Elimu ya Josephat Gwajima inatia mashaka

Elimu ya Josephat Gwajima inatia mashaka

pia kupeleka watu marekani
destateful lies
JamiiForums1315415046.jpg
 
Kwa elimu hii ya hapa na pale aka magumashi, sishangai tena kusikia Birmingham ipo Marekani!
 
Tatizo langu siyo chama. Tatizo langu lilikuwa kwenye maneno ya Gwajima na Elimu yake. Nilikuwa napata shida kwenye kulinganisha matamko yake na elimu yake. Sasa nimegundua kwamba jamaa ni mweupe kichwani.
Mkuu hata mimi nilikuwa napata tabu sana kichwani kwangu nikilinganisha maneno yake na mipasho yake pamoja na elimu yake.
Sasa leo umenisaidia kupata jibu nililokuwa najiuliza kwa muda mrefu.
 
Sifa za kuwa mbunge ya chini awe darasa la Saba ndio maana Tunduma mgombea ubunge wa Chadema Tunduma ambaye pia alikuwa mbunge wa chadema Jimbo Hilo ni darasa la Saba pure anaitwa Mwakanjoka
Wa CCM yupo Kibajaji, Musukuma na wengine watunga Sheria wetu mahili.
 
ROBERT HERIEL
Hebu njoo utie neno hapa.

TULIPANDA TRENI YAKE, SASA TUTAPANDA BOAT. TUTAMCHAGUA.

Na, Robert Hereil

Mara yangu ta kwanza kupanda Treni ilikuwa kipindi natoka Mwenge naelekea Bunju B, nikienda kumsalimia Mjomba huko Mabwepande. Sikuwahi kufikiri kuwa Usafiri wa Treni ni mzuri kiasi kile. Nilipouliza ile Treni ni ya Nani, nikajibiwa ni Treni ya Askofu Gwajima, aliinunua. Nilimongeza kimoyo moyo, nikisema; huyu ndiye mtumishi wa Mungu.

Sasa, Askofu Gwajima anaomba Kura za Wana Kawe. Nawaomba wana Kawe mumchague, Mpeni kura zote za ndio.

Wote tuliopanda Treni yako tutakuchagua Ndugu Mgombea. Wote tuliopata huduma ya pipi ndani ya Treni yako tutakuchagua.

Wana Kawe kuanzia Lugalo, Mbezi Beach, Kunduchi, Tegeta, Mbweni, Boko, Bunju, na Mabwepande wote tutakuunga Mkono.

Gwajima anamoyo wa kutoa sana, hatuna cha kumlipa zaidi ya kumpa kura zetu za ndio.

Tutakuchagua Gwajima
Tutakupigia Kampeni
Tutahakikisha unapata kura zote.

Kama kuna mwana Kawe ambaye hajapanda Treni yako, anyoshe mikono juu, huyo anahaki ya kutokukuchagua.
Kama kuna mwana Kawe ambaye hapata huduma ya Pipi kwenye Treni yako huyo asikuchague.

Lakini sisi Tutakuchagua,

Hima tukamchague aliyetuletea Treni kutoka Mwenge Mpaka Bunju B.

Baada ya kutimiza ahadi ya Treni na wote tunaiona na tumeipanda. Sasa katuahidi endapo tukimchagua atafanya makubwa zaidi. Atanunua Boat za kisasa za uvuvi, si mnajua Jimbo letu la Kawe limepakana na Bahari ya Hindi, tutavua mpaka tukome, Piga kelele kwa Gwajimaaa! Woyooo!

Kama aliweza kununua Treni na sasa inafanya kazi na tunapanda kila siku kutoka Mwenge mpaka Bunju, kwa nini tusimuamini kuwa atanunua Boat, kisha atanunua Ambulance, woyooo!

Gwajima ni msema kweli
Kawe inamfahamu
Kawe itamchagua

Kawe ya Treni, Kawe ya Boat, Kawe ya Uvuvi, Kawe ya AMbulance.

Hima tumchague mtimiza ahadi.

Maboss wangu wa KAWE, Wazee wangu wa KAWE, Wamama wa kawe, Vijana wa Kawe. Tumchague Gwajima.
Ila Kama hukuwahi kupanda Treni yake, wala hujawahi kuiona basi usimchague.

Yapendeza Treni Yake, Yang'aa Boat zake.

Mtumie mwana Kawe yeyote unayemfahamu ujumbe huu, ili Gwajima apate kura zote.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
 
Nimekuwa napata shida sana kutokana na elimu ya Gwajima . Tokea kipindi akitangazia umma na akiliamsha dude pale Kanisani kwake, basi ,nikawa napata shida kutokana na matamshi yake.

