Elimu ya Josephat Gwajima inatia mashaka

Elimu ya Josephat Gwajima inatia mashaka

Luthertz

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2018
Posts
206
Reaction score
832
Nimekuwa napata shida sana kutokana na elimu ya Gwajima . Tokea kipindi akitangazia umma na akiliamsha dude pale Kanisani kwake, basi ,nikawa napata shida kutokana na matamshi yake.

Kila kazi ina miiko yake. Askofu hatakiwi kutoa siri za muumini wake hata kama huyo muumini amelihama kanisa lake. Hapa niliona kwenye YouTube Gwajima akisema mambo ya siri ya mke wa Dkt. Slaa.

Leo nimeangalia tovuti ya kanisa la Gwajima. Katika hii tovuti ambayo ameandaa yeye mwenyewe nimeona mambo yafuatayo:
  • Gwajima amezaliwa mwaka 1970
  • Amemaliza shule ya msingi mwaka 1985
  • Amemaliza shule ya sekondari Olevel mwaka 1993. Alichelewa kumaliza secondary sababu ya maradhi.
  • Alimaliza Advanced Diploma in Bible and Theology mwaka 1994 mjini Nairobi Kenya. Hapa ndo pana ufisadi wa elimu. Yaani alisoma stashahada ya juu kwa mwaka mmoja tena baada ya kumaliza olevel. Kwa maoni yangu, huyu alichosoma ni level ya certificate. Matatizo ya Gwajima it yanaanzia hapa.
  • Baada ya hiyo Advanced Diploma yake ambayo ni magumashi, alijiunga na chuo kinaiitwa Japan Bible Institute na kusomea Master’s degree in Christian Missions June 2006 mpaka February 2008. Hapa nilitaka kujua ni kwanini hiyo institute ilikubali kumpa admission mwanafunzi ambaye ambaye ana only post secondary study ya mwaka mmoja tu, nikakuta hiyo institute yenyewe nayo ni ya kimagumashi. Hiyo institute haina hata physical address . Ni Chuo cha kwenye mtandao na pia kinatoa degree by experience. Yaani waweza pewa hata degree kwa kuwa una uzoefu. Hii masters degree yake kumbe ni utata mtupu na achilia mbali kwamba hana sifa za kujoin hata kozi ya degree ya kwanza.
  • Mwaka 2015 alipewa PhD na chuo cha kidini cha Afrika ya Kusini kinaitwa Omega Global University. Kwenye tovuti ya chuo hiki pana maelezo kwamba kinatoa honorary PhD. Gwajima haoneshi kwenye tovuti yake ni mwaka gani alijoin hiki chuo wala lini alimaliza. Pia, hiyo miaka, Gwajima alishakuwa na kanisa la misukule huko Ubungo na baadae kuhahmia Kawe. Tena ni mwaka ambao alikuwa mshenga wa kumleta Lowassa Chadema na baadaye kututobolea siri ya vyeti vya mkuu wa mkoa aitwaye Bashite. Hivyo basi, PhD hii ni ya heshima.
  • Mwisho, kwa maoni yangu, elimu ya Gwajima ambayo haina mashaka kabisa ni ile ya form four mwaka 1993.
References
 
Vyuo vya dini vingi haviko Accredited na serikali sababu ya separation Kati ya dini na serikali. Hivyo sifa za kujiunga ziko tofauti na Hivyo vyuo accredited vya serikali.Sababu serikali hazina dini nyingi Huwezi mpelekea mtu asiye na dini akutengenezee syllabus ya dini hivyo vyuo vingi vya dini vigezo huwa tofauti kabisa.

Ndio Maana waweza mkuta shehe ana PhD ya elimu ya kiislamu lakini alisoma madrasa tu hajawahi kanyaga hata shule ya msingi lakini kasoma madrasa na vyuo vya kiislamu Hadi kufikia ngazi ya PhD.

Kwenye makanisa mengine mfano darasa la Saba aweza Soma vyuo vyao.Diploma na degee bila shida wao elimu wanayojikita nayo Ni ya dini Yao tu Sio mlundikano wa masomo mengi la hasha wanatengeneza msomi w dini yao tu.

Kuhusu PhD ya Gwajima hiyo alipewa na hicho chuo kutokana na kazi yake anayofanya kwenye jamii; walifanya assessment wakaona ni mtu kafanya kazi kubwa kwenye jamii, kaandika vitabu 32 na vimetafsiriwa kwa lugha zaidi ya 20 duniani na vinasomwa nchi tofauti za lugha tofauti na kutumia vyuoni vya dini ndio wakamtunuku hiyo PhD.

Hiyo PhD hicho chuo waliotunukiwa nacho ni pamoja na marehemu Dk Reginald Mengi yeye PhD yake ni ya hicho chuo naye alitunukiwa kwa kazi yake kwenye jamii mwingine Ni Marehemu Dk Getrude Rwakatare pia PhD yake alipewa na hicho chuo.
 
Vyuo vya dini vingi haviko Accredited na serikali sababu ya separation Kati ya dini na serikali .Hivyo sifa za kujiunga ziko tofauti na Hivyo vyuo accredited vya serikali...

"...Separation ya dini na serikali..." na sasa mtu huyo huyo anaingia serikalini huku akiwa bado kiongozi kwenye mambo ya kidini.
 
Hahaha yani unaumiza kichwa na elimu ya Gwajima?!

CCM sijui walimpitishaje?
Sifa za kuwa mbunge ya chini awe darasa la Saba ndio maana Tunduma mgombea ubunge wa Chadema Tunduma ambaye pia alikuwa mbunge wa chadema Jimbo Hilo ni darasa la Saba pure anaitwa Mwakanjoka
 
"...Separation ya serikali na dini..." na sasa mtu huyo huyo anaingia serikalini huku akiwa bado kiongozi kwenye mambo ya kidini.
Separation ya serikali na dini kwenye elimu ndiko ni ndiko naongelea.Kwenye kugombea uongozi katiba ya Nchi inaruhurusu Kila mtu kugombea bila kubagua.Ha i separate

Anatumia Haki yake ya kikatiba.Hakuna popote katiba inatamka kuwa mgombea ubunge anatakiwa kuacha kazi yake ya kidini au ya private sector Ni serikalini tu
 
Separation ya serikali na dini kwenye elimu ndiko ni ndiko naongelea.Kwenye kugombea uongozi katiba ya Nchi inaruhurusu Kila mtu kugombea bila kubagua.Ha i separate

Anatumia Haki yake ya kikatiba.Hakuna popote katiba inatamka kuwa mgombea ubunge anatakiwa kuacha kaxi yake ya kidini au ya private sector Ni serikalini tu

Uko sahihi kabisa, kwenye dini unatakiwa utumikie dini ndio maana elimu yao imejikita huko.

Kwa dhehebu letu mchungaji anatakiwa kuwa neutral.
 
Uko sahihi kabisa, kwenye dini unatakiwa utumikie dini ndio maana elimu yao imejikita huko.

Kwa dhehebu letu mchungaji anatakiwa kuwa neutral.

Asante.Dini Ni imani na juna tofauti kubwa za kiimani Kati ya dhehebu na dhehebu wengine wanaruhusu viongozi wa Dini kishiriki siasa wengine hawataki huruhusu waumini tu lakini kiongozi akitaka siasa lazima aache uongozi wa Kanisa,

wengine hutoa likizo bila malipo kwa kiongozi mtaka siasa wengine huweka masharti kuwa mambo yake ya siasa yasiathiri au kuingilia utendaji wa ndani wa Kanisa, wengine hutakiwa kukabidhi shughuli muhimu na maamuzi kwa wengine yeye anakuwa hayuko kwenye key decisions anakuwa dormant nk
 
1600052367126.png

Tapeli katika ubora wake
 
Sifa za kuwa mbunge ya chini awe darasa la Saba ndio maana Tunduma mgombea ubunge wa Chadema Tunduma ambaye pia alikuwa mbunge wa chadema Jimbo Hilo ni darasa la Saba pure anaitwa Mwakanjoka.

Tatizo langu siyo chama. Tatizo langu lilikuwa kwenye maneno ya Gwajima na Elimu yake. Nilikuwa napata shida kwenye kulinganisha matamko yake na elimu yake. Sasa nimegundua kwamba jamaa ni mweupe kichwani.
 
Back
Top Bottom