Elimu ya Mnyika

Elimu ya Mnyika

Status
Not open for further replies.
Elimu haiwasaidii wanasiasa wa Africa katu!
Chenge Mzee wa vijisenti went to Havard.
Kigoda went to Vanderbilt.
Mkapa went to Columbia.
Lakini angalia madudu yao bora hata hao walioenda State universities
 
Kweli hii ndo Tanzania na hatufiki.. yaani tunajadili elimu ya Mnyika ili itusaidie nini..!?
 
Mnyika ni kipaji, jembe la ukweli, akina bi Kiroboto & Ndugai wanalitambua hilo! Watz tunahitaji viongozi wazalendo na si wasomi wezi/mafisadi!!
 
Samahani wapendwa, naona kama kuna harufu ya vita binafsi kwa hawa ndugu wanaozungumzia jambo hili. Sipendi kwenda huko lakini kwa maneno machache tuu nijaribu kuangalia kati ya wasomi wenye shahada nyingi na wasio nazo waliowahi kuongoza vizuri nchi.

Namkumbuka Lyatonga Mrema sijui kama alikuwa na shahada alipoongoza wizara fulani na nikimlinganisha na aliepo leo kwenye wizara husika sijui mnapembuaje mnapozungumzia shahada zenu! Nadhani labda niite tuu karatasi mnazopewa mkikaa pale mlimani kwa muda fulani.

Sitaki kuamini kwamba kila aliyepita pale kawekeza kichwani !! Kuna wengine aibu hata kuwatambulisha kitaaluma " kuna mkuu wa wilaya fulani huko tanga aliziita degree za ch...". Hii ni kutofautisha nini kinakutambulisha kama umekaa pale ukatoka na nini kichwani.

Kuna wengine wanaitwa madoctor huku lakini kiwango chao cha maamuzi na upembuzi wa mambo bora wangeishia form two. Mifano mnayo ya kutosha. Kila anayesoma hapa anamjua mmoja au wawili ama kadhaa katika hili.

Hebu tuangalie hoja ya maji ubungo,Mnyika ni mbunge wa ngapi tangu uhuru?

Wakati mnaomba kura za uraisi mlisemaje? Ile meli kule mwanza imeshalowekwa ziwani?

Kigoma imeshakuwa dubai?

Hivi hichokitu walichoshindwa kukifanya sisiem kwa miaka 52 huyu Mwampamba na Juliana ndiyo wataweza?

Hata kama watanzania ni wajinga sana lakini tunaangalia kabla ya mkutano nilikuja na nini kichwani na baada ya mkutano naondoka na nini?

Itafika mahali hamtapewa nafasi kuzungumza matusi, mwulizeni nchemba kule igunga watu waliondoka. Hamzungumzi hoja mnaongea mambo ya chupini. Hayabadilishi maisha ya kesho.

Kina Nape walizunguka nchi nzima wakiimba ufisadi hebu leteni mrejesho! Wapo wapi. Nyie mtazunguka mkiimba nini habari itakuwa kiporo hiyo.

Tupeni pia na Elimu ya Nape
 
Kweli hii ndo Tanzania na hatufiki.. yaani tunajadili elimu ya Mnyika ili itusaidie nini..!?

Hakuna asiyejua kwamba hakuna uhusiano wa moja kwa moja baina ya kusoma na kuongoza.

Swali, kwanini aliwadanganya wapiga kura wake?

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Utaonekana ni mtu wa ajabu (hata huyo Mh. Mnyika mwenyewe atakushangaa) kama utatetea kitendo chake cha kuwadanganya wapiga kura wake kuhusu kiwango chake cha elimu.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Kama huna elimu nzuri utawezaje kuchambua mambo ya bajeti za wizara au utaishia kufoka bungeni tu kuhusu ufisadi.
 
Kama huna elimu nzuri utawezaje kuchambua mambo ya bajeti za wizara au utaishia kufoka bungeni tu kuhusu ufisadi.

Swali lako la kwanza "watanzania wanataka kujua elimu ya mnyika" lilikua relevant sana. But hili la sasa hivi umeiacha uchi akili yako, kuchambua budget wewe umeitizama in a broad term but hata mwananchi aliepo pale nangurukuru, sengerema ama nanyumbu anaweza kuchambua bajeti sema terms za kiuchumi hatazitaja kama zilivyo. Ritz huwa kwenye thread the more you comment the more you become common na ujinga wako unashtukiwa, you are more powerful ukiongea kidogo au ukikaa kimya..nliwahi kukwambia!
 
