Einstein theories of relativity..Mambo magumu kuelezea

Einstein theories of relativity..Mambo magumu kuelezea

Nimecheck walioelezea wote sijaona aliyeelezea kwa urahisi kabisa. Mwafizikia na mshindi wa tuzo ya Nobel Richard Feymann alisema ukishindwa kumwelekeza kitu mtoto mdogo naye akaelewa basi utakuwa bado hata wewe hujaelewa kitu hicho. Kwahiyo nitajaribu kuelezea concept ya Black hole na General Relativity theory lakini hiyo ya special relativity bado natafuta lugha nyepesi kabisa.

Black holes.

Kuna kitu kinaitwa gravity, ni force ambayo hata duniani yetu inayo, hii force bhana inategemeana na ukubwa/mass wa kitu(sayari ama Nyota). Kwahiyo basi huwa inavuta vitu vyote kuja kwake at the center. Kama dunia ambavyo ukiruka unarudi chini. Sasa kuna kitu wanaita escaping velocity, yaani unahitaji speed gani uwe nayo ili uweze kutoka katika gravity ya sayari fulani. Kwamfano minimum speed ya kuescape dunia 11.186 km/s, kwahiyo ya speed hiyo basi utaishi kuunguka duniani. Hii ni sawa na wewe unavyorusha jiwe hewani, ukirirusha kwa speed kali linaenda mbali juu, ukilirusha kwa speed ndogo then litaenda mbali kidogo linashuka lakini ukiweza kulirusha likawa na speed ya 11.186km/s kwenda juu basi linaweza kutoka kabisa kwenye gravity ya dunia. Escaping velocity ya jua ni 618 km/s (Imeongezeka kwa sababu jua ni kubwa (mass) na kwahiyo hata gravity yake ni kubwa, ndo maana unahitaji speed kali kabisa ili nguvu ya jua kukuvuta uachane nayo.

Sasa jua siyo nyota kubwa pekee. Kuna manyota makubwa hatari ambayo mass yake ni kubwa sana, kama ni makubwa sana basi hata gravity yake inakuwa kubwa sana, na kama gravity ni kubwa basi hata escaping gravity yake inakuwa kubwa sana

View attachment 1077629
Mfano wa nyota kubwa na jua.

Sasa speed ya mwanga ni 299,792km/s sasa kwa concept ya hapo juu basi kuna manyota makubwa sana ambayo escaping velocity yake ni kubwa kuliko hata speed ya mwanga, kwahiyo mwanga ukijaribu kutoka unaenda kidogo then unadondoka ahahahha (yaani kama unavyorusha jiwe tu hapa duniani na linadondoka).

Sasa kama mwanga unashindwa kutoka basi hata sisi tunashindwa kuona ndani kunanini kwa maana tunahitaji mwanga uakisi kitu ndo tuone bila mwanga kutoka hatuwezi ona kitu ndo maana tunaita Black holes. "Once you enter the black hole, no one will see you disappearing" hatari na nusu.

Kina Einstein walitumia concept hiyo hiyo kutabiri kwamba kuna kitu kinaitwa black holes hata kabla hawajakiona (yaani unaimagine vitu na unavitengenezea logic [emoji16][emoji16][emoji3])

NOTE : kwa gravity hiyo ya kuzuia hadi mwanga kutoka unafanya hata star nyewee inacollapse maana kila kitu kinavuta kwenda katika kwa nguvu kubwa sana. Sasa kwa kuwa hiyo force sio kitu wala haoccupy space, basi itavuta kila kitu mpaka vinakusanyika katika yaani kwa udogo usio na kipimo, yaani usio na mwisho (infinitely small) maana utakuwa unavuta tu kwenda katikati na kitu ambacho hakipo(yaani force tu) sasa ukifikia huu udogo usio na mwisho unakuwa umeingia kitu kinaitwa singularity,,. Yaani hapo kwenye singularity mjomba ni hatari sana. Maana inasemekana ndo mwanzo wa duniani [emoji16][emoji16], yaani mda ulipoanza according to the theory of relativity(tutaiongelea baadaye)

View attachment 1077637

Hiyo ni comparison ya black hole na solar system [emoji3][emoji3][emoji3] nadhani umeelewa tunaongelea kitu gani. Neil Degrasse Tyson anayaita "cosmos beasts" yanakula kila kitu.

Haya tuachane na hayo madudu ya black hole twende kwenye theory ya General Relativity.

