Edward Lowassa special thread

Edward Lowassa special thread

Lowasa haendi popote.eti anatishia kwenye vyombo vya habari kwamba asipopitishwa patachimbika.hili zee mwehu kabisa na hai waganga njaa wanaompigia debe wajiandae kisaikolojia.
 
kaka umekula.chakula gani kinachokufanya uhalee uaroooo kama wakoo
 
Nimekuelewa...kwamba ni analzimisha kuwe na deal...yaani aendelee kula mema hata kama amekatwa na kukubali kuisupport ccm.it is a wise but not intellectual game!
Mkuu,
Lowassa anaifahamu vizuri sana CCM.

Mbinu anayotumia Lowassa ni copy and paste ya mbinu aliyotumia Rais Kikwete katika kutafuta kuteuliwa kuwa mgombea Urais.

Hoja ya msingi, kama Rais Kikwete alitumia mbinu hii na kupata alichokuwa anakitafuta, itakuwaje leo akione ni haramu?
 
Mtikila anamsubiri kisutu, Lowassa ngumu sana na wanaomshabikia mambulula kama yeye...
 
  • Thanks
Reactions: G3T
Pamoja na nguvu kubwa ya mazingaombwe aliyokua nayo ya kucheza na media pamoja na fedha chafu hizi ndo sababu maalum hawezi kupita hata mchujo wa kwanza wa NEC(5 bora).

1. Ana tuhuma nzito za ufisadi wa richmond uliosababisha kujiuzulu na kutikisika kwa serikali 2008.Tuhuma hizi hakuweza kusafishwa mahakamani(walimbeba ) jambo linalopelekea tuhuma kusimama palepale kisheria.

2. Operation VUA GAMBA, target ya hii kauli mbiu ilikua ni lowassa,Mara baada ya kujeruhiwa bungeni 2008 chama chake kiliona ufisadi ni tatizo kikaanzisha operation ambayo ilipanga kumwangamiza kabisa kisiasa ndugu Ngoyayi alikwepaje tumuulize NAPE ,hapa maana yake chama chake chama chake HAKIMTAKI.
kumbuka kauli ambayo aliitoa katibu mkuu pale mwanza wakati anamaliza ziara za cha,a namnukuu "Tunairudisha misingi ya chama cha mapinduzi ,kiwe chama cha wakulima na wafanyakazi kama alama zinavyoonyesha, CCM sio chama cha wafanya biashara tena ,hawa wafanya biashara ndo wanatuletea ESCROW,RICHMOND,EPA ect" ni nani hajui kama manywele ni businesman?nani hajui kama hela anazogawa kama njugu kuna support kubwa ya business influence?

3. Amekiuka sheria ya gharama za uchaguzi ya mwaka 2011 kifungu Namba 14(1_2)mma kifungu namba 20(1-4) sambamba na kifungu namba 24 cha sheria hiyo ambayo inakataza mgombea yoyote wa nafasi ya urais,ubunge au udiwani .Ikumbukwe hadi sasa Lowassa ametumia zaidi ya billioni 50 kwa ajili ya kuwahonga waandishi wahabari,wenyeviti wa CCM wa mikoa,wabunge,waandesha bodaboda,maaskofu,mashekhe na hivi juzi ametumia zaidi ya shilingi billion 35.5 kuwahonga REDET.

4. Lowassa amezungukwa na wapambe ambao wana criminal records za kifisadi baadhi ni Rostam,Andrew chenge,Nazir Karamagi,Anna Tibaijuka,Kingunge etc.

5. Ugonjwa wake ,mzee ana mgogoro wa Afya si vizuri kuweka details zote hapa lakini hata nyie wenyewe mmeshajionea ameanguka mara kadhaa katika safari tu za kutafuta wazamini kutkana na power ya media manipulation hamkutangaziwa.

6. Alianza kampeni kabla ya wakati ,hamna asiyetambua yeye na wenzake walianza kampeni mapema hadi ikasababishia adhabu ,hata hivyo kipindo cha adhabu alikua bado anaendelea na kampeni hii tafsiri yake ni UTOVU WA NIDHAMU .

7.Visasi hapa nadhani mnanisoma mnakijua akina mwakyembe kiliwapata nini na wengine wakakoswakoswa

8.Makundi -Huyu ndo muasisi wa ccm ya walikua nacho na have nots ,NEC hawawezi wakafanya kosa la ku hype matabaka

9.Kashfa ya tuhuma ya kutaka kuutenganisha uenyekiti wa chama na urais hii siyo ndogo ipo bado kwenye records

Ni hayo tu
kama ana tuhuma mbona mnasita kumfikisha mbele ya mahakama ili haki itendeke kama ilivyotokea kwa mramba na yona? au hamna ushahidi? whats behind all these secrets, kama hamna ushahidi mimi naamini huko ni kuchafuana
 
Mtu ulikuwa kiongozi mkubwa tuu tena waziri mkuu,na haukusaidia kubadirisha hali ya uchumi zaidi ya ufisadi na kuchumia tumbo lake tu.