Last edited by a moderator:
Why elimu ya Mnyika leo? kuna kitu Mnyika aliwaahidi wenzake na sasa maewazunguka? maana hakuna uhusiano wa yanayoendelea leo na elimu yake. Mnyika amekuwa akisaidia sana hata bungeni kurekebisha miswada mbalimbali ambayo bila hivyo ni janga la taifa. Nini wapi hasa amekosea hadi tuwe na mashaka na elimu yake? na je kwa nini tumeruka kwenda kwenye elimu kabla ya kuchambua udhaifu wa hoja zake ili kuweka vyema mashaka ya elimu yake?
 
dhaifu si ana digilii mbonaànapwaya?

Dhaifu ana kipaji cha kuhudhuria misiba Uraisi kadandia tu ndio maana anapwaya. Akimaliza Uraisi atafungua mochwari ya binafsi pale kibaha na huduma za mazishi kwa bei rahisi kwa watu wasio na uwezo. Mpaka sasa atakua amepata uzoefu wa kutosha na atapata wateja lukuki.
 
Hivi bado tunajadili elimu ya Genious Mnyika?

Si ajabu Bill Gate angekuwa Mtanzania angesutwa na hawa wenye ma certificate yasiyowasaidia hata kuzilea vizuri familia zao!
 
Kama huna elimu nzuri utawezaje kuchambua mambo ya bajeti za wizara au utaishia kufoka bungeni tu kuhusu ufisadi.

Hata hao wasomi waliotengenezaga hizo bajeti mbona wana kesi mahakamani (Daniel Yona, Basili mramba na Mgonja)
 
mnyika namfahamu alisoma kwa wakatoliki akafaulu vizuri sana form four.

ili ahangaike na siasa dar akaamua asome tambaza na kuwakimbia wakatoliki. akafeli na kuambulia division three.

chuo kikuu hakuchaguliwa. akasoma masomo ya jioni mlimani yakamshinda.

ana uwezo wa shule lakini wanasiasa walimdanganya. hajasoma na zitto.

mnyika una uwezo hata kama huna degree. waambie watu ukweli. ukikaa kimya hata wapambe wako wanapodanganya hapa na wewe pia unaonekana unadanganya.

pia bungeni weka cv yako halali. ubungo wamekuchagua kwasababu unaweza na sio kuwa na degree.
 
form 4 div 1 pts 7 na A(9) out 10 maua
sec, A level div 1 pts 3 Tambaza sec then
akajiunga chuo (udsm) kamaliza BBA
wakati wakiwa udsm na akina zitto na
mdee walianzisha mtandao wao ulikuwa
unaitwa Tz students netwek prgm(TSNP)
ambayo mara ya mwisho m/kiti alikua
owawa, mmoja kati ya waanzilishi wa asasi
za kijamii kama UNA, TYVA na pia
muanzilishi wa n.g.o inaitwa UDI. Hiyo
kwa kifupi 2. Aligombea ubungo mwaka
2005 mara 2 alipomaliza chuo na akiwa na
umri wa miaka 24. in short ni m2 mwenye
kipaji cha pekee.

Mimi nimesoma BBA pale UDSM nimejiunga mwaka 2005 na kuhitimu 2008. Utaratibu wa BBA ya pale mlimani ni kwamba wanafunzi hufanya project work (utafiti) mara baada ya kumaliza course work(mafunzo ya darasani). wakati huo najiunga chuo kikuu, Mnyika alikuwa amemaliza course work na anafanya project work na kipindi hicho alikuwa akigombea ubunge jimbo la ubungo. Ninadhani alimaliizia project work na kuhitimu shahada ya BBA.
 
bill gate hajawahi ficha elimu yake.

mnyika aweke elimu yake sahihi kule website ya bunge.

Hivi bado tunajadili elimu ya Genious Mnyika?

Si ajabu Bill Gate angekuwa Mtanzania angesutwa na hawa wenye ma certificate yasiyowasaidia hata kuzilea vizuri familia zao!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom