali wanakiri kwa yakini kuwa ni waislamu basi hujizuia kula na kunywa.

Katika mazingira yenye watu wa imani tofauti, mathalani mtaani, shuleni au hata kazini sio wote wanaofunga, na wengine hutembea na vyakula vyao.

SWALI HUWA, JE, NAWEZA KULA MBELE YAKO AU MBELE YA WATU WENGINE?

Jibu lake hutegemeana na mtu na mazingira husika. Kuna wale ambao hawana tatizo lolote kwa mtu kula mbele yake anapokuwa amefunga, ila wengine wanatafsiri ukifanya kitendo hicho kama kutowaheshimu na kuwapa majaribio ya kiimani kwa makusudi. Kama upo kazini ama shuleni, ni vyema zaidi ukatumia maeneo maalumu yaliyotengwa kwa chakula.

Mazingira ya eneo pia huchangia katika hili. Katika nchi nyingi ambazo zinafuata sheria za kiislamu, kula hadharani wakati wa mchana wa mwezi wa Ramadhani huwa ni kosa. Na ukifanya hivyo unaweza kujipata mikononi mwa vyombo vya usalama, Ambapo jambo hili sio sheria wala sio Fundisho la Islam sawa na Mtukufu Mtume Muhammad saw alivyotuelekeza na Kutufundisha.

Ndiyo maana Ramadhani kwa hakika inahusu kujiboresha katika ngazi zote: kujenga uhusiano wa kina zaidi na Mwenyezi Mungu, kutimiza vyema haki za wanadamu wenzetu, na kurekebisha maadili na matendo yetu wenyewe ili kuwa watu bora zaidi.

RUHUSA ZA MTU KULA NDANI YA MWEZI WA RAMADHANI.

1️⃣ Ugonjwa
Yaruhusiwa kwa mgonjwa kula ndani ya mwezi wa Ramadhani; kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

اَيَّامًا مَّعۡدُوۡدٰتٍؕ فَمَنۡ كَانَ مِنۡكُمۡ مَّرِيۡضًا اَوۡ عَلٰى سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنۡ اَيَّامٍ اُخَرَؕ وَعَلَى الَّذِيۡنَ يُطِيۡقُوۡنَهٗ فِدۡيَةٌ طَعَامُ مِسۡكِيۡنٍؕ فَمَنۡ تَطَوَّعَ خَيۡرًا فَهُوَ خَيۡرٌ لَّهٗ ؕ وَاَنۡ تَصُوۡمُوۡا خَيۡرٌ لَّـکُمۡ اِنۡ كُنۡتُمۡ تَعۡلَمُوۡنَ‏

Kwa siku zilizohesabiwa. Lakini miongoni mwenu awaye mgonjwa au katika safari, basi atimize hesabu katika siku zingine. Na wale wanaoweza, watoe fidia kwa kumlisha maskini. Na atakayefanya wema kwa radhi ya nafsi yake, basi ni bora kwake; na kama mkifunga ni bora kwenu, ikiwa mnajua.

2️⃣ Safari
Inaruhusiwa kwa msafiri kula ndani ya Mwezi wa Ramadhani, na inamlazimu kuilipa saumu hiyo baadaye, kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

اَيَّامًا مَّعۡدُوۡدٰتٍؕ فَمَنۡ كَانَ مِنۡكُمۡ مَّرِيۡضًا اَوۡ عَلٰى سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنۡ اَيَّامٍ اُخَرَ

Kwa siku zilizohesabiwa. Lakini miongoni mwenu awaye mgonjwa au katika safari...

3️⃣ Wajawazito na Wanyonyeshao n.k
 
Hizo sheria zipo kabla wewe hujazaliwa tena hilo kosa hukumu yake ni mwaka mmoja jela na viboko 12 sita ukiingia jela na sita ukitoka tii sheria bila shuruti huwezi baki kwenu tanganyika
Sawa mtakatifu unayeifahamu Kabisa mbingu ya kuishi siku ukifa
 
Zanzibar sio Nchi inayoongozwa na Sheria za Kiislamu, Zanzibar ni nchi inayoongozwa na katiba huru.

Inakuwaje unamkamata mtu kwa sababu ya kutokufunga Ramadhan, ni wapi kwenye katiba wamesema kwamba usipofunga inapaswa kuswekwa Ndani. Mkianza kutuletea sheria za kiarabu Kwenye ardhi za Tanzania basi kuna uwezekano mkaleta pia mambo ya Udini na vikundi vyenye itikadi kali kama ilivyo kwenye majimbo ya Nchi ya Nigeria yanayoongozwa na sheria kali za kiislamu. Na maeneo hayo hayo ndio makazi ya vikundi kama Boko Boys au Boko Haram.

Uwezi kumlazimisha mtu kufunga kwa sababu hiyo ni kati yake yeye na MUNGU wake, ukimpazimisha mtu kufunga kama hajasadiki au kuridhia ni sawa na kutwanga maji tu kwa sababu hatopata swawabu yoyote kwa mujibu wa imani ya kiislamu atafunga kwa kuwaridhisha watu tu. Mwili ni wake, mbona hakikosa chakula hamuwapelekei kuwalazimisha wale kama jinsi mnavyowalazimisha kushinda njaa.

Badala ya kushurutisha watu kushinda njaa kwa lazima, wafundisheni misingi ya Dini ya kiislamu na wafundisheni umuhimu wa mfungo wa ramadhani hili mtu atambue umuhimu wa kufunga na afunge kiroho safi.

Sheria hiyo ya kamata kamata watu wasiofunga inakiuka haki za mtanzania na vifungu vya katiba.

Pia Soma:
- Watu 12 wakamatwa kwa kula hadharani mchana Zanzibar
Sehemu yoyote yenye majority muslim, ipo siku watatska political islam ideology itawale maisha ya watu,
Hawa kenge ni wabaya sana, wanajifanya wema,, ngoja wawe wengi! Miaka ya 90 walianzisha chokochoko wakitaka kusiwe na bucha za nguruwe kwenye maeneo wanayoishi wa Islam wengi! Temeke,tandale,nk, wakavamia na kuvunja, alichowafanya Mkapa, mpaka kizazi kijacho hawatasahau
 
Zanzibar sio Nchi inayoongozwa na Sheria za Kiislamu, Zanzibar ni nchi inayoongozwa na katiba huru.

Inakuwaje unamkamata mtu kwa sababu ya kutokufunga Ramadhan, ni wapi kwenye katiba wamesema kwamba usipofunga inapaswa kuswekwa Ndani. Mkianza kutuletea sheria za kiarabu Kwenye ardhi za Tanzania basi kuna uwezekano mkaleta pia mambo ya Udini na vikundi vyenye itikadi kali kama ilivyo kwenye majimbo ya Nchi ya Nigeria yanayoongozwa na sheria kali za kiislamu. Na maeneo hayo hayo ndio makazi ya vikundi kama Boko Boys au Boko Haram.

Uwezi kumlazimisha mtu kufunga kwa sababu hiyo ni kati yake yeye na MUNGU wake, ukimpazimisha mtu kufunga kama hajasadiki au kuridhia ni sawa na kutwanga maji tu kwa sababu hatopata swawabu yoyote kwa mujibu wa imani ya kiislamu atafunga kwa kuwaridhisha watu tu. Mwili ni wake, mbona hakikosa chakula hamuwapelekei kuwalazimisha wale kama jinsi mnavyowalazimisha kushinda njaa.

Badala ya kushurutisha watu kushinda njaa kwa lazima, wafundisheni misingi ya Dini ya kiislamu na wafundisheni umuhimu wa mfungo wa ramadhani hili mtu atambue umuhimu wa kufunga na afunge kiroho safi.

Sheria hiyo ya kamata kamata watu wasiofunga inakiuka haki za mtanzania na vifungu vya katiba.

Pia Soma:
- Watu 12 wakamatwa kwa kula hadharani mchana Zanzibar
hajakamatwa kwa sababu hajafunga amekamatwa kwa sababu amekula hadharani
 
sheria yenu ya muungano haifanani na sheria ya zanzibar kwa baadhi ya mambo msiforce...utaratibu ufatwe.
 
Kuhusu watu kuadhibiwa kula hadharani ZANZIBAR hilo naliunga mkono. Imani za watu ziheshimiwe

Unajua nashindwa kuelewa watu wanatokwa na povu kwa suala dogo kama hili kwani haswa wakati taratibu za wenzetu zipo wazi?

ZANZIBAR hakuna aliyelazimishwa kufunga ispokua utaratibu wa kule unakataza mtu kula hadharani hasa kipindi hiki cha Mwezi mtukufu wa Ramadhan

Na mnajua ZANZIBAR asilimia 99.999 ni waislam, na lazima tamaduni za watu ziheshimiwe kama unataka kula mchana we kula tu lakini sio vizuri kula hadharani maana yake utakua unafundisha nini jamii?

Kwa huku bara hata mtu ukila ni sawa tu maana humu tumechanganyikana watu wa dini tofauti ZANZIBAR wengi ni waislam na nashangaa watu mnatokwa na mapovu kwenye hili

Ni ushetani mkubwa kutokua na haya na kwenda kula public mwezi wa ramadhan katika jamii ambayo ni waislam watupu kwanini usitafute mahala kwako au ndani kwako ukala?Kwanini ule hadharani?

Kuna mtu kahoji kwahiyo mbona sisi kwaresma huwa hatuwagusi waislam ambao unakuta hawajafunga?Swali ni mkristo yupi anafungaga kwaresma?Mimi nimekulia sehemu zenye Christian majority sijawahi kuona mtu kafunga hata kwa bahati mbaya....Kwahyo msipende kucompare dini za watu, kama mnaridhika imani ni nyie ila sio uislam.

Uislam sio dini ya masihara na mchezomchezo ndo maana ndo dini inakua kwa kasi kidunia na ipo tokea karne pamoja na kupigwa vita vya kimwili na kiroho.Watu washaacha dini yao ishaharibiwa huko na kuchezewa vya kutosha sasa wanataka uislam iwe dini ya hivyo hilo No!!

Mnaotokwa na mapovu kuhusu sakata la kula kumbukeni ZANZIBAR asilimia 99 ni waislam kwahyo tamaduni za walowengi ziheshimiwe..

Kama ulikua na mikiu yako ya kula ungeenda kujifungia ndani ule kwa raha zako!! Msipende kuwaponza waliofunga!!Mimi naunga mkono wachapwe tu.kila mtu aheshimu imani ya mwenzake kama ambavyo yake huheshimiwa.

Binafsi yangu nimeishi kwenye jamii nyingine ambazo ni za imani tofauti na mimi au tamaduni tofauti ila nilifanikiwa pakubwa kuishi nao kwasababu niliishi kwa kutii taratibu zao na mambo yalienda vizuri tu.
 
Back
Top Bottom