Edward Lowassa aumbuka Arumeru Mashariki

jana nimeona thread kuwa EL anaumwa, leo meseji ya EL imekutwa kwenye cm ya mollel tuamini lipi sasa au kapona. ngoja tusubiri tutaona mwisho wake
 
Rafiki zangu wa karibu sana Mheshimiwa Pasco & Matola,

Niliwaambia Lowassa alishapotezwa siku nyingi wakanibishia sijui mpaka leo na baada ya kusoma kisa hiki bado wana amini Lowassa is next President ?.

Kitendo cha Lowassa kumuumbua Mwenyekiti wake ndani ya kikao cha Halmashauri kuu ya taifa kwamba alijua kila kitu katika ule mradi tata wa RICHMOND & DOWANS na kwamba alipelekewa jina la Rostam Aziz na kulikubali wakati mwenyekiti alishajitetea hamjui mmliki wa RICHMOND & DOWANS alikuwa akitengeneza jeneza lake kwa mikono yake mwenyewe.Lowassa alikwenda mbali sana alipohakikisha mazungumzo yake yanawafikia wahariri wa magazeti kupitia simu za kiganjani ndani ya kikao cha Halmashauri kuu !.


 
usijitoe akili kiasi hicho, bakisha angalau za kuchambia.
mathias manga ni diwani wa mlangarini .el.ni mbunge monduli takukuru fuatilieni kwa karibu mtagundua mengi ndani ya wahusika
 

Mkuu kwanza maaskofu na viongozi wote wa madhehebu ya kiroho waliokubali kuchambiwa na lowasa wanapaswa kuwajibishwa na waumini wao. Ni ujinga kuendelea kulamba wachafu miguu ili kupata pesa zao hata kama ni kwa njia zosozohalali. Hivi kwa nini hawa viongozi wa kiroho hawakatai pesa zinazonuka? Mbona Roma Catholic wanamuendekeza huyu bwana wao? KKKT na makanisa-uchwara yamekubali kuzini na wafalme wa dunia hii, ole wao nasema. hawa ndio wanaotupoteza sisi waumini, na tusipoangalia mambo haya kwa jicho makini, ya Rwanda yatajirudia hapa.
 

Sasa Mkuu wangu Ngongo naomba unisome vizuri na kwa umakini, Personal mimi kama Matola siwezi kuipigia kura CCM over my dead body, na hata nikipewa sharti kati ya kifo na kuipigia kura CCM mimi nitachaguwa kifo.

Back to Lowasa, mimi nimejiondowa kwenye ushabiki wa kulishwa sumu za chuki dhidi ya Lowasa baada ya kubaini kumbe ni ugomvi wa watu binafsi ambao Taifa limeaminishwa kwamba Lowasa ni adui wa Taifa hili, napinga si kweli. Hakika huyu angekuwa anaitwa Alhaji Abdalah Lowasa wote wanaomsumbuwa wangeshanyamazishwa siku nyingi na matamko makali ya Bakwata na shura ya Maimamu, au hamkuwahi kusikia kwamba Kikwete anasakamwa kawa sababu ya uislamu wake?
Rudia kuisoma post yako mwenyewe vizuri ndio utagunduwa ni kwa nini mimi nimejitoa katika upuuzi wa kumshambulia Lowasa halafu tunamchekea Kikwete.

Kifuta jasho:
Yaliojiri jana Mahakama ya kisutu katika kesi ya Costa Mahalu.

Mahalu alidai kuwa katika mazungumzo hayo, Kikwete alimuuliza mama huyo, "Hivi ni kwanini kunakuwa na mikataba miwili? na mama huyo alimjibu kuwa hiyo ni kawaida kwa Italia ukitaka kununua jengo kwa bei nafuu.

Profesa Mahalu aliendelea kudai kuwa baada ya kupewa jibu hilo, Kikwete hakuzungumza tena zaidi ya kucheka na kwamba mwenye jengo alimkumbusha kuhusu malipo ya awali ya Dola za Marekani milioni moja ambapo aliafiki na kuahidi kuwa zingelipwa kabla ya mwisho wa mwaka.
 
Huu ndo mwisho wa Lowasa. Ama kweli mbio za sakafuni huishia ukingoni
 
Mimi naona hii ni thread ya promo tu kwa maggamba... ili badae ionekani aliyebaki ni msafi!!!

ukiona wezi wanaliana timing, funga milango, weka makufuli kaa macho na panga, wakipatana utakoma!!!

Mkuu umenifungua macho kuhusu hii thread..... lol
 
Hakuna dini inayohubiri Umaskini!!
 
Usiwe kama huwajui takukuru na usanii wa serikali ya Tanzania.

Mwakalebela ashinda kesi ya rushwa, aula Shirika la Makumbusho
 
Ngongo,
Nimeshindwa kuelewa kwa nini kura za maoni zinarudiwa kule AruMeru Mashariki. Sababu alooitoa Nape ni ya uongo kwa kuwa wapo wagombea kama akina Dr Kigwangala walikuwa na kura chache mno lakini wakateuliwa kugombea.
 
hahahaha.. kwa kweli nimeamini na sasa namkubali lowassa fuluu. yaani akiwekwa tu, lazima ukute page 5-10. kweli jamaa ni tishio kubwa sana, sio bure huyo rais/mwenyekiti wa chama anakosa usingizi akimfikiria lowassa. humu ndani nimeshaona watu wengi sana wanamkubali, nilitegemea leo mngechambua hotuba ya jana ya rais. lakini naona mmeanza unafiki wa msg zimekutwa. izo message ziko wapi. kama kweli wangeanika, ni fikra za mtu tu.hamna jipya

mi nilitegemea nitakuta labda hoja ya mgombea wa chadema arumeru, au jinsi mbowe alivyokusanya hela kumfanikisha ashinde.

ivi kweli kwa mtu kama lowassa ataweza kukaa na kuchat aagize watu wakachukue hela. lazima anawatendaji wengi tu wa kufanya ivyo. acheni zengwe
 
hahaha..nimependa ulivyomjibu kwa iyo picha..hahahaha
 
Hii inaweza kuwa kamba ya mtu mzima edo na wanae anatuma sms hawana mkwanja wa kutwanga ?
 
KIM K, hoja zako huwa hazina mashiko kutokana na CHUKI na UDINI
 
Usianze kuhukumu sio kila aitwaye doctor ni doctor kweli. Hali kadhalika professor wote sio ma professor kweli. Huyu ni kijana mchimba madini aliyejipatia fedha zake pale mererani ndo vijana wa hawa wakubwa anaitwa Askofu. Alinunua jengo pale Arusha linaitwa Pallsons Hotel. Sumaye naye anaye wake anaitwa Sunda anamiliki Mount Meru! Akina Kinana na BWM
wanaye wao anaitwa Mrema anamiliki Impala, Naura na ile Ngurdoto. Mkuu kila suruali ina kiraka chake!
 
sasa maneno ya baba wa Taifa aliyoyaongea pale Diamond Jubilee mwaka 1992 yanatimia...
 
Kweli Jakaya kaamua kula hiki kichwa jumla.
Lowassa anatakiwa kutafutwa popote alipo na yeye awekwe ndani
OTIS
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…