Einstein theories of relativity..Mambo magumu kuelezea

Einstein theories of relativity..Mambo magumu kuelezea

Nimecheck walioelezea wote sijaona aliyeelezea kwa urahisi kabisa. Mwafizikia na mshindi wa tuzo ya Nobel Richard Feymann alisema ukishindwa kumwelekeza kitu mtoto mdogo naye akaelewa basi utakuwa bado hata wewe hujaelewa kitu hicho. Kwahiyo nitajaribu kuelezea concept ya Black hole na General Relativity theory lakini hiyo ya special relativity bado natafuta lugha nyepesi kabisa.

Black holes.

Kuna kitu kinaitwa gravity, ni force ambayo hata duniani yetu inayo, hii force bhana inategemeana na ukubwa/mass wa kitu(sayari ama Nyota). Kwahiyo basi huwa inavuta vitu vyote kuja kwake at the center. Kama dunia ambavyo ukiruka unarudi chini. Sasa kuna kitu wanaita escaping velocity, yaani unahitaji speed gani uwe nayo ili uweze kutoka katika gravity ya sayari fulani. Kwamfano minimum speed ya kuescape dunia 11.186 km/s, kwahiyo ya speed hiyo basi utaishi kuunguka duniani. Hii ni sawa na wewe unavyorusha jiwe hewani, ukirirusha kwa speed kali linaenda mbali juu, ukilirusha kwa speed ndogo then litaenda mbali kidogo linashuka lakini ukiweza kulirusha likawa na speed ya 11.186km/s kwenda juu basi linaweza kutoka kabisa kwenye gravity ya dunia. Escaping velocity ya jua ni 618 km/s (Imeongezeka kwa sababu jua ni kubwa (mass) na kwahiyo hata gravity yake ni kubwa, ndo maana unahitaji speed kali kabisa ili nguvu ya jua kukuvuta uachane nayo.

Sasa jua siyo nyota kubwa pekee. Kuna manyota makubwa hatari ambayo mass yake ni kubwa sana, kama ni makubwa sana basi hata gravity yake inakuwa kubwa sana, na kama gravity ni kubwa basi hata escaping gravity yake inakuwa kubwa sana

View attachment 1077629
Mfano wa nyota kubwa na jua.

Sasa speed ya mwanga ni 299,792km/s sasa kwa concept ya hapo juu basi kuna manyota makubwa sana ambayo escaping velocity yake ni kubwa kuliko hata speed ya mwanga, kwahiyo mwanga ukijaribu kutoka unaenda kidogo then unadondoka ahahahha (yaani kama unavyorusha jiwe tu hapa duniani na linadondoka).

Sasa kama mwanga unashindwa kutoka basi hata sisi tunashindwa kuona ndani kunanini kwa maana tunahitaji mwanga uakisi kitu ndo tuone bila mwanga kutoka hatuwezi ona kitu ndo maana tunaita Black holes. "Once you enter the black hole, no one will see you disappearing" hatari na nusu.

Kina Einstein walitumia concept hiyo hiyo kutabiri kwamba kuna kitu kinaitwa black holes hata kabla hawajakiona (yaani unaimagine vitu na unavitengenezea logic [emoji16][emoji16][emoji3])

NOTE : kwa gravity hiyo ya kuzuia hadi mwanga kutoka unafanya hata star nyewee inacollapse maana kila kitu kinavuta kwenda katika kwa nguvu kubwa sana. Sasa kwa kuwa hiyo force sio kitu wala haoccupy space, basi itavuta kila kitu mpaka vinakusanyika katika yaani kwa udogo usio na kipimo, yaani usio na mwisho (infinitely small) maana utakuwa unavuta tu kwenda katikati na kitu ambacho hakipo(yaani force tu) sasa ukifikia huu udogo usio na mwisho unakuwa umeingia kitu kinaitwa singularity,,. Yaani hapo kwenye singularity mjomba ni hatari sana. Maana inasemekana ndo mwanzo wa duniani [emoji16][emoji16], yaani mda ulipoanza according to the theory of relativity(tutaiongelea baadaye)

View attachment 1077637

Hiyo ni comparison ya black hole na solar system [emoji3][emoji3][emoji3] nadhani umeelewa tunaongelea kitu gani. Neil Degrasse Tyson anayaita "cosmos beasts" yanakula kila kitu.

Haya tuachane na hayo madudu ya black hole twende kwenye theory ya General Relativity.

Kwanza hii ilitakiwa ijadiliwe baada ya kujadili kwanza theory ya special relativity lakini kwa kuwa ni rahisi kidogo kuieleza basi ngoja nianze.

Bhana kuna kajamaa kanaitwa Newton kalisema kwamba tunda linaanguka kwa sababu limevuta na gravity ya dunia, lakini Einstein baada ya theory yake ya special relativity kulikuwa kama na mismatch na alichokisema Newton ndo ikabidi atengeneza theory ya kuoanisha theory yake ya special relativity na ile ya gravity ya Newton ili mambo yaende sawa ( ilimchukua zaidi ya miaka kumi kufanikisha jambo hilo ahah[emoji3])

Sasa Newton alisema kwamba kinachofanya kitu kimove sio pull force bali ni push force. Yaani tunda linaanguka sio kwamba limevutwa na dunia bali limesukumwa na kitu. Mmmh sasa hicho kitu kinachosukuma wewe au tunda lirudi kuanguka chini ni nini tena wewe Einstein?)

Einstein akasema majitu makubwa kama dunia waga yanafanya uwazi/space uliopo upinde/ubonye kwenda chini. Yaani kwa mfano unasimama kwenye kitu jamaa aliyesimama anakubonyeza kichwani urudi chini. Kwahiyo kila tukiruka ama tunda likiwa juu linabonyezwa na space kushuka chini. Kwahiyo hata jua sio kwamba linatuvuta tubaki kwenye orbit hapana bali kwa kuwa ni zito limebonyeza space kwenda chini likafanya kama kadimbwi ambako sisi tunakuwa kama tunazunguka kudumbukia juani lakini kwa kuwa na sisi tumepindisha space kwenda chini basi tunabaki kwenye orbit yetu. Picha hapo chini

View attachment 1077665

Sasa hii theory ya General Relativity ikawa imeoanisha gravity na theory ya special relativity ambayo ilikuwa inaongelea space na time.

Hint: Einstein kwenye theory yake ya special relativity alisema alisema space na time vimeshikana na huwezi kuvitenganisha kwahiyo kama gravity inapindisha space basi pia inaweza pindisha muda/time. Basi hayo yote yapo kwenye theory ya special relativity.

Theory of Special Relativity

Hii mpaka nile kwanza maana inahitaji urahisi mkubwa wa kuielezea, but i will try.

NOTE: mimi sio astrophysicist lakini napenda tu kusoma mambo mengimengi, the picture is my personal phone library na baadhi ya vitabu nilivyo soma, utaona baadhi ni vya Neil, Carl Sagan, Stephen Hawking na Richard Feynman na kuna vingine

View attachment 1077678

Any views are welcome. Kama kuna type errors mnisamehe maana nimeandika bila kuproof read.
Umejitahidi Sana. Ni wachache Sana kwenye hii dunia wanaohitaji kusumbua vichwa vyao kwa mambo magumu yasiyo na malipo. But nakuhakikishia hao ndio watu pekee wenye uwezo wa kuibadilisha dunia.
 
Dunia haizunguki mkuu ni fix tu.
Bila shaka umemaanisha "fiksi/uongo" sio "fix". refer; http://lmgtfy.com/?q=fix. Ikiwa umetumia "fix" kurefer kitu tofauti na "uongo/fiksi" na ulimaanisha kuweka "?" na sio nukta mwisho wa sentensi yako, then on the retrospect ukisahihisha sentensi yako kuwa inavotakiwa, ambapo litageuka kuwa swali / nadhani ulimaanisha liwe swali, utakua umeuliza swali zuri sana. Otherwise rudi darasani kajifunze tena lugha uielewe vizuri then ndo uje kujadili Physics, next time usikurupuke kuandika pumba kabla hujaitathimini, otherwise unatazidi kudhibitisha jinsi gani ulivo mpuuzi mbele ya kadamnasi.
 
Usipaniki mkuu ambo ya kawaida haya.naoa imekukea sana kama we ndo uliibeba mimba ya physics.

Pole sana mkuu samahani kwa kukukera
Bila shaka umemaanisha "fiksi/uongo" sio "fix". refer; http://lmgtfy.com/?q=fix. Ikiwa umetumia "fix" kurefer kitu tofauti na "uongo/fiksi" na ulimaanisha kuweka "?" na sio nukta mwisho wa sentensi yako, then on the retrospect ukisahihisha sentensi yako kuwa inavotakiwa, ambapo litageuka kuwa swali / nadhani ulimaanisha liwe swali, utakua umeuliza swali zuri sana. Otherwise rudi darasani kajifunze tena lugha uielewe vizuri then ndo uje kujadili Physics, next time usikurupuke kuandika pumba kabla hujaitathimini, otherwise unatazidi kudhibitisha jinsi gani ulivo mpuuzi mbele ya kadamnasi.
 
Wakuu Hii NYUMBU MNAISOMA AU[emoji851]......[emoji2960]

Are you smart enough to quote me? To simplify the question for you, maana najua hujalielewa, Either, "Can you pin point unyumbu wangu upo wapi?" or "Unaweza kuquote post yangu yoyote kwenye hii thread inayoonesha/justify unyumbu wangu?" or "Can you pin point any logical inconsistency ya post yangu yoyote kwenye uzi huu?". NOTE; unyumbu/ujuha == (ni sawa na) being illogical / absurdity, since najua hutoweza kupin point any logical inconsistency kwenye post yangu yoyote kwenye uzi huo, then nani ni nyumbu? mimi au wewe?

PS; Tafadhali nipe jibu fupi ili tusipotezeane muda. Yaani jibu la "kati ya mimi na wewe nani haswa anapaswa kuitwa nyumbu?", linatakiwa kuwa either "mimi/ Arduino Sentinel" au "wewe/ Emmak". The clock is ticking.
 
Nyumbu Ni wewe Arduino [emoji851]
 
Kiukweli mkuu wewe ni nyumbu.
Mana naona una maneno mengi kama mwari wa kizaramo.
 
Uzi umeanza kupoteza utamu wake sasa kisa nyie mnaozinguana hapo juu
 
Poa Tu mkuu uko huru kuelezea hisia zako juu yangu.
Kuwa huru kijana....
Kuna tofauti kubwa kati ya "ukweli/fact" na "hisia". Sihisi kwamba wewe ni mjinga, bali najua kwamba ni kweli wewe ni mjinga. Swali ni, "nimeprove vipi kwamba wewe ni mjinga?" yaani kama hakuna facts za kuonesha kwamba wewe ni mjinga maana yake mimi ninahisi na sio kweli kwamba wewe ni mjinga. Jibu ni, "mimi siye niliyeprove kwamba wewe ni mjinga bali wewe mwenyewe ndiye uliye prove kwapost bandiko lisemalo,
Dunia haizunguki mkuu ni fix tu.

Bila shaka sasa tunaanza kuelewana after all your absurdity.
 
Bila shaka umemaanisha "fiksi/uongo" sio "fix". refer; http://lmgtfy.com/?q=fix. Ikiwa umetumia "fix" kurefer kitu tofauti na "uongo/fiksi" na ulimaanisha kuweka "?" na sio nukta mwisho wa sentensi yako, then on the retrospect ukisahihisha sentensi yako kuwa
inavotakiwa, ambapo litageuka kuwa swali / nadhani ulimaanisha liwe swali, utakua umeuliza swali zuri sana. Otherwise rudi darasani kajifunze tena lugha uielewe vizuri then ndo uje kujadili Physics, next time usikurupuke kuandika pumba kabla hujaitathimini, otherwise unatazidi kudhibitisha jinsi gani ulivo mpuuzi mbele ya kadamnasi.
Wewe unajiona kuwa upo smart zaidi kumbe umeandika mkorogo tu...!
Lugha yenyewe unayomwambia mwenzako akajifunze, bado kwako ni chenga tu!
 
Kuna tofauti kubwa kati ya "ukweli/fact" na "hisia". Sihisi kwamba wewe ni mjinga, bali najua kwamba ni kweli wewe ni mjinga. Swali ni, "nimeprove vipi kwamba wewe ni mjinga?" yaani kama hakuna facts za kuonesha kwamba wewe ni mjinga maana yake mimi ninahisi na sio kweli kwamba wewe ni mjinga. Jibu ni, "mimi siye niliyeprove kwamba wewe ni mjinga bali wewe mwenyewe ndiye uliye prove kwapost bandiko lisemalo,

Bila shaka sasa tunaanza kuelewana after all your absurdity.
Naona blaa blaa nyingi na manenomeeengi yaliyojaa kughafilika yakidhaniwa ni ufundi.[emoji23][emoji23][emoji23].
 
