ECG Makongo na ibada ya kula nyama Ijumaa Kuu

ECG Makongo na ibada ya kula nyama Ijumaa Kuu

Kwani wee wamekukosea nini hao ECG? Au ni chuki tu binafsi?
wanauchafua ukristo !!! kwa kwenda kinyume. Waasisi wao walipotengana na ukristo kwa kushindwa sheria zake ingebidi wajipe jina jingine sio kuendelea kujiita wakristo huku kwa makusudi kabisa wakienda kinyume na desturi za wakristo
 
Wanataka Yesu yupi?
Hawa manabii uwa wanamchukulia Yesu alikuwa nabii wa kawaida tu ingawa bado wanatumia jina lake, ndio maana wana hadi mitume ambao wanafanya kazi kwa ajili yao kama Yesu mfano mtalemwa ni mtume wa bushiri tanzania na sio wa Yesu
 
Hawa manabii uwa wanamchukulia Yesu alikuwa nabii wa kawaida tu ingawa bado wanatumia jina lake, ndio maana wana hadi mitume ambao wanafanya kazi kwa ajili yao kama Yesu mfano mtalemwa ni mtume wa bushiri tanzania na sio wa Yesu
Kuna mtu ambaye physically kaitwa Na YESU?
 
Kuna mtu ambaye physically kaitwa Na YESU?
Wapo wengi tu, kuanzia mtume paulo, hujaona mtume paulo alivyoitwa na Yesu mwenyewe kabla ya kuanza huduma yake??? Au ndo uwa hamsomi biblia?? Na hata sasa wapo watu Mungu anawaita na wanampa Yesu kristo wa nazareth utukufu......hao manabii utukufu ni kwa Mungu wa nabiii.. .. Je huyo Mungu wa nabii ni Yesu wa nazareth??? Mitume wote walifundisha habari za Yesu na miujiza yao ilikuwa dhahiri, hata leo bado Yesu anawatokea watumishi na kuwapa huduma, pia sio lazima Yesu akutokee ww moja kwa moja ndo uanze huduma ila unatakiwa uwe mtume/nabii wa Yesu sio wa baba yako wa kiroho, baba yako ni kama kiunganishi tu na Yesu, Yesu ndiye mtenda miujiza mwenyewe naye ndio anatakiwa kuwa promoted na sio nabiii/mtume.
 
Baada ya Yesu hakukuwa na nabii au mtume ambaye Mungu wake aliabudiwa ila wote walitangaza habari za Yesu wa nazareth, maana Yesu ndio Mungu pamoja nasi na ndo anaishi ndani yetu tunatakiwa kumwabudu yeye, hao wengine wa Mungu wa sijuia nabii nani, hao wanamkataa Yesu wa nazareth ndio maana hata mitume wa Yesu walikuwa wanasema Yesu wa nazareth ndio anafanya miujiza yote, ila leo hii eti Mungu wa mtume/nabii ndo anafanya!!!! Umeona wapi hii baada ya ujio wa Yesu??
Kama hata 10% ya Wakristo wangekuwa na upeo kama wako, nina uhakika kabisa Imani ya Kikristo ingekuwa nguzo kuu ya maisha ya wakristo tofauti na ilivyo sasa ambapo huwezi kutofautisha wakristo na wapagani.

Yaani wakristo wengi wa sasa wamemuacha kabisa Yesu wao, wako busy kweli kweli na madhehebu yao, Manabii, Mitume nk.
 
Mathayo : Mlango 26

26 Nao walipokuwa wakila Yesu alitwaa mkate, akabariki, akaumega, akawapa wanafunzi wake, akasema, Twaeni, mle; huu ndio mwili wangu

Marko : Mlango 14

22 Nao walipokuwa wakila, alitwaa mkate, akabariki, akaumega, akawapa, akasema, Twaeni; huu ndio mwili wangu.

Kutakuwa Na ibada ya kula nyama siku ya Ijumaa Kuu kwenye kanisa la ECG Makongo Juu linalo ongozwa Na Chief Apostle Mtalemwa Deonis.
Wote mnakaribishwa.
Bujibuji nitakuwepo kusonsomola misosi, tena Kitimoto ndio ijiandae kabisa kuandika maumivu.
Don't dare to miss
Mkuu ulivyoanza Verses za Mikate nikadhani hata huko ni kwa huyo Jamaa ni Mikate pia,
Sasa issue za nyama zimetoka wapi tena?