Sipati picha hali alyonayo sasaivi,wa mkate tuu.
 
Kuirudisha tena ccm madarakani wakati huu ni kujitafutia majanga ya ajabu kwenye nchi hii
 
Kama atakatwa kwa hila atahama kweli na huo ndiyo utakuwa mwisho wa ccm.
 
pumba katika ubora wake.

TAARIFA KWA 4U MOVEMENT DODOMA.

Habari, Wana 4u movement mliopo Dodoma na Watanzania wote wenye mapenzi mema na Edward Lowassa tunawaasa kutovaa T-shirt zozote za 4u movement au zenye jina la Edward Lowassa katika kipindi chote cha mikutano ya Chama.

Najua na kutambua hadi jana tarehe 07/07/2015 zaidi ya wana 4u movement 3600+ plus wamewasili Dodoma lakini wingi wetu usiwe sehemu ya kuwa chanzo cha vurugu ya Aina yeyote.

Tuna Taarifa za kuaminika kuna watu wenye mpango wa kutumia T-shirt zetu za 4u movement kufanya vurugu ndani ya Mji wa Dodoma kwa makusudi ili kuiondelea sifa ya utulivu na umakini wa Movement yetu. Yeyote atakae husika kufanya fujo au vurugu zozote kwa Makusudi huku akitumia jina letu tutakuwa msatari wa Mbele kumshughulikia.

Tunawaasa na kuwaomba wana 4umvt na Watanzania wote kuwa watulivu na wavumilivu na kuwapa nafasi Wajumbe wote wa vikao vya Maamuzi kwa kutii na kufuata kanuni za chama kufanya maamuzi kwa Utulivu maana ule wakati mabadiliko uliotabiriwa na Baba wa Taifa kuwa ukifika Basi mabadiliko tutayapata ndani ya CCM na tukikosa tutayapata nje ya ccm lakini ipo nafasi kubwa sana ya kuyapata Mabadiliko haya ndani ya CCM chini ya Balozi wetu wa 4u movement Mh Edward Lowassa.

Ahsanteni

Hemedy Ally
Mratibu Taifa (National Coordinator)
@4u movement
# UTUMISHI
# UWAJIBIKAJI
# UMOJA
# UZALENDO
 
Hayati Moringe Sokoine alimuamini ndugu yake Lowassa na ndio maana akampeleka akapigane Vita vya Idd Amin akiwa kati ya wasomi vijana toka Chuo Kikuu Dar-es-salaam, na baada ya vita kapelekwa na Nyerere UK kusomea Uchumi.

LOWASSA NA AWAMU ZOTE 4

Awamu ya 1: imani juu ya Lowassa ipo pale pale kwa Nyerere alipomteua katibu katika taasisi nyingi za Serikali japo alikuwa mdogo sana kiumri.

Awamu ya 2: Mzee Mwinyi alimuamini sana Lowassa na kumteuwa Mkurugenzi wa AICC japo alikuwa kijana mdogo, na pia kumpeleka katika Baraza la Mawaziri.

Awamu ya 3: Mzee Mkapa alimuamini sana Lowassa, alimpa Wizara zinazohitaji uchapaji kazi wa hali ya juu na uzalendo ulio tukuka.

Awamu ya 4: Prof Jakaya Kikwete kwa zaidi ilidhihirika imani juu ya umakini na utendaji wa Lowassa, kwani alimpa Uwaziri Mkuu wa Tanzania na hadi sasa Serikali nzima bado ina imani kubwa kwani yeye ndie Mwenyekiti katika Bunge Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama.

CCM: Wadhamini aliowapata Lowassa peke yake ni zaidi ya 90% ya wagombea wengine wote wa CCM.
ZANZIBAR: Sultani wa Pemba Maalim Seif pamoja kuwa ni Kiongozi wa CUF lakini aliwataka Wapemba wachukue haraka Kadi za CCM ili Lowassa apate udhamini wa kutosha Pemba, na kweli Lowassa pekee alipata Wadhamini 450 ndani ya nusu saa, wengine walisota siku kibao na kuondoka bila udhamini.

Baada ya hayo, sisi Wananchi sasa ni zamu yetu, tuleteeni Lowassa tumpe kura za Watanzania wote hadi upinzani.
By Sipano Kilimanjaro
Kiwengwa Zanzibar
 
Back
Top Bottom