Elimu ya Mnyika

Elimu ya Mnyika

Status
Not open for further replies.
Basi tumetosheka na elimu ya Mnyika tujaili na ya Jaa people, Deo Sanga wa CCM na hata Lukuvi anaeongoza kwa kuwa na certificate nyingi kuliko wabunge wote.
 
Mnyika rudi shule kama Mrema.

Ritz sio ajabu mtu kurudi shule kusoma. Mrema ni mmmojawapo wa viongozi wengi wanaoendelea kusoma, wakiwemo wabunge, mawaziri na wakuu wa taasisi za umma na binafsi.
 
point 15 ni sawa na e tatu.

ilikuwaje maua a tisa lakini tambaza akaruka kutoka a mpaka e. mtu mwenye uwezo wa shule hata akijisomea mwenyewe nyumbani hawezi kupata e.

maua walikuwa wanaibiwa mitihani nini.

mnyika weka cv yako halali bungeni.
 
Ishu sio kwamba Mnyika ni jembe, shoka au koleo, ishu ni je, anasema ukweli kuhusu elimu yake???
Iwapo hasemi ukweli, je ni kwa malengo gani? na je, aaminiwe kwenye lipi?
 
1. Elimu ya mnyika kwangu mimi sio kitu muhimu sana hasa nikiangalia mchango wake kwa wananchi wa Ubungo, michango yake na hoja zake Bungeni pamoja na mchango wake na nafasi yake kwenye chadema.

2.Ukiangalia elimu za watu au cv zao na michango au mchango wake kwa taifa na vyama vyao utaona kuwa hoja hii haina mashiko mujarabu. Mfano weka kwenye mzani hoja kuhusu maji kati ya mnyika na profesa maghembe. Pima ufanisi wa dr kawambwa wizara ya elimu na michango yake bungeni, pima kwenye mzani hoja na michango ya dr nchimbi na mnyika wawapo bungeni. Lakini nenda mbali zaidi chuja mchango wa dr balali kwa taifa hili kwa miaka yake 5 kama governor na pima mchango wa mnyika wa miaka 2 kama mbunge.

3. Ifike mahali tuheshimu sana michango ya watu na uwezo wao katika taifa kuliko kuangalia kigezo cha elimu pekee, mfano baba wa taifa hili Mwl Nyerere hakuwa na elimu ya PhD lakini aliyo yafanya ni zaidi ya elimu ya kwenye mashule yanayo fundishwa na walimu hapa duniani.

4. Huko duniani! Kuna mijitu ni college drop out lakini michango yao kwenye huu ulimwengu huwezi kuifananisha na wasomi alio bobea. Mfano ni Bill gates na kijana mmiliki wa facebook. Wote walinusa elimu ya chuo kikuu kisha wakatokomea mitaani kufanya mambo yao! Mshindo wa walicho kifanya hata mwenye ukame wa maono anakijua.

5. Wanao hoji elimu ya mnyika wako sahihi na wanaweza kupatiwa majibu kutoka kwa mhusika kama ataona inafaa lakini kwangu mimi sioni kuwa ni swala muhimu sana na hitaji kwa taifa hili au wananchi wa ubungo kwa sasa. Wananchi wa ubungo wanahitaji waone maji yanayotoka muda wote sio elimu kubwa kwenye vyeti vya Mnyika huku wakiwa hawana maji.

6. Mkwamo wetu kama taifa kwa sasa sio elimu ya mnyika ambaye tayari alisha maliza kidato cha sita. Tuna changamoto nyingi kama taifa ambazo kwa uelewa na umakini wa Mnyika tukimtumia vizuri kama mbunge na kiongozi tunaweza kuondoka kwenye hili tope tulilomo au ingalau kufanyia kazi mawazo yake ili wananchi wa ubungo wapate maji safi na salama muda wote.

Sikumbuki ni mzungu gani alisema "Simple mind discuss about people..."

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Ishu sio kwamba Mnyika ni jembe, shoka au koleo, ishu ni je, anasema ukweli kuhusu elimu yake???
Iwapo hasemi ukweli, je ni kwa malengo gani? na je, aaminiwe kwenye lipi?

Mkuu ZeMarcopolo sikuwa nafahamu kama na wewe ni M.puuzi kwa Kiwango hiki.

Yaani Unataka Mnyika apande Jukwaani asema

1. Nilimaliza Shule ya Msingi mwaka 1994 Nikaongongoza Kitaifa?
2. Nikamaliza Form Four Mwaka 1998 Niokaongoza Kitaifa?
3. Nikamaliza Tambaza Form Six Mwaka 2001 Nikapata Div Three?
4. Nikajiunga Chuo nikapata BBA?

Ama Hakika Mnyika akijitokeza na akazungumza hayo anatakuwa M.puuzi zaidi yako
 
Last edited by a moderator:
Mkuu ZeMarcopolo sikuwa nafahamu kama na wewe ni M.puuzi kwa Kiwango hiki.

Yaani Unataka Mnyika apande Jukwaani asema

1. Nilimaliza Shule ya Msingi mwaka 1994 Nikaongongoza Kitaifa?
2. Nikamaliza Form Four Mwaka 1998 Niokaongoza Kitaifa?
3. Nikamaliza Tambaza Form Six Mwaka 2001 Nikapata Div Three?
4. Nikajiunga Chuo nikapata BBA?

Ama Hakika Mnyika akijitokeza na akazungumza hayo anatakuwa M.puuzi zaidi yako

Matusi ni hulka tuliyokwishaizoea kutoka kwa wafuasi wa chadema.
Swali liko palepale, Mnyika anayo degree au hana?
 