Kwani Mikate haipatikani mpaka mtumie Nyama?? Na kuna kiingilio chochote au mchango??
Natangaluzia shukrani Kaka
 
Kama hata 10% ya Wakristo wangekuwa na upeo kama wako, nina uhakika kabisa Imani ya Kikristo ingekuwa nguzo kuu ya maisha ya wakristo tofauti na ilivyo sasa ambapo huwezi kutofautisha wakristo na wapagani.

Yaani wakristo wengi wa sasa wamemuacha kabisa Yesu wao, wako busy kweli kweli na madhehebu yao, Manabii, Mitume nk.
Siwashangai sana maana hata mimi katika kipindi cha ukuaji wa kiroho nimepitia changamoto nyingi sana ambazo zinaendana na hizo kama kushindwa kutambua imani ya kweli ni ipi, na nini msingi wa madhehebu na dini tofauti, nikaja kugundua watu wote ambao wanataka kuwa wafuasi wa Yesu, imani yao inatakiwa iwe kwa Yesu wa nazareth, na wamhubiri yeye na kile ambacho mitume wake walikihubiri, sasa leo hii unakuta kuna nabii/mtume naye anawafuasi wanamwabudu yeye au Mungu wake, wanashindwa kujua wote tu wafuasi wa Yesu kwa kuamini injili na Mungu wetu ni mmoja ambaye ni Yesu mwenyewe, kwani ndiye aliyedhihirishwa katika mwili, sasa watu wengi wamejengwa katika msingi wa kidini/madhehebu/mitume/manabii wa kileo ambao wengi wao wamejiita na wanatumiwa na mashetani/kuzimu, na msingi wao ni mmoja tu kupotosha kweli ya Mungu,

Imefika hatua kwa sasa jina la Yesu aliponyo tena watu wanaishia kuwa na maji/mafuta ya upako as kitu cha kumponya mtu, badala watu kujazwa roho mtakatifu na kupokea nguvu ya kuponya watu wanatembea na maji/mafuta/vitambaa/pete nk
 
UNAVYO JIHISI KIFO.
Mtu huwa hatambui kuwa amekufa pale anapokufa. Yeye hujihisi anaota anakufa, anajihisi analia, anaoshwa, anafungwa na anateremshwa kaburini.
Bado anajihisi kuwa anaota anapofunikwa na mchanga. Kisha hulia kwa makelele na hakuna anae msikia.
Baadae kila mtu anapotawanyika na ameachwa pekee chini ya ardhi, Mungu huirudisha roho yake. Anafungua macho na kuamka kutoka "ndoto yake mbaya". Mwanzoni, hufurahi na kushukuru kuwa alikuwa anaota tu, na sasa ameamka kutoka usingizini. Kisha hujigusa mwili wake ambao utakuwa umefunikwa na kitambaa cheupe,na kwa mshangao hujiuliza "shati/gauni langu liko wapi?"
Kisha ana anza kujihisi "niko wapi?" "hii ni sehemu gani?" Mbona kuna harufu ya udongo kila mahali? Ni nini haswa ninacho kifanya hapa?
Hapo ndipo atakapo anza kugundua kuwa yuko chini ya ardhi na alicho kihisi haki kuwa ndoto!
Ndiyo, anagundua kuwa ni kweli yeye amekufa, na amezikwa.
Anapiga kelele kadri anavyoweza kuwaita watu waliokuwa karibu nae ambao wangeweza kumuokoa:
"baba"
"mama"
"kaka"
"dada"
"rafiki"

Hakuna anaemjibu. Kisha anagundua kuwa Allah ndio tegemeo lake pekee. Akilia na kumuita huku akimuomba msamaha :
"Yaa Allaaaaah...
Yaa Allaaaaaah...
Nisamehe mimi
Yaa Allaaaaaah!!!

Anaita akiwa na hofu kubwa,ambayo hakupata kuwa nayo alipokuwa hai .

Kama alikuwa mtu mwema na mcha Mungu, malaika wawili wakiwa na uso ulio na furaha watamkalisha na kumliwazana kumhudumia vizuri.

Kama alikuwa mtu mbaya na hakuwa mcha Mungu, malaika wawili watamwongozea hofu yake na kumpa mateso kufuatana na amali zake mbaya.