Kwanza hii ilitakiwa ijadiliwe baada ya kujadili kwanza theory ya special relativity lakini kwa kuwa ni rahisi kidogo kuieleza basi ngoja nianze.

Bhana kuna kajamaa kanaitwa Newton kalisema kwamba tunda linaanguka kwa sababu limevuta na gravity ya dunia, lakini Einstein baada ya theory yake ya special relativity kulikuwa kama na mismatch na alichokisema Newton ndo ikabidi atengeneza theory ya kuoanisha theory yake ya special relativity na ile ya gravity ya Newton ili mambo yaende sawa ( ilimchukua zaidi ya miaka kumi kufanikisha jambo hilo ahah[emoji3])

Sasa Newton alisema kwamba kinachofanya kitu kimove sio pull force bali ni push force. Yaani tunda linaanguka sio kwamba limevutwa na dunia bali limesukumwa na kitu. Mmmh sasa hicho kitu kinachosukuma wewe au tunda lirudi kuanguka chini ni nini tena wewe Einstein?)

Einstein akasema majitu makubwa kama dunia waga yanafanya uwazi/space uliopo upinde/ubonye kwenda chini. Yaani kwa mfano unasimama kwenye kitu jamaa aliyesimama anakubonyeza kichwani urudi chini. Kwahiyo kila tukiruka ama tunda likiwa juu linabonyezwa na space kushuka chini. Kwahiyo hata jua sio kwamba linatuvuta tubaki kwenye orbit hapana bali kwa kuwa ni zito limebonyeza space kwenda chini likafanya kama kadimbwi ambako sisi tunakuwa kama tunazunguka kudumbukia juani lakini kwa kuwa na sisi tumepindisha space kwenda chini basi tunabaki kwenye orbit yetu. Picha hapo chini

View attachment 1077665

Sasa hii theory ya General Relativity ikawa imeoanisha gravity na theory ya special relativity ambayo ilikuwa inaongelea space na time.

Hint: Einstein kwenye theory yake ya special relativity alisema alisema space na time vimeshikana na huwezi kuvitenganisha kwahiyo kama gravity inapindisha space basi pia inaweza pindisha muda/time. Basi hayo yote yapo kwenye theory ya special relativity.

Theory of Special Relativity

Hii mpaka nile kwanza maana inahitaji urahisi mkubwa wa kuielezea, but i will try.

NOTE: mimi sio astrophysicist lakini napenda tu kusoma mambo mengimengi, the picture is my personal phone library na baadhi ya vitabu nilivyo soma, utaona baadhi ni vya Neil, Carl Sagan, Stephen Hawking na Richard Feynman na kuna vingine

View attachment 1077678

Any views are welcome. Kama kuna type errors mnisamehe maana nimeandika bila kuproof read.
yaan hapa hata wale ambao tunaanza physics tumeelewa .....ila sasa haya madude ntasoma nikiwa univerxity au huku huku A_level nayapata mkuu
 
Lifecoded hapakani humu jamni maana huyu masaai nahixi ni ndugu na lifecoded wa intellegent
 
Relativity theories hasa inaongelea maswala ya time travel kwenye space ni kwamba kunauwezekana wakusafiri au kufika mahali ambapo kwa speed ya vyombo vya kawaida kama rocket ni ngumu sana kufika huko kutokana na speed yake. Kwa mfano hii galaxy yetu ya milk way hipo karibu sana na dunia lakini kuna galaxy kama Andromeda Galaxy ambayo ipo mbali sana na dunia lakini pia ndo galaxy ambayo ipo karibu na milk way galaxy nyota ambazo zipo kwenye Andromeda Galaxy zinatumia 2.537 million years mwanga wake kufika duniani kwaiyo ningumu sana mwanga wake kufika duniani sasa hiyo relativity theories inajaribu ku calculate kitu ambacho kitakuwa na uwezo wa kusafiri kwa speed kama mwanga au zaidi ili kuweza kufika maeneo ambayo yapo mbali zaidi na dunia yetu hii kama kwenye Andromeda Galaxy
Mkuu galaxy ya milky-way itakuwaje karibu sana na dunia wakati dunia ipo ndani ya milky-way?
 
Kuna watu dunia hii walikuwa na akili na wameacha faida kubwa kuliko mitume na manabii.

