SoC01 Elimu Fedha (Financial Literacy) itawakomboa watu wengi kiuchumi

Stories of Change - 2021 Competition

sungura23

Member
Apr 1, 2013
52
73
Habari wana JF, poleni na hongereni kwa shughuli za ujenzi wa Taifa letu. Andiko langu litaangazia jambo ambalo halizungumziwi sana ama halionekani wazi wazi lakini lina mantiki kubwa kwenye ukuaji wa uchumi kuanzia ngazi ya mtu mmoja mmoja.

Nitaanza kwa kufafanua elimu fedha ni nini, kuna umuhimu gani kufahamu elimu fedha, na jinsi ambavyo elimu fedha imekuwa na mchango tofauti tofauti baina ya mtu mmoja na mwingine. Mwishoni nitatoa mapendekezo kadhaa yatakayomwezesha msomaji wa andiko hili kujua namna gani anavyoweza kujiboresha juu ya masuala ya kumudu rasilimali fedha.

Tunaona watu wengi wana miliki mali tofauti ikiwemo biashara, nyumba, usafiri ukiwemo magari lakini kinachotofautisha baina yao waliopiga hatua na wengi wasiokuwa nacho ni kuwa kundi hili la wenye mali wengi wana elimu fedha (financial literacy). Ni rahisi mtoto wa tajiri kuwa tajiri kwa sababu licha ya elimu ya darsani anayoipata huwa wanarithishwa njia mbalimbali za kumiliki, kuendesha na kutengeneza pesa.

Elimu Fedha ni Nini?

Elimu Fedha ni uelewa, ufahamu au utambuzi wa kutambua upatikanaji, utunzaji, uzungushaji pamoja na utumiaji sahihi wa rasilimali fedha. Kwenye kufahamu elimu hii kuna mambo kama uwekezaji, kusoma alama za nyakati, kutambua thamani, mahali (eneo) pamoja na washirika.

Elimu hii sio lazima uipate shuleni ila kwa baadhi ya wasomi hufundishwa darasani hasa wanaokuwa wamebobea kwenye masomo yanayohusu fedha (finance).

Kwenye andiko hili tutaangazia mwananchi wa kawaida anayeweza kusoma, kuandika na kuhesabu na anayejikimu kwa shughuli zake za kila siku.

Dhana Kuhusu Rasilimali Fedha:

Kuna mambo mengi yanayohusu rasilimali fedha ila hapa nitaongelea kwa machache ambayo hujitokeza zaidi.

