asante kwa taarifa yako kaka hemedi,TAARIFA KWA 4U MOVEMENT DODOMA.
Habari, Wana 4u movement mliopo Dodoma na Watanzania wote wenye mapenzi mema na Edward Lowassa tunawaasa kutovaa T-shirt zozote za 4u movement au zenye jina la Edward Lowassa katika kipindi chote cha mikutano ya Chama.
Najua na kutambua hadi jana tarehe 07/07/2015 zaidi ya wana 4u movement 3600+ plus wamewasili Dodoma lakini wingi wetu usiwe sehemu ya kuwa chanzo cha vurugu ya Aina yeyote.
Tuna Taarifa za kuaminika kuna watu wenye mpango wa kutumia T-shirt zetu za 4u movement kufanya vurugu ndani ya Mji wa Dodoma kwa makusudi ili kuiondelea sifa ya utulivu na umakini wa Movement yetu. Yeyote atakae husika kufanya fujo au vurugu zozote kwa Makusudi huku akitumia jina letu tutakuwa msatari wa Mbele kumshughulikia.
Tunawaasa na kuwaomba wana 4umvt na Watanzania wote kuwa watulivu na wavumilivu na kuwapa nafasi Wajumbe wote wa vikao vya Maamuzi kwa kutii na kufuata kanuni za chama kufanya maamuzi kwa Utulivu maana ule wakati mabadiliko uliotabiriwa na Baba wa Taifa kuwa ukifika Basi mabadiliko tutayapata ndani ya CCM na tukikosa tutayapata nje ya ccm lakini ipo nafasi kubwa sana ya kuyapata Mabadiliko haya ndani ya CCM chini ya Balozi wetu wa 4u movement Mh Edward Lowassa.
Ahsanteni
Hemedy Ally
Mratibu Taifa (National Coordinator)
@4u movement
# UTUMISHI
# UWAJIBIKAJI
# UMOJA
# UZALENDO
Vijana mbalimbali mkoani kigoma,wameapa kuwapa UKAWA ushindi katika uchaguzi mkuu ujao iwapo CCM kwa makusudi itaamua kuondoa jina la lowasa bila sababu za msingi.
CCM ujumbe ndio huo,sauti ya wengi ni sauti ya MUNGU,kazi kwenu.
sasa wewe naona unakua nape wa pili aliyesema kikwete akishinda nahama nchi,watanzana kwa midomo hatujambo ila action zerooo........ukijinyonga uache na wosia kua ni sababu ya lowasa kupitishwa tuache midomo mbelembele kama chiriku...Akipitishwa tu Lowasa najinyonga pale MTO makiri. Lemudava.
Hayati Moringe Sokoine alimuamini ndugu yake Lowassa na ndio maana akampeleka akapigane Vita vya Idd Amin akiwa kati ya wasomi vijana toka Chuo Kikuu Dar-es-salaam, na baada ya vita kapelekwa na Nyerere UK kusomea Uchumi.
LOWASSA NA AWAMU ZOTE 4
Awamu ya 1: imani juu ya Lowassa ipo pale pale kwa Nyerere alipomteua katibu katika taasisi nyingi za Serikali japo alikuwa mdogo sana kiumri.
Awamu ya 2: Mzee Mwinyi alimuamini sana Lowassa na kumteuwa Mkurugenzi wa AICC japo alikuwa kijana mdogo, na pia kumpeleka katika Baraza la Mawaziri.
Awamu ya 3: Mzee Mkapa alimuamini sana Lowassa, alimpa Wizara zinazohitaji uchapaji kazi wa hali ya juu na uzalendo ulio tukuka.
Awamu ya 4: Prof Jakaya Kikwete kwa zaidi ilidhihirika imani juu ya umakini na utendaji wa Lowassa, kwani alimpa Uwaziri Mkuu wa Tanzania na hadi sasa Serikali nzima bado ina imani kubwa kwani yeye ndie Mwenyekiti katika Bunge Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.
CCM: Wadhamini aliowapata Lowassa peke yake ni zaidi ya 90% ya wagombea wengine wote wa CCM.
ZANZIBAR: Sultani wa Pemba Maalim Seif pamoja kuwa ni Kiongozi wa CUF lakini aliwataka Wapemba wachukue haraka Kadi za CCM ili Lowassa apate udhamini wa kutosha Pemba, na kweli Lowassa pekee alipata Wadhamini 450 ndani ya nusu saa, wengine walisota siku kibao na kuondoka bila udhamini.
Baada ya hayo, sisi Wananchi sasa ni zamu yetu, tuleteeni Lowassa tumpe kura za Watanzania wote hadi upinzani.
By Sipano Kilimanjaro
Kiwengwa Zanzibar
Kwa wasiofahamu vizuri, Edward Lowassa ni front man tu katika hizi vulugu za kutafuta kuteuliwa kuwa mgombea Urais wa Tanzania.
Watu walioko nyuma ya Lowassa hawawezi kuruhusu Lowassa kuihama CCM labda kama kwa sasa wana amini CCM haichaguliki tena. Mpaka sasa hakuna vielelezo vinavyoonyesha kama CCM haichaguliki katika kiti cha Urais.
Ikumbukwe kuwa katika siasa za Tanzania a winner-takes-all.
Uchafu wa Lowassa na kundi lake ni mwingi sana kiasi kwamba hawawezi kuruhusu CCM iwe chama cha upinzani kwa sababau itakuwa ni kukaribisha zimwi wasilolifahamu kwenye nyumba yao iliyojaa uchafu wa kisiasa, kiuchumi na kijamii. Hii ni sawa na kuwa member wa drug cartel halafu baada ya muda ukataka kuachana na biashara hiyo. Haiwezekani member wenzako wakakuacha uondoke huku ukiingiza oxygen mwilini!
Timu Lowassa wanafahamu the stakes are too high, the costs are too dear, and they are ridiculous afraid to keep fighting, but on the other hand, CCM establishment will never allow that to happen…thanks to CCM doctrine and advanced internal intimidation.
Kuna baadhi ya watu wanashangaa wakisikia Lowassa anasema kama kuna mtu hamtaki ndani ya CCM, basi huyo mtu aondoke yeye na siyo Lowassa. Lowassa na timu yake are there to stay!
CCM na Timu Lowassa (Wanamtandao) ni kama drug cartel!
Leo wanatupiana maneno lakini kesho utawaona kwenye majukwaa wakipongezana na kuombeana kura.
Ninawashangaa kidogo wale ambao hawaifahamu CCM vizuri!
chaguo la wapuuzi walioshindwa kutumikisha vichwa vyao kwa umakini...."think and decide with the help of Tumbo"TYPEMaamuzi ya kukatwa nama kutokukatwa kutolewa kwa utaratibu wa vikao na vikao hivyo vya maamuzi bado havijaanza, nasikitika sana kusema kuwa uelewa aidha kwa ushabiki wako ni mdogo, LOWASSA ndiye chaguo la watu na watu hao wameshapaaza sauti ya kumhitaji, poleni sana wanafiki
Movement ya majambazi na mkikamatwa mpigwe adi kufa mafisadi wakubwa
ha ha ha eti akili yako? basi sawaAkili yangu yaniambia mapema kabisa EL kashakatwa.