Ewe Mola, nisamehe dhambi zangu, dhambi za baba yangu, mama yangu, mke/mume wangu na wanangu na jamaa zangu na marafiki.

Ewe Allah, usiuchukue uhai wangu ila pale nitakapo kuwa tayari kukutana nawe.

Kaka na dada katika uislam,una chaguo mbili hapa:

1.Uache ilimu hii hapa isomwe na hakuna kitakacho tokea.
2. Isambaze ilimu hii kwa marafiki zako,.na wote wengine.
In Sha Allah itakuwa na manufaa kwao, na wewe utafaidika.

Ameen.
 
wanauchafua ukristo !!! kwa kwenda kinyume. Waasisi wao walipotengana na ukristo kwa kushindwa sheria zake ingebidi wajipe jina jingine sio kuendelea kujiita wakristo huku kwa makusudi kabisa wakienda kinyume na desturi za wakristo
Ukristo ni upi?
 
Kwa hiyo hawamuhubiri Yesu?
Nini tofauti kati ya Mungu wa Yakobo, Shadrach, Meshach, Ibrahim Elijah Na huyu Mungu wa Major 1.
Je ECG hawatumii Biblia?
Mkuu mantiki ya Mungu kujitambulisha kupitia Ibrahimu, Isaka na Yakobo ilikuwa ni njia ya Mungu kujitofautisha na miungu iliyokuwa ikiabudiwa kabla Mungu hajajifunua rasmi kwetu.

Sisi ni kizazi chenye bahati maana Mungu kupitia Yesu Kristo amejifunua kwetu hivyo hao wanaopenda kumuita Mungu kwa kupitia imani za watumishi wao ni sawa na kusema bado Mungu hajajifunua kwao.

Alafu hii tabia ya kusema Mungu wa TB Joshua sijui Major 1 n.k ni hatari mno! Wapo watumishi wasio wa Mungu na inawezekana hujafahamu, kumuita Mungu wa mtumishi unaweza kuwa unaita miungu bila kujua.

Wapo watumishi hasa manabii wa kizazi hiki wakikuona mgeni wanakutabiria alafu wanakwambia ili akusaidie lazima uungane na madhabahu ya Mungu wake kupitia sadaka. Hii ni HATARI mno!!! unaweza kujaunganishwa na madhabahu za kuzimu bila kujua. Jamani Mungu wenu ni yule aliyejifunua kupitia Yesu Kristo ACHENI kuishi kale na hayo majina!!

Ukitaka kutumia majina ya kale yapo mengi kama Jehova kwanini uanze kuita miungu ya watumishi wako kisa wanatenda miujiza??? Mnafikiri shetani hatendi miujiza??? Majina tunayoruhusiwa ni yale yaliyotumia kwenye Biblia tu! Kanisa kwa uangalifu ndio maana haliruhusu hata Majina ya Malaika ambayo hayajatajwa kwenye Biblia (ni moja ya sababu ya kitabu cha enock kukataliwa maana kimetaja majina mengi ya malaika kinyume na maandiko mengine).

Kaeni makanisani kwenu zipo huduma nzuri sana badala ya kuhangaika hadi mnalishwa matango pori. Kanisa Katoliki kuna Karistimatiki nenda pale Emaus au parokia yeyote wapo na wanafanya vizuri chini ya ulezi wa mapadre pia youtube tafuta hefsiba tv ujifunze mwenyewe .

KKKT wapo walimu akina Christopher Mwakasege, Grace Elirehema n.k nendeni youtube mtajifunza mengi huko na kujisimamia wenyewe kupitia watumishi ambao mnajua walikotoka na mafundisho yao hayako kinyume na Kanisa.

Wewe mkristo ACHA kuita miungu usiyoijua! Muite Yesu Kristo pekee ambaye kupitia yeye Mungu alijifunua kwa jina lake halisi ndio maana Yesu anasema yeye amerithi jina lake kutoka kwa Baba. "Kwa JINA LAKO ULILONIPA" Soma hii nukuu ya maneno ya Yesu mwenyewe;

"12 Nilipokuwapo pamoja nao, mimi naliwalinda kwa jina lako ulilonipa, nikawatunza; wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, ila yule mwana wa upotevu, ili andiko litimie.
Yohana 17 :12"
 