Yaani hawa wateule wa Bwana hawajavumbua hata kijiko halafu ndio wanadaiwa kupitia kwao tutaenda mbinguni na kuketi na Mkuu wa Mbingu na ardhi na vyote vilivyomo!

Logically, mzee Newton ni bora zaidi ya Bwana Yesu na Ndugu Muhammad!
 
unawachokoza wafia dini
 
Mkuu uxixeme hvyo kuwa newton bora than hao watu... Kama xkosei kuna kitabu flan hv kimejadili kuhusu wanasayanxi wa dunia nikakuta newton ni wa pili aftr mohhamadd fatilia vitabu utajua mengi
 
Mkuu uxixeme hvyo kuwa newton bora than hao watu... Kama xkosei kuna kitabu flan hv kimejadili kuhusu wanasayanxi wa dunia nikakuta newton ni wa pili aftr mohhamadd fatilia vitabu utajua mengi
Mohammed huyuhuyu aliesema jua linazama kwny matope????
 
Hivi unausoma huo upuuzi at least twice kabla hujaupost?
Ijapokua mtoa mada ameuliza swali lake in a fictional point of view, ila point yake kubwa ni kwamba anataka kueleweshwa/faamishwa Einstein's Theory of relativity in simplified logical explanation, either scientifically ila ina a layman terms au fictional via recommendation ya sci-fi movie/any literature whatsoever. Ila unachofanya wewe ni kujibu kipuuzi kwa kudisprove kabisa scientific breakthrough ambazo zimekua proved mathematically kua sio sci-fi na zimefanya great scientists walio zingundua kuzawadiwa tunzo kubwa kama za Nobel, na pia kuleta greatest technological revolution apart from kushinda zawadi. Upuuzi uliojibu ni sawa na kusema wewe unaexist katika fantasy world. Acha upuuzi, next time soma upuuzi wako zaidi ya mara moja kabla ya kuupost. Kama Einstein's Theory of relativity tu huielewi, Quantum Mechanics je? Bila shaka hutumii password kulogin JF! Huna tofauti na wapuuzi wengine wanaoamini Dunia ni flat(Flat Earthling maggots).

Pole sana. Shida kubwa elimu tunazopewa they dont educate us but we are only indoctrinated. Wewe ni moja wa wanaojifanya wameelimika lakini hawajiulizi maswali magumu.

You talk of flat earth...fanya research kabla ya kuanza kutukana wengine. Kama wao wanaproof kuwa earth is flat kutokana na research walizofanya; wewe umefanya research gani to prove them wrong kuwa earth is a spinning ball in a vacuum of space? zaidi ya ile uliyokuwa indoctrinated/brainwashed darasani, wewe binafsi umefanya research gani? nimekupa hiyo kidogo ya earth's spinning speed, earth's circulation speed to the sun, na speed ya jua in a solar system na speed ya galaxy...umechanganyikiwa umeishia kutoa mapovu na kutukana. Haya ni mambo ambayo unapaswa kujiuliza in relation to relativity and the so called big bang theory.

Labda nikuchanganya kidogo, any vacuum must be created in a measured phenomenon like a container. Hiyo vaccum of space inatoka wapi, where is the space's container that creates that vaccuum.....think boy, THINK!

Hata hivyo sikulaumu hatakidogo. Ni kwa sababu shuleni ulikuwa unakariri tu upate vyeti ili uajiriwe. Huna uwezo wa kujiuliza maswali magumu na ndiyo laana ya nchi hii.
 
Nyie ndo mnastahili kuitwa wasomi sio huyo fwalah uliyemqoute hapo.

Nyie ndo mmeelimika mnajua kwamba watu wanajiuliza maswali juu ya jambo fulani,sio huyo bweggeeh ambae yeye anadhani kila alichosoma watakubali watu wote bila kuuliza na kuhoji.

Umeongea kitu kizuri sana.haya mambo hayahitaji jazba yanahitaji kujadiliwa huku wasomi wakituvumilia na kutuelekeza kwa utaratibu juu ya research zao.

Binafis napata tabu sana kuwaza juu ya nadharia mbali mbali lakini naona huyo jamaa siwezi kujadiliana nae. Anadharau za kikeh kikeh.
Pole sana. Shida kubwa elimu tunazopewa they dont educate us but we are only indoctrinated. Wewe ni moja wa wanaojifanya wameelimika lakini hawajiulizi maswali magumu.