Kila kazi ina miiko yake. Askofu hatakiwi kutoa siri za muumini wake hata kama huyo muumini amelihama kanisa lake. Hapa niliona kwenye YouTube Gwajima akisema mambo ya siri ya mke wa Dkt. Slaa.

Leo nimeangalia tovuti ya kanisa la Gwajima. Katika hii tovuti ambayo ameandaa yeye mwenyewe nimeona mambo yafuatayo:
  • Gwajima amezaliwa mwaka 1970
  • Amemaliza shule ya msingi mwaka 1985
  • Amemaliza shule ya sekondari Olevel mwaka 1993. Alichelewa kumaliza secondary sababu ya maradhi.
  • Alimaliza Advanced Diploma in Bible and Theology mwaka 1994 mjini Nairobi Kenya. Hapa ndo pana ufisadi wa elimu. Yaani alisoma stashahada ya juu kwa mwaka mmoja tena baada ya kumaliza olevel. Kwa maoni yangu, huyu alichosoma ni level ya certificate. Matatizo ya Gwajima it yanaanzia hapa.
  • Baada ya hiyo Advanced Diploma yake ambayo ni magumashi, alijiunga na chuo kinaiitwa Japan Bible Institute na kusomea Master’s degree in Christian Missions June 2006 mpaka February 2008. Hapa nilitaka kujua ni kwanini hiyo institute ilikubali kumpa admission mwanafunzi ambaye ambaye ana only post secondary study ya mwaka mmoja tu, nikakuta hiyo institute yenyewe nayo ni ya kimagumashi. Hiyo institute haina hata physical address . Ni Chuo cha kwenye mtandao na pia kinatoa degree by experience. Yaani waweza pewa hata degree kwa kuwa una uzoefu. Hii masters degree yake kumbe ni utata mtupu na achilia mbali kwamba hana sifa za kujoin hata kozi ya degree ya kwanza.
  • Mwaka 2015 alipewa PhD na chuo cha kidini cha Afrika ya Kusini kinaitwa Omega Global University. Kwenye tovuti ya chuo hiki pana maelezo kwamba kinatoa honorary PhD. Gwajima haoneshi kwenye tovuti yake ni mwaka gani alijoin hiki chuo wala lini alimaliza. Pia, hiyo miaka, Gwajima alishakuwa na kanisa la misukule huko Ubungo na baadae kuhahmia Kawe. Tena ni mwaka ambao alikuwa mshenga wa kumleta Lowassa Chadema na baadaye kututobolea siri ya vyeti vya mkuu wa mkoa aitwaye Bashite. Hivyo basi, PhD hii ni ya heshima.
  • Mwisho, kwa maoni yangu, elimu ya Gwajima ambayo haina mashaka kabisa ni ile ya form four mwaka 1993.
References
Fanyeni rejea ya "KIHIYO" case endapo atashinda kumweungua kwenye Ubunge
 
Vipi kuhusu kumpa uenyekiti wa Chadema Mbowe ambaye Ni form Six division zero na kumwacha mtu Kama Profesa Baregu mwana Chadema Profesa wa Siasa mwenyewe PhD ya Political Science

Nani mwenye Merit hapo aliyestahili kupewa?
Umepiga wasipopatakaaaaa
 
Lawama ziko kwa CCM na maamuzi yao. Walishindwa kuelewa maana ya nafasi ya ubunge. Gwajima alistahili kuangaliwa kwa ubora wake na hata waumini wake. Ubora wake uko chini na hata waumini wake ni wa aina hiyo hiyo! Hili ni tatizo kwa vyma vyote lakini kwa CCM ni kubwa kutokana na ukongwe wao. Ndo maana Bunge linageuka kuwa ni kikao cha watu wabovu na rais anaamua kujipangia matumizi yeye mwenyewe.

Ni kweli haikuwa ajabu mtu anayejiita askofu kujipiga picha akifanya ngono? Bila kujali sababu ya kitendo hicho, hakutakiwa hata kusikilizwa kwenye kura za maoni. Ni mtu mchafu tu! Tamaa ya CCM ni ile ile; kuwa na wabunge wengi bila kujali ubora wao.
Kusema ukweli ccm nilikuwa nawakubali ila kwa hapa wameteleza itabidi tu kura yangu nikampe mdee japo haikuwa lengo langu
 
Hahaha hivi uki fail form six ukapata zero unakuwa na eliu gani?! A-level au O-level?!

Gwajima O-level ali fail alipata daraja la nne lililo egemea zero, leo ana PhD.
CCM akili zenu mnazijua wenyewe.

Eti kasema anajua kaongea kijapani na kaandika vitabu vya kijapani, mara katuambia anatuletea Ambulance, !!!

Kampeni za hivyo angeenda Koromije.
Kawe Ambulance za nini tuna magari yetu, halafu sisi sio wagonjwa, au anagombea uganga wa zahanati?!

Kwahiyo na wananchi wa kawe sio muda mrefu wataanza kuongea kijapan?
 
Nimekuwa napata shida sana kutokana na elimu ya Gwajima . Tokea kipindi akitangazia umma na akiliamsha dude pale Kanisani kwake, basi ,nikawa napata shida kutokana na matamshi yake.

Kila kazi ina miiko yake. Askofu hatakiwi kutoa siri za muumini wake hata kama huyo muumini amelihama kanisa lake. Hapa niliona kwenye YouTube Gwajima akisema mambo ya siri ya mke wa Dkt. Slaa.

Leo nimeangalia tovuti ya kanisa la Gwajima. Katika hii tovuti ambayo ameandaa yeye mwenyewe nimeona mambo yafuatayo:
  • Gwajima amezaliwa mwaka 1970
  • Amemaliza shule ya msingi mwaka 1985
  • Amemaliza shule ya sekondari Olevel mwaka 1993. Alichelewa kumaliza secondary sababu ya maradhi.
  • Alimaliza Advanced Diploma in Bible and Theology mwaka 1994 mjini Nairobi Kenya. Hapa ndo pana ufisadi wa elimu. Yaani alisoma stashahada ya juu kwa mwaka mmoja tena baada ya kumaliza olevel. Kwa maoni yangu, huyu alichosoma ni level ya certificate. Matatizo ya Gwajima it yanaanzia hapa.
  • Baada ya hiyo Advanced Diploma yake ambayo ni magumashi, alijiunga na chuo kinaiitwa Japan Bible Institute na kusomea Master’s degree in Christian Missions June 2006 mpaka February 2008. Hapa nilitaka kujua ni kwanini hiyo institute ilikubali kumpa admission mwanafunzi ambaye ambaye ana only post secondary study ya mwaka mmoja tu, nikakuta hiyo institute yenyewe nayo ni ya kimagumashi. Hiyo institute haina hata physical address . Ni Chuo cha kwenye mtandao na pia kinatoa degree by experience. Yaani waweza pewa hata degree kwa kuwa una uzoefu. Hii masters degree yake kumbe ni utata mtupu na achilia mbali kwamba hana sifa za kujoin hata kozi ya degree ya kwanza.
  • Mwaka 2015 alipewa PhD na chuo cha kidini cha Afrika ya Kusini kinaitwa Omega Global University. Kwenye tovuti ya chuo hiki pana maelezo kwamba kinatoa honorary PhD. Gwajima haoneshi kwenye tovuti yake ni mwaka gani alijoin hiki chuo wala lini alimaliza. Pia, hiyo miaka, Gwajima alishakuwa na kanisa la misukule huko Ubungo na baadae kuhahmia Kawe. Tena ni mwaka ambao alikuwa mshenga wa kumleta Lowassa Chadema na baadaye kututobolea siri ya vyeti vya mkuu wa mkoa aitwaye Bashite. Hivyo basi, PhD hii ni ya heshima.
  • Mwisho, kwa maoni yangu, elimu ya Gwajima ambayo haina mashaka kabisa ni ile ya form four mwaka 1993.
References
Gwajima ni muhuni mwenzetu ndani ya kivuli cha dini.
Gwajima anakula kondoo na watenda kazi
Gwajima anapiga sarakasi za kufufua maiti, alisema angemfufua Amina chifupa na hakuweza. Maiti zimejaa mortuary na hajawahi kwenda huko kuzifufua
Gwajima ni janjajanja tu kama BOB LUSE Lusekelo.
Gwajima ni agent wa shetani, hamna mtumishi wa MUNGU ambaye ni mwanasiasa
 
1600063336026.png

Someni kitabu hicho mjifunze jinsi ya kufufua wafu.

Kawe hakutokuwa na misiba mkimchagua Gwajima.
 
Hahaha yani unaumiza kichwa na elimu ya Gwajima?!

CCM sijui walimpitishaje?
Walimpisha kwa vile anajua kusoma na kuandika, maana ndivyo vigezo hata vya wakuu wa wilaya na mikoa katika serikali wanayoongoza!!
 
Back
Top Bottom