Waterbender
JF-Expert Member
- Oct 2, 2018
- 7,913
- 10,718
Efootball haihitaji wingers ni maplaymekers,hole players wawe kwenye wing sides kama, mfumo wa 4222 ndo best formation kwa sasaNimebadrisha mfumo kutoka 4-2-3-1 kwenda 4-3-1-2(Old Meta).
4-2-3-1, huu mfumo uko vizuri kwenye ushambuliaji na uzuiaji na ni mzuri kwa LBC na OW, changamoto niliyokuwa naipata ni striker kutembea eneo kubwa peke yake na kupelekea kutokuwa kwenye eneo husika kwa wakati, ukikutana na mtu anaetumia back 5 unaweza lia.
4-3-1-2(Old Meta), huu mfumo pia uko vizuri kwenye ushambuliaji na uzuiaji na ni mzuri kwa QC na PSSN unaweza tumia LBC pia, inakuhitaji kuwa na viungo imara na wepesi maana huu mfumo unahitaji kutawala eneo la kati ili kutengeneza nafasi, changamoto inakuja pale ambapo utakutana na mpinzani ambae yuko vizuri kwenye kutumia nafasi za pembeni zilizoachwa na viungo wakati unashambulia.
Kwa sasa 4-3-1-2 ndo mfumo ambao naufanyia mazoezi, natunza coins kwaajili ya Xabi Alonso mwenye mfumo wake wakati huo namvizia Kante wa free 😂.
Yani hili game linaweza kukufanya ukahisi tayari umekuwa kocha bado kupata leseni na timu tu 😂.
Ukiweka stiker mmoja kila muda kawekwa mtu kati😂