Matusi ni hulka tuliyokwishaizoea kutoka kwa wafuasi wa chadema.
Swali liko palepale, Mnyika anayo degree au hana?

Nimekuuliza Unataka Jibu kutoka kwa Mnyika? Kama Ndivyo unavyotegemea basi Wewe ni M.puuzi sana na Kama Mnyika atajitokeza kujibu hayo Mswali hapo Juu naye atakuwa M.puuzi zaidi yako
 
Mijitu inashadadia tu hapa Elimu ya Mnyika Elimu ya Mnyika wakati wenyewe elimu zao za Kuunga Unga

Unaweza kukuta mtu kama Ritz au ZeMarcopolo

1. Darasa la saba alifeli kama Mwigulu akatumia jina la Mtu kurudia huko Nangurukuru
2. Form ame re seat Mpaka amezeeka mpaka akapata Vicredit Vitatu
3. Form Six akafeli akingia Chuo kwa kutumia Mature Entry Examination baada ya Form six kukosa sifa za kuingia chuo
4. Chuo Akadesaaaa Mpaka akamaliza na GPA yake ya 2.0
5. Akaenda Mzumbe akahonga walimu wampe Thesis na sasa hivi ana ka MBA

Halafu wanaleta U.puuzi hapa na watu wanakesha Kujadili. Hivi mtu kama Mwampamba aliyeenda Ualimu baada ya Kufeli Form Six anaweza akaongelea Elimu ya Mnyika Kweli?

Acheni U.puuzi jamani
 
Last edited by a moderator:
no wonder anawazidi watu wa serikali kwa upeo wa mbali sana. mtu aliyepata A -10 kati ya 11 form four ni genius anakuwa na upeo wa kipekee. mimi hapa nilipata A moja tu form four ila bado natesa :becky:

FUSO, A-10 kati ya 11. Hapa umekosea, nnachojua mimi kwa mtahiniwa yeyote wa form 4, haruhusiwi kufanyia mtihani zaidi ya masomo kumi. Sasa hizo A-10 kati ya 11 amefanyia wapi. Mi nafikiri umekusudia A 9 kati ya masomo kumi aliyofanyia mtihani
 
Last edited by a moderator:
Samahani wapendwa, naona kama kuna harufu ya vita binafsi kwa hawa ndugu wanaozungumzia jambo hili. Sipendi kwenda huko lakini kwa maneno machache tuu nijaribu kuangalia kati ya wasomi wenye shahada nyingi na wasio nazo waliowahi kuongoza vizuri nchi.

Namkumbuka Lyatonga Mrema sijui kama alikuwa na shahada alipoongoza wizara fulani na nikimlinganisha na aliepo leo kwenye wizara husika sijui mnapembuaje mnapozungumzia shahada zenu! Nadhani labda niite tuu karatasi mnazopewa mkikaa pale mlimani kwa muda fulani.

Sitaki kuamini kwamba kila aliyepita pale kawekeza kichwani !! Kuna wengine aibu hata kuwatambulisha kitaaluma " kuna mkuu wa wilaya fulani huko tanga aliziita degree za ch...". Hii ni kutofautisha nini kinakutambulisha kama umekaa pale ukatoka na nini kichwani.

Kuna wengine wanaitwa madoctor huku lakini kiwango chao cha maamuzi na upembuzi wa mambo bora wangeishia form two. Mifano mnayo ya kutosha. Kila anayesoma hapa anamjua mmoja au wawili ama kadhaa katika hili.

Hebu tuangalie hoja ya maji ubungo,Mnyika ni mbunge wa ngapi tangu uhuru?

Wakati mnaomba kura za uraisi mlisemaje? Ile meli kule mwanza imeshalowekwa ziwani?

Kigoma imeshakuwa dubai?

Hivi hichokitu walichoshindwa kukifanya sisiem kwa miaka 52 huyu Mwampamba na Juliana ndiyo wataweza?

Hata kama watanzania ni wajinga sana lakini tunaangalia kabla ya mkutano nilikuja na nini kichwani na baada ya mkutano naondoka na nini?

Itafika mahali hamtapewa nafasi kuzungumza matusi, mwulizeni nchemba kule igunga watu waliondoka. Hamzungumzi hoja mnaongea mambo ya chupini. Hayabadilishi maisha ya kesho.

Kina Nape walizunguka nchi nzima wakiimba ufisadi hebu leteni mrejesho! Wapo wapi. Nyie mtazunguka mkiimba nini habari itakuwa kiporo hiyo.

Mkuu hoja yako kama inanivutia vile ila haiendani na kichwa cha habari ulichokiweka
 
Matusi ni hulka tuliyokwishaizoea kutoka kwa wafuasi wa chadema.
Swali liko palepale, Mnyika anayo degree au hana?

Mkuu.
Haya, mfano Mnyika anasema nimesoma masoma ya shahada (BBA) evening program pale udsm lakini sija tunukiwa shahada hiyo (kwa maana hiyo hana shahada inayotambuliwa kisheria na kitaaluma japo amesoma shahada)
Ndio maji yatakuja ubungo na kueleza ubadhirifu wa mabilioni ya fedha kwenye mradi wa mchina?!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Masalia naona wameamua kuanza na Gear namba nne kuendesha Gari. Hakika wameshindwa. Hakuna hata Salia mmoja anayeweza kujifananisha na J J Mnyika. Narudia tena hakuna.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom