mmaranguoriginal.
JF-Expert Member
- Jan 1, 2014
- 4,060
- 460
pamoja sana Mkuu hemed
pamoja tutashinda.
pamoja tutashinda.
Wanajukwaa!!!
Macho na masikio ya watanzania walio wengi yameelekezwa Dodoma ambapo CCM, Chama kikubwa na kikongwe kabisa hapa nchini na Afrika kwa ujumla kipo katika mchakato wa kumpata mtu wa kupeperusha bendera katika kumrithi Mhe Jakaya Kikwete.
Chambuzi nyingi za siasa kuelekea Magogoni 2015 zimekuwa zikiangaza nani atapitishwa na Chama, uimara wake na udhaifu wake.
Wapo wanaochambua kwa mapenzi, chuki, kutokujua na wengine kwa utaalamu wa hali ya juu.
Mimi kama mchambuzi wa siasa hesabu zangu zinanielekeza kuwa Mhe Edward Lowassa ana nafasi kubwa ya kuibuka mshindi akiwa ndani ya CCM na hata akiwa nje ya CCM.
Matokeo ya uchambuzi wangu hadi kufikia hitimisho kuwa Lowassa ana nafasi kubwa ni baada ya tafakuri ya kina ya mwenendo wa kisiasa tangu mwaka 2005 hadi sasa.
Mwaka 2005, Mhe Kikwete wa CCM alipata zaidi ya 80% ya kura zote na hivyo kuonesha namna gani wananchi walivyokuwa na kiu na imani kubwa kwa Kikwete binafsi na hata CCM kwa ujumla.
Miaka mitano (05) baadaye Mhe Kikwete aliporomoka kwa karibu 20% na hivyo kuambulia kura 5,276,827 sasa na 61.17% ya kura zote. Wapinzani kwa upande wao tunaona Chadema walipata kura 2,271,941; CUF kura 695,667 na NCCR kura 26,388 (hawa ndio UKAWA)
Sasa, tuangalie hesabu za Sayansi ya Siasa vipi zinambeba Lowassa ikiwa atakatwa jina lake na kuamua kuhamia katika mwamvuli wa UKAWA na wenye UKAWA wakampokea??
Kwanza, wakati wakiwa katika zoezi la kutafuta wadhamini Lowassa alijipatia jumla ya wadhamini 874,297 ambao tunaamini kuwa wapo tayari kumpigia kura popote atakapokuwa. Na iwapo kila mdhamini atashawishi watu watatu (03) ni kwamba Lowassa atakuwa na mtaji wa watu 2,532,891.
Sasa (wadhamini x 3)+(mtaji wa UKAWA 2010) =Kura kibindoni
2,532,297 + 2,993,996 = 5,526,293
Kwa hiyo, kama ataingia na mtaji huo katika uchaguzi mkuu atakuwa amebakiza kazi ndogo tu ya kushawishi undecided group na kwa kuzingatia kundi kubwa la vijana ambao hawakuweza kupiga kura 2010 kutokana na kuwa na umri chini ya miaka 18, ambao hakuna ubishi kuwa wengi ni wafuasi wa vyama vya upinzani na hivyo watampa kura mgombea wa Upinzani, ni dhahiri kuwa Lowassa ana nafasi kubwa ya kushinda ikiwa atagombea kupitia CCM au atapitia Muungano wa UKAWA.
Hizo ni hesabu zangu nikiwa mchambuzi huru.
.. Kasha kwatwa, vaeni tu !
Maamuzi ya kukatwa nama kutokukatwa kutolewa kwa utaratibu wa vikao na vikao hivyo vya maamuzi bado havijaanza, nasikitika sana kusema kuwa uelewa aidha kwa ushabiki wako ni mdogo, LOWASSA ndiye chaguo la watu na watu hao wameshapaaza sauti ya kumhitaji, poleni sana wanafiki
Hesabu zingine hizi hapa,
Lowassa naurais
Ndani ya CCMkuna udicteta ndani ya democrasi ya kwao,kuna chombo kinaitwa kamati kuu(CC)chombo hiki kina maamuzi mkubwa ambayo hayaruhusiwi kukatiwa rufaamahakamani,Lowassa alilaaniwa na Nyerere kila mtu anajua kwamba hafai kuwa Raiswa Tanzania kwa ajili alijilimpikizia mali,Mangula aliitwa kwenye chama tokakijijini kwake Mtwango alikokuwa analima viazi akawa makamo wa mwenyekiti nakuwa mjumbe wa CC kwa mjibu wa wadhifa wake, aliitwa aingie kwenye chombo hichokwa kazi moja tu, KULIPIGA LULA JINA LA LOWASSA PINDI WAKIANZA KUWAJADILIWAGOMBEA WATAOCHUKUA FORM KWA TIKITI YA CCM, hiyo ni moja.
Pili raismwenyewe majuzi alisema atapenda amwachie urais kijana,siyo mzee kama yeye
Kwa mantikihiyo Lowassa hawezi kuwa rais wa inchi hii
Mwisho Lowassaanautaka urais kwa udi na uvumba hivi anataka afanye nao nini?
.. Kasha kwatwa, vaeni tu !
Kwa wasiofahamu vizuri, Edward Lowassa ni front man tu katika hizi vulugu za kutafuta kuteuliwa kuwa mgombea Urais wa Tanzania.
Watu walioko nyuma ya Lowassa hawawezi kuruhusu Lowassa kuihama CCM labda kama kwa sasa wana amini CCM haichaguliki tena. Mpaka sasa hakuna vielelezo vinavyoonyesha kama CCM haichaguliki katika kiti cha Urais.
Ikumbukwe kuwa katika siasa za Tanzania a winner-takes-all.
Uchafu wa Lowassa na kundi lake ni mwingi sana kiasi kwamba hawawezi kuruhusu CCM iwe chama cha upinzani kwa sababau itakuwa ni kukaribisha zimwi wasilolifahamu kwenye nyumba yao iliyojaa uchafu wa kisiasa, kiuchumi na kijamii. Hii ni sawa na kuwa member wa drug cartel halafu baada ya muda ukataka kuachana na biashara hiyo. Haiwezekani member wenzako wakakuacha uondoke huku ukiingiza oxygen mwilini!
Timu Lowassa wanafahamu the stakes are too high, the costs are too dear, and they are ridiculous afraid to keep fighting, but on the other hand, CCM establishment will never allow that to happen thanks to CCM doctrine and advanced internal intimidation.
Kuna baadhi ya watu wanashangaa wakisikia Lowassa anasema kama kuna mtu hamtaki ndani ya CCM, basi huyo mtu aondoke yeye na siyo Lowassa. Lowassa na timu yake are there to stay!
CCM na Timu Lowassa (Wanamtandao) ni kama drug cartel!
Leo wanatupiana maneno lakini kesho utawaona kwenye majukwaa wakipongezana na kuombeana kura.
Ninawashangaa kidogo wale ambao hawaifahamu CCM vizuri!