Wewe unajiona kuwa upo smart zaidi kumbe umeandika mkorogo tu...!
Lugha yenyewe unayomwambia mwenzako akajifunze, bado kwako ni chenga tu!
Tofautisha kati ya typing error i.e "unatazidi(unazidi)" na absolute absurdity i.e"fix(fiksi)" . Mmoja kakosea kuandika, na mwingine kamaanisha alichokiandika kwa point ya amesimplfy kuandika neno "fiksi" kwa kuomit "ksi" na kuweka "x', absolute stupidity.
 
Wewe unajiona kuwa upo smart zaidi kumbe umeandika mkorogo tu...!
Lugha yenyewe unayomwambia mwenzako akajifunze, bado kwako ni chenga tu!
Ndo mana nazidi kumuona ni mtu mnung'aze tu kwa sababu anashindwa kujua mambo ya kimazingira.

Mfano katika lugha ya kiarabu neno "KAIFA" ina maana ya "VIPI" ila waswahili wengi utawasikia wanasema "lete kaifa" wakikusudia ya kwamba "lete habari" lakini kwa tafsiri sahihi inatafsirika "lete vipi" sasa tunaambiana hivyo na watu na tunajua wamekusudia nini walipotumia neno hilo japo sio maana yake katika kiarabu.

Sasa huyo bwana hata hasomeki.
 
Kwa mwingine yeyote yule anayefikiria kuquote post yangu yoyote ndani ya uzi huu,

Hakikisha unajua facts zako ipasavyo ili kuweza kubackup argument yoyote itakayoibuka baada ya hapo. Vinginevyo ili tusiendelee kuhuaribu uzi huu mzuri, tuendelee na mada kuu ambayo ni kumjibu/kumuelekeza mtoa mada. Kama huna/ hujisikii kumjibu mtoa mada, basi tafadhali kaa kimya ili wajuzi wengine wenye facts / jibu la kumpa mtoa mada wapate chance ya kuchangia/kumjibu mtoa mada. Bila shaka sote tutajifunza kitu on the process. Thanks in advance.
 
Daa jamaa kasha tia doa uzi kazngua kinyama Daa ulikuwa unaenda vzur pataam Binadamu wengine bwana[emoji36]
 
Mwendelezo
MWENDELEZO

Kabla ya yote tujue kwamba Newton alitwambia nini mwanzo kabla haka kajama kanakoitwa Einstein hakajazaliwa. Newton alisema kwamba ili ujue/upime speed ya kitu kwa ufasaha kabisa ni lazima wewe unayepima uwe stationary/yaani usiwe unamuvu kuelekea upande wowote. Kwa mfano ukiwa umepanda Bus unaenda Mwanza, bus lingine likawaovertake utaliona speed yake ni ndogo. Lakini kama mkipishana na bus linatoka mwanza utaona speed yake ni kali sana.
(Yaani hata kama bus zote mbili lililowaovertake na mlilopishana nalo yakiwa na speed sawa yote bado utaliona linalowaovertake lina speed ndogo ukilinganisha na mnalopishana nalo).

Kwahiyo ili uweze kupima speed ya kitu kwa usahihi ni lazima uwe stationary kama huyu dogo hapa chini.

View attachment 1078024
Image

(Kama unavyomuona hapo dogo kasimama kabisa. Basi according to Newton huyo dogo ndo anaweza kupima kwa usahihi speed ya hilo baloon juu kuliko mtu anayekimbia kuelekea upande linakwenda ama anakimbia kuelekea upande linakotoka. Lakini kuna fala mmoja anaitwa Einstein anakwambia huyo dogo hajasimama wala nini [emoji3][emoji3][emoji3]), Einstein anakwambia huyo dogo anamuvu mbona na wala hayuko stationary kabisa [emoji3][emoji3][emoji3], kimbembe cha Theory of relativity kinaanzia hapa sasa.)

Einstein cha kushangaza yupo sahihi kwa 100%, kama nitakavyoeleze hapo chini [emoji3][emoji3][emoji3], tena wewe unayeamini dogo kasimama ndo utajiona fala namba moja [emoji3][emoji3]. Einstein alikuwa mtu wa imagination sana, jamaa alikuwa anapenda kuimagine sana, ndo maana alikuwa anasema "Genius will take you from point A to point B, but imagination will take you anywhere".