Mkuu nilitaka nichangie hapo kwenye kutaja Mungu wa fulani ila naona mwishoni ume eleza kitu kizuri kwamba " ili mradi huyo Mungu awe anaunganishwa Na YESU KRISTO wa Nazareth".Hapo nikupe kikazi kidogo usiwe mwepesi wa kujibu bali tafakari na ukisema uwe na ushahidi wa kutosha,je mungu wa huyo Major wewe una uhakika gani ameunganishwa na Yesu wa Nazareth?Ukiwa na evidence nzuri hapo itakuwa safi.Mungu akubariki

Kula nyama siku ya ijumaa kuu siyo shida kwani ambao hawali wanajua ni maagizo ya kanisa wala si ya Mungu.Kwa hiyo wale walioambiwa kwa mujibu wa imani zao wasile itakuwa kosa wakila,ila mimi kwa imani nikutana na nyama siku hiyo nakula.Kuanzia kitabu cha Mwanzo hadi ufunuo,hakuna palipozuia,so ni makubaliano ya wanadamu.
Nakubaliana na wewe kwa sehemu lakini kosa mnalofanya ni kutenganisha maagizo ya Kanisa na ya Mungu. Hili mnahitaji shule kwelikweli.

Kwa mfano ni wapi Mungu anasema wanadamu wawe na Biblia yenye vitabu fulani tu? Kanisa kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu likafanya hilo. Kama umekubali agizo la Kanisa kuwa Biblia unayotumia ndio sahihi kwanini upinge maagizo mengine?

Ukusoma matendo ya Mitume utaona mitume waliagiza waamini wauze kila walichonacho wagawane kwa usawa na kuishi kishirika. Watu waliuza na yule mtu na mke wake walipodanganya kiasi walichopata walipata mauti kwa kukaidi lile agizo. Je ingekuwa wewe si ungesema ni agizo la wanadamu na si Mungu? au imendikwa wapi tuuze kila kitu na kugawana sawa? Leo ambao hatufanyi hayo makanisa yote tunakosea? Nani alisitisha hili?

Ijumaa kuu tumeagizwa kutokula nyama na Kanisa likatoa sababu ili dunia nzima tusichinje au kumwaga damu kama ilivyokuwa desturi zamani ya kumwaga damu za wanyama ili kuondolewa dhambi.

Ijumaa kuu hatumwagi damu za wanyama maana damu yenye thamani imemwagwa pale msalabani. Ni njia tu ya kuinjilisha na kutukumbusha ukomo wa kutumia damu za wanyama kuondoa dhambi!

Hakika Wakatoliki hatutokula nyama (maana yake msimwage damu siku hiyo) na siku hiyo idadi ya ngombe, kuku, nguruwe n.k itayochinjwa itakuwa ndogo tofauti na siku nyingine hivyo automatically kule kutii kutomwaga damu siku hiyo ni utii wa kutambua iko damu yenye thamani pale msalabani!! Zipo namna nyingi za tafakari ya neno la Mungu na utii kwa Kanisa si shauri ni lazima kama wewe ni Mkristo.
 
Ninachoshindwa kuwaelewa ECG ni mda mwingi kutumia kusema i receive, kila mtume akiongea nao wanapokea i receive, na wanamwomba Mungu wa major one, sasa sijui kwa nini mnashindwa kumuomba Yesu kristo wa nazareth? Mnaomba kwa jina la Mungu wa major??
halafu huyo Major one wanamtukuza kuliko Yesu
 
Hahah,hilo kanisa siwez lisahau mkuu,..nilipeperushiwa ndege wangu hiv hiv......wanahuduma ya kutabiri na maono bas dem wangu aliambiwa mim si muoaji na ikiwezekana aachane namim,..hahaah,au la niende hapo church nkaombewe,hahah,mim ni RC dam dam siwez kubal dram hyo...makanisa haya yana maigizo sana ukuhudhuria,dem huyo alinishawish mara 2,ila kwa style ile ya mahubir na huduma,nkamwona mtalemwa mjasiriamali mwenzangu tuu,skwenda teeena,..ila magar yanayopak pale ni balaa,kuna watoto balaa na watu maaruf.

Hyo I RECEIVE na kupigia magot pastor ndo iliniacha hoi
hilo kanisa litanifaa.
nitakwenda.
 
Ivi ile campaign ya bushiri must fall imefikia wapi maana prophet kabaki kutoa vitisho vya mauti tuu
 
Back
Top Bottom