Wakuu njoeni tutete kwanza huko dvn kumekuwa kugumu kwa upande wangu, niseme tu wengi hawajui kucheza na hawataki kujifunza kucheza 😂, sina maana mbaya ila napata tabu kuwafunga wanaocheza kwa kubutua yaani wakati mimi nataka kuburudika kwa kucheza mpira mzuri na kupata ushindi wao wanaburudika kwa kupata ushindi tu mpira mzuri hawataki 😂.
Mechi 12 nimeshinda 2, sare 2, kufungwa 8, hizo sare 2 nilikutana na pira biriani wenzangu na hizo 2 za ushindi 1 nimekutana na pira biriani mwenzangu ila bahati haikuwa upande wake ila hiyo 1 sasa nikakutana na kanyaga twende namie nikasema kanyaga twende pia nauweza na bahati ikawa upande wangu ila kwa mbinde 😂, hizo nilizofungwa zote nimekutana na wasiojua kucheza.
Vuta picha unakutana na mtu anatumia possession game lakini ukienda uwanjani mwanzo mwisho ni ndege tu.
View attachment 3301146
Hii ndo hali yangu huko, nyie ambao mko dvn 1 na 2 nipeni mbinu ya kuwafunga hao jamaa.