Sasa check maneno. Einstein aliimagine akiwa amesimama nje ya dunia kwenye sayari nyingine huko (labda Jupiter) then amwangalie huyo dogo aliyesimama. Je atamuona kasimama? Jibu ni hapana? Maana dunia inazunguka jua, basi na dogo ataonekana anamuvu na dunia kwa speed ambayo dunia inazunguka jua (dogo si kasimama juu ya dunia? Si dunia pia inamuvu kuzunguka jua? Basi kama dunia inamuvu basi na dogo anamuvu [emoji3][emoji3]. Mfano kwa picha hiyo chini.

View attachment 1078025
(Hapo kama mtu akiwa nje ya dunia atamuona dogo aliyesimama duniani naye anamuvu kwahiyo sio stationary observer kama Newton alivyosema. Speed ya Dunia kuzunguka juu ni 107,000 km/h. Kwahiyo ndugu hata kama umekaa hapo kwenye sofa basi ujue haujakaa bali anakimbia na dunia. Kaa hapo kwa lisaa limoja na utakuwa umekula route ya 107, 000km [emoji3][emoji3]) yaani sawa na kutoka Dar es salaam to New York mara 4 kwenda na kurudi.)

Sasa dogo aliyesimama na kupima speed ya hilo balloon hatapata speed sahihi. Yaani ni sawa na mtu yupo kwenye Bus apime speed ya abiria mwenzake anayetembea ndani ya bus atamuona anatembea kawaida tu but kwa mtu aliyesimama nje ya bus atamuona anatembea kwa speed, maana atajumulisha speed ya abiria anayetembea na speed ya bus alilomo.

Kwahiyo Dunia inazunguka, Solar system Inazunguka, Galaxy yetu ya milk way nayo inazunguka hata universe nayo inasemakana inazunguka, kwahiyo inategemeana na wewe unaangalia kitu ukiwa wapi (ndo tunapata neno "relativity"). Ukiwa umesimama ndani ya bus, aliyesimama nje ya bus atakuona unamuvu, hata aliyesimama ardhini naye, ataonekana anamuvu akiangaliwa na mtu aliyesimama Jupiter/juani, aliyesimama Jupiter au juani, ataonekana anamuvu akiangaliwa na mtu aliyesimama nje ya solar system, aliyesimama nje ya solar system, akiangaliwa na mtu ambaye yupo galaxy nyingine (andromeda galaxy) ataonekana anamuvu na speed ya galaxy yetu ambayo pia inazunguka. Kwahiyo mlolongo unaenda bila mwisho [emoji3][emoji3].

Basi relativity inaathiri kila kitu kilicho kwenye universe kama: space, time, matter, motion, mass, gravity, energy and light.

Sasa kwa kuwa aliyeuliza swali amejikita kwenye time basi nitajaribu kuelezea kuhusu theory inaapply je kwenye time

Vitu vya kukubaliana kwanza.

1. The speed of light is constant (299,792km/per second)
2. Speed = distance/time.

Kwenye mwendelezo ujao nitaongelea hivo viwili na relation yake na mambi ya time travel, yaani kama unaweza ukasafiri kwenda Jana [emoji3][emoji3]. Kukuibia siri tu, it is possible theorically lakini practically kuna ka ugumu kadogo mpaka wanasayansi wakikaweka sawa ndo tunaweza safari kwenda juzi bila wasi kabisa.

Typo Errors mnivumilie kama zipo.
Kwenye post ya mwisho tulikubaliana vitu viwili

1. The speed of light is constant.(299,792 kilometers per second

2. Speed = distance/time.

The speed of light is constant.(299,792 kilometers per second.

Maana ya hii kitu ni kwamba speed ya mwanga ni constant regardless ya movement yako.
mfano ukiwa kwenye gari linaspeed ya 320km/s halfu mtu wa nyuma yako akamulika torch kwa nyuma ya gari yako, speed ya mwanga haitapungua kama tulivyoona kwenye relativity ya mabus mawili yanavyoovertake utaona speed ya bus linalowaovertake utaliona lina speed ndogo na basi mnalopishana nalo utaona linaspeed kali. Lakini kwa kuwa speed ya light ni constant regardless ya mwanga/light unapishana nayo au unakuovertake amesimama unauangalia speed ya mwanga haitachange utaiona the same. [emoji3].

2. Speed = distance/time

Sasa kama tumekubaliana speed ya mwanga ni constant haichange uwe umesimama, unamuvu speed haichange utaiona vilevile. Hebu imagine mtu awe na kioo ambacho mwanga unareflect na kurudi chini kama kwenye hii picha hapa.

