Edward Lowassa special thread

Edward Lowassa special thread

Hawana kazi ya kufanya na wamelipiwa kila kitu na mafisadi Kwa nini wasiwe Dodoma?nitawashangaa ccm kuchagua MTU kwa shinikizo la fedha.shame on you mafisadi.

takukuru mko wapi??mbona tayari huu niushahidi huwezi peleka watu 3600 kukaa Dodoma wiki nzima bila kz na wakati huu dom kila kitu ni gharama.takukuru hatuwaeleweni kabisaaaaaa
 

CCM%2BVijana%2BMwanza4.jpg

Hussein. A. Kimu Mw/kiti UVCCM(W) Nyamagana Mwanza.


Wednesday, July 8, 2015

YAH: TAMKO LA KUPONGEZA KAULI YA MKUU WA MKOA WA MWANZA NDUGU STANSLAUS MAGESA MULONGO

Ndugu wanahabari na watanzania wote. Kwanza nitumie fursa hii kuwashukuru kwa kuitikia wito na kukubari kuja kuungana nasi kwa lengo la kuwajuza watanzania kwa kile kinachoendelea katika mkoa wetu Wa mwanza kwa faida na manufaa ya watanzania wote.

Siku ya 6/7/2015, mkuu wetu wa mkoa Wa mwanza alitoa maelekezo kwa makamanda wa polisi kuzuia watu wasio kua na malengo mazuri kwa nchi yetu na taifa letu. Wanao kwenda Dodoma kwa lengo la uvunjifu wa amani,katika kipindi hiki cha mchakato wa vikao vinavyoendelea vya kuchuja na kupata kiongozi atakae peperusha bendera ya chama cha mapinduzi, Huo ni wajibu wake akiwa ni mwenyekiti Wa kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa, na ndio muwakirishi Wa rais kwa ngazi ya mkoa anawajibu na kila sababu ya kukemea,kuonya,kushauri na kuelekeza mambo yote yanayohusu raia na Mali zao hivyo sisi wana mwanza na watanzania kwa ujumla hatukuona ubaya Wa aina yeyote kwa kauli ya mkuu wetu wa mkoa.


Cha kusikitisha Jana 7/7/2015. Kuona katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari mtu
anae jiita mtemi Sylvester Yared. ambae ndio mratibu Wa genge la vijana wahuni wanaojiita 4U movement. Akidhihaki na kupinga tamko la mkuu wetu Wa mkoa wa mwanza. Binafsi nilishitushwa sana


Katika Katiba yetu ya chama cha mapinduzi na kanuni zake tuna jumuiya tatu

1.Jumuiya ya wanawake(UWT)
2.Jumuiya ya wazazi
3.Jumuiya ya vijana (UVCCM) Ndani ya cham cha mapinduzi hatuna taasisi wala jumuiya inayoitwa 4Umovement. Swali la kujiuliza jeuri, kiburi na mamlaka ya kuunda chombo kisicho rasmi chenye lengo la kuvuruga,kuhatarisha mustakabari wa chama chetu na Taifa letu kwa maslahi ya mtu binafsi,anaetumia kundi la vijana wasio jitambua kwa gharama yeyote ili aingie ikulu,na huyu si mwingime bali ni ndugu Edward Lowasa.

Ninayaongea haya kwa ushahidi, ninao hapa viongozi wawili kutoka kundi la mabaunsa na machinga,wa mkoa wa mwanza ambao walifatwa na kupewa kazi ya kuandaa na kukusanya vijana wasiojielewa kwa lengo la kwenda Dodoma. Kushinikiza viongozi Wa chama kumchagua mgombea wao, na kundi jingine la vijana na akina mama Wa CCM kusimama njiani kusimamisha misafara ya wajumbe Wa NEC, na mkutano mkuu wa chama Taifa kuwapa shinikizo na vitisho, kwamba lazima warudi na mgombea wao ndugu Edward Lowasa.


Hayo yote yanafanywa kwa malipo, Na kila kijana atalipwa tsh 100,000.kwa kila siku ,kwa siku zote atakazo fanya kazi, mpaka kieleweke.


Ndugu wanahabari Mimi kijana mzalendo wa Tanzania ninapata wakati mgumu na Mashaka makubwa pindi ninapo ona mtu ambae hakubaliki katika jamii ya watanzania mwenye madoa na kashfa chungu nzima tena afya yake ikiwa ya kususua analazimisha kwa kutumia gharama kubwa ili afike Ikulu mtu huyu kwa kauli ya hayati baba Wa Taifa,namnukuu, Tumuogope kama ukoma hafai.mwisho wa kunukuu.


Nimalizie kwa kuwashukuru na kuwapongeza viongozi wetu wakuu wa chama na serikali kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kujenga na kuimarisha chama na serikali kwa kutatua na kusimamia maslah ya watanzania, Mwisho kwa nafasi ya kipekee niwashukuru wanahabari wote mlio hudhuria na watanzania wote mnao nisikiliza na kunitazama.Mungu kibariki chama chetu CCM, Mungu ibariki Tanzania.


