Edward Lowassa hukukidhi kiu ya wanawake!

Edward Lowassa hukukidhi kiu ya wanawake!

Kaka Yericko kati ya watu nimekuwa nikiwafatilia na kuwapa like kwenye article zao nyingi ni wewe.

Chonde Chonde, weka mahaba pembeni Fanya upembuzi yakinifu uje tena kuchangia Uzi huu. Naamini utafanya hivyo kwani wewe ni kati ya watu makini.

Queen Esther

Pole sana mwanaccm uliyevamia mkutano!

Sera yoyote kwa sasa haiwezi kuzungumzwa kwakuwa sera ipo kwenye ilani ambayo itazinduliwa jumamosi viwanja vya jangwani.

Ukawa tupo tofauti na ccm huko kwenu mgombea anaropoka ahadi hewa bila kujua awaahidio leo washaahidiwa tangu 1995 mpaka 2010 na sasa wamechoka! Hawataichagua ccm tena bali Ukawa
 
Kama kweli mko 'siriazi' basi acheni usanii, kipindi hiki cha kampeni sio wakati wa kufanya maigizo na kuyarusha 'laivu' kwenye luninga!

Ivi nyie mlitegemea Lowassa aanze kuongea uongo kama mlivyozoea. Huyo ndio Lowassa,io ndio Chadema hao ndio Ukawa. Kwanza mkutano ulikuwa ni wa Bawacha Lowassa alikaribishwa na katika kukaribishwa kwake yeye aliwaomba akina mama KURA. Kuomba kura sio lazima useme nitawagaia kila mama mifuko ya viroba, cjui mjirodheshe, mara ooh nitafungua mahakama ya mafisadi. Yote hayo yapo katika katiba ya Tanzania wala haliitaji kusema ingia madaraka na kuvitekeleza. Unataka awe kama Tezi dume nitawanunulia meli, nitawajengea uwanja wa ndege. Kiongozi utakiwi kuongea sana onyesha kwa vitendo hapa kwa Chadema/Ukawa hakuna maneno mengi. NI UTEKELEZAJI TU SUBIRI KUANZIA TAREHE 26/10/15
 
....cha kujiuliza hivyo hivyo alivyo ndivyo watu wanavyompenda,na hivyo hivyo tunamtaka awe Rais wetu,tunahitaji maneno machache vitendo zaidi.
 
Heshima kwenu wana JF.

Nimefatilia kwa karibu sana sana hotuba ya Mhe. Mgombea u Rais kupitia UKAWA aliyoitoa hapa LAPF kwenye kongamano la wanawake BAWACHA na kubaini jambo moja kubwa sana.

Kauli mbiu ya kongamano ni "LOWASA NA HATMA ZA CHANGAMOTO ZA WANAWAKE TANZANIA"

Nimesikitika kuwa nilitegemea kwenye hotuba Yake ataweza kuelezea mikakati ya ukombozi huo wa mwanamke. Nasikitika kuwa sikuona mahali popote akiongelea changamoto hizo na jinsi ya kuzitatua.

Ameishia kuimba Wimbo wa Mhe. Magufuli "Alinselema Hadija, mchaka mchaka chinja" na kuzungumza mambo ya MAHABA!!!!!!!!

Nasikitika kusema mimi kama mwanamke nimeondoka na kiu yanguuuu!!!!!!!!!! Ngoja nimsubiri mzee original wa Alinselema. I hope atatuondolea kiu hii!!!!!! Tunataka kuona SERA za ukweli za kumkomboa mwanamke, sio MAIGIZO.

Naomba kuwasilisha.

Queen Esther

Asante sana mdau kwa uliyonena
 
Hatuzungumzii katiba hapa lipi kazungunza lowassa la maana?

hv unadhani kuzungumza pekee inatosha? ata kama angezungumza mipango na michakato yote juu ya ukombozi wa kinamama na wote mngetoka mmefurah bt yote yangebaki kama story anazopiga m2 na mkewe chumbani bt 2kitaka kweli wanawake wa tanzania wakomboke na uharamia huu na ahadi za uongo wa wanasiasa au kupewa viti maalum bungen yote hayo ni danganya toto tu ukiangalia wanaofaidika na fursa hyo ni wachache sana bt kama leo wanawake wa tanzania wangejua ni ktba ya warioba ndo ilikuwa mkombozi wao na c lowassa au magufuli na samia leo hata mtu akija akasema kuanzia leo wakinamama mtapata hiki na hiki au mtakuwa hv au 2tawafanyia hv bt kama hakuna strong institution ambayo ni katiba na mambo yote yanayowahusu yakaweka humo ata aje ccm,cuf,chadema,act watawale wanawake wa tanzania watakuwa haki zao vko vlevle badala ya kusubilia huruma ya wanaume ndo wafanikiwe ktk mambo yao
 
Yapo maneno yanazungumzwa kuhusiana na badhi ya Wagombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka huu wa 2015 kuwa ni MABUBU, HAWEZI KUJIELEZA NA HWAWEZI KUTUMIA MUDA MREFU KUZUNGUMZA NA WANANCHI
Sababu nyingi sana zinatolewa, kwamba kwa sababu ya afya zao kutokuwa thabiti, kwamba ni asili yao, kwamba ni watu wa vitendo siyo wazungumzaji, kwamba wana viburi kwa sababu ya jeuri ya pesa walionayo.
Naomba niongelee hili la viburi kutokana na jeuri ya pesa. Siyo wote wenye utajiri hususan wa pesa ni MABUBU, la hasha. Sitataja sina la mtu, ila nataka niwakumbushe kuwa Nchi yetu imejaliwa kuwa na Watu matajiri wa pesa/mali nyinginezo wengi tu wengine wakiwa wafanyabiashara, wengine watumishi wa Serikali n.k
Nataka pia tutambue wote hao historia za utajiri wao zinajulikana, mahusiano ya wao kwa wao yanajulikana. Wapo ambao utajiri wao hauna mashaka hata kidogo, lakini wapo ambao hata mtoto mdogo anajua utajiri wao ni wa mashaka kabisa(wana pesa haramu). Pesa zao zimetokana na ufisadi, rushwa, biashara haramu n.k.
Utafiti wa unaonesha kuwa Watu wote(narudia wote) ambao utajiri wao ni wa mashaka wanayo laana ya MUNGU, hawezi kabisa kujieleza na hata wakiongea mbele za watu, hawawezi kuwatazama wananchi machoni kwa kujiamini. Hii ni Laana ya Mungu kudhihirisha kuwa wana VIBURI vinavyotokana na matendo yao haramu.

Hii siyo kwa mtanzania tu, ni kwa Binadamu yeyote anayeyaishi maisha haya. Mali Haramu wanazomiliki zinachukua nafasi katika kufikiri ni kama mwanafunzi aliyezoea kuibia mtihani Darasani, hawezi kujibu hata swli rahisi bila ya kuwa na majibu pembeni au kuigilizia kwa mwenzake. Hiyo ni hulka na haina mjadala.

Sasa hili ni la mhimu sana:
Ukikubali kurubuniwa na watu wa aina hii, dhambi hiyo inaendelea kwako, huwezi tena kujitambua . Kwa nje nje unaona kama UMEPATA lakini kwa ndani unabaki Dhamira inakusuta, unakuwa kama umelaaniwa vile

Ni hayo tu kwa leo, tuchukue tahadhari na hawa Mabubu hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu.
 
Janet Magufuli ni kati ya wanawake wachache ambao nina hakika akiwa First Lady hatasumbua.

Siku zote nina mfananisha mama Janet Magufuli na Mama Maria Nyerere. Huyo atakuwa mama wa wa TZ wote na Mhe. Magufuli baba wa TZ wote.

Mhe. Magufuli na mkewe Madame Janet Mambo ya kuchanganya kazi na familia hawataki. Kama umeisikiliza speech na mama Akilimali Leo amemuonya Madame Regina aachane na hayo Ma NGO na ajikite kuwasaidia wanawake na watoto.

Fanya analysis basi kabla ya kuponda.

Queen Esther

Mama Salma Kikwete wakati mmewe anaingia ikulu alikuwa na NGo yoyote? WAMA si iliundwa baada ya mmewe kuingia madarakani mbona mnajitoa ufahamu kama vile hamjui mfumo wa chama cha mapinduzi?
 
Kikao kilikuwa cha mama Lowassa au Lowassa?
Maskini Regina anajaribu kumfichia aibu mumewe. Unless anataka kuwa shadow president nashauri Lowassa ajitahidi kuongea mwenyewe.

Bora hata mama lowasa amejaribu kumfichia mmewe siri .Je Magufuri hana mke ? Je ameonekana wapi ? Sana sana anaendaga kwa mapadri kumshitaki Magufuri kuwa ana mahawala wengi hadi anawauzia nyumba za serikali
 
Labda nikuulize wewe.

Mimi ni Queen Esther. Uwanja wa kina mama ndio haswa unaonihusu. Nitafungua Uzi mwingine wa Madame Samia wakati ukifika. Kwa hapa zingatia kichwa cha habari tafadhali. Usitoke nje ya mada.

Queen Esther

ni kweli samia mkataa mume alisema tuna miaka mil mia mbili ya kuchimba chuma?
 
Kaka Yericko kati ya watu nimekuwa nikiwafatilia na kuwapa like kwenye article zao nyingi ni wewe.

Chonde Chonde, weka mahaba pembeni Fanya upembuzi yakinifu uje tena kuchangia Uzi huu. Naamini utafanya hivyo kwani wewe ni kati ya watu makini.

Queen Esther
Huyu kaka ameshapoteza credibility humu, nilikuwa namuamini sana kama credible and respectable source wa info kutoka jikoni enzi za ESCROW! Sasa hivi kaweka mahaba mbele, "anaimba" taarab!
 
HUYU KUJUA KWAKE KUONGEA KULIMSAIDIA NINI HAPA?

attachment.php
 
Wewe utakuwa huijui Katiba ya JMT. Wapi pameainishwa kazi za First Lady???

Madame Regina mwenyewe kasema namwachia mume wangu atoe kiu yenu. Mbona tumeondoka na kiu yetu????

Queen Esther

umeondoka na kiu yako we ni mmojawapo wa wasioridhika hata ukimpata wa kuongea kwa masaa 2
 
Umetoka kwenye hoja unamtukana Mhe. Magufuli.

Jitahidi basi kuwa GT hata kwa kuigiza. Soma tena kichwa cha habari ndipo uchangie.

Aidha Kama kuna hoja yoyote ya Mhe. Magufuli basi ifungulie thread yake.

Rudi kwenye mada tafadhali, usichepuke......

Queen Esther

Bora hata mama lowasa amejaribu kumfichia mmewe siri .Je Magufuri hana mke ? Je ameonekana wapi ? Sana sana anaendaga kwa mapadri kumshitaki Magufuri kuwa ana mahawala wengi hadi anawauzia nyumba za serikali
 
Mwanaume haongei saana na mwanamke anaonyesha matendo kama umezoea kudanganywa kwa maneno kwa Lowasa kuna matendo tu maneno kwenye KANGA.
 
KUMBE NDIO MAANA KINA CHENGE,TIBAIJUKA,MUHONGO NA NGELEJA HATUWASIKII KABISA WAKIONGEA? Ahsante sana kwa kutujuza hilo mkuu.
 
Hanna akili! Mlitaka akidhi kiu yenu wakati kampeni haijazinduliwa? Angeeleza kwa basis IPI ilihali ilani ya uchaguzi haijatangazwa. Huhitaji PhD kujua hili!
 
Yapo maneno yanazungumzwa kuhusiana na badhi ya Wagombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka huu wa 2015 kuwa ni MABUBU, HAWEZI KUJIELEZA NA HWAWEZI KUTUMIA MUDA MREFU KUZUNGUMZA NA WANANCHI
Sababu nyingi sana zinatolewa, kwamba kwa sababu ya afya zao kutokuwa thabiti, kwamba ni asili yao, kwamba ni watu wa vitendo siyo wazungumzaji, kwamba wana viburi kwa sababu ya jeuri ya pesa walionayo.
Naomba niongelee hili la viburi kutokana na jeuri ya pesa. Siyo wote wenye utajiri hususan wa pesa ni MABUBU, la hasha. Sitataja sina la mtu, ila nataka niwakumbushe kuwa Nchi yetu imejaliwa kuwa na Watu wa aina hiyo wengi tu wengine wakiwa wafanyabiashara, wengine watumishi wa Serikali n.k
Nataka pia tutambue wote hao historia za utajiri wao zinajulikana, mahusiano ya wao kwa wao yanajulikana. Wapo ambao utajiri wao hauna mashaka hata kidogo, lakini wapo ambao hata mtoto mdogo anajua utajiri wao ni wa mashaka kabisa(wana pesa haramu). Pesa zao zimetokana na ufisadi, rushwa, biashara haramu n.k.
Utafiti wa unaonesha kuwa Watu wote(narudia wote) ambao utajiri wao ni wa mashaka wanayo laana ya MUNGU, hawezi kabisa kujieleza na hata wakiongea mbele za watu, hawawezi kuwatazama wananchi machoni kwa kujiamini. Hii ni Laana ya Mungu kudhihirisha kuwa wana VIBURI vinavyotokana na matendo yao haramu.
Mali Haramu wanazomiliki zinachukua nafasi katika kufikiri ni kama mwanafunzi aliyezoea kuibia mtihani Darasani, hawezi kujibu hata swli rahisi bila ya kuwa na majibu pembeni au kuigilizia kwa mwenzake. Hiyo ni hulka na haina mjadala.

Sasa hili ni la mhimu sana:
Ukikubali kurubuniwa na watu wa aina hii, dhambi hiyo inaendelea kwako, huwezi tena kujitambua . Kwa nje nje unaona kama UMEPATA lakini kwa ndani unabaki Dhamira inakusuta, unakuwa kama umelaaniwa vile

Ni hayo tu kwa leo, tuchukue tahadhari na hawa Mabubu hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu.

Unaalikwa kama mgeni rasmi utaongea dakika 4 tu yaani dakika nne alafu unachoka Unataka kupumzika... Pole....
 
Lowassa aliwaita wan awake kuwapa maelekezo na wameita kuwa watafanya wewe unataka wapiga filimbi vitendo zero.huko tumetoka sasa in mabadiliko na Lowassa .ujumbe ulikuwa kufanya kazi kwa kwa mchakamchaka asiyeweza na atupishe.watanzania mmezoea kupewa hotuba za masaa Sita vitendo zero.
 
Back
Top Bottom