  • Watu wengi wanaamini rasilimali fedha ni pesa taslimu tu (cash). Rasimali fedha inaweza kuwa kwenye namna nyingi, mfano inaweza kuwa kwenye mfumo wa hisa ama mfumo wa vitu ya thamani kama dhahabu n.k.
  • Watu wengi wanaamini kuhifadhi pesa (saving money) ni njia bora zaidi ya kujilinda kiuchumi. Kuhifadhi pesa ni jambo jema sana kiuchumi lakini thamani ya pesa huwa haidumu kwa muda mrefu. Mfano: Ikiwa mwaka wa fedha uliopita uliweza kununua kilo ya sembe kwa Shilingi 700 na mwaka mpya wa fedha bei ya kilo moja ya sembe ikawa ni shilingi 1,000 ina maana pesa imeshuka thamani. Shilingi elfu moja ambayo ungeweza kupata kilo moja ya sembe na chenji ikabaki mwaka wa fedha uliopita ina maana mwaka mpya wa fedha shilingi 300 iliyokuwa ikibaki awali haipo tena.
  • Watu wengi wanaamini ukipata pesa za kutosha basi ni muhimu ununue eneo. Watu wengi sana wana imani hii kuwa ukipata pesa za kutosha cha kwanza ni kununua eneo. Nina mfano mzuri wa rafiki yangu wa karibu alipata tenda ya kutengeneza mabango akapata jumla ya shilingi zisizopungua milioni 20. Akanunua eneo na akaendelea na biashara zake. Sasa hivi ni mwaka wa nne kiwanja kimekaa tu anadai bora hyo pesa angewekeza sehemu ambayo ingemletea pesa zingine angenunua kiwanja kwa mkopo wa kulipa kidogo kidogo. Ukipata pesa za kutosha angalia dira yako nimeona hii dhana watu wengi wanasema wakipata pesa anaenda kununua eneo. Je hilo ndio lengo lako halisi la maisha?
  • Watu wengi wameingia hasara kwa kupata ushauri mbovu ama kuiga. Watu wengi wanafuata ushauri wa watu wa karibu kama ndugu, marafiki, wenza wa kimapenzi n.k. Tunafuata ushauri wa watu wetu wa karibu kwa sababu tunawaamini (trust). Wakati mwingine ushauri wao unaweza kukuweka kwenye risk kwa kuwa imani yako ipo kwake na sio kwenye uwekezaji unaoenda kuufanya. Wakati mwingine watu wetu wa karibu hutushauri kwa upendo lakini watakushauri kutokana na uzefu wao (experience and exposure) ambayo wewe utakapoingi akwenye uwekezaji huo unajikuta unafeli kwa sababu uzoefu uliohitajika na tabia (character) za kumudu huo uwekezaji wewe hauna.
  • Watu wengi wamefilisiwa na mikopo walioshindwa kurejesha. Mikopo imesaidia watu wengi sana lakini pia watu wengi wamerudishwa nyuma kimaisha kwa sababu ya kuchukua mikopo. Moja ya makosa makubwa ambayo nimeshuhudia mimi mwenyewe ni pale mtu anaenda kuchukua mkopo ili aanzishe biashara. Mkopo unatakiwa utumike kupanua ama kuongeza nguvu kwenye biashara ambayo imeshaanza kufanya kazi na imeshaota mizizi. Hapo inakuwa rahisi kukuza mtaji, kumudu mzunguko wa pesa na kupeleka marejesho.
  • Watu wengi hawajui mali fedha (financial wealth) inatengenezwa taratibu na inachukua muda. Chochote kinachoanza ghafla huwa kinakufa ghafla pia. Mali fedha hujengwa kwa muda mrefu na huwa ina misingi yake. Ndio maana wafanyabiashara wakubwa biashara zao haziwezi kufa ghafla. Mfano mzuri ni baadhi ya watu tunashuhudia wanauza nyumba lakini baada ya muda kadhaa unakuta huyo aliyeuza nyumba ana maisha magumu sana. Kwanini? Kwa sababu amekutana ghafla na mali fedha na hakuwa na misingi thabiti ya kuisimamia na kuiendesha. Kumiliki mali fedha kunataka uwe na misingi na misingi hii hujengwa na wakati.
  • Watu wengi hawana mipango ya muda mrefu ya kifedha. Watu wengi wanaishi kwa mipango ya muda mfupi mfupi. Sio vibaya kutokana wengi wana vipato ambavyo ni vidogo ukilinganisha na mahitaji yao. Lakini, mfano mmoja mdogo ni manunuzi ya vocha za simu. Ukinunua vocha ya shilingi 500/= kila siku ina maana kwa mwezi (siku 30) ni shilingi 15,000/=. Lakini kuna vifurushi vya mitandao vinakupa huduma mwezi mzima kwa shilingi 10,000/= tu. Hapa kuna shilingi 5,000/= ambayo unaweza kuiokoa.
Mambo ya kufanya ili ufanikiwe kifedha:

  • Tambua na zingatia kipato chako na matumizi yako.
  • Kabla ya kuwekeza kwenye kitu chochote, tafuta ushauri wa kitaalamu. Kuna watu wanaitwa washauri fedha au washauri wa biashara (financial consultants au businesss consultants). Hawa ni wataalamu wa uchumi na fedha na kazi yao ni kutoa ushauri juu ya masuala hayo. Sio lazima uwe mfanyabiashara ili kuonana nao wakati mwingine hata kama na mshahara mdogo wanaweza kukuonyesha fursa ambazo zinaweza kuwa na faida kwako pamoja na mshahara wako mdogo. Ndani ya miaka mitatu hadi mitano unakuwa umepiga hatua. Kikubwa ni kuwa mvumilivu.
  • Usiige wala usifanye maamuzi yoyote kwa kuwa fulani alifanya akaweza kufikia malengo. Kila mtu ana uwezo wake, malego yake, tabia zake, mipango yake, ndoto zake, mbinu zake, washirika wake na kadhalika hivyo unapofanya maamuzi ya kifedha jiangalie wewe na mazingira yako pamoja na washirika wako. Usiige kwa kuwa huwezi jua kuna siri gani nyuma ya mafanikio ya huyo unayemwona.
  • Kuweka akiba peke yake haitoshi. Kuweka akiba ni muhimu kwa kuwa kunakupa ulinzi ila pesa iliyokaa tu haizunguki kiuhalisia kwa uchumi wa nchi kama Tanzania pesa hyo ina nafasi kubwa ya kushuka thamani kadri siku zinavyokwenda. Kama unaweza, wekeza mahali ambapo pesa yako itakuwa inazunguka na kukuletea pesa nyingine.
  • Buni kitu kipya ambacho kitavutia watu. Kuna kitu kinaitwa masala chips. Ni chips zilezile ila mfanyabiashara ameongeza masala na anauza. Tafuta pombe ya mnazi, itengenezee packaging nzuri ipeleke mahotelini. Wazungu wanaipenda sana. Pika maandazi ya ladja tofauti peleka maofisini. Mfano pika maandazi ya mdalasini, ya maziwa na ya chocolate jumla yawe kama 150. Utauza yataisha yote.
Ikiwa kama huna kipato chochote kwa sasa fanya yafuatayo:

