ECG Makongo na ibada ya kula nyama Ijumaa Kuu

ECG Makongo na ibada ya kula nyama Ijumaa Kuu

ijumaa kuu haitakiwi kuwa siku ya huzuni ilitakiwa kuwa Siku ya shangwe kuliko zote katika mwaka.
 
Katika injili ya Math:26:26 - 28 Bwana Yesu Kristu mwenyewe alifafanua hilo jambo la Mwili na Damu yake.

Baada ya kuona hata wanafunzi hawakuipata hiyo dhana ya kula na kunywa kwa mwili na damu yake. Ndiyo akaumega mkate usiyotiwa chachu na kusema HUU NDIYO MWILI WANGU PIA AKACHUKUWA KIKOMBE CHA DIVAI ZAO LA MZABIBU NA KUSEMA HII NDIYO DAMU YANGU. Akaongeza kusema kuwa ndiyo agano lake jipya.

Kanisa Katoliki limeundwa si kwa kurupuka. Hata mambo yote na maadhimisho yote siyo mawazo ya mtu mmoja kwa kisingizio cha kuwa NABII. HAKUNA nabii aliyeseti mambo yake yakawa ndiyo utaratibu wa kanisa. Hata zamani zile manabii hawakuunda taratibu za kuishi kikanisa kama taasisi. Bali waliyachunguza maandiko yote ndipo wakaseti mfumo wa kanisa. Kanisa katoliki usiliangalie leo kama makanisa yaliyokuja na kukuta vitu vimeandaliwa tayari.
Ni juhudi zake hata kuchunguza vitabu gani vinavyofaa kuwa pamoja na kutumika kanisani kama ilivyo leo hiyo biblia wanayoitumia na kuwapa kiburi. Hidharau mapokeo lakini wajue kuwa mapokeo hayo ndiyo yalikuwa maisha ya kanisa la kwanza ka Mitume hata kabla ya kupokea hicho kitabu. Nao mitume waliyaishi hadi kuwa watakatifu na qalioifia imani. Nyaraka zote zilikuwa ni kwa ajili ya makanisa Mahalia wakati ule ila Kanisa katoliki ndiyo ilifanya juhudi kukusanya nyaraka zote hizo kuwa kitabu cha agano jipya. Lakini kipindi hicho chote kanisa lilikuwapo ulimwenguni katika Roho mmoja huyo. Si maamuzi ya mtu mmoja walifanya hayo maamuzi yote karne ya 3 kama miaka ya 312 wababa haohao walikaa siku 90 bila kupumzika ndani ya conference na bila kupokea rushwa waliachambua mambo yapo mengine waliyaacha na mengine waliyapokea. Ila yapo katika maktaba ya kumbukumbu huko Vatican. Kumbe.
Nao ndiyo walioseti hata Tarehe ya kikanisa kwa ajili ya maadhimisho muhimu kama hayo ya Christmas na ya kipasaka Pasaka ( kama Alhamisi kuu, Ijumaa kuu Na kufufuka kwake)
Hao wakaweka na tafsiri ya maana ya kuwa Mkristo nini pamoja na Imani yake huyo Mkristo. Someni historia ili ujijue kuwa unapoabudu unaamini nini juu ya hiyo unayemwabudu.
 
Back
Top Bottom