Imeandaliwa na

Hussein. A. Kimu
Mw/kiti UVCCM(W) Nyamagana Mwanza
 
YAH.TAMKO LA KUPONGEZA KAULI YA MKUU WA MKOA WA MWANZ NDUGU STANSLAUS MAGESA MULONGO.



Ndugu wanahabari na watanzania wote.

Kwanza nitumie fursa hii kuwashukuru kwa kuitikia wito na kukubari kuja kuungana nasi kwa lengo la kuwajuza watanzania kwa kile kinachoendelea katika mkoa wetu Wa mwanza kwa faida na manufaa ya watanzania wote.






Siku ya 6/7/2015, mkuu wetu wa mkoa Wa mwanza alitoa maelekezo kwa makamanda wa polisi kuzuia watu wasio kua na malengo mazuri kwa nchi yetu na taifa letu. Wanao kwenda Dodoma kwa lengo la uvunjifu wa amani,katika kipindi hiki cha mchakato
wa vikao vinavyoendelea vya kuchuja na kupata kiongozi atakae peperusha bendera ya chama cha mapinduzi,Huo ni wajibu wake akiwa ni mwenyekiti Wa kamati ya ulinzi na usalama
wa mkoa, na ndio muwakirishi Wa rais kwa ngazi ya mkoa anawajibu na kila sababu ya kukemea,kuonya,kushauri na kuelekeza mambo yote yanayohusu raia
na Mali zao hivyo sisi wana mwanza na watanzania kwa ujumla hatukuona ubaya Wa aina yeyote kwa kauli ya mkuu wetu wa mkoa.



Cha kusikitish Jana 7/7/2015. Kuona katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari mtu

anae jiita mtemi Sylvester yared. ambae ndio mratibu Wa genge la vijana wahuni wanaojiita 4U movement. Akidhihaki na kupinga tamko la mkuu wetu Wa mkoa wa mwanza. Binafsi nilishitushwa sana


Katika Katiba yetu ya chama cha mapinduzi na kanuni zake tuna jumuiya tatu
1.Jumuiya ya wanawake(UWT)
2.Jumuiya ya wazazi
3.Jumuiya ya vijana (UVCCM)
Ndani ya cham cha mapinduzi hatuna taasisi wala jumuiya inayoitwa 4Umovement.
Swali la kujiuliza jeuri, kiburi na mamlaka ya kuunda chombo kisicho rasmi chenye lengo la kuvuruga,kuhatarisha mustakabari wa chama chetu na Taifa letu kwa maslahi ya mtu binafsi,anaetumia kundi la vijana wasio jitambua kwa gharama yeyote ili aingie ikulu,na huyu si mwingime bali ni ndugu Edward Lowasa.




Ninayaongea haya kwa ushahidi, ninao hapa viongozi wawili kutoka kundi la mabaunsa na machinga,wa mkoa wa mwanza ambao walifatwa na kupewa kazi ya kuandaa na kukusanya vijana wasiojielewa kwa lengo la kwenda Dodoma. Kushinikiza viongozi Wa chama kumchagua mgombea wao, na kundi jingine la vijana na akina mama Wa CCM kusimama njiani kusimamisha misafara ya wajumbe Wa NEC, na mkutano mkuu wa chama Taifa kuwapa shinikizo na vitisho, kwamba lazima warudi na mgombea wao ndugu Edward Lowasa.Hayo yote yanafanywa kwa malipo, Na kila kijana atalipwa tsh 100,000.kwa kila siku ,kwa siku zote atakazo fanya kazi, mpaka kieleweke.






Ndugu wanahabari Mimi kijana mzalendo wa Tanzania ninapata wakati mgumu na Mashaka makubwa pindi ninapo ona mtu ambae hakubaliki katika jamii ya watanzania mwenye madoa na kashfa chungu nzima tena afya yake ikiwa ya kususua analazimisha kwa kutumia gharama kubwa ili afike Ikulu mtu huyu kwa kauli ya hayati baba Wa Taifa,namnukuu, Tumuogope kama ukoma hafai.mwisho wa kunukuu.





Nimalizie kwa kuwashukuru na kuwapongeza viongozi wetu wakuu wa chama na serikali kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kujenga na kuimarisha chama na serikali kwa kutatua na kusimamia maslah ya watanzania, Mwisho kwa nafasi ya kipekee niwashukuru wanahabari wote mlio hudhuria na watanzania wote mnao nisikiliza na kunitazama.Mungu kibariki chama chetu CCM, Mungu ibariki Tanzania.






Imeandaliwa na
Hussein.A.kimu
Mw/kiti UVCCM(W)nyamagana mwanza.

hussen ni mganga njaa Wa membe.
 
TAARIFA KWA 4U MOVEMENT DODOMA.

Habari, Wana 4u movement mliopo Dodoma na Watanzania wote wenye mapenzi mema na Edward Lowassa tunawaasa kutovaa T-shirt zozote za 4u movement au zenye jina la Edward Lowassa katika kipindi chote cha mikutano ya Chama.