  • Tambua lengo lako. Ni shughuli gani unaitaka? Unataka kuajiriwa? Unataka kujiajiri? Ungependa ufanye shughuli gani katika maisha yako ya kila siku? Ukishatambua hilo fuata hatua inayofuata.
  • Usichague kazi. Fanya kazi yoyote itakayokupa kipato kwa sababu ukiendelea kukaa bila kuingiza chochote ina maana hupigi hatua yoyote kuelekea kwenye lengo lako. Fanya vibarua, tafuta kazi za saidia fundi, pakua/pakia mizigo, pika, fanya kazi za usafi ilimradi usikae tu.
  • Weka akiba kidogo kidogo kwa hicho kidogo unachokipata. Asilimia kubwa ya watu huamini kuweka akiba ni hadi uwe na kipato kikubwa. Sio kweli. Kidogo kidogo unachoweka kila siku baada ya muda utagundua kinaweza kukusaidia kufanya jambo kubwa.
  • Jenga mahusiano ya karibu na watu ambao wanaendana na malengo yako. Unapojenga mahusiano na watu wanaojishughulisha na malengo yako inakusaidia kukujengea imani kwao, inakupa uzoefu na hatimaye itakujengea hali ya kujiamini ni mwishoni utaweza kuifanya wewe mwenyewe.
  • Usijibane kwenye shughuli moja. Wakati mwingine inaweza kukuchukua muda mrefu kufikia malengo lako, hivyo unapaswa kuwa mjanja. Usiogope kubadili shughuli unayofanya ama usiogope kuwekeza kwenye shughuli nyingine ilihali una uhakika inakusogeza mbele.
Hitimisho:

Kuna fursa nyingi sana za kujiinua kiuchumi nchini Tanzania tatizo kubwa ni kuwa taarifa juu ya fursa hizi wanazo watu wachache. Kuna shughuli nyingi sana za kufanya ila wengi tumebaki kuajiriwa, tumebaki kuiga ujasiriamali ama kuchagua shughuli ambayo ipo kwenye mazingira ambayo hatuyaogopi (comfort zone).

Kama unayo shughuli unafanya, kazana zaidi na angalia kwenye andiko hili ni wapi ujiboreshe. Kama huna shughuli kabisa, amka, dunia haimsubiri mtu ila pesa inamsubiri anayeitafuta.

Natumaini andiko hili litakuwa na msaada nami nashukuru kwa muda wenu.

Ahsante
 
Yote uyasemayo yana ukweli ndani yake lakini baadhi yetu watanzania ni wavivu sana wa kusoma na kujifunza kwa umakini zaidi,kwani sisi kila kitu tunakichukulia poa.Na hata maisha tunayachukulia poa hiyo poa mwisho wake sio mzuri kwetu

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Ubongo wa binadamu ni computer ambayo binadamu hatokuja itengeneza. Itakachopandikizwa na kuwekewa mkazo (reinforcement) inaweza Fanya maajabu. Tatizo kila binadamu anakazia akipendacho wengine mpira, wengine music, masomo, pombe, nk. Mtu, Familia, jamii au Taifa litakalo jikita kwenye uchumi litakuwa kiuchumi. Michezo vivo hivyo, Ukahaba vivo hivyo, Nikupe mfano #kunabinadamu yani ukifunua Bible ukura wowote ukasoma anakutajia aya mstari mpaka mwandishi... Hivyo ukiona unakwama ktk lolote usimlaumu mtu niwewe umeweka nguvu kidogo.
 
Asante sana kwa elimu nzuri, wengine tuna mifani hai, tushapigika kwa kutokuwa na elimu nzuri kama hii matokeo yake now tunajuta na kupambana kurekebisha hali!
 
In formal education hii elimu ya mtaani muhimu saana. Kazi nzuri mtoa mada

Sent from my SM-A500H using JamiiForums mobile app
 
Nimekuelewa vizuri endelea kutupa madini 💪
 
Back
Top Bottom