UnfitKindHypacrosaurus-size_restricted.gif

stationary.gif

Sasa hiyo picha hapo juu ni kama hicho kioo kimetulia hivyo lakini imagine mtu kapanda kwenye rocket inayoenda kwa speed ya light na hicho kioo cha kureflect mwanga and wewe ukawa umesimama unamshuhudia utakachoona sio kama hapo juu bali kama hichi hapa chini.

ShockedRelievedKangaroo-size_restricted.gif

GvQB.gif

Maana the time it takes the light to reach the mirror hapo juu na rocket nayo itakuwa imemuvu kwenda mbele, kwahiyo mpaka mwanga ufike kwenye kioo wewe hutaona kama umenda juu tu na kushuka, bali utaona mwanga umeenda juu na mbele pia kama kwenye hizo image hapo juu.

Lakini kama ukiangalia utaona kama kuna kadistance mwanga umesafiri.., hiyo distance jamaa wa kwenye rocket hawezi iona maana yeye mwanga umeenda juu na kushuka ila wewe mwanga umeuona umeenda juu na mbele na kuanza kushuka ukielekea mbele tena.

Sasa hebu fikiria kama distance imeongezeka kwako, lakini wote jamaa wa kwenye rocket mmeshuhudia ukipanda na kushuka at the sametime, sasa huu mwanga umeweza je kuongeza distance kwako lakini kwa jamaa wa kwenye rocket haujaongeza distance lakini umesafiri kwa muda sawa.? Yaani labda kwako wewe mwanga uliongezeka speed? [emoji3].

Jibu ni hapana mwanga haukuongezek speed kwako maana speed ya mwanga ni constant haichange kwa mtu anayemuvu au aliyesimama. Kinatokea hapo ni kitu watoto wa malkia wanakiita "time dilation".

Kama ilivyo kwenye hii formula speed = distance/time (kama unavyoona kwenye gari 120km/h kwahiyo mtu akisafiri masaa mawili kwa speed hiyo atakuwa amesafiri distance ya km 240. 120km/h = 240km/2h. Sasa vipi jamaa akisafiri km 360km kwa masaa mawili? Jibu litakuwa jamaa alikuwa speed sana yule, maana ake aliongeza speed kutok 120km kwa lisaa na kufikia km 280 kwa lisaa ndo maana japokuwa distance iliongezeka lakini alitumia masaa yale yale mawili.

Sasa ili twende sawa tufanye assumption kwamba umbali wa morogoro kutoka Dar ni km 240 lakini Dar to Dodoma ni Km 360. Sasa assume unamwendesha Mh. Majalia and kakwambia speed isizidi wala kupungua ni 120km kwa lisaa (kwa kumanisha speed ni constant haibadiliki). Kwahiyo mtatumia masaa 2 kufika morogoro lakini mtachukua masaa 3 kufika Dodoma. Sasa hebu imagine kuna gari mbili zote zinaenda Dodoma lakini cha ajabu wewe tu ndo unaoona kuna kunakuongezeka kwa umbali kutoka Moro kwenda Dodoma lakini jamaa mwingine yeye anaona hakuna umbali ulioongezeka kwani anaona Dodoma ndo Morogoro (unashangaa?) Ulichokiona hapo juu ndo hicho ulichokishuhudia mwanga wewe unauona umeongezeka distance ya kusafiri lakini jamaa wa kwenye rocket haoni distance yoyote iliyoongezeka. Kwahiyo wewe ambaye umeona mwanga umeongezeka utatumia masaa matatu lakini jamaa ambaye hajaona distance imeongezeka atatumia masaa mawili. Sasa wewe wa masaa matatu utakuwa umezeka lisaa limoja kuliko jamaa aliyetumia masaa mawili.
Speed of light is constant ambayo ni 299,792 kilometers per second

Kwahiyo 299,792km/s = distance/time.

Sasa in case unaona distance imeongezeka and jamaa wa kwenye rocket haoni distance yoyote kuincrase and kumbuka speed of light ni constant regardless ya movement yake basi kinachobadilika hapo ni time tu ili kucompansate distance iliyoongezeka kwa mwanga uliouona wewe. Maana ake hapa mda wa jamaa aliye kwenye rocket unaslowdown ukilinganisha na mda wako wewe.

Moja ya matumizi ya hii concept ni kwenye issu ya GPS. bila hiyo theory hapo juu basi google maps, uber na taxify ingekuwa ndoto. Kwahiyo ukiwa unapanda uber ama taxify, jaribu kumshukuru Einstein hata kidogo [emoji3][emoji3]
 
Back
Top Bottom