Najua na kutambua hadi jana tarehe 07/07/2015 zaidi ya wana 4u movement 3600+ plus wamewasili Dodoma lakini wingi wetu usiwe sehemu ya kuwa chanzo cha vurugu ya Aina yeyote.

Tuna Taarifa za kuaminika kuna watu wenye mpango wa kutumia T-shirt zetu za 4u movement kufanya vurugu ndani ya Mji wa Dodoma kwa makusudi ili kuiondelea sifa ya utulivu na umakini wa Movement yetu. Yeyote atakae husika kufanya fujo au vurugu zozote kwa Makusudi huku akitumia jina letu tutakuwa msatari wa Mbele kumshughulikia.

Tunawaasa na kuwaomba wana 4umvt na Watanzania wote kuwa watulivu na wavumilivu na kuwapa nafasi Wajumbe wote wa vikao vya Maamuzi kwa kutii na kufuata kanuni za chama kufanya maamuzi kwa Utulivu maana ule wakati mabadiliko uliotabiriwa na Baba wa Taifa kuwa ukifika Basi mabadiliko tutayapata ndani ya CCM na tukikosa tutayapata nje ya ccm lakini ipo nafasi kubwa sana ya kuyapata Mabadiliko haya ndani ya CCM chini ya Balozi wetu wa 4u movement Mh Edward Lowassa.

Ahsanteni

Hemedy Ally
Mratibu Taifa (National Coordinator)
@4u movement
# UTUMISHI
# UWAJIBIKAJI
# UMOJA
# UZALENDO
tunashukuru kwa taarifa kiongozi wetu. ni jambo zuri na lenye nia njema kwani nguvu ya siasa aliyonayo Lowassa ni zaidi ya mwiba kwa wagombea wengine hivyo hilo la kutumia siasa chafu ili kutafuta huruma na visingizio si tu linawezekana bali lipo, limepangwa na kwa taarifa hii ni dhahiri iumeshaharibu mipango yao.
 
Safi sana ni vyema na haki kuzuia nchi kuchukuliwa kwa hila na ghilba.
 
Lowassa apeta Maadili ,Membe, na Makongoro wanaswa na tuhuma za Rushwa.

Taarifa za kutoka ndani za kikao cha Maadili kinachoendelea hivi sasa mjini Dodoma kimeonyesha njia Salama kwa baadhi ya Makada wa CCM na pia kuwa kichungu kwa Wengine. Makada wa ccm waliopeta kwa urahisi ni Edward Lowassa, Gharibu Bilal na Asha Rose Migiro.

Makada walio kutana na kikwazo cha kamati ya Maadili ni Bernad Membe ambaye Amekutwa na tuhuma za Rushwa zisizo na kificho katika mtanange wa kusaka Udhamini. Taarifa ya Usalama na TAKUKURU ambao ni walikwa zimefanana bila hiana kwa Baadhi ya Wagombea ambao walidiriki kutumia Rushwa kupata wadhamini wameanikwa bila kificho mkoa kwa mkoa, Wagombea hao ni Bernad Membe , January Makamba , Mwigulu Nchemba, Samweli Sitta, Makongoro Nyerere, Jaji Ramadhan na Magufuli.

Aidha Mwenyekiti wa Chama Amekuwa mkali kuliko matarajio ya wajumbe walivyo dhani kuwa itakuwa, Nape na Mangula wameonekana kuwa wapole mpaka sasa kwani report ya usalama na TAKUKURU inaonyesha kuwatisha na kuwatia Simanzi kinyume na Matarajio kwa mgombea wao.

Nipo hapa Dodoma mmaranguoriginal best wa John Okello nitakuletea kila kinachoendelea hapa Dodoma.
 
hivi kuna haja gani ya kumtangazia mhalifu kuwa mmegundua atafanya uhalifu na kumuomba asifanye uhalifu badala ya kwenda kumkamata huyo mhalifu??
 
Hongera kwa kuonesha ukomavu ndani ya chama na taifa kwa ujumla. Haya Maneno yalipaswa kukemewa na wazee kama vile Mzee Bulembo.
 
Hili ni tamko la wahuni,diallo naona kawalipa wahuni hata wasiokuwa na kadi za uwanachama na kujiita uvccm,
 
Not only that but also kukubali matokeo ambayo nina UHAKIKA,hamta ya kubali
 
Khaa!!! Hii ndiyo raha ya demokrasia hasa pale wenye akili wakiwa wachache na wajinga wakawa wengi :sleepy:
 
ukawa hatutaki ufisadi pamoja na kura zao, hizo kura wampe kiongozi mkuu.
 
Pamoja na nguvu kubwa ya mazingaombwe aliyokua nayo ya kucheza na media pamoja na fedha chafu hizi ndo sababu maalum hawezi kupita hata mchujo wa kwanza wa NEC(5 bora)....


Kumeza kisu huwezi ila Unaweza kujiwekea Nazir ya kujitia Kidole kama kawaida yako .... Lowassa ndo Rais wa JMT 2015 - 2020...
 
Back
Top Bottom