You talk of flat earth...fanya research kabla ya kuanza kutukana wengine. Kama wao wanapro0f kuwa earth is flat kutokana na research walizofanya; wewe umefanya research gani to prove them wrong kuwa earth is a spinning ball in a vacuum of space? zaidi ya ile uliyokuwa indoctrinated/brainwashed darasani, wewe binafsi umefanya research gani? nimekupa hiyo kidogo ya earth's spinning speed, earth's circulation speed to the sun, na speed ya jua in a solar system na speed ya galaxy...umechanganyikiwa umeishia kutoa mapovu na kutukana. Haya ni mambo ambayo unapaswa kujiuliza in relation to relativity and the so called big bang theory.

Labda nikuchanganya kidogo, any vacuum must be created in a measured phenomenon like a container. Hiyo vaccum of space inatoka wapi, whre is the space's contain that creates that vaccuum.....think boy, THINK!

Hata hivyo sikulaumu hatakidogo. Ni kwa sababu shuleni ulikuwa unakariri tu upate vyeti ili uajiriwe. Huna uwezo wa kujiuliza maswali magumu na ndiyo laana ya nchi hii.
 
Kijana kasema wapi kama jua lazama kwenye matope.?
Muhammad alikuwa Zaidi ya mwana sayansi yeyote unayemjua alikuwa ni mwana sayansi ambae sio wa kupingwa kwa wenye akili.
Mohammed huyuhuyu aliesema jua linazama kwny matope????
 
Nyie ndo mnastahili kuitwa wasomi sio huyo fwalah uliyemqoute hapo.

Nyie ndo mmeelimika mnajua kwamba watu wanajiuliza maswali juu ya jambo fulani,sio huyo bweggeeh ambae yeye anadhani kila alichosoma watakubali watu wote bila kuuliza na kuhoji.

Umeongea kitu kizuri sana.haya mambo hayahitaji jazba yanahitaji kujadiliwa huku wasomi wakituvumilia na kutuelekeza kwa utaratibu juu ya research zao.

Binafis napata tabu sana kuwaza juu ya nadharia mbali mbali lakini naona huyo jamaa siwezi kujadiliana nae. Anadharau za kikeh kikeh.

Msamehe bure....hawa watu wanaoitwa flat earther wamefanya research za kwenye maandiko hasa Biblia. Kijiografia na hata wamekwenda angani sana katika Thermosphere na kuona dunia ilivyo kwa chini. Ukienda youtube kuna clips za Generali mmoja wa kijeshi wa marekani anaitwa Bird alivya utafiti sana antartica. Ukiipata isikilize kwa makini.

Na mtu unapaswa kujiuliza ni kwa nini hairusiwi kufika antactica pasipo kibali cha pentagon? Antactica treaty imeweka wazi kuwa ukikutwa antarctica pasipo kibali unauawa hapo hapo.....kama ni bara la kawaidi kama mabara mengine kwa nini iko hivyo??

Msikilize huyu jamaa kwenye hii clip.
 
Attachments

  • FLAT.mp4
    2.3 MB
  • FB_IMG_1531200208318.jpg
    FB_IMG_1531200208318.jpg
    24.3 KB · Views: 31
  • FB_IMG_1531245578201.jpg
    FB_IMG_1531245578201.jpg
    21.1 KB · Views: 35
  • FB_IMG_1531453008573.jpg
    FB_IMG_1531453008573.jpg
    9.4 KB · Views: 35
  • FB_IMG_1532087055027.jpg
    FB_IMG_1532087055027.jpg
    7.5 KB · Views: 31
Kijana kasema wapi kama jua lazama kwenye matope.?
Muhammad alikuwa Zaidi ya mwana sayansi yeyote unayemjua alikuwa ni mwana sayansi ambae sio wa kupingwa kwa wenye akili.

Mkuu sidhani kama unaweza kutetea hoja yako kwamba jamaa alikuwa Mwanasayansi zaidi utaishia kusema vitu visivyoweza kuthibitika kisayansi.

I dare you unielezee sayansi yake ilikuwaje na alimajor kwenye maeneo gani: Hesabu? Fizikia? au? Labda kama alikuwa mtaalamu wa social science kwa sababu alikuwa na marafiki wengi muda wote pamoja na wanafamilia.

Mwanasayansi asijue kusoma wala kuandika?
 
Kati ya sayansi na mtu kipi kimemvumbua mwenziwe?
 
